MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI


1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES.


Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza kumsaidia.


2.Kusema Ahsante.


Wateja wengi hujisikia wana thamani pale wanashukuliwa baada ya kupata mahitaji yao.


3. Kuweka Concentration yote kwao pale unapowahudumia.


Kama ulikuwa unaongea na simu, unaweza kusema samahani naomba nikupigie baadae nikimaliza kumhudumia mteja badala ya kusema nimalizane na kimeo na maneno mengine ya ajabu.


-Hii humfanya mteja ajione ana thamani kwako.


4.Kusikiliza Malalamiko ya Mteja na kuyafanyia kazi mapema iwezekanavyo na si kuzi challenge Complain zake.


Mala nyingi mteja hujihisi ana haki zaidi kuliko wewe


Unaweza kumpa offer nyingine kama malalamiko yake ni ya kweli na kumuomba msahamaha kwa usumbufu uliojitokeza



5. Hakikisha unamfanya mteja ajisikie na awe na amani kwamba anafanya maamuzi sahihi kupata huduma zako.


Kumbuka hili, Wapo wateja ambao hawafati muonekano mzuri wa duka lako ila wanakufuata wewe kutokana na namna bora unavyowahudumia.


6. Kupungukiwa na bidhaa ni jambo la kawaida.


Ikiwa una nafasi ya kwenda kumchukulia kwa jirani yako anayeuza bidhaa kama zako au kumuelekeza wapi anaweza kukipata si kumpoteza mteja bali hukujengea mahusiano mazuri na  mteja.


Huyo ni mteja wako  tena wa siku za usoni.


7.Huduma na bidhaa zako ziendane na hali ya ushindani iliyopo ndani ya soko ili uweze kuvuna wateja wengi zaidi.


8.Kubali Mapungufu yako na yafanyie kazi.


Anayekwambia ukweli ndiye anayekupenda .


Mteja anayekuambia ya moyoni kuhusiana na mapungufu yako ndiye anayekusaidia.


#MALOSHA

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...