SIMULIZI : PENIELA (Season 2 Ep 9)
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Niambie haraka sana ninyi ni akina na nini kazi zenu?
“ Sisi kazi zetu ni wizi wa magari.Huwa tunaiba magari ndani na nje ya nchi.Vile vile huwa tunafanya shughuli za ujambazi ,kuvamia mabenki na kupora fedha n.k Hizo ndizo shughuli zetu” akasema yule jamaa na kuuma meno kwa maumivu makali .Bado alikuwa amefungwa miguu na mikono katika kitanda.
“ Kwa nini mnamfutilia Eva? Nani kawatuma mumfuatilie Eva? Akauliza
“ Sisi hatumjui Eva na wala hatujawahi kumuona”
‘ Kama hamumjui kwa nini mnamfuatilia? Akauliza Mathew
“ ouh kaka ninaumia sana.Naomba unifungue walau mikono .Ninasikia maumivu makali sana.Nitakueleza kila kitu unachokitaka naomba uniamini”akasema yule jamaa.Mathew akamtazama na kuamua kumfungua
“ Ukweli wako ndio utakaokuweka hai.Niambie ukweli mtupu.Kwa nini mnamfuatilia Eva ” akasema Mathew
“ Nitakueleza kila kitu ila naomba usiniue” akasema yule jamaa baada ya kufunguliwa mikono
ENDELEA……………………………
Yule jamaa bado alikuwa katika maumivu makali na damu iliendela kumtoka sehemu ile ambayo Mathew alimtoboa na kile kifaa cha kutobolea
“ Sisi hatukuwa tukimfahamu Eva hadi wiki hii.” Akasema Yule jamaa na kuuma meno kwa maumivu makali aliyokuwa akiyasikia
“ Ilikuwaje mkafahamu Eva na kuanza kumfuatilia? Hicho ndicho kitu ambacho nahitaji kukifahamu” akasema Mathew kwa ukali
“ Ni jambo lenye mlolongo mrefu kidogo lakini nitakuweleza ila ahhgggh ! ..yule jamaa akashindwa kuendelea akagugumia kwa maumivu makali sana.Akajikaza na kusema
“Kuna mzee mmoja anaitwa mzee Kitwana.Yeye ni mzee maarufu sana hapa mjini na ni mtu mwenye uwezo mkubwa kifedha.Ana magari mengi tu ya kubeba mizigo pamoja na biashara nyinginezo nyingi.Huyu ndiye aliyekuwa mfadhili wetu mkuu wa kazi zetu.Mzee Kitwana alikuwa na mtandao mkubwa wa watu na alikuwa akipata taarifa nyingi kwa hiyo kila alipokuwa akipata taarifa Fulani kuhusiana na fedha mahala Fulani basi huwa anatutafuta na kutupa kazi hiyo ya kwenda kuvamia na kuiba.Siku moja alitufuata na kutuambia kwamba kuna kazi ambayo anataka kutupa na yenye pesa nyingi mno tofauti na ujambazi.Alisema kwamba kuna kitu Fulani kinatakiwa na watu wa kutoka nje ya nchi lakini hakututajia ni kitu gani hicho na ni akina nani hao ambao walikuwa wakikitafuta hicho kitu.” Akanyamaza akafumba macho kidogo na kusema
“ Tafadhali kaka naomba unisaidie kuzuia damu hii isiendele kutoka Nitakufa” akasema Yule jamaa.
“Nimekwambia nieleze kila kitu ,na kama usipofanya hivyo you’ll bleed to death.” Akasema Mathew
“ Ok nitakueleza kaka lakini naomba baada ya kumaliza kukueleza ukweli unitafutie dawa.Nihurumie ninasikia maumivu makali sana” akasema Yule jaama
“ Kitu hicho alichokuwa anakiongelea mzee Kitwana kilikuwa kinatakiwa kutoka Ikulu. Na ili kukipata walilazimika kujenga mtandao .Kulikuwa na yeye mzee Kitwana halafu kukawa na mzee Matiku.Huyu alikuwa ni mwanajeshi mstaafu na aliwahi kuwa mlinzi wa rais kwa miaka ya nyuma.Baada ya huyu mzee Matiku kukawa na kijana mmoja anaitwa Edson ambaye alikuwa akifanya kazi Ikulu na ndiye aliyefanikisha kila kitu hadi kitu hicho kikapatikana.
Mathew aliposikia jina Edson likitwajwa akahisi nywele zikimsimama na mwili wote ukastuka.
“ Ouh my God ! Edson “ akasema kwa sauti ndogo na kumkazia macho Yule jamaa
“ Umesema Edson? Ni Edson Kobe? Akauliza Mathew
“Ndiyo Edson Kobe.Kumbe unamfahamu aagghhhhh..! akaguugumia kwa maumivu makali
“ Dah ! Ahsante Mungu tumefika katika ukweli” akawaza Mathew
“ Endelea ! akasema
“Baada ya kukipata kitu hicho,alikabidhiwa mzee Matiku ili akihifadhi wakati wakisubiri kulipwa fedha zao na watu waliokuwa wakikihitaji . Mzee Kitwana aliungana na Edson kwa siri wakamzunguka mzee Matiku na kuikiiba kitu hicho wakimtumia mpenzi wa mzee Matiku aliyeitwa Brigita.Edson alijenga mahusiano ya siri na Brigita na hivyo wakafanikiwa kuiba kitu hicho kwa lengo la kukiuza bila kumshirikisha mzee Matiku.Mzee Matiku alifanya uchunguzi na kugundua kwambna ni washirika wake Kitwana na Edson ndio waliomzunguka na kukiiba kitu kile.Alikasirika sana na hivyo kuamua kuvujisha siri kwa wakuu wa Edson kuhusiana na wizi wa kitu kile.” Akanyamaza na kisha akaendelea
“ Edson aliuawa wiki moja tu baada ya mzee Matiku kuvujisha siri kwa wakubwa zake.”Akasema Yule jamaa na kabla hajaendelea zaidi Mathew akauliza
“ Nani alimua Edson?
Yule jamaa akamuangalia na kusema
“ White house”
“ White house ?unamaanisha nini?
“ Watu toka ndani ya Ikulu”akasema Yule jamaa .Mathew akakaa kimya kwa muda.Mambo mengi sana yakamjia kichwani .
“ Endelea” akamuamuru yule jamaa
“ Wiki mbili baada ya Edson kuuawa ,KItwana akatuamuru tumuue Brigita ambaye ndiye aliyekiiba kitu hicho kwa mzee Matiku .Matiku na Kitwana waliendelea na malumbano ya wao kwa wao na ikamlazimu Kitwana aamuru Matiku auawe,tukamuua.Baada ya hapo tukagundua njama mbaya ya mzee Kitwana.Alikuwa akitaka kuipata pesa yote peke yake kwa hiyo alipanga mpango wa kutumaliza ili abaki peke yake na kuchukua pesa yote peke yake.Kwa bahati mbaya watu aliowatafuta kwa ajili ya kutuua ni wa washirika wetu wa karibu na walipotueleza hatukukawia ikatulazimu kumuua mzee Kitwana na sisi kubaki na biashara hiyo.Tulipomuua Kitwana tuligundua kwamba kitu hicho hakikuwepo nyumbani kwake lakini baadae tuligundua kwamba alikuwa amekificha kwa msichana mmoja ambaye walikuwa na mahusiano ya kimapenzi.Tulimsaka msichana huyo na kumfungia mle ndani kwa muda wa miezi saba sasa tukitaka atuonyeshe mahala alipokificha hicho kitu.Baada ya kumpa mateso mengi hatimaye aliamua kutueleza ukweli kwamba kitu hicho amekificha kwa msichana mmoja anaitwa Eva.Kwa kuwa hatukuwa tukimfahamu Eva ni nani ilitulazimu kuanza kumtafuta ili kumfahamu ni nani na tukafanikiwa kumfahanmu kwamba ni mfanykazi wa idara ya usalama wa taifa kwa hiyo basi ikatulazimu kuanza kuzifuatilia nyendo zake ndipo tulipomtafuta mtaalamu mmoja wa program za kompyuta na kumuomba atutengenezee program yenye kuweza kumfuatilia mtu na leo hii ndiyo ametukabidhi kazi tuliyomtaka atufanyie.Kwa hiyo hivyo ndivyo ilivyokuwa hadi tukamfahamu Eva.Nimekwisha kujibu maswali yako naomba sasa unisaidie jeraha hili lisiendele kutoa damu” akasema Yule jamaa na kujaribu kuizuia damu isiendee ktoka kwa kutumia mkono wake
“ Nani mnunuzi wa hicho kitu ? Mlitaka kumuuzia nani? Akauliza Mathew
“ Mnunuzi ambaye anakitaka hicho kitu anaitwa Habib soud anatokea Saudi Arabia” akasema Yule jamaa.
“ Mna mawasiliano na huyo jamaa?
“ Ndiyo huwa tunawasiliana naye na tuliwasiliana naye hata juzi na akatuambia kwamba muda wowote tukifanikiwa kukipata tumtaarifu ili aweze kutupa maelekezo ya namna tukavyoipata pesa yetu” akasema Yule jamaa
Mathew akainama akafikiri kwa muda halafu akainua kichwa
“ Una bahati sana.Una maisha marefu zaidi ya paka.Sintakufanyia kile ambacho nilipanga kukufanyia.Nitakutibu jeraha lako lakini sintakuachia huru” akasema Mathew na kutoka mle chumbani akaenda chumbani kwake akarejea na kisanduku cha huduma ya kwanza.Akafungua kichupa Fulani kilichokuwa na unga unga akamimina unga ule katika kidonda cha yule jamaa ambaye alipiga ukele mkubwa sana na kumfanya Anitha aliyekuwa sebuleni kufika haraka mle chumbani kuangalia kuna nini.
“ Mathew whats going on? Akauliza Anitha
Mathew hakujibu kitu akaendelea na kazi ya kulifunga jeraha la Yule jamaa. Anitha aliogopa sana kwa namna damu ilivyokuwa imetapakaa mle ndani .Mathew naye alikuwa amechafuka damu
“ Eva tayari amekwisha rejea na daktari anamuangalia Yule msichana” akasema Anitha
“ Muite Yule msichana tuliyetoka naye kule kwa hawa jamaa aje afanye usafi ndani ya hiki chumba “ akaamuru Mathew na Anitha akakimbia haraka kwenda kumleta msichana Yule.Wakati akiendelea na kusaficha mle chumbani Mathew na Anitha wakatoka moja kwa moja wakaelekea sebuleni.Eva alikwisha mleta daktari na alikuwa anaendelea kumuhudumia Yule msichana.Mathew akamuita Eva pembeni
“ Eva do you trust this doctor?
“ Ndiyo ninamuamini sana.Anaifahamu kazi ninayoifanya na amekuwa akinisaidia sana kila ninapohitaji msaada wa tiba kama huu”
“ Ok Good.Sasa tuna mtu mwingine naye anahitaji matibabu anatakiwa atibiwe jeraha|” akasema Mathew halafu akaomba waongozane hadi katika chumba ambacho hupangia kazi
“ Mathew poleni sana kwa misuko suko mliyoipata.Nashukuru sana kwa msaada huu mkubwa na ninashukuru sana kwa kunisaidia kumpata Sabina”
“ Yule msichana anaitwa Sabibna? Akauliza Anitha
“ Ndiyo anaitwa Sabina.Sina cha kuwapa kwa kunisaidia kumpata.Nilikuwa naumiza kichwa sana nitampata wapi lakini nashukuru Mungu alikuleta kwangu na umenisaidia nimempata.” Akasema Eva
“ Usijali Eva hata sisi ulitusaidia sana kuweza kumpata kanali Adolf na kwa kupitia yeye tuliweza kuifanikisha kazi tuliyokuwa tunaitaka.Nilikuahidi kukusaidia na nimeitekeleza ahadi yangu.”
“ Ahsante sana Mathew.Sina neno zuri la kushukuru.By the way who are these people? Mmefahamu ni kwa nini walikuwa wananifuatilia? Kwa nini walimteka Sabina? Akauliza Eva
“ Watu hawa wanafanyakazi ya ujambazi kama alivyodai mmoja wao ambaye nimetoka kumuhoji sasa hivi.Walimteka Sabina ili awaonyeshe mahala kilipo kitu Fulani ambacho ni Sabina pekee anafahamu kilipo.Baada ya kumtesa sana Sabina aliwaambia kwamba kitu hicho alikupatia wewe umfichie na siku ile alipokupigia na kukutaka umsaidie alipewa simu ili awasiliane nawe.Baada ya hapo walianza kukufuatilia ili wakufahamu nyendo zako na ili kulifanikisha hilo wakamtumia mtaalamu mmoja wa program za kompyuta kutengeza programu itakayowawezesha wao kukufuatilia na leo hii ndiyo maana walikuwa wanakufuatilia ili waweze kutega kifaa katika gari lako cha kuweza kukufuatilia.Kwa hiyo Eva Sababu kubwa iliyowafanya wakufuatilie ni hiyo .Kuna kifaa anacho Sabina na walikuwa wakikihitaji sana.” akasema Mathew na kumuacha Eva akishangaa
“ Eva ni kweli kifaa hicho Sabina alikukabidhi umfichie? Akauliza Mathew
“ Hapana hakunipa.Yawezekana kuna mahala kwingine amekiweka kwa sababu mimi wala sina mazoea naye ya kufikia hatua hiyo.Mimi ninamfahamu kama mteja mzuri wa baa yangu.Ni kitu gani hicho wanachikitafuta hawa jamaa?
“ Eva ni hadithi ndefu sana tutaongea baadae.Kinachotakiwa kwa sasa ni kujitahidi Sabina apate fahamu na atueleze ni wapi alikokiweka kitu hicho.Kwa sasa naomba nenda kamsaidie daktari .Nina maongezi na Anitha” akasema Mathew.Alipohakikisha Eva ametoka Mathew akasema
“ White house killed Edson” akasema Mathew baada ya Eva kutoka mle chumbani.
“ Ouh my God ! Anitha akashangaa
“ Anitha suala hili si suala dogo kama tulivyokuwa tunalifikiria.Ni jambo kubwa na zito” akasema Mathew na wote wakabaki kimya.
MATHEW ANAGUNDUA SABABU YA KIFO CHA EDOSN NINI KITAKACHOFUATA? JAJI ELIBARIKI YUKO WAPI? TAFADHALI ENDELEA KUFUATILIA SIMULIZI HII KILA SIKU HAPA MASIMULIZI
No comments
Post a Comment