PENIELA (Season 2 Ep 4)

SEASON 2

SEHEMU YA 4

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

“ Watu hawa wanaomfuatilia Eva ni akina nani? Nafahamu Eva ana fanya kazi kwa siri katika idara ya usalama wa taifa.lazima kuna wau watakuwa wanataka kumchunguza.Hizi kazi niza hatari sana.Siku zote unaishi kama ndege.” Akawaza Mathew na mara Anitha na Noah wakaingia kujumuika naye pale mezani

“Anitha umefikia wapi kuhusu ile program ?

“ Ninaendelea na hiyo kazi .Lakini huyu jamaa Arnold anaonekana ni mtu anayeifahamu sana kompyuta .Nimeangalia namna alivyoitengeneza ile program dah ! yuko vizuri sana” akasema Anitha

“ Nimezungumza na Elibariki kwamba atajitahidi kufika jioni ya leo ili tuweze kuongea naye kuhusu lile suala la Peniela.Yeye ndiye tutakayemtumia katika kumchunguza Peniela.Peniela lazima kuna kitu anakifahamu kuhusiana na kifo cha Edson na Team SC41.Ili tuufahamu ukweli yatubidi tumfanyie uchunguzi mkubwa sana na nina hakika yeye ndiye atakayetuongoza kwenye ukweli ”akasema Mathew


ENDELEA…………………………

Jua limeanza kupungua nguvu yake kuashiria kwamba siku inaelekea ukingoni.Shughuli ya kuuaga mwili wa Dr Flora ilimalizika katika viwanja vya ukombozi halafu ukapelekwa katika makazi binafsi ya rais ambako ungelala kule kabla ya kusafirishwa kesho yake asubuhi kuelekea kijijini alikozaliwa kwa mazishi.Zoezi lilichukua muda mrefu zaidi ya ilivyokuwa imetazamiwa kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza kumuaga mwanamama huyu ambaye katika kipindi cha uhai wake alijitoa sana katika kuwakomboa kiuchumi wanawake na vijana.

Nyumbani kwa rais mwili wa Dr Flora uliwekwa katika chumba maalum ambako watu mbali mbali ambao hawakupata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho katika viwanja vya ukombozi walikuwa wanaendelea na zoezi hilo.Watu walikuwa wengi sana na ulinzi ulikuwa mkali

Saa kumi na mbili na dakika nane za jioni Dr Joshua akaingia katika chumba alichokuwamo Flaviana akiwa na mdogo wake Anna pamoja na binamu zao watatu

“ Flaviana pole sana.Nilipata taarifa kwamba ulipoteza fahamu ghafla ukakimbizwa hospitali.Nilimuagiza Amos aje akutazaame.Unaendeleaje hivi sasa?akauliza Dr Joshua

“ Ninaendelea vizuri sana baba.Madaktari walinipima wakasema kwamba uchovu wa mwili na mawazo mengi ndivyo vilisababisha hali ile kunitokea.Dr Amos naye ametoka hapa kunipima muda si mrefu na kila kitu kinakwenda vizuri hakuna shida yoyote” akasema Flaviana

“ Pole sana Flaviana hali kama hiyo ni ya kawaida sana kwa nyakati kama hizi.Unachotakiwa ni kujipa mapumziko ya kutosha.Tomorrow we’ll have a big day.I need you all to be strong” akasema Dr Joshua

“ Usihofu baba,tutajitahidi “ akajibu Anna

“ Ok ! Kuna watu ninaohitaji kuonana nao mida hii .Tutaonana baadae “ akasema Dr Joshua na kutaka kutoka Flaviana akamuita

“ baba vipi kuhusu lile suala ? Umekwishaanza kulifanyia kazi?

“ Ndiyo .Tayari limekwisha fanyiwa kazi na tayari nimepokea taarifa ya madaktari walioufanyia uchunguzi mwili wa mama yenu ili kujua chanzo cha kifo chake”

“ really? Akauliza Flaviana

“ Inasemaje? Wamegundua nini?akauliza Anna

“ Bado sijaifungua na kujua kilichomo ndani yake .Nilitaka tuifungue tukiwa wote kesho baada ya kurejea toka katika mazishi.Ile ni taarifa ya familia kwa hiyo inabidi ifunguliwe na sisi sote.Nadhani tulifanye zoezi hilo kesho baada ya kurejea toka katika mazishi”akasema Dr Joshua

“ Dady can we open it today? Akauliza Flaviana

“ It’s ok .Tunaweza kuifungua ripoti hiyo hata leo.Tukutane katika chumba cha maongezi baada ya dakika ishirini .Kuna watu ambao nahitaji kuonana nao sasa hivi”akasema Dr Joshua na kutoka akiwa ameongozana na walinzi wake.Baada tu ya Dr Joshua kutoka,Flaviana akachukua simu na kumpigia mumewe

“ Hallow Flaviana unaendeleaje? Akauliza jaji Elibariki

“Ninaendelea vizuri.Dr Amos ametoka hapa kunipima muda si mrefu na kila kitu kinaendelea vizur.Uko wapi ?

“ Niko na wafanyakazi wenzangu wamekuja kutupa pole kwa msiba” akasema Elibariki

“ Ok vizuri.Eli unaweza ukaja mara moja huku ndani ? Baba anatuhitaji kuna kitu anataka kutuambia” akasema Flaviana

“ Ok ninakuja” akasema jaji Elibariki

Baada ya dakika ishirini Dr Joshua akafika katika chumba cha maongezi kama alivyokuwa amewaahidi wanae.Alionyesha mshangao Fulani baada ya kumkuta Jaji Elibariki ndani ya kile chumba.Ilionekana wazi hakuwa amependezwa kumkuta jaji Elibariki mle ndani.Wakasalimiana halafu akaketi

“ Elibariki nimeshukuru na wewe umefika katika kikao hiki.Nimewaambia wenzako tukutane hapa kuna jambo nataka tulizungumze” akasema Dr Joshua .Flaviana ,Anna,jaji Elibariki walikuwa kimya kabisa wakimsikiliza

“ Kufuatia kifo cha ghafla cha mama yenu ,ilinilazimu kufanya uchunguzi kuhusiana na nini kilisababisha kifo chake” akanyamza kidogo halafu akaendelea

“Niliunda timu ya madaktari bingwa toka katika hospitali kuu ya taifa kwa ajili ya kufanya uchunguzi huo na kubaini sababu ya kifo cha ghafla cha mma yenu.Leo mchana wametoa ripoti yao.Anna hebu fungua mlango na mwambie Captain Amos ailete ile ripoti hapa atusomee ” akasema Dr Joshua.Jaji Elibariki ambaye alionekana kuwa katika mshangao kidogo akauliza

“ Mzee ni uchunguzi gani tena uliofanyika? Ulifanya uchunguzi mwingine kuhusiana na kifo cha Dr Flora ukiacha mbali ule ambao tuliufanya sisi?

“Najua utashangaa Elibariki kwamba kuna uchunguzi mwingine ulifanyika lakini ilinilazimu kufanya uchunguzi kwa kuwatumia madaktari bingwa ili kubaini nini chanzo cha kifo cha Dr Flora” akasema Dr Joshua katika sauti ambayo ilionyesha wazi kwamba hakuwa akihitaji tena maswali yoyote toka Elibariki

“ Lakini mzee uchunguzi si tulishaufanya na nikawaletea ripoti kuhusiana na kilichosababisha kifo cha mama na wewe mwenyewe ukaahidi kulifanyia kazi sasa uchunguzi juu ya uchunguzi inakuwaje hapa? Akauliza Jaji Elibariki

“ Elibariki suala hili ni suala zito linahusu uchunguzi wa kifo cha mtu ,tena mke wa rais,hivyo lazima ufanyike uchunguzi mkubwa na kina.Ninashukuru kwa kujitahidi kufanya uchunguzi wako lakini sisi katika serikali huwa hatufanyi kazi kwa kutegemea taarifa ya kutengenezwa,taarifa isiyokuwa na kichwa wala mkia,taarifa isiyo na uthibitisho wowote wa daktari anayetambuliwa na serikali.Nakupongeza kwa juhudi zako na kwa kujali lakini wataalamu wangu hawakuwa tayari kuifanyia kazi taarifa uliyoitoa.Taarifa itakayofanyiwa kazi ni taarifa ambayo imefanyiwa kazi na madaktari bingwa na kuthibitshwa na daktari mkuu wa serikali na si taarifa ya kuokoteza okoteza.” Akasema Dr Joshua katika hali iliyoonyesha wazi alikuwa akimkebehi Jaji Elibariki kwa ripoti aliyoileta.Jaji Elibariki akasimama na kutaka kusema jambo lakini kabla hajasema chochote Captain Amos daktari wa familia ya rais akaingia akiwa na bahasha mkononi

“Karibu sana Captain Amos.Familia yote imekutana tayari kuipokea ripoti ya madaktari.Tafadhali tusipoteze wakati ifungue na utuambie ni kitu gani kimeandikwa na madaktari” akasema Dr Joshua

“ Ripoti hii ni ya uchunguzi wa kubaini sababu ya kifo cha ghafla cha Dr Flora.” Akasema Captain Amos.Akaipitia ripoti ile yenye karatasi tano ,kisha akasema

“ Kwa mujibu wa madaktari bingwa waliofanya uchunguzi huu wamebaini kwamba kifo cha ghafla cha Dr Flora kilisababishwa na shinikizo la damu.Hawajaona kitu kingine chochote kilichosababisha kifo chake” akasema Captain Amos daktari wa familia ya rais

“ Ahsante Amos.Unaweza kwenda”akasema Dr Joshua.Captain Amos akatoka

“ Nyote mmeisikia taarifa ya madaktari bingwa .Mama yenu alikufa kutokana na shinikizo la damu na si sababu nyingine yoyote. Taarifa hii ya madaktari bingwa inapingana na taarifa aliyotuletea mheshimiwa jaji ambayo inasema kwamba kifo cha mama yenu kilisababishwa na sumu.Ukiachana na taarifa hiyo nimepokea pia taarifa toka kwa vijana wangu niliowatuma wafanye uchunguzi kuhusiana na mambo yale mliyoniambia kwamba inawezekana kuna watu walihusika katika kusababisha kifo cha mama yenu.Taarifa ya vijana wangu inasema kwamba hakuna mtu yeyote ambaye alihusika katika kusababisha kifo cha Dr Flora na wala hakuna uzembe wowote uliofanyika.Mlimzungumzia Dr Kigomba kwamba alisikika akipiga simu kuzuia uchunguzi usifanyike lakini ukweli ni kwamba Dr Kigomba alipata taarifa ya kwamba kuna watu waliokuwa wakifanya uchunguzi wa siri na ndiyo maana akatoa amri kwamba watu hao wazuiliwe haraka sana kwa sababu tayari kulikuwa na mpango wa kuufanyia uchunguzi wa kina mwili wa mama yenu kwa kuwatumia madaktari bingwa .Dr Flora ni mtu mkubwa kwa hiyo uchunguzi wa kifo chake unatakiwa uwe maalum pia na si kwa kuwatumia madaktari wa kuokoteza mitaani.Sijaongea chochote kuhusiana na kitendo cha kihuni kilichofanywa na Elibariki na wenzake .Naomba leo niweke wazi kwenu kwamba nimechukizwa sana na kitendo kile na ninaomba kisijirudie tena.Sijataka kuchukua hatua zozote kwa sababu Elibariki wewe ni mwanangu na ninakuheshmu sana lakini wewe na wenzako mlipaswa kupewa adhabu kali sana kwa kitendo cha kihuni mlichokifanya.Mmefanya uhuni na kutuletea taarifa ya uongo ambayo imetusababishia matatizo makubwa ndani ya familia yetu na kwa watu wetu wa karibu tunaowaamini.Dr Kigomba ambaye mmemtuhumu kwamba anahusika katika kusababisha kifo cha Dr Flora ni mtu wangu wa karibu na nimefanya naye kazi kwa muda mrefu ni mtu ninayemuamini sana lakini mmetaka kunifanya niamini kwamba ni mtu mbaya.Sintafanya lolote kuhusiana na jambo lile lakini naomba mfahamu kwamba nimechukizwa sana .Kwa maana hiyo basi mjadala mzima wa kuhusina na sababu ya kifo cha mama yenu nimeufunga rasmi leo na sitaki kabisa kuendelezwa kwa mambo yasiyokuwa na ukweli wowote.Tayari madaktari bingwa wamekwisha thibitisha kwamba mama alikufa kifo cha kawaida kilichosababishwa na shinikizo la damu.” Akasema Dr Joshua halafu akamuomba Flaviana watoke wakaongee nje.Jaji Elibariki alibaki amepigwa na butwaa hakujua aseme nini.Alikuwa na hasira zisizomithilika.Dr Joshua na Flaviana wakatoka nje ya kile chumba

“ Flaviana I’m so disappointed with you” akasema Dr Joshua ambaye uso wake ulionyesha wazi kwamba alikuwa amechukia sana

“ Why father?akauliza Flaviana

‘ kwa nini umemjumuisha Elibariki katika kikao cha familia?

“ Baba,Eli ni mume wangu na ni sehemu ya familia yetu pia.Mbona katika mambo yetu mengine mengi ya kifamilia anashirikishwa? Niliona nimuite kwa sababu hata yeye kikao kile kilimuhusu kama mmoja wa wanafamilia

“ Ulifanya kosa kubwa Flaviana.Elibariki hakutakiwa kuwepo katika kikao kile.Kikao kile kilituhusu sisi pekee na si watu wengine wa hovyo hovyo”

“ dady ! Elibariki ni mume wangu na si mtu baki wala wa hovyo hovyo”

“ Vyovyote unavyomchukulia I don’t care lakini ninachokwambia na kwamba sitaki kumuona katika vikao vyetu vyovyote vya kifamilia.Ni kijana mshenzi sana yule.Ametaka kunisababishia matatizo makubwa na watu wangu wa karibu ninaowaamini na kufanya nao kazi kwa karibu.Ameleta ripoti ya kihuni na kutusababishia matatizo makubwa ndani ya familia yetu.Ninakuweka wazi kwamba ninamchukia sana huyo unayemuita mumeo.Ninasikitika sana kwa kukubali kuolewa na mtu kama yule.Ninashangazwa pia na jinsi unavyosimama na kumtetea leo wakati ni hivi majuzi tu ulikuja hapa ukilia na kusema humtaki tena yule mwanaume.”akasema Dr Joshua kwa ukali

“ dady ,Elibariki hapaswi kulaumiwa katika hili.Mimi ndiye ninayepaswa kubeba lawama kwa sababu ni mimi ndiye niliyemtuma baada ya kuhisi kwamba kuna sintofahamu kuhusiana na sababu ya kifo cha mama na hasa baada ya daktari mmoja pale katika hospitali kuu ya jeshi kuniambia kwamba kuna taarifa iliwafikia kwamba wasifanye uchunguzi wa kuhusiana na kifo cha mama.Yawezekana taarifa aliyopewa Elibariki na madaktari waliomsaidia kufanya uchunguzi ndiyo yenye matatizo na haikuwa na ukweli.Mimi ndiye ninayepaswa kuzibeba lawama hizi kwa sababu Elibariki alifanya kazi ile kwa shinikizo langu” akasema Flaviana

“ Flaviana naomba unisikilze mwanangu,hata wewe ulifanya kosa kubwa sana,ulipaswa kabla ya kushirikiana na mumeo kufanya jambo la hatari kama lile uje kwanza kwangu kunieleza na kwa pamoja tungeona nini cha kufanya.Lakini pamoja na hayo endapo angeleta taarifa yenye ukweli ndani yake basi kusingekuwa na tatizo lakini yeye ameleta taarifa ya uongo mkubwa ambayo imetusababishia sisi matatizo makubwa ndani ya familia,hata mimi taarifa ile imenipa wakati mgumu sana.Sielewi lengo lake ni nini hasa kwa kutuletea taarifa ile ya uongo.Nimejizuia kuchukua hatua zozote kwa sababu yako lakini kama angekuwa si mumeo angepata adhabu kali sana.Siku nyingine kama kuna jamo unataka kulifanya tafadhali usimuamini mumeo,njoo kwangu moja kwa moja.” Akasema Dr Joshua halafu akaondoka na kuelekea katika chumba chake akachukua simu na kumpigia Dr KIgomba

“ Hallow mzee” akasema Dr Kigomba

“ Dr Kigomba naomba tuonane ndani ya dakika tano”

“ Ok mzee ninakuja sasa hivi” akasema Dr Kigomba

Dr Joshua akavuta pumzi ndefu akakaa juu ya kitanda

“ Tayari nimekwisha limaliza lile suala ambalo lilitaka kutuletea matatizo makubwa.Nimewaondoa hofu kuhusiana na kifo cha mama yao kwa kuwasomea ripoti ile.Kwa sasa wote wanaamini kwamba kilichomuua mama yao ni shinikizo la damu.Tatizo linabaki kwa mtu mmoja tu ambaye ni Elibariki.Huyu ndiye anayeufahamu ukweli japokuwa tayari nimemjengea mazingira ya kutokuaminiwa tena lakini bado ni hatari kwetu.Kumuacha hivi hivi ni sawa na kulishikilia bomu mkononi na muda wowote linaweza kutulipukia.Siko tayari Elibariki awe ni mtu wa hatari kwetu eti kwa kuwa tu nimume wa mwanangu.Sintojali hilo na lazima ashughulikiwe haraka sana.Vile vile wanatakiwa wafahamike watu ambao alishirikiana nao kuifanya kazi ile ili nao washughulikiwe haraka sana .Jambo hili si la kufanyia mzaha hata kidogo.Na yotehaya yamesababishwa na Flaviana .Bila yeye tusingefika hapa tulipo hivi sasa.” Akawaza Dr Joshua



Flaviana alihisi kuchanganyikiwa na hakujua afanye nini.Alishindwa amuamini nani kati ya baba yake au mumewe Elibariki

“ Who is telling the truth? Nimuamini nani? Akajiuliza

“Lakini inawezekana baba akawa sahihi kwamba taarifa aliyoileta Elibariki haikuwa imejitosheleza.Haikuwa na usahihi ndani yake .Sina uhakika na uwezo wa madaktari waliomsadia kuufanya uchunguzi huo.Taarifa ile ya baba nadhani ndiyo sahihi kwani imefanyiwa kazi na madakari bingwa.Kinachofuata hapa sasa ni kulifunga rasmi jambo hili ililisiendelee kutuchanganya.” akawaza Flaviana na kurejea katika chumba cha maongezi alikomuacha mumewe.Jaji Elibariki alikuwa ameinama akiwaza.Flaviana akamsogelea karibu

“ Eli naombausiwaze sana mume wangu kuhusu mambo aliyoyasema baba” akasema Flaviana

“ Flaviana please believe me,taarifa hiyo anayoisema baba yako haina ukweli wowote.Rais amedanganywa,amepewa taarifa isiyo ya kweli.Tafadhali naomba usiiamini taarifa hiyo hata kidogo.Kuna kitu kinafichwa hapa ,believe me something is going on” akasema Elibariki

“ Elibariki hata mimi nimechanganyikiwa na sijui niamini lipi lakini nimeamua ni vyema endapo tutaachana na suala hili kwani litatuchanganya sana.” akasema Flaviana

“ Flaviana my love, kama kuna wakati unaopaswa kuniamini basi ni sasa.Please believe me,we did everything to get that report.Uhai wa mtu umepotea katika kuutafuta ukweli lakini matokeo yake taarifa yangu inakataliwa na kuonekana ni ya kuunga unga .Fumbua macho Flaviana something is going on here”

“ Eli I’m confused right now.Sielewi niende upande upi.Ninyi nyote ni watu ninaowaamni lakini …” Flaviana akasita kidogo

“ lakini nini? Akauliza Elibariki

“ Nashindwa nifanye nini.Please Eli I need to be alone for now” akasema Flaviana.Elibariki akamtazama kwa makini na kuuliza.

“ So you don’t trust me?

“Si kwamba sikumaini Eli but ……” akajibu

“ Its ok ..ninajua unachotaka kukisema” akasema Elibariki na kutoka kwa hasira akaubamiza mlango


*******


Dr Kigomba alifika haraka kuitika wito wa mheshimiwa rais

“ Kigomba tayari nimelimaliza lile suala”akasema Dr Joshua

‘ “That’s good news Mr President”akasema Dr Kigomba huku akitabasamu

“ Nimetoka kuongea na familia na wote wameridhika na ripoti ile uliyoileta.Umefanya kazi nzuri sana .Kwa sasa wote wanaamini kwamba mama yao alifariki kwa shinikizo la damu na si kwa kuchomwa dawa yenye sumu kama alivyodai yule muhuni.Pamoja na hayo bado tuna tatizo “

“ Tatizo gani mheshimiwa rais?

“ Ni Jaji Elibariki.Lile ni bomu tumelishika na siku moja linaweza kutulipukia na kutujeruhi.Sitaki nitakapokuwa nimemaliza muda wangu wa uongozi nianze tena kupata usumbufu wa aina yoyote ile.Ninataka baada ya kumaliza uongozi wangu niishi maisha ya raha mustarehe kwa hiyo kitu chochote kinachoonekana kuwa ni kikwazo katika mpango wetu basi nitakiondoa mara moja kama nilivyofanya kwa Flora.Elibariki anaufahamu ukweli wa kifo cha Flora na nina hakika siku moja anaweza akatulipua.Ninahitaji ashughulikiwe haraka iwezekanavyo.” Akasema Dr Joshua

“Unataka tumshughulikie vipi mzee? Ukumbuke huyu ni mkweo”

“ Take him away,but in a proffesional way.No mistake “ akasema Dr Joshua

“ Are you sure about this Mr President? Akauliza Dr Kigomba

“ Yes I’m sure.Hili ni bomu na tunatakiwa kulitegua haraka sana.Lakini kazi hii inatakiwa ifanyike kwa uangalifu mkubwa sana.Wakabidhi kazi hii vijana ambao wana ujuzi wa hali ya juu.Ninarudia tena no Mistake this time.Elibariki ni hatari sana kwetu kuliko hata Flora.Baada ya Elibariki tutaangalia namna ya kumuondoa pia na Captain Amos” Akasema Dr Joshua

“ Ok Mr president nimekwisha kuelewa.Nitalifanyia kazi hilo suala” akasema Dr Kigomba na kuondoka

“ Siko tayari kuona kizingiti chochote katika mpango wangu huu mkubwa ambao uo mbioni kukamilika.Yeyote atakayeonekana kuwa ni kikwazo kwangu nitamuondoa hata kama ni mwanangu “akawaza Dr Joshua


*******


“ Kuna jambo linaendelea hapa ikulu si bure.Ukweli wa kifo cha Dr Flora unazidi kufichwa na sasa hata rais amekubali kudanganywa na taarifa ya uongo na akaiamini.Hata familia yake wote wameonekana kuiamini taarifa ile.Nimeumizwa sana na maneno aliyoyasema Dr Joshua dhidi yangu.Amediriki kuniita mimi muhuni .Mimi na heshima zangu leo hii ninaitwa muhuni .Ninajuta kwa kukubali kuifanya kazi ile ya Flaviana.Juhudi zote za kutaka kuupata ukweli zimekuwa ni kazi bure na badala yake nimeambulia matusi.Kinachoniumiza kichwa ni kwa nini ukweli unafichwa? Kwa nini Dr Flora aliuawa? Akajiuliza jaji Elibariki

“ Ninamuamini sana Mathew na katu hawezi kunipa taarifa isiyo ya kweli.Yeyena timu yake wamehangaika sana na kuhatarisha maisha yao kwa sasabau tu ya kuipata taarifa ile .Hapana siwezi kukubali juhudi zao zipotee bure.Lazima tufahamu ni kwa nini ukweli wa kifo cha Dr Flora unafichwa? Lazima kuna kitu kinaendelea pale ikulu.Lazima nionane na Mathew na nimueleze kuhusu jambo hili ili tuone namna ya kuweza kulifanyia uchunguzi na kuubaini ukweli.NImeanza kuwa na wasi wasi sana hata kuhusiana na kifo cha Edson kwani hata naye alikuwa ni mfanyakazi wa ikulu” akawaza Elibariki halafu akachukua simu na kumpigia Mathew

“ Hallow Mathew” akasema jaji Elibariki

“hallow Elibariki”

“ Mathew kuna tatizo limetokea tena ndugu yangu”

“ Tatiza gani Eli?

“ Siwezi kukuelaza simuni.Uko nyumbani”

“ Ndiyo niko yumbani lakini nitatoka muda si mrefu kuna mahala nitaelekea”

“ Ok nakuja sasa hivi” akasema Elibariki na kukata simu akaelekea katika gari lake na kuondoka”


TUKUTANE SEHEMU IJAYO………

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...