SIMULIZI: PENIELA (Season 2 Ep 16)
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPA
“ Huyu mzee anaonekana kifo cha mkewehakijamgusa kabisa.Hainiingii akilini eti hata mkewe hajamaliza siku moja kaburini tayari ameanza kufikiria masuala ya kuioa.laiti angenijua wala asingeongea upuuzi ule .Lakini mbona ninaanza kuingiwa na shaka sana kuhusiana na kauli hizi za Dr Joshua? Toka kipindi kile hata mkewe bado hajafariki alikuwa akinitamkia kwamba mke wake atakufa hivi karibuni na mimi nitakuwa first lady.Ninapatwa na wasiwasi kwamba ya wezekana kifo cha dr Flora kikawa ni cha kupangwa ili mambo anayoyataka Dr Joshua yaweze kutimia” akawaza peniela wakati aiingia chumbani.Akaiweka simu mezani na kupanda kitandani akajilaza pembeni ya jaji Elibariki
“ Elibariki kuna kitu nataka kukuuliza” akasema Peniela
“Uliza Penny”akasema Elibariki
“ Nini kilimuua Dr Flora? Akauliza Peniela na kumstua sana Elibariki
” kwa nini unauliza hivyo Penny?
“ Ninahitaji tu kufahamu” akasema Penny
“ Dr Flora alikufa kwa shinikizo la damu”
“ Are you sure? Akauliza penny
‘ yes I’m sure” akajibu jaji Elibariki na kuendelea kushangaa kwa nini Peniela alimuuliza maswali kama yale.
ENDELEA……………..
Peniela aliendelea kumtazama jaji Elibariki kwa macho malegevu huku akimsugua sugua kifuani.Alijisikia furaha sana moyoni
“ Haya ni maisha ambayo nimekuwa nikiyaota kila siku kuishi yaani kuwa na mtu wangu ambaye ninaamini ni wangu peke yangu ambaye nitakuwa nikilala naye na kuamka naye.Elibariki ameifufua ndoto yangu ya miaka mingi ambayo nimekuwa nikiota kumpata mwanaume wangu lakini kwa sababu ya Team SC41 imeshindwa kutimia.Safari hii lazima ndoto yangu iwe kweli lazima nimpate mwanaume ambaye moyo wangu utafunguka kwake.Nadhani Elibariki ni mtu anayenifaa sana japokuwa ni mume wa mtu lakini silijali hilo kwani yeye mwenyewe amekwisha onyesha kila dalili kwamba ananipenda na ndiyo maana pamoja na kilichotokea siku ile lakini bado amechagua tena kuja kukaa hapa kwangu.Amekwisha nitamkia kwamba ananipenda sana na hata mimi ninahisi kumpenda.Ni mwanaume mwenye vigezo vyote vya kuwa mume.Amenitamkia yeye mwenyewe kwamba kwa sasa yeye na mke wake wana mikwaruzano nadhani hii ni fursa pekee ya kuanza kuandaa mazingira ya kumuweka katika himaya yangu ili nitakapokamilisha tu opreseheni 26 B basi tayari kuwe na mzizi imara na nianze maisha mapya na Elibariki kwani sitaki tena kufanya kazi yoyote na Team SC41 na hata John amenihakikishia kama hataki tena mimi kuwa sehemu ya Team SC41 na baada ua kukamilisha opereshen 26B basi nitaanza maisha mapya.” Akawaza Peniela.
“ kwa mara ya kwanza leo hii umenifanya nibadili msimamo wangu.Ninataka kuendelea kuishi tena kwa sababu yako.Nataka niyatengeneze maisha yako upya kwani ni mimi niliyeyaharibu kwa kukuingiza huku Team SC41.”
Kauli hii ya John Mwaulaya ikamjia kichwani.Akafumba macho na kwambali akahisi macho yake yakiloa machozi
“ Kwa nini John aliamua kuningiiza katika Team SC41? Kwa nini hakuniacha nikaishi maisha yangu ya kawaida niliyokuwa nikitaji kuishi ? Ndoto yangu kubwa ilikuwa ni kuwa mtaalamu wa wanyama lakini badala yake nimeangukia katika mikono ya Team SC 41 na kufanya kazi ambazo sikuwahi kuota kuzifanya.” Peniela akageukia upande wa pili ili Elibariki asigundue kama analia .
“ Siwezi kuisahahu siku ile ,siku ambayo maisha yangu yaliharibika” akawaza Peniela na kumbu kumbu zikamrudisha mbali sana baada ya kumaliza kidato cha sita
Ni siku ya jumanne Peniela akiwa ametulia sebuleni katika jumba lake kubwa mara akapigiwa simu ya mmoja wa rafiki zake akimtaarifu kwamba matokea ya kidato cha sita yametoka.Haraka haraka Peniela akachukua kompyuta yake akafungua tovuti ya baraza la mithani la taifa na kutazama matokeo.Ilikuwa amefaulu vizuri sana kwa daraja la kwanza.Aliruka kwa furaha sana .
‘ Thank you Lord.Nilijua tu lazima nitafanya vizuri.Sasa ndoto zangu zinakwenda kutimia” akasema Peniela kwa furaha kubwa.
Jioni ya siku ile akapigiwa simu na kupewa pongezi na mfadhili wake John Mwaulaya .
“ Peniela pamoja na pongezi zote nilizokupa nina zawadi nyingine kwako.”
“ Zawadi gani baba? Akauliza Peniela ambaye alizoea kumuita John baba
“ Unakwenda kusoma nje ya nchi.Na tayari nimekwisha kutafutia chuo kizuri sana kinachotoa elimu bora.” Akasema John.Peniela akashindwa kuizuia furaha yake machozi yakamtoka
“ Ninashukuru sana baba kwa zawadi hii.Ni ndoto yangu kubwa sana kwenda kusoma nje ya nchi .Ninaamini zile ndoto zangu zote zinakwenda kutimia.” Akasema Peniela
“ Usijali Peniela kila kitu kitatimia.Kila kitu tayari kimekwisha andaliwa na safari ni jumatatu ijayo kwa hiyo anza kufanya maandalizi madogo madogo “ akasema John
Siku zilienda kwa kasi na hatimaye siku ya Peniela kuondoka nchini ikawadia.Ilikuwa ni siku yake yenye furaha sana na iliyojaa matumaini.Dege alilopanda lilipaa na kuiacha ardhi ya Tanzania .
“ Ningejua siku ile kama maisha yangu yatakwenda kubadilika kule Marekani nisingeingia katika ile ndege.” Akawaza Peniela na machozi yakamtoka na kumbu kumbu zimkamrejesha tena alipofika jijini New York Marekani
Donald Stevens alimpokea Peniela katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jf kennedy .
“ Karibu sana New York” akasema Donald na kumuongoza Peniela hadi katika gari moja la kifahari akafunguliwa mlango akaingia na moja kwa moja akapelekwa katika hoteli kubwa ijulikanayo kama The Plaza.Peniela hakukaukiwa na tabasamu kwa kila alichofanyiwa.Hakuwa ametegemea mapokezi yale makubwa aliyofanyiwa na kumfanya azidi kujiuliza huyu mfadhili wake John mwaulaya ni mtu wa namna gani hadi akamfanyia yale yote? Alikaa katika hoteli ile ya kifahari kwa siku saba akimsubiri mwenyeji wake Donald ili ampeleke katika chuo alichokuwa ameandaliwa.Wakati wote aliokuwa pale hotelini alikuwa akiwasiliana na John na kumfahamisha namna alivyopokelewa na namna anavyohudumiwa.
Ilikuwa ni siku ya jumatatu Donald alipomfuata Peniela pale hotelini na kumtaka achukue mizigo yake kwani anampeleka katika chupa alichokuwa ameandaliwa.Peniela alifurahi sana na kuchukua mizigo yake wakaelekea uwanja mdogo wa ndege wakapanda ndege ndogo ambayo ukiacha na rubani abiria walikuwa ni wawili tu peniela na Donald.
Ndege le ilitua katika uwanja mmoja mdogo wa ndege wakashuka.Kulikuwa na majengo kadhaa mahala pale na palionekana kama chuo Fulani.Vijana wawili waliovalia nadhifu wakampokea Peniela mizigo yake na kuondoka nayo halafu yeye na Donald wakaelekea katika jengo moja la ghorofa tatu.ndani ya jengo lile wakaingia katika ofisi moja kubwa iliyokuwa kama chumba cha mikutano na kuwakuta watu zaidi ya saba wakiwa wameizunguka meza na ilionekana wazi kwamba walikuwa wakimsubiri Peniela awasili.Mara tu Peniela alipoingia ndani ya kile chumba wakasimama na kusalimiana naye kwa heshima na kisha akakaribishwa kiti pale mezani.Bado Peniela alikuwa akishangaa sana kwa namna watu walivyokuwa wakimnyenyekea na mwanzoni alidhani labda watu wale walikuwa ni wakuu wa chuo alichokwenda kukisoma.
“ Peniela karibu sana ,hapa ni chuo cha mafunzo cha Team SC41 “akasema mzee yule aliyefahamika kama Michael macksons .
“ team SC41 ? Peniela akashangaa.
“Ndiyo hapa uko katika chuo cha Team SC41” akajibu Michael
“ Sikuambiwa kama ninakuja kusoma katika chuo hiki.Hapa mnatoa kozi gani? Akauliza Peniela kwa mshangao
“ Kuna kozi nyingi zinazotolewa hapa lakini nakuomba usiwe na haraka sana na utafahamishwa kila kitu”
Peniela alianza kueleweshwa kuhusu team SC41 ilivyo ,nia na madhumuni yake vilevile na faida yake kwa Marekani na kwa nchi ambazo zina vikosi vya team SC41.Pamoja na maelezo mengi aliyopewa lakini Peniela alishindwa kukubaliana nao na hakutaka kuendelea kukaa pale akaomba wamruhusu aondoke kwani kilichompeleka marekani ni kusomea masuala ya wanyama na si kusomea mambo ya Team SC41.
“ Juhudi za kumashawishi Peniela akubali kujifunza masuala ya Team SC41 zilishindikana ikawalazimu kutumia nguvu.Waliitwa watu wawili wakamchukua Peniela na kwenda kumfungia katika kiti Fulani katika chumba kilichokuwa na mitambo mingi.Kilichofuata hapo taa zikazimwa na chumba chote kikawa giza.Peniela hakujua chochote kilichoendelea baada ya hapo kwani alifumbua macho na kujikuta akiwa amelala katika chumba kimoja na wasichana wawili mmoja wa kijapani na mwingine mzungu.Hawa walikuwa rafiki zake na kwa pamoja wote walikuwa wakijifunza kuhusiana na Team SC41.
“ Sielewi watu wale walinifanya nini kwani nilipofumbua tu macho sikuwa tena na ule upinzani wangu niliokuwa nao kabla ya kuingizwa katika chumba kile.Nilijikuta nikitamani sana kuifahamu Team SC41.Lakini ninaamini kuna kitu wale jamaa walinifanyia ndani ya kile chumba .Walicheza na akili yangu .Pale ndipo waliponiharibia maisha yangu kwani baada ya kutoka ndani ya kile chumba sikuwa ni mimi Peniela wa zamani.Nilijiona kama mtu mpya kabisa mwenye mawazo mapya.Nilijisikia fahari kuwa mmarekani na sikutaka kabisa kuitwa Mtanzania.They destroyed me” akawaza Peniela na kushindwa kujizuia kulia kwa kwikwi na kumstua jaji Elibariki aliyekuwa pembeni yake
“ Peniela kuna nini? unalia nini ? Akamuuliza jaji Elibariki na kumeuza Peniela akamtazama usoni.Macho yake yalikuwa yameloa machozi
“ Unalia nini Peniela? Una tatizo lolote Penny? Tafadhali nieleze nini kinakuliza? Akasema jaji Elibariki.Peniela akafuta machozi na kusema
“ Elibariki nimekuwa nikiwaza sana kuhusiana na maisha yangu na namna ulivyonitendea nikajikuta nikishindwa kujizuia kuangusha machozi.Ninawaza nini nitakuiipa kwa wema wako ule ninashindwa kupata jibu” akadanganya Peniela
“ Ouh Peniela come here” akasema jaji Elibariki na kumkumbatia Peniela.
“ Hutakiwi kudondosha machozi Peniela.Uso huu wa kimalaika unatakiwa kuwa na furaha wakati wote.Niliweza kukuachia huru wakati ule kwa sababu niliamini kwamba hukutenda lile kosa.Wengine walikuwa wakikutazama kwa macho ya kawaida lakini mimi nilikuwa nikikutazama kwa macho ya moyoni na ndiyo maana pamoja na ushahidi wote uliotolewa mahakamani ambao ungeweza kukutia hatiani lakini bado niliweza kufanya maamuzi yale niliyoyafanya na nilifanya vile kwa sababu mbili .Moja ni kwa sababu hukutenda kosa na pili ni kwa sababu moyo wangu tayari ulikwisha kupenda.Peniela niamini kwamba nilikupenda sana toka siku ya kwanza nilipokabidhiwa kesi yako.Nilipokuona tu mahakamani moyo wangu ulistuka sana na nikajua kwamba wewe ndiye yule ambaye uliumbwa kwa ajili yangu.Niliumia sana kwa wewe kuendelea kukaa mahakamani na ndiyo maana kesi yako haikuchukua muda mrefu kama kesi nyingine.Sikutaka uendelee kuteseka mahakamani”akasema jaji Elibariki
“ Elibariki nashukuru sana na sina neno zuri la kuweza kusema ahsante lakini ni Mungu pekee anayeweza kujua namna moyo wangu unavyokushukuru.Lakini naomba nikuulize swali moja dogo sana”
“ Uliza Penny”
“ Endapo ungeridhika kwamba nina hatia na kweli nimeua ungenifunga gerezani?
Swali lile likambabaisha kidogo jaji Elibariki akatabasamu na kusema
“ Peniela swali lako gumu lakini zito sana.Walisema kwamba mapenzi ni upofu na katika penzi kila kitu kinawezekana.kwa kuwa tayari moyo wangu ulikwisha niambia kwamba wewe ndiye yule ambaye ninaaminini mtu sahihi kwangu basi nisingekupa adhabu yoyote.Ningekuachia huru hata kama ungekuwa na hatia.Ningepindisha sheria ili kuhakikisha kwamba unakuwa huru.”
“ real ?! akauliza Peniela kwa mshangao
“ Ndiyo nigefanya hivyo.Siwezi kumuacha mwanamke ninayempenda afungwe gerezani .Niko tayari kwa lolote lile kwa sababu ya mtu ninayempenda”akasema jaji Elibariki na kuufanya mwili wa Peniela usisimke sana.Peniela akamkumbatia kwa nguvu na kumpa busu zito
“ Ahsante Mungu.Huyu ndiye mwanaume niliyekuwa nikimuota.Mwanaume ambaye yuko tayari kufanya lolote kwa ajili yangu.mwanaume ambaye yuko tayari kuipoteza furaha yake kwa sababu yangu.Elibariki ndiye mtu sahihi kwangu na ambaye ninataka kuanza maisha mapya nikiwa naye.”akawaza Peniela.
“ Elibariki bado kuna swali naomba nikuulize” akasema Peniela
“ Uliza kitu chochote Peniela usihofu”
“ Do you love your wife?
Ilimchukua zaidi ya dakika moja jaji Elibariki kulijibu swali lile
“ Peniela nilikwambia kwamba maswali yako madogo lakini mazito sana.Kwa ufupi ni kwamba nilikutana na Flaviana wakati tukiwa chuoni.Mimi nilikuwa nasomea shahada ya pili ya sheria na yeye alikuwa shahada ya kwanza.Mazingira ya kukutana kwetu yalikuwa ya kiajabu sana kwani nilikutana na Flaviana katika sherehe ya kuwakaribisha wanachuo wapya.Siku hiyo Flaviana alilewa sana pombe na rafiki zake wakaniomba nimsadie kumbeba na kumpeleka chumbani kwake.Nilifanya hivyo na kesho yake akanitafuta kunishukuru kwa msaada wangu ule.Huo ukawa ni mwanzo a kujuana kwetu na hadi tukafikia hatua ya kufunga ndoa.Kukujibu swali lako ni kwamba ninaishi katika kiapo cha ndoa lakini si kila anayeapa kanisani ana mapenzi ya kweli na mwenzake.Hata mimi sina hakika kama kilichokuwepo wakati ule tunaapa kanisani kipo hadi leo hii.Sina hakika kama tunapendana kweli” akasema Jaji Elibarii
“ Elibariki nimekuuliza swali ambalo jibu lake ni fupi tu .Ulipaswa kunjibu ndiyo au hapana na si kutoa historia.Nataka kusikia kwa ulimi wako je unampenda mkeo? Akauliza Peniela
“ I’m not sure if I still love her” akajibu jaji Elibariki
“ Ahsante sna ,hilo ndilo jibu nillokuwa nataka kulisikia toka kwako.Naomba sasa ulale upumzike Elibariki.Ninakupenda sana
“ akasema Peniela na kumbusu .Halafu akachukua zile namba za simu za daktari alizopewa na John akaziandika katika simu yake akatoka mle chumbani na kupiga.Simu ikaita na baada ya muda ikapokelewa
“ hallow” ikasema sauti ya mwanamke upande wa pili
“ hallow.Naongea na nani” akasema Peniela
“ Unaongea na Dr Christine .Wewe ni nani mwenzangu? Akauliza Dr Christne
“ Ninaitwa Peniela ninapiga simu toka Tanzania.Dr Christine uko wapi?
“ Niko nchini Israel .Nikusaidie nini Peniela? Akauliza Dr Christne
“Nimepewa namba zako na John Mwaulaya”
“ John Mwaulaya? Akauliza Christine
“ Unamfahamu John?
“ Ndiyo ninamfahamu sana John japokuwa ni muda mrefu hatujawasiliana.Anasemaje John ?
“ John anaumwa sana kwa sasa.Ana tatizo katika mishipa ya fahamu na anahitaji msaada wa matibabu na amenitaka niwasiliane nawe nikueleze hivyo”
“ Ouh masikini John.Ninalifahamu tatizo lake kwa muda mrefu na anahitaji kufanyiwa upasuaji na nililimshauri kwa muda mrefu lakini hakuwa tayari kuusikia ushauri wangu.”
“ Dr Christine naomba umsaidie John.Kwa sasa yuko tayari kufanyiwa upasuaji.Tafadhali sana naomba umsaidie .Hali yake si nzuri hata kidogo”
“ Wewe ni nani wake?
“ Mimi ni mtoto wake.Ninaitwa Peniela”
“ Mtoto wake? John Mwaulaya hakuwahi kunitamkia kama ana mtoto “
“ Mimi ni yatima na amekuwa akinilea toka nikiwa mtoto mdogo kwa hiyo nimamuheshimu kama baba yangu.”
“ Ok vizuri kwa kuwa sasa hivi niko likizo basi nitakuwa na nafasi nzuri ya kuja kumuangalia ,nitawaomba wataalamu wengine wawili waongozane nami kuja kumshughulikia John.Lakini kuna kitu ambacho nitakihitaji ili kuweza kufanya upasuaji huo”
“ sema chochote Dr Christine” akasema Peniela
“ Ntahitaji kufanya upasuahi huo katika hospitali kubwa yenye vifaa vya kufankisha upasuaji huo kwa hiyo mwambie John kwamba aanze kufanya mipango kutafuta hospitali ambayo tutaitumia kwa upasuaji huo” akasema Dr Christine na kuagana na Peniela akamuahidi kumpigia simu mara tu atakapokamilisha taratibu za safari ya kuja Tanzania
“ Ahsante sana Mungu .Leo imekuwa ni siku nzuri sana na kila kitu kinakwenda vizuri.Kuhusu suala la hospitali hakuna shida nitaongea na Dr Joshua.Kwangu hana kauli na anawea kufanya kila jambo kwa ajili yangu.Kwa sasa nina hakika John atakuwa mzima.Bado nina mambo mengi sana ambayo ninahitaji kuyafahamu toka kwake. “ akawaza Peniela
******
Ni saa tano na nusu za usiku,Gari moja aina ya BMW lenye rangi nyeusi linawasili katika makazi ya John Mwaulaya na kufunguliwa geti.Toka ndani ya gari lile wakashuka watu wawili mwanamke na mwanaume na kisha wakaongozwa na Josh hadi katika chumba cha John mwaulaya.John mwaulaya aliyekuwa amekaa kitandani akijisomea kitabu chake uso wake ukachanua kwa tabasamu baada ya kuwaona watu wale wawili
“ hallow John” akasalimu yule mwanaume
“ Captain Amos hujambo kijana wangu?
“ Sijambo mzee vipi maendeleo yako ?
“ninamshukuru Mungu ninaendelea vizuri sana kwa sasa .” akasema John na kumtupia macho yule mwanamke alyekuwa ameambatana na Captain Amos
“ Jesica hujambo mama ? Akasema John
“ Sijambo mzee shikamoo”
“ Marahaba .karibuni sana vijana wangu.Nimefurahi sana kuwaona.Natumai mmekuja na habari nzuri zenye matumaini” akasema John mwaulaya.Captain Amos na Jesica wakavuta viti na kuketi kandoni mwa kitanda cha john
“ Mzee ni muda kidogo umepita hatujaleta ripoti yoyote lakini leo hii tumekuja na ripoti nzuri yenye kutia matumaini” akasema captain Amos
“ Operesheni inakwenda vizuri sana japokuwa kumekuwa na vizingiti vya hapa na pale.Kuna watu ambao walilifahamu jambo hili na kutaka kulivuruga.Wa kwanza alikuwa ni Dr Flora mke wa Dr Joshua .Huyu aliambiwa kinachoendelea na mume wake na akataka kuwaeleza mabinti zake lakini rais alilifahamu hilo na akaamuru tumuwahi kabla hajawaeleze wanae kitu kinachoendelea.Dr Flora tulimuondoa lakini kikaibuka tena kikwazo kingine,kuna mtu alifanya uchunguzi wa nini kilichomuaa Dr Flora na kugundua kwamba alichomwa sindano ya sumu.Huyu ni jaji wa mahakama kuu na amemuoa mtoto mkubwa wa rais.Rais aliogopa kwamba jaji Elibariki anaweza kuwa hatari na akaamuru tumuue lakini nilimpa maelekezo Jessica ahakikishe kwa namna yoyote ile jaji Elibariki hauawi kwani ni mtu muhimu sana kwetu na tunaweza tukamtumia.Jesica alilifanikisha hilo na kufanikiwa kumuokoa Elibariki.Labda kwa kukufahamisha tu ni kwamba huyu ndiye jaji ambaye alimuachia huru Peniela”
“ Good Job Jessica.Ulifanya vizuri sana kutomuua.Huyu jaji anaweza akawa ni msaada mkubwa sana kwetu.Yukowapi sasa hivi?
“ Nilipomuokoa nilimtaka anieleze sehemu ipi anadhani inaweza kuwa salama sana kwake kujificha na moja kwa moja akachagua kwa Peniela.Kwa hivi sasa yuko kwa Peniela”
“ Peniela?! John mwaulaya akastuka
“ Ndiyo yuko kwa peniela.Inavyoonekana kuna kitu kinaendelea kati yao na ndiyo maana Elibariki akachagua kwenda kujificha pale”
“ Mna hakika kwa Peniela ni sehemu salama ambayo Elibariki hatagundulika? Kwa sasa vyombo vya usalama vitakuwa vikimtafuta katika kila kona je itakuwaje iwapo atagundulika yuko pale? Sitaki Peniela apatwe na tatizo lolote”
“ Usiogope mzee suala hili liko ndani ya uwezo wetu na endapo kutatokea jambo lolote lile la kuhatarisha usalam a Peniela basi tutalishughulikia” akasema Captain Amos
“ Ok good,operesheni 26B inakwendaje?
“ Operesheni inakwenda vizuri.Jioni ya leo rais ametuita mimi na Dr Kigomba na kutueleza kwamba kwa kuwa kumeanza kujitokeza vikwazo kadhaa katika biashara ile kwa hiyo ameamua kwamba biashara ifanyike haraka sana .Amesema ataongea na wale wanunuzi ili wajiandae na baada ya wiki mbili wawe tayari mchakato wa mauziano uanze.Hii ni fursa yetu ya kuikamilisha operesheni yetu.”
“ Good Job Amos.Mmefanya kazi nzuri sana.Mpaka sasa hvi hakuna wasiwasi wowote kwamba wewe na Jessica ni sehemu ya team SC41? Hawajawatilia shaka yoyote? Akauliza John
“Dr Joshua tayari ameanza kuwa na hisia kwamba kuna mtu anayetoa habari.Tukio la kunusurika kwa jaji Elibariki limempa wasiwasi sana na anahisi kwamba huenda vijana tunaowapa kazi kuna mmoja wao atakuwa amevujisha siri kwa Elibariki na kumfanya atoroke.Ameamuru uchunguzi ufanyike lakini hakuna watakachoweza kukifahamu kwa hiyo usitie shaka kuhusu jambo hilo.Hawataweza kamwe kugundua chochote kuhusu sisi “
“ Ok vizuri sana Cap[tai Amos kwa hiyo nini kinafuata i?
“ Kuna kitu ambacho tunatakiwa tukifanye” akasema Captain Amos.Akamtazama John kisha akaendelea
“ Ni Dr Joshua pekee ambaye anafahamu mahala mzigo ule ulipo . Atauchukua mzigo ule halafu atamkabidhi Dr Kigomba ambaye atauficha na yeye ndiye atakayefanya makabidhiano yote na wanunuzi.Kitu ambachotunatakiw a kukifanya kwa sasa Peniala anatakiwa aanzishe mahusiano ya haraka sana na Dr Kigomba”
“ Again?! Mahusiano mengine tena? Akauliza John
“ John ili tuweze kufanikisha operesheni hii tunamuhitaji sana Peniela.Bila yeye hatuwezi kuimaliza operesheni hii.Please I beg you John.Najua unampeda sana Peniela lakini katika hili hakuna namna tunavyoweza kufanikiwa bila ya Peniela.” Akasema Captain Amos.John akafumba macho akawaza na kusema
“ ok hatuna namna nyingine ya kufanya .Itabidi afanye hivyo” akasema John
TUKUTANE SEHEMU IJAYO……
No comments
Post a Comment