SIMULIZI: PENIELA (Season 2 Ep 17)

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

“ Ok vizuri sana Captain Amos kwa hiyo nini kinafuata i?


“ Kuna kitu ambacho tunatakiwa tukifanye” akasema Captain Amos.Akamtazama John kisha akaendelea

“ Ni Dr Joshua pekee ambaye anafahamu mahala mzigo ule ulipo . Atauchukua mzigo ule halafu atamkabidhi Dr Kigomba ambaye atauficha na yeye ndiye atakayefanya makabidhiano yote na wanunuzi.Kitu ambachotunatakiw a kukifanya kwa sasa Peniala anatakiwa aanzishe mahusiano ya haraka sana na Dr Kigomba”


“ Again?! Mahusiano mengine tena? Akauliza John


“ John ili tuweze kufanikisha operesheni hii tunamuhitaji sana Peniela.Bila yeye hatuwezi kuimaliza operesheni hii.Please I beg you John.Najua unampeda sana Peniela lakini katika hili hakuna namna tunavyoweza kufanikiwa bila ya Peniela.” Akasema Captain Amos.John akafumba macho akawaza na kusema

“ ok hatuna namna nyingine ya kufanya .Itabidi afanye hivyo” akasema John


ENDELEA…………………


Baada ya Captain Amos na Jessica kuondoka John Mwaulaya alibaki katika mawazo mengi sana.Suala la kutakiwa kumruhusu Peniela aingie katika mahusiano mengine na katibu wa rais Dr Kigomba lilimchanganya sana akili yake.


“ Amos amenichanganya sana kwa kutaka Peniela aingie katika mahusiano mengine tena na Dr Kigomba .Kwa sasa Peniela amekuwa ni kama chombo cha starehe ,mwiliwake umekuwa ukitumika kama silaha ya kufanikisha mipango ya Team SC41.Ninaumia sana kwa kumfanya Peniela namna hii.” Akawaza John

“ Lakini kwa hapa tulipofikia tuko mwishoni mwa operesheni yetu na hakuna namna nyingine ya kufanya zaidi ya kukubali Peniela aingie katika mahusiano mengine na Dr Kigomba.Ninaumia sana lakini sina namna nyingine.Nitahakikisha baada ya operesheni hii kumalizika ninamfanyia Peniela mambo makubwa kulipia yale mambo ambayo nimemfanyia.Nitayatengeneza upya maisha yake.Nitamfanya awe ni mwenye furaha na hata kama nikifa basi niwe nimuacha Peniela ni mwenye amani na anayafurahia maisha yake tofauti na sasa ambapo amekuwa ni kama chombo kinachotumika ili kuwastarehesha watu na kufanikisha mipango ya Team SC41.Lazima nimuondoe katika kundi hili pindi tu operesheni hii itakapokamilika.” Akawaza John halafu akabonyeza kitufe cheusi kilichokuwa chini ya kitanda chake na Josh mlinzi wake akaingia.


“ Josh naomba uwasiliane na Peniela na mwambie kwamba ninahitaji kumuona kesho saa tatu za subuhi “ akasema John na kumpatia Josh namba za simu za Peniela na bila kupoteza wakati Josh akampigia simu .

Peniela akiwa kitandani na jaji Elibariki mara simu yake ikaita akainuka na kwenda kuipokea.Namba zlizoonekana katika kioo cha simu zilikuwa ngeni kabisa katika simu yake


“ hallow” akasema penny


“ hallow peniela,ni Josh hapa ninaongea kutoka kwa John Mwaulaya”


“ Ouh Josh,habari yako? Kuna nini hadi ukanipigia usiku huu?


“ Nimeelekezwa na John nikwambie kwamba anahitaj kukuona kesho saa tatu asubuhi hapa nyumbani kwake”

“ Ok ahsante sana kwa taarifa nitafika muda huo.Hali yake inaendeleaje?

“ Hali yake inaendelea vizuri “ akajibu Josh na kukata simu .


*******


Kumekucha tena Tanzania na habari kubwa magazetin i bado ilikuwa ni ya kupotea kwa jaji Elibariki .Peniela kama kawaida yake aliamka asubuhi na mapema akafanya mazoezi halafu akafanya usafi wa nyumba na kumuandalia jaji Elibariki kifungua kinywa.


“ Najisikia furaha sana kuamka asubuhi na kumuandalia Elibariki kifungua kinywa.Natamani kama maisha yangu yangekuwa namna hii ningefurahi sana.Hata hivyo nina tumaini siku moja na mimi nitaishi maisha ya kawaida kama wenzangu.Nitaamka asubuhi na kumuandalia kifungua kinywa mume wangu na kama Mungu akinijalia nitakuwa na watoto wawili .Hayo ndiyo maisha ambayo nimekuwa nikiota kuyaishi kwa miaka mingi kabla ya kuingia katika kundi hili la Team SC41.” Akawaza Peniela wakati akiendelea na kuandaa mlo wa asubuhi. Alipomaliza akamfuata jaji Elibariki chumbani akiwa amebeba sinia llilosheheni mlo wa asubuhi.


“ Wake up Elibariki.Its a new day “ akasema Peniela akiwa na uso uliopambwa na tabasamu zito.jaji Elibariki akatabasamu

“Ahsante sana Peniela kwa kunijali.Sijawahi kujaliwa kama unavyonijali.”

“ Usijali Elibariki.Unastahili kupewa kila aina ya huduma.Amka upate kifungua kinywa” akasema peniela .


“ Nashukuru sana Peniela” akasema jaji Elibariki na Peniela akamuandalia kifungua kinywa pale pale kitandani.

Kisha pata kifungua kinywa jaji Elibariki akaingia bafuni kwa ajili ya kujimwagia maji,alihisi joto.Wakati akiendelea kuoga Peniela akaingia na wakaoga pamoja .Kisha oga Peniela akajindaa kwa ajili ya kuelekea kwa John Mwaulaya.

“ Elibariki nitakuacha tena kwa siku ya leo kwa masaa machache kuna mahala nitaelekea lakini sintakawia sana.Kuna mtu ambaye ninahitaji kumuona “ akasema Peniela


“ usihofu Peniela.Unaweza ukaendelea na shughuli zako wala usiwe na wasi wasiwowote na mimi.”


“ Nashukuru sana Elibariki kwa kunielewa .Nitakapotoka huko nitapita kununua mahitaji kwa ajili yetu.” Akasema Peniela na simuyake ikaita akataarifiwa kwamba dereva atakayemchukua kumpeleka kwa John Mwaulaya tayari amekwisha wasili.Peniela akamsogelea Elibariki akambusu na kutoka mle chumbani

“ Dah ! Peniela ameniteka akili yangu yote.Ni mwanamke mrembo sijapata kuona na mambo anayonifanyia yanazidi kunipagawisha na kunifanya nisitake hata kuondoka hapa kwake.Nitafanya nini ili niweze kuwa na huyu msichana? Nina hakika huyu ndiye mwanamke ambaye ninatakiwa kuwa naye maishani.Ana kila kitu ninachokihitajikwa mwanamke ninayemuhitaji katika maisha yangu.Peniela yuko tofauti sana na Flaviana na wanawake wengine.Pamoja na uzuri wake lakini hana dharau,ana adabu na anajali kupita kiasi,anajua kuliwaza na hata mapenzi mamboyale ya kitandani amebobea vilivyo..Flaviana hajawahi kunifanya mambo kama haya anayonifanyia Peniela .” akawaza jaji Elibariki akiwa dirishani akichungulia nje kulikokuwa na bustani nzuri .


“ laiti kama ningeweza kuitengua ndoa yangu ili niweze kuishi na peniela ningefurah I sana.lazima nikubaliane na ukweli kwamba ndoa yangu kwa sasa inapumulia mashine.Ndoa yangu haina uhai mrefu.Hilo ni jambo ambalo siwezi kupingana nalo.Ni wakati sasa wa kuchukua maamuzi magumu kwa ajiliya kuitafuta furaha ya maisha yangu.Lazima nifanye kila linalowekana ili niweze kuwa na Peniela.Najua ni suala lenye changamoto nyingi lakini nitakabiliana nazo tu.Siwezi kuendelea kuishi maisha ya maigizo ,tukiigza kwamba tunapendana na ndoa yetu ina fuaha na amani wakati ukweli ni kwamba mapenzi hakuna katika ndoa yetu tofautina watu wanavyofikiri.Lazima nifanye maamuzi.Lazima nifanye kila linalowezekana niachane na Flaviana.Ninahitaji mwanamke ambaye atanipenda na kunijali kama anavyonijali peniela.Nahitaji mwanamke ambaye atakuwa tayari kunizalia mtoto.Umri unazidi kwenda na Flaviana mpaka leo haonyeshi dalili zozote za kutaka kunizalia mtoto.Nimechoshwa na maisha haya.” Akawaza jaji Elibariki.


“ japokuwa ninampenda Peniela na nina hakika moyovvvh wangu umemkubali lakini bado ninahitaji sana kumfahamu vizuri.Nahitaji kujua anakwendaga wapi kila siku? Anakwenda kuonana na nani? Halafu mbona kuna baadhi ya simu akipigiwa huwa hataki kuongelea mbele yangu? Kuna kitu gani anakificha? Jioniya leo lazima nitamuuliza kuhusiana na mambo haya.Mimi nimekuwa huru kumueleza kila kilichomo moyoni mwangu lakini kuna vitu ambavyo amekuwa akinificha ficha.Lazima nimuulize jioni ya leo ili nimfahamu kwa sababu muda si mrefu nitafanya maamuzi magumu kwa sababu yake.” akawaza jaji Elibariki na picha za shambulio lile ikamjia kichwani


“ Natamani sana kufahamu kinachoendelea huko nje.Natamani sana kufahamu kama watu waliofanya shambulio lile wamekamatwa au bado.Natamani kuwasiliana na watu wangu wa karibu lakini siwezi kufanya hivyo.Yule mwanamke aliyeniokoa alinikataza kuwasha simu yangu kwa sababu za kiusalama.Lakini nitaishi hivi hadi lini? Nitaendelea kukaa humu ndani hadi lini? Lazima juhudi zifanyike ili kulimaliza suala hili na mimi niweze kuwa huru.Suala hili litamalizwa kwa kuwapata watu waliofanya jambo hili na mtu pekee anayeweza kufanya kazi hii ni Mathew.Nitawasiliana naye jioni ya leo ili niweze kufahamu maendelo yake na kama Noah amekwisha zikwa ama bado.” Akawaza jaji Elibariki


*******


Peniela aliwasili katik a makazi ya John Mwaulaya na kupokelewa na Josh na kisha akamuongoza hadi ghorofani chumbani kwa John .


“ karibu tena Peniela.Nimefurahi sana kukuona tena” akasema John

“ Ninashukuru john ,hata mimi nimefurahi kupata nafasi ya kukuona tena baba yangu.Mungu ni mkubwa kwa sababu kila siku afya yako inazidi kuboreka na uso wako unaonyesha nuru “ akasema Peniela na kukaa katika kitanda cha John


“ unajisikiaje leo? Akauliza Peniela

“Ninajisikia vizuri sanaPeniela.maendeleo yangu si mabaya.Ninaanza kupata nguvu kidogo kidogo. Kwa leo ninaweza hata kunyanyua mguu “ akasema John Mwaulaya


“ Nafurahi sana kusikia hivyo .Hizo ni habari nzuri za kutia matumaini,halafu baba sijamuona Osmund kuanzia jana na nikashangaa nilipopigiwa simu na Josh jana usiku badala ya Osmund.Ossy Amesafiri? akauliza Peniela.John akamtazama Peniela kwa makini usoni na kumwambia


“ Osmund hayuko tena na sisi.He’s dead”

“ Ouh jamani.Nini kimemuua?! Peniela akastuka sana

“ Osmund alifanya makosa makubwa sana ambayo yameigharimu Team SC41 kwa hiyo ilimlazimu kuondolewa kwani hakufaa katika uongozi.”


“ This is weird John.Is this how team SC41 works? Mtu akikosea anauliwa? Akauliza Peniela


“ Hapana si hivyo Peniela lakini kuna sababu nyingine ambayo ilipelekea pia auawe”


“Ni sababu gani hiyo? Na yule daktari aliyesema anakuja kukuangalia Dr Burke yuko wapi? Haji tena? Akauliza Peniela


“ Dr Burke naye hatuko naye.Naye amefariki pia”


“ John whats going on? Kwa nini watu wawili wote wamekufa kwa wakati mmoja? Kuna kitu gani hapa?


“ Peniela siwezi kukuficha kitu ukweli ni kwamba Dr Burke alikuwa anakuja kwa lengo la kunai kuniua na si kuja kuchunguza afya yangu.?


“ kukuua? Peniela akashangaa


“ Kukuua kwa kosa lipi ?


“ Peniela naomba tuachane na mambo hayo yana historia ndefu.Vipi wewe maendeleo yako? Unaendeleaje? Maisha yako yanaendeleaje?

“ Mimi ninaendelea vizuri sana na maisha yangu pia yanaendelea vizuri.Hofu kubwa iko kwako.Lakini hata hivyo nimekuja na habari njema .Jana nimeongea na Dr Christine kumbe anakufahamu sana na tatizo lako analifahamu pia.Anasema kwamba siku nyingi amekuwa tayari kukufanyia upasuaji lakini wewe hukuwa tayari hata hivyo baada ya kumueleza hali yake amesema kwamba anajiandaa kwa safariya kuja Tanzania yeye na wataalamu wenzake watatu kwa ajili ya kuja kukufanyia upasuaji.Hata hivyo kitu ameombakifanyike kabla hajafika”

“Nashukuru sana Peniela.Ni kweli mmi na Dr Christine tunafahamiana kwa miaka mingi na ni kweli alikuwa tayari kunifanyia upasuaji lakini mimi sikuwa tayari kwa sababu sikuwa na tumaini la kupona.Kwa sasa ninataka niendelee kuishi kwa sababu yako.Ameomba kitu gani kifanyike?

“ Anataka tutafute hospitali ambako uasuaji huo utafanyika.Anasema kwamba anahitaji hospitali kubwa ambayo itakuwa na vifaa vya kumuwezesha kuufanya upasuaji huo.”

“ Mhh ! kitu anachokiomba ni kigumu sana na hakiwezekani. Wewe ulimjibu nini? Akauliza John


“ Relax father.Jambo hili liko ndani ya uwezo wangu na nitalishughulikia.Tutapata hospitali nzuri na yenye vifa anavyovihitaji Dr Christine.Nitafanya kila niwezalo hadi nihakikishe kwamba umekuwa mzima tena”akasema Peniela na kuufanya uso wa John ujenge tabasamu.

“ Ninashukuru sana Peniela.Bado naendelea kusisitiza kwamba nina deni kubwa kwako.Nina kazi kubwa ya kufanya kuyajenga upya maisha yako.Sitaki uendelee kuishi maisha ya namna hii.Nitayafanya maisha yako yawe mazuri sana yenye furaha na amani tofauti na maisha unayoishi sasa hivi” akasema John.

“ Ahsante sana John” akasema Peniela na baada ya muda John akasema


“ Peniela nimekuita kuna jambo ambalo nataka nikufahamishe.Ni kuhusu operesheni 26 B” akasema John akatulia na kumtazama Peniela kwa muda halafu akasema

“ Mambo yamebadilika kidogo katika operesheni ile na inaweza ikawa na urahisi kwetu tofauti na tulivyokuwa tumetegemea.Jana Captain Amos na Jessica wamekuja kuniona na kunipa taarifa nzuri za maendeleo ya operesheni yetu.Ni kwamba rais Dr Joshua tayari ameamua kufanya kuuza ule mzigo kwa kwa haraka zaidi baada ya kuingiwa na wasi wais kutokana na vikwazo ambavyo vimeanza kujitokeza.Usiku wa jana alikuwa na kikao na Captain Amos pamoja na katibu wake Dr Kigomba na kukubaliana kwamba ndani ya mwezi huu biashara ifanyike.Ana wasi wasi kuna watu tayari wamekwsha fahamu kinachoendelea.Ni Dr Joshua pekee anayefahamu mahala mzigo ulikofichwa ndani ya ikulu kwa maana hiyo basi atauchukua mzigo ule na kumkabidhi Dr Kigomba ambaye ndiye atakayefanya makabidhiano yote na wanunuzi kwa niabaya rais.Kwa hiyo basi kuna jambo ambalo lazima tulifanye japokuwa ni gumu na japokuwa siafikiani nalo lakini lazima lifanyike ili tuweze kuikamilisha operesheni hii.” Akasema John na kumtazama Peniela

“Hizo ni habari njema sana.Ni afadhali operesheni hii ikafikia ukingoni.Nina hamu sana ya kutaka kuishi maisa mapya.Ni jambo gani hilo ambalo ni lazima tulifanye ambalo huafikiani nalo?


“Peniela ,unatakiwa uinge katika mahusiano na Dr Kigomba “ akasema John na kimya kikatanda mle chumbani wakabaki wakitazamana.Baada ya muda John akasema

“ Peniela sikuwa tayari kwa wewe uingie tena katika mahusiano mengine lakini hatuna namna nyingine ya kufanya ili tuweze kuupata mzigoni zaidi ya kuingia katika mshusiano na Dr Kigomba. Inaniuma sana Peniela.Ninaumia sana kuyafanya maisha yako yawe namna hii na ndiyo maana nikasema kwamba nina deni kubwa kwako la kuhakikisha kwamba ninayatengeneza upya maisha yako ambayo ni mimi ndiye niliyaharibu.Ni mimi ndiye niliyepoteza ndoto zako zote za maisha kwa kukuingiza katika Team SC41.” Akasema John kwa uchungu.Peniela akamtazama halafu akasema


“ Usisikitike sana nitafanya hivyo.Ninatamani sana hata jambo hili limalizike leo ili na mimi nianze maisha yangu mengine kama ulivyoniahidi.Nitaingia katika mahusiano na Dr Kigomba kwa kusudi moja tu la kukamilisha operesheni hii.Nitaomba kabla ya kukutana naye nipatiwe taarifa zake na kisha a Amos atengeneze tukio ambalo ,litanikutanisha na Dr Kigomba.”


“ Peniela ahsante sana kwa kulikubali hilo.Narudia tena kukuahidi kwamba baada ya kumalizika kwa operesheni hii basi utakuwa ni mwisho wako ndani ya Team SC41.Naomba uniamini “

“ Ninakuamini John.Ninakuamini baba yangu lakini naomba iwe kama hivyo unavyoniahidi”


“ Usijali Peniela.Kila kitu kitakwenda kama nilivyokuahida.Ila unatakiwa uwe makini sana .Simfahamu Kigomba lakini nasikia ni mtu hatari ,unatakwa uwe naye makini.Kwake kutoa roho ya mtu ni kitu cha sekunde moja tu” akasema John

“ Usijali mzee,kama niliweza kumuingia rais ,siwezi kushindwa kwa Kigomba.Nitafanya kazi nzuri na tutaimaliza operesheni hii .”

“ Nashukru sana Peniela.”

“ Usijali baba.Wasiliana na Amos na umtaarifu kwamba nimekubali na nitaingia katika mahusiano na Kigomba na aanze kufanya mipango ya kunikutanisha naye tu na mimi nitamaliza kila kitu.Kwa sasa naomba niondoke ninakwenda kuanza kushughulikia suala la kupata ile hospitali kwa ajili ya operesheni yako” akasema Peniela huku akichukua mkoba wake


“ Peniela kabla hujandoka kuna jambo nataka kukuuliza”

“ Ni jambo gani?Uliza usiogope”

“ Ni kuhusu jaji Elibariki.Nimeambiwa kwamba yuko kwako”

Peniela akastushwa sana na taarifa zile na kushindwa ajibu nini


“ Usiogope Peniela sijakuuliza kwa ubaya.Kuna kitu ambacho nataka ukifahamu ni kwa nini Elibariki alitaka kuuawa na nani aliyetaka kumuua.” Akasema John

“ Unawafahamu waliotaka kumuua? Akauliza Peniela


“ Ndiyo ni Dr Joshua .”


“Dr Joshua? ! Peniela akashangaa.


“ Dr Joshua alimuua mke wake baada ya kutaka kuvujisha siri za kuhusiana na biashara anayotaka kuifanya.Jaji Elibariki akishirikiana na wenzake walifanya uchunguzi na kugundua kwamba Dr Flora alichomwa sindano yenye sumu.Baada ya kugundua kwamba siri ya kilichomuua m,ke wa rais imevuja, Dr Joshua akaamuru Elibariki auawe haraka na ndiyo maana shambulio lile likapangwa.Kwa msaada wa captain Amos Elibariki akaokolewa na Jessica ambaye naye yupo katika mtandao wetu na ndipo alipoamua kuja kujificha kwako.” Akasema John .Peniela bado aliendelea kumtumbulia macho hakuwa na cha kuongea


“ Kwa sasa kuna juhudi kubwa za kumtafuta Elibariki yuko wapi na ndiyo maana nikawa na wasi wasi kidogo endapo itagundulika kwamba yuko kwako inaweza ikakuletea matatizo na kuharibu mipango yetu” akasema John na Peniela akajibu


“ Ni kweli niko na Elibariki na sikuwa nimekueleza kuhusiana na jambo hili kwa sababu sikutaka mtu yeyete afahamu na nimestuka sana baada ya kusikia kwamba tayari unafahamu jambo hili.Ukweli ni kwamba nilipigiwa simu na msichana mmoja nadhani ndiyo huyo Jesica akanitaka nikamchukue Elibariki sehemu fulani alikonielekza.Nilimkuta akiwa amejeruhiwa na alinieleza mkasa mzima namna tukio zima lilivyotokea nikamuonea huruma sana.Alihitaji sehemu ya kwenda kujificha hivyo na aliamini kwangu atakuwa salama hivyo nikaondoka naye na kwenda kumhifadhi nyumbani kwangu na mpaka sasa ninaishi naye pale kwangu.Usihofu chochote hakuna anayeweza kufahamu kama Elibariki yuko pale kwangu.Ni sehemu salama sana kwake kwa sasa.Alinisaidia sana katika kesi yangu na mimi lazima nimsaidie.”akasema Peniela


“ Peniela umefanya jambo zuri kukubali kumsaidia jaji Elibariki Lakini kuna jambo moja ambalo nahitaji kulisikia toka kwako.Do you love him? Akauliza John na Peniela akabiki anamuangalia.Alistukizwa swali ambalo lilimpa ugumu kidogo kujibu

“ usiogope kunijbu Peniela.Mimi ni mtu ambaye hutakiwi kunificha jambo na zaidi ya yote nina maana yangu kukuuliza hivyo” akasema John.Peniela akatafakari na kusema


“ yes I do love him.Lakini tayari ana mke wake”

“ How do you feel around him? Are you happy? Akaulzia John 


“ I feel more than happy around him.”

“ Kama angekuwa hana mke unadhani anasifa za mwanaume ambaye umekuwa ukimuota awe mume wako? Akaulzia John.Peniela akatabasamu na kusema


“ Endapo angekuwa hana mke basi Elibariki ni mtu ambaye ana kila sifa ya mwanaume ninayemuhitaji katika maisha yangu.Ana vigezo vyote vya kuwa mume mzuri”

“ Ahsante nashukuru sana kwa kuwa muwazi kwangu..”

“kwa nini umeniuliza hivyo? Akauliza Peniela


“ Nilihitaji tu kuufahamu ukweli wako.Na kwa kuwa hujanificha kitu sasa unaweza kwenda kuendelea na shughuli zako nitawasiliana nawe baada ya kuongea na captain Amos” akasema John na kisha Peniela akatoka mle ndani akaingia garini na kuondoka


“ Sasa nimepata jibu nililokuwa nalitafuta .Kumbe ni Dr Joshua ndiye aliyemuua mke wake na ndiye aliyetoa amri ya kuuawa kwa Elibariki.Namshukuru sana Captain Amos kwa kumuokoa Elibariki.Sasa nimeamini Team SC41 ni mtandao uliokita mizizi yake hadi ikulu.Sikuwa nikimfahamu yule mwanamke Jessica kama naye ni mmojawapo wa Team SC41..” Akawaza Peniela wakati akitoka chumbani kwa John na kuingia garini akamuamuru yule dereva ampeleke mjini kwa ajili ya kufanya manunuzi aliyoyahitaji.Akiwa ndani ya gari akachukua simu ambayo huitumia kuwasiliana na Dr Joshua na kumpigia

“ Hallow Peniela.Habari yako malaika wangu” akasema Dr Joshua

“ Habari nzuri Dr Joshua.Unaendeleaje?”


“ Ninaendelea vizuri sana.Usiku mzima wa jana nilikuwa nakuota wewe tu.Unasemaje malkia wangu ? si kawaida yako kunipigia muda kama huu” akasema Dr Joshua na kumfanya Peniela atabasamu


“ Dr Joshua nimekupigia ili kukuomba kama utapata nafasi nionane nawe leo jioni katika ile nyumba mpya.Nina hamu sana ya kukuona.Nimekukumbuka sana .Unaweza kupata nafasi ? akauliza peniela


“ Kwa leo nina kazi nyingi muhimu lakini kwa ajili yako nitafanya kila niwezalo kupata muda ili nije nionane nawe.Hata mimi ninakuwaza sana Peniela.”

“ Nashukuru sana Dr Joshua.Nitakuwepo pale nyumbani kuanzia saa mbili za usiku wa leo.” Akasema Peniela na kukata simu.


“ Nina imani atakuja tu.Hana kauli juu yangu .Nimemteka akili yake yote haambiwi lolote ju yangu .Angejua ninavyomchukia yule mzee..Siku nikiachana naye sijui nitaoga na sabuni gani ili kuondoa shombo yake.Simpendi sana” akawaza Peniela akiwa garini kuelekea supermarket kufanya manunuzi ya vitu mbali mbali vya ndani


********


Saa sita za mchana gari nne nyeusi ziliwasili katika makaburi ya mkwajuni. Mojawapo ya gari hizo lilikuwa limebeba jeneza lenye rangi nyeupe.Magari yalisimama na watu wakashuka.Wanaume sita wakalitoa jeneza lile ndani ya gari na kulibeba hadi katika kaburi liilokwisha andaliwa. Wakaliweka pembeni katika meza na watu wale wasiozidi ishirini wakalizunguka kaburi lile.Wote walikuwa wamevaa mavazi meusi .Mchungaji aliyekuwa ameongozana na watu wale akaanzisha ibada fupi kabla ya mazishi.Haya yalikuwa ni mazishi ya Noah .Familia yake ilisafiri kutoka jijini Harare na kuja kumzika jijini dare s salaam .

Mchungaji aliongoza ibada fupi na kutoa maneno machache ya kuwakumbusha waombolezaji kuhusiana na kujiweka tayari saa yoyote kwani kifo hakina hodi.Baada ya ibada ile fupi kilifuata kipindi cha kila mmoja aliyekuwapo pale makaburini kutoa maneno machache ya namna alivyomfahamu Noah.Alianza baba yake ,halafu kaka yake.Mama yake alishindwa kabisa kuongea chochote kutokana na huzuni kubwa aliyokuwa nayo.Zamu ya dada yake naye alishindwa kuongea chochote.Mathew aliongea kwa niaba ya marafiki wa Noah.Alikuwa amesimama akimtegemeza Anitha ambaye hakuwa na nguvu Baada ya hapo jeneza likashuswa kaburini na mafundi wakaanza mara moja kazi ya kulifunika.Kaburli lilipofunikwa watu wakaingia katika magari yao na kuondoka.Safari ya maisha ya Noah ikaishia hapo.Ilikuwa ni siku ngumu sana kwa Mathew na Anitha ambao walikuwa ni watu wa karibu sana wa Noah.

Toka makaburini wakaelekea moja kwa moja katika hoteli walikofikia familia ya Noah kulikokuwa kumeandaliwa chakula na baada ya kula wakaendelea kukaa na wafiwa wakiwafariji .Saa kumi na mbili za jioni Mathew ,Anitha na Jason ambayealikuwa nao katika kipindi chote cha msiba wa Noah wakawaaga wafiwa wakaondoka na kurejea nyumbani.



“ Ni vigumu sana kuamini kama sintamuona tena Noah maishani.Inauma sana” akasema Anitha akiwa amekaa sofani baada ya kufika nyumbani kwa Mathew


“ Anitha kifo tumeumbiwa sisi wanadamu na hakizoeleki.Ni vigumu kuelezea uchungu nilionao kwa kifo cha Noah lakini pamoja na hayo lazima tukubaliane kwamba Noah is gone and we’ll never see him again.Life goes on and we have to move on too.Kwa sasa nguvu yetu kubwa tunatakiwa tuielekeze kwa Elibariki ili kuhakikisha usalama wake” akasema Mathew

“ Elibariki sijui yuko wapi .Mpaka sasa juhudi za kumtafuta zinaendelea lakini hajapatikana.Nina wasi wasi atakuwa alitekwa nyara na watu waliofanya shambulizi lile” akasema Jason amabey naye alikuwapo pale sebuleni

“ Elibariki yupo hai na yuko salama’ akasema Mathew

“Yuko salama? Mnafahamu mahala aliko? akaulzia Jason


“ ndiyo yuko sehemu salama .Baada ya kuokoka katika shambulio lile amekwenda kujificha kwa peniela”akasema Mathew akiamini Jason na Elibariki ni marafiki wakubwa.Hakuwa na taarifa za kilichotokea kati yao.

“ Peniela?! Jason akastuka sana.

“ Elibariki yuko kwa Peniela? akauliza

“ Ndiyo .Amekwenda kujificha kwa Penela. Kuna tatizo lolote? Akauliza Mathew baada ya kugundua Jason alistuka sana baada ya kusikia Elibariki yuko kwa Peniela.

“ Hakuna tatizo lolote Mathew .” akasema Jason na kuomba kuondoka .

“ Elibariki yuko kwa Peniela ! akawaza Jason akiwa garini.

“ Nilitegemea baada ya kipigo cha siku ile basi asingerejea tena kwa Peniela lakini bado hajakoma na amerejea tena.Huyu jamaa ana mke wake kwa nini anaingilia mali za watu? Peniela ni mpenzi wangu mimi na sintokubali Elibariki anipindue na siwezi kukubali aendelee kukaa pale kwa Penny.Siwezi kukubali aendelee kukaa na mwanamke ambaye nimemuhangaikia mpaka nikamuweka huru.Ninampenda Peniela na kwa ajili yake niko tayari kwa lolote.Nikizubaa ninaweza kunyang’anywa mtu wangu hivi hivi nikiona.Lazima nipambane na Elibariki.lazima nimtoe kwa Peniela na asikanyage tena pale.Najua atakuwa amemdanganya Peniela kwamba yeye ndiye aliyemuachia huru.Mimi ndiye niliyefanikisha hadi peniela akaachiwa huru.Bila mimi kusimama imara na kutoa ushahidi wenye nguvu asingepata nguvu ya kumuachia huru peniela.Nilipambana kufa na kupona kwa sababu ninampenda Peniela.Vita hii na Elibariki haitakwisha na lazima nimuonyeshe kwamba sisi ndio watoto wa mji huu” Akawaza Jason


JASON ANATAKA KUFANYA NINI ? TUKUTANE SEHEMU IJAYO……………..

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...