PENIELA (Season 2 Ep 8)
SEASON 2
SEHEMU YA 8
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Elibariki get down..!!!!!!!.. akasema na kumrukia Elibariki akamgandamiza katika kiti.Milio ya risasi ikarindima mahala pale na kusababisha taharuki kubwa.Watu wakashuka katika magari na kukimbia hovyo ili kujinusuru .Kwa takribani dakika tano risasi ziliendelea kurindima eneo lile.Mara kukawa kimya halafu mlango wa gari ya jaji Elibariki ukafunguliwa na mtu mmoja aliyekuwa na bastora mkononi na usoni akiificha sura yake kwa kofia nyeusi na kuacha sehemu ya macho.
“ Elibariki….!!” Akaita mtu Yule ambaye alikuwa ni mwanamke.Elibariki aliyekuwa amegandamizwa na Noah alishindwa kuitika alikuwa amechanganyikiwa .
Yule mwanamke akamsukuma Noah aliyekuwa amemgandamiza Elibariki kitini.Hakuwa na uhai tena.Alikuwa hatazamini kwa namna alivyoharibiwa na risasi.Jaji Elibariki alikuwa ameloa damu na hakuwa na hata nguvu za kusimama.Yule mwanamke akamshika mkono na kumtoa ndani ya lile gari na kumpeleka hadi katika gari ra rangi nyeusi lililokuwa nyuma ya gari la Elibariki halafu wakaondoka kwa kasi kubwa.Eneo lote halikuwa na mtu hata mmoja.Magari yalikuwa matupu watu walikuwa wameyaacha na kukimbia kuokoa maisha yao.
ENDELEA………………….
Dr Kigomba akiwa katika chumba kimoja pamoja na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Joshua wakiwa na baadhi ya wageni waliokuja kumpa pole mheshimiwa rais,simu yake ikaita akaitoa mfukoni na kutazama mpigaji halafu akainuka na kutoka nje ya kile chumba akajitenga pembeni mahala kusikokuwa na watu akaipokea
“ Hallow Festo” akasema Dr Kigomba kwa sauti ndogo
“ Mzee nimekupigia kukupa taarifa kuhusiana na ile kazi.”
“ Enhee nipe ripoti.Mmeimaliza tayari? Kila kitu kimekwenda vizuri? Akauliza Dr Kigomba
“ Tayari mzee tumeifanikisha .Nilikuwepo eneo la tukio nikishuhudia namna vijana walivyoifanya kazi lakini kuna tatizo moja lilitokea.”
“ Tatizo gani Festo?
“ Wakati vijana wakiifanya kazi yao kuna mtu ambaye hatumfahamu alitokea na kujaribu kupambana na vijana wetu kwa kujibizana nao risasi.Vijana wetu wawili wamejeruhiwa kwa risasi zilizotoka kwa huyo mtu.”
“ C’mon Festo kwa nini hakumdhibiti ? Akauliza Dr Kigomba
“ Mzee hatukufanikiwa kumfahamu mtu huyo ni nani lakini anaonekana ni mtu aliyekuwa amejiandaa sana na ni mtaalamu hasa wa kutumia silaha kwa namna alivyokuwa akifanya mashambulizi yake.Kazi ile ilituchukua zaidi ya dakika tano kitu ambacho hatukuwa tumekipanga.Sisi tulipanga iwe ni kazi ya dakika moja au mbili lakini ilituchukua muda zaidi kwa ajili ya kupambana na mtu yule ambaye alionekana kutaka kutuzidi nguvu.”
“ Kwa hiyo hakuna hata kijana mmoja aliyepoteza maisha?
“Zaidi ya kujeruhiwa kwa risasi zilizotoka kwa yule mtu hakuna hata kijana mmoja aliyepoteza maisha.”
“ Ok vizuri.Kazi yetu ya msingi ilifanikiwa? Kwa sababu hicho ndicho kitu kikubwa kuliko vyote”
“ Kwa kiasi kikubwa ninaweza kusema kwamba kazi ilikwenda vizuri kwa sababu gari la jaji limeharibiwa vibaya sana kwa risasi.Nina hakika hakuna ambaye angeweza kutoka salama.”
“ so you didn’t confirm that he’s dead? Akauliza Dr Kigomba
“ Mzee ilitulazimu kuondoka haraka eneo lile ili kuepusha mapambano zaidi na yule jamaa tusiyemfahamu aliyekuwa akijibizana nasi kwa risasi.Tatizo ni kwamba yeye alikuwa akituona lakini sisi hatukuwa tukimuona kwa hiyo ilikuwa ni ngumu sana kwenda kuhakikisha kama mtu wetu amefariki .Lakini nina uhakika mkubwa sana kwamba kutokana na shambulio lile hataweza kutoka hai” akasema festo
“ Ouh Festo ,Festo…hilo ndilo jambo ambalo nilikuonya toka mwanzo kwamba lazima uwe makini na uhakikishe kila kitu kinakwenda vizuri.Kwa sasa hatuna uhakika kama Elibariki amekufa ama vipi.Oh Festo unazidi kuniweka katika wakati mgumu sana”
“ Mzee usihofu nina uhakika mkubwa kwamba hawezi kutoka hai ndani ya gari lile.Halikuwa shambulio dogo.Hata kama ikitokea akawa amenusurika basi ni kwa mkono wa malaika lakini ninakuhakikishiaa kwamba tutamsaka kokote na kumpata .Hawezi kutukimbia ” Akasema Festo
“ Festo unanipa wakati mgumu sana .Nitakupigia tena baadae.Nimechanganyikiwa na sijui nini cha kufanya.” akasema Dr Kigomba na kukata simu.akaegeemea mti na kuvuta pumzi ndefu
“ Dah ! NImechanganyikiwa na sijui nifanye nini.” Akawaza Dr Kigomba
“ I have to inform Dr Joshua”
Dr Kigomba akatembea kwa kasi hadi katika chumba kile alichokuwamo mheshimiwa rais na wageni wake,akamfuata na kumnong’oneza kitu sikioni halafu dr Joshua kawaomba radhi wageni wake akatoka mle chumbani na Dr Kigomba wakaelekea katika chumba cha maongezi wakajifungia
“ Dr Kigomba kuna nini? Mbona unaonekana hauko kawaida? Akauliza Dr Joshua
“ Dr Joshua kazi uliyonipa kwa ajili ya kumshughulikia Elibariki imefanyika na nimepokea simu muda si mrefu toka kwa vijana kwamba zoezi hilo limefanyika lakini kulikuwa na tatizo dogo.”
“ Tatizo gani Kigomba? Akauliza Dr Joshua
“ Kama nilivyokutarifu mapema kwamba njia ya ajali ingekuwa ngumu hivyo kwa kuwa suala lenyewe ulitaka lifanyike haraka ,ilitulazimu kutumia njia ya shambulio ili ionekane kama vile Elibariki alivamiwa na watu wasiofahamika wakamuua.Vijana waliandaa shambulio la kustukiza lakini katika shambulio hilo kulitokea upinzani.Kuna mtu ambaye bado hajafahamika ambaye alikuwa akishambuliana na vijana wetu na kuwajeruhi wawili .Kutokana na mazingira ya mahali hapo ilikuwa ni vigumu kwa vijana wetu kumfahamu mtu huyo na hivyo baada ya kutekeleza shambulio lao ikawalazimu kutoweka haraka sana eneo lile” akasema Dr Kigomba
“ Dr Kigomba bado sijakuelewa,naona unaniambia maneno mengi .Nataka neno moja tu Elibariki amekufa ama bado” akasema Dr Joshua
“ Kwa mujibu wa Festo ni kwamba hana uhakika kama amefariki ama bado lakini anadai kwamba lilikuwa ni shambulio zito ambalo Elibariki hawezi kutoka hai”
“ Ouh my God !!... akasema Dr Joshua na kushika kiuno
“ so you are not sure if he’s dead or not? Akauliza Dr Joshua
“ Mzee sina uhakika bado kama amefariki ama bado ” akasema Dr Kigomba
Dr Joshua akafikri kwa muda na kusema
“ Dr Kigomba kwa nini jambo hili limekwenda hivi? Nilikuonya toka mwanzo kwamba jambo hili linahitaji umakini mkubwa lakini kwa nini hukuliwekea uzito wa kutosha?
“ Dr Joshua suala hili tumelichukulia kwa uzito unaostahili lakini hatukujua kama kunaweza kutokea jambo kama lililotokea la huyo mtu asiyejulikana.Lakini kama kujitahidi tumejitahidi na kilichobaki ni kupata uhakika kama Elibariki amefariki au bado.”
“ You didn’t do enough Kigomba!! Akasema kwa ukali Dr Joshua.
“ Kama kazi hii ingefanyika inavyotakiwa basi tusingekuwa hapa tunakaa roho juu juu hatuelewi kama Elibariki ni mzima ama vipi.Endapo vijana hawakufanya kazi vizuri na Elibariki akawa mzima basi tutakuwa tumeharibu kila kitu.Mambo yatazidi kuwa mabaya kwa upande wetu.Ouh Kigomba umenichanganya sana ..”
“ Dr Joshua hatuna muda wa kuendelea kulaumiana .Kazi imekwisha fanyika na kinachotakiwa hivi sasa ni kupata uhakika kama ilifanikiwa ama vipi.Kwa hiyo badala ya kuendelea kunilaumu kwamba sikufanya kazi inavyotakiwa chukua simu na umpigie kamanda wa polisi na umuulize kama Elibariki ni mzima ama vipi.Nina hakika mpaka mida hii tayari atakuwa amekwisha pewa taarifa za tukio hilo” akasema Dr Kigomba.Dr Joshua akainama akafikiri halafu akachukua simu na kumpigia Kamishna John adungile kamanda wa polisi kanda maalum ya Dare s salaam
“ Hallow mzee” akasema kamishna John
“ Kamishna nimepata taarifa muda si mrefu kwamba kuna yule kijana wangu jaji Elibariki ameshambuliwa na watu wasiojulikana.Naomba unithibitishie taarifa hizi ni za kweli? Akauliza Dr Joshua
“ Mheshmiwa hizi ni taariza za kweli kabisa.Tukio hilo ni kweli limetokea katika makutano ya barabara za Mkwavinyika na Kilimanjaro.Kwa mujibu wa mashuhuda ni kwamba wakati gari zikiwa zimesima zikisubiri taa za kuongozea magari ziwaruhusu wapite zilitokea piki piki mbili zikiwa na watu wawili kila moja na kisha wakaanza kulishambulia gari la mheshimiwa jaji kwa risasi.”
“ Jaji Elibariki alikuwemo ndani ya gari hilo? Kama alikuwemo ni mzima? Akauliza Dr Joshua
“ Kwa taarifa nilizozipata toka kwa kamanda wangu aliyeko katika eneo la tuko hivi sasa ni kwamba katika gari la mheshimiwa jaji kumekutwa mtu mmoja tu na ambaye amekutwa amekwisha fariki.Lakini wameshindwa kumtambua ni nani kutokana na kuharibiwa vibaya kwa risasi.Kwa hiyo ni vigumu kuthibitisha kaam jaji Elibariki alikuwemo ndani ya hilo gari wakati wa shambulio ama vipi.Mwili wa mtu huyo aliyekutwa ndani ya gari umepelekwa katika hospitali ya taifa kwa utambuzi”
“ Ok kamishna .Mpaka sasa kuna fununu zozote za kuwafahamu watu hao waliofanya shambulio hilo?
“ Mpaka sasa bado hatujawafahamu watu hao ni akina nani lakini nakuhakikishia mzee kwamba tutawasaka watu hawa katika kila kona ya jijii na tutawapata.”
“ Ahsante sana kamishna kwa taarifa hii.Ninaomba ufanye kila linalowezekana ili uweze kuwabaini watu waliofanya kitendo hicho”
“ Tututajitahdi sana mzee na ninakuhakkishia kwamba lazima tutawapata tu” akasema Kamishna na Dr Joshua akakata simu akamgeukia Dr Kigomba
“ Kwa mujibu wa kamishna ni kwamba kuna mtu mmoja aliyekutwa ndani ya gari la jaji Elibariki lakini wameshindwa kumtambua kutokana na kuharibiwa vibaya kwa risasi.Kwa hiyo tuna uhakika kwamba kuna mtu amekufa ndani ya gari lakinihatuna uhakika kama kweli ni Elibariki.”
“ Ok Dr Joshua niachie mimi kazi hii.Ninakwenda sasa hivi hospitali kwenda kumtambua mtu huyo kama ni elibvariki.”
“ Vipi kuhusu Flaviana ? Kuna haja ya kumweleza chochote kuhusiana na jambo hili ?
“ Kwa sasa hakuna haja ya kumueleza chochote hadi hapo tutakapokuwa na uhakika kwamba aliyefariki ni mumewe.Ninakwenda huko hospitali sasa hivi kuthibitisha kama ni yeye kweli ama vipi ” akasema dr Kigomba.
“ Sawa Kigomba fanya hivyo Ili tuwe na uhakika kama zoezi letu limefanikiwa ama vipi.hata hivyo ninawas………..” kabla hajamaliza kuongea ,simu yake ikaita .Alikuwa ni Flaviana.Dr Joshua na Kigomba wakatazamana.
“ Nina hakika tayari atakuwa amekwishapata taarifa za tukio.What am I going to tell her? Akauliza Dr Joshua
“ Ongea naye mweleze kwamba hata wewe umezipata taarifa hizi sasa hivi “ akasema Dr Kigomba.Dr Joshua akabonyeza kitufe cha kupokelea simu
“ Hallow Flaviana”
“ Baba uko wapi ? Akauliza Flaviana huku akilia
“ Niko huku ndani katika chumba cha maongezi.Kuna nini Flaviana mbona unalia?
“ Baba mume wangu..Eli ame…”
“ Flaviana …” akasema Dr Joshua lakini tayari simu ilikwishakatwa
“ Tayari ana taarifa.Siku hizi taarifa huwa hazichelewi.Kigomba nenda hospitali mara moja kathibitishe ili tujue nini cha kufanya “ akasema Dr Joshua .Kabla hawajatoka ndani ya kile chumba Flaviana akafika akikimbia .Machozi yalikuwa yanamtoka.Alikuwa ameongozana na Anna mdogo wake.Alipomuona baba yake akamkumbatia huku akilia
“ Baba ! mume wangu.Elibariki amepigwa risasi....” akasema Flaviana
“ Flaviana nyamaza kulia kwanza.Hata mimi nimezipata taarifa hizo sasa hivi nimepigiwa simu na kamishna wa polisi kanda maalum na amenithibitishia kwamba ni kweli kuna watu wasiofahamika wamelishambulia gari la mumeo na kuna mtu mmoja amekutwa amekufa lakini wameshindwa kumtambua mtu aliyekuwemo ndani ya gari hilo kama ni mumeo .Hakuna mwenye uhakika kama mumeo alikuwemo ndani ya hilo gari.Elibariki ni mtu maarufu hapa mjini kama angekuwa ni yeye basi tungekwisha jua.”
“ dady its him..Ouh Eli….Nimetoka kuongea naye usiku huu” Akasema Flaviana huku akilia
“ Usilie Flaviana.Nimemtuma Dr Kigomba aende huko hospitali ili akathibitishe kama kweli ni Eli ndiye aliyekuwamo ndani ya hilo gari ama vipi” akasema Dr Joshua
“ Ninakwenda naye.Nataka nikathibitishe kama kweli mume wangu ameuawa “ akasema Flaviana.Dr Joshua alishindwa kumkatalia mwanae kwenda hospitali
“ Dr Kigomba ongozana na Flaviana kwenda hospitali.Mimi nitabaki na wageni walioko hapa.Mtanipa taarifa baada ya kuthibitisha kama kweli mtu huyo ni Elibariki” akasema Dr Joshua
Kwa haraka Dr Kigomba akaongozana na akina Flaviana wakaingia katika gari wakaelekea hospitali.Njia nzima Flaviana alikuwa analia.Walifika hospitali wakapokewa na kupelekewa katika chumba cha maiti wakaonyeshwa maiti iliyokuwa imetolewa ndani ya gari la jaji Elibariki.Ilikuwa imeharibiwa vibaya kwa risasi
“ This is not him.This is not my husband.” Akasema Flaviana.Watu wote mle ndani wakaangaliana
“ Flaviana are yousre this is not him? Akauliza Dr Kigomba
“ This is not him.Ninamfahamu mume wangu vizuri na nimetoka kuongea naye usiku huu kwanza haya si mavazi aliyokuwa amevaa,hakuwa amevaa kaptura .This is someone else.Mume wangu si huyu..” Akasema Flaviana na kuchukua simu yake akajaribu kupiga namba ya simu ya mumewe lakini hazikuwa zikipatikana.
“ Where is my husband? Akajiuliza Flaviana huku akihisi kuishiwa nguvu akakaa chini.Dr Kigomba alihisi kuchanganyikiwa.
“ Eli bariki hajafa.Yuko wapi ? Swali hili lilimuumiza sana kichwa.
*******
Mlinzi aliwafungulia geti akina Mathew wakaingia ndani .Nyumba ilikuwa kimya .Noah hakuwepo.Mathew akamtoa yule msichana ambaye hali yake iliendelea kuwa mbaya akampeleka sebuleni na kumlaza katika sofa .Akamtazama na kumuonea huruma sana
“ Hali yake inazidi kuwa mbaya.Anahitaji msaada wa haraka” akawaza Mathew na kumpigia simu Eva
“ Eva uko wapi? Ninakuhitaji haraka.Mimi tayari niko hapa nyumbani”
“ Niko njiani Mathew.Nilikwama kidogo katika foleni lakini ndani ya dakika tano nitakuwa nimefika hapo kwako” akasema Eva.
Mathew akaenda katika gari lake na kufungua buti akamtoa yule jamaa aliyekuwa amemfungia mle akambeba na kumuingiza ndani.Moja kwa moja akampeleka katika chumba alichokuwa amemfungia Arnold mchana akamlaza katika kitanda na kumfunga miguu na mikono akamuacha na kurejea sebuleni .Wakati huo huo gari la Eva likafunguliwa geti na kuingia ndani.
“ Eva karibu sana” akasema Mathew akimpokea Eva
“ Mathew ahsante sana.Kuna tatizo gani? Akauliza Eva kwa wasi wasi.Mathew hakumjibu kitu akamuongoza Eva hadi sebuleni.Mstuko alioupata Eva hauelezeki
“ We found her” akasema Mathew.Eva alishindwa kujizuia akainama na kumkumbatia msichana yule aliyekuwa amelala pale sofani huku hali yake ikionekana mbaya sana.Machozi yakamtoka
“ Mmempata wapi? Wamemfanya nini? Akauliza Eva
“ Eva ni hadithi ndefu lakini kwa sasa tunachotakiwa kukifanya ni kumpatia matibabu.Inasemekana kwamba amegoma kula chakula siku ya ya tatu leo.Hiyo ndiyo sababu kubwa iliyomfanya adhoofu namna hii.Tunatakiwa kumpatia huduma ya haraka.Unafahamiana na daktari yeyote ambaye anaweza kumuhudumia kwa haraka? Akauliza Mathew
“ Ndiyo ninafahamiana nao.Ninaombeni dakika kumi nikamchukue daktari .”akasema Eva na kutoka mbio hadi katika gari lake akamfuata daktari
“ Its time to find the truth now.” akasema Mathew na kuingia katika chumba Fulani ambacho ameweka vifaa vingi akachukua sanduku lenye rangi nyekundu halafu akaenda katika chumba alichomuweka yule jamaa ambaye tayari alikwisha zinduka .Mathew akammulika katika macho kwa kutumia tochi ndogo halafu akachukua kidude Fulani kidogo mithili ya chupa ya dawa akakifungua na kukiweka katika pua za yule jamaa na kumfanya apige chafya mfululizo.Mathew akavuta kiti na kuketi.Akamtazama yule jamaa kwa macho makali na kusema
“ Wenzio wote ulio kuwa nao wamekwisha fariki dunia umebaki wewe tu na maisha yako kwa sasa nimeyashikilia mimi.Nitakuwa na maneno machache sana ya kuongea nawe na nitaomba nitakachokuuliza unijibu kwa usahihi ama sivyo nitakufanyia kitu kibaya ambacho huajwahi kuona binadamu akimfanyia binadamu mwenzake.” Akasema Mathew kwa ukali na mara mlango ukafunguliwa akingia Anitha.
“ Anitha tafadhali naomba unipishe .Hutakiwi kukaa ndani ya chumba hiki.Hutakiwi kuona mambo yatakayofanyika humu” akasema Mathew.Anitha hakuongea kitu akaufunga mlango akatoka.Aliogopa kwa namna Mathew alivyokuwa amebadilika.Yule jamaa palekitandani alikuwa anatetemeka kwa woga.Mathew akamsogelea na kumwambia
“ Nataja uniambie ninyi ni akina nani? Mfanya kazi gani?
Yule jamaa hakutaka kumchezea Mathew alimuona namna alivyokuwa amekasirika hivyo akarekebisha koo lake na kusema kwa sauti yenye kukwaruza
“ Kusema ukweli sisi ni..” akasita .Mathew akamtazama kwa hasira halafu akaenda katika kile kisanduku chekundu akachukua kifaa cha kutobolea
“Nilikwambia kwamba nina muda mchache sana wa kuongea nawe.Sihitaji kabisa kuchezewa akili yangu.” Akasema Mathew na kukiwasha kidude kile akakichomeka katika mguu wa Yule jamaa ambaye alitoa ukulele mkubwa wa maumivu.
“ Nadhani sasa umekwisha nielewa mimi ni nani.Kwa hiyo nieleze haraka ninyi ni akina nani na nini shughuli zenu? Akasema Mathew.Yule jamaa bado aliendelea kulia kwa maumivu makali huku damu ikimtoka.
“ Naona bado hujanifahamu vizuri.” Akasema Mathew na kuchukua tena kile kifaa akakiwasha na kutaka kukizamisha katika mguu wa yule jamaa.Akapiga ukulele mkubwa akimtaka asifanye vile.
“ tafadhali usiniumize tena.Nitakueleza kila kitu” akasema yule jamaa huku akilia kwa maumivu makali aliyokuwa akiyasikia
“ Niambie haraka sana ninyi ni akina na nini kazi zenu?
“ Sisi kazi zetu ni wizi wa magari.Huwa tunaiba magari ndani na nje ya nchi.Vile vile huwa tunafanya shughuli za ujambazi ,kuvamia mabenki na kupora fedha n.k Hizo ndizo shughuli zetu” akasema yule jamaa na kuuma meno kwa maumivu makali .Bado alikuwa amefungwa miguu na mikono katika kitanda.
“ Kwa nini mnamfutilia Eva? Nani kawatuma mumfuatilie Eva? Akauliza
“ Sisi hatumjui Eva na wala hatujawahi kumuona”
‘ Kama hamumjui kwa nini mnamfuatilia? Akauliza Mathew
“ ouh kaka ninaumia sana.Naomba unifungue walau mikono .Ninasikia maumivu makali sana.Nitakueleza kila kitu unachokitaka naomba uniamini”akasema yule jamaa.Mathew akamtazama na kuamua kumfungua
“ Ukweli wako ndio utakaokuweka hai.Niambie ukweli mtupu.Kwa nini mnamfuatilia Eva ” akasema Mathew
“ Nitakueleza kila kitu ila naomba usiniue” akasema yule jamaa baada ya kufunguliwa mikono
WATU WALE NI AKINA NANI? KWA NINI WANAMFUATILIA EVA? TUKUTANE TENA SEHEMU IJAYO…
No comments
Post a Comment