PENIELA (Season 2 Ep 2)
SEHEMU YA 2
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Mathew na Anitha waliendelea kusubiri pale nje ya jengo lile na baada ya dakika kumi na mbili gari moja likawasha endiketa kuashiria kwamba linakata kona kuingia katika jengo lile la maegesho,na mara simu ya Mathew ikaita.Alikuwa ni Eva
“ Mathew ninaingia sasa katika jengo,gari yangu umeiona? Ninatumia hii BMW nyekundu”
“ Nimekuona Eva.Jamaa wao wanatumia gari gani?
“ Wanatumia Harrier yenye rangi nyeusi”
“ Ok Good ,Endelea kwenda mpaka juu kabisa.UKifika egesha gari na utoke garini ujifiche mahala ili tujue lengo lao ni nini” akasema Mathew na kukata simu.Gari la Eva likaingia ndani ya jengo lile na baada ya dakika mbili Toyota Harrier lenye rangi nyeusi nalo likakata kona kuingia ndani ya jengo lile.
“ Jamaa wenyewe ni hawa hapa.Its show time” akasema Mathew akaiwasha piki piki yake nao wakaingia ndani ya jengo lile wakiifuata ile gari iliyokuwa ikimfuatilia Eva.
ENDELEA……………………………..
Lile gari lililokuwa likimfuatilia Eva ,lilipanda ghorofani na nyuma yake walikuwepo Mathew na Anitha wakiwa na piki piki
“Watu hawa ni akina nani? Kwa nini wanamfuatilia Eva? Akaendelea kujiuliza Mathew.Wakapanda hadi walipofika ghorofa ya pili ,watu wale wakasimamisha gari na mmoja wao akashuka na kuangaza angaza katika magari yaliyokuwa yameegeshwa ,alikuwa akilitafuta gari la Eva.Alipolikosa akarejea garini wakaendelea na kupanda juu zaidi.Mathew akachukua simu na kumpigia Eva
“ Eva jamaa wanapandisha huko juu.Egesha gari kisha shuka ujibanze mahala.Sisi tunaendela kuwafuatilia ili kufahamu nini lengo lao.” Akasema Mathew
“ Tayari nimekwisha shuka nimejibanza katika chumba cha mlinzi “ akasema Eva
Mathew na Eva waliendelea kulifuatilia lile gari hadi maegesho ya juu kabisa.Watu watatu wakashuka toka ile gari.Walianza kuangaza angaza huku na kule kana kwamba kuna gari walikuwa wanalitafuta.Mawazo ya Mathew yalikuwa sawa kwani watu wale walikuwa wakilitafuta gari la Eva.Jamaa mmoja akachungulia ndani ili kuona kama kuna mtu lakini hakukuwa na mtu ndani.Akatoa kidude Fulani kidogo na kukinasisha chini ya gari la Eva kwa haraka.Mathew ambaye macho yake alikuwa ameyaelekeza kwa Yule jamaa alikiona kile kitendo
“ Kuna kidede amekiweka katika gari la Eva.Ninahisi ni kifaa cha kumfuatilia na kuonyesha kila mahala alipo” akasema Mathew kwa sauti ndogo wakiwa wamejificha nyuma ya gari moja
Baada ya kuweka kifaa kile mtu Yule alirejea katika gari lao halafu wakaondoka.
“ Endesha piki piki tuendelee kuwafuata” akasema Mathew wakarukia piki piki yao na kuendelea kuwafuata wale jamaa.Mathew aliyekuwa nyuma akatoa simu na kumpigia Eva.
“ Eva tunaendelea kuwafuatilia wale jamaa ili tuwafahamu ni akina nani .Kuna kitu wamekitega katika gari lako nadhani ni kwa ajili ya kutaka kukufuatilia na kuzijua nyendo zako.Nataka tufahamu nini lengo la kutaka kukufuatilia na kujua kila mahala unakokwenda? “ akasema Mathew
“ Mathew nashukuru sana.Lakini watu hawa ni akina nani na kwa nini wanifuatilie? Akauliza Eva
“ Ni mapema sana kufahamu watu hawa ni akina nani na kwa nini wanakufuatilia .Kwa sasa endelea na kazi zako kama kawaida isipokuwa kitoe kifaa kile na ukibandike katika gari lolote la karibu Nitakupigia simu baadae kukufahamisha tumefikia wapi.Mpaka muda huo nitakapowasiliana nawe tena tafadhali chukua tahadhari” akasema Mathew na kukata simu
Waliwaendelea kuwafuatilia wale jamaa kwa ufundi sana bila ya wao kufahamu kama walikuwa wakifuatiliwa.Wale jamaa walizunguka sehemu kadhaa na hatimaye wakasimama katika mgahawa mmoja mkubwa ulioko kati kati ya jiji maarufu kama City centre.Wakashuka na kuelekea sehemu ya baa.Anitha na Mathew nao wakawafuata ndani ya ile baa,wakatafuta sehemu moja nzuri ambayo iliwawezesha kuwafuatilia wale jamaa vizuri.Waliagiza nyama choma na vinywaji baridi ,wakaendelea kula huku macho yao yakiwa makini kwa kila walichokifanya wale jamaa ambao walikuwa wakipata nyama choma na bia na waliendelea na maongezi yao bila wasi wasi
“ Mathew hawa jamaa hawaonekani kama wana mpango wa kuondoka hapa hivi karibuni.Wameagiza tena raundi nyingine ya vinywaji.Tutakaa sana hapa tukiwafuatilia na kupoteza muda mwingi ambao tungeutumia kwa kazi nyingine.Tunataka kujiingiza katika kazi nyingine wakati tayari tuna jukumu zito mbele yetu na bado hatujafika popote.Tumekwisha gundua lengo lao lilikuwa ni kumfuatilia Eva na anachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kuongeza umakini na endapo atahitaji msaada wetu tena katika kuwafahamu zaidi watu hawa basi tutamsaidia baada ya kumaliza shughuli yetu ya msingi” akasema Anitha.Mathew bado aliendelea kuwakazia macho wale jamaa
“ Mathew are you listening to me? Akauliza Anitha
“ Anitha wait for a second” akajibu Mathew na kuendelea kuwakazia macho wale jamaa
Baada ya kama dakika tano hivi mmoja wa wale jamaa aliyekuwa amevaa suruali ya jeans ya bluu na shati jeupe akaitoa simu yake mfukoni ,alikuwa amepigiwa na mtu akabonyeza kituife cha kupokelea akaongea na alipomaliza akaufungua mkoba wake na kutoa simu ile kubwa aina ya Tablet akaelekezana jambo na wenzake wakagonganisha mikono ishara kwamba jambo lao limekwenda vizuri kisha Yule jamaa akatoka akiwa na ile tablet.
“ Nisubiri nakuja sasa hivi” akasema Mathew na kuinuka akatoka nje kumfuata Yule jamaa ambaye alielekea katika maegesho ya magari hadi katika gari moja aina ya Rav 4 rangi nyeusi.Kioo cha mlango wa dereva kikafunguliwa na ndani ya lile gari akaonekana mtu moja aliyevaa miwani myeusi.Jamaa aliyetoka ndani ya mgahawa akasalimiana na Yule jamaa ndani ya gari halafu wakaongea kidogo na akamkabidhi ile tablet.Yule jamaa wa ndani ya gari akaitazama tablet ile halafu wakaonekana kama wanaelekezana jambo Fulani na kisha akaiweka pembeni akafungua mkoba wake na kutoa bahasha ya khaki akamkabidhi Yule mwenzake ,kisha akafunga kioo cha gari lake na kuondoka.Mathew akampigia simu Anitha na kumtaka atoke mara moja.Bila kupoteza muda Anitha akatoka wakapanda piki piki na kuanza kumfuata yule jamaa aliyekuwa amepewa ile tablet
Toka katika mgahawa wa City Centre Yule jamaa alielekea hadi katika jengo Fulani zuri la ghorofa nne .Kabla ya kuingia ndani ya jengo lile kulikuwa na geti lililokuwa likilindwa na walinzi wa kampuni binafsi ya ulinzi.Yule jamaa mwenye Rav 4 alipita pale getini bila matatizo na walipofika akina Mathew wakasimamishwa na askari ambaye shida yake ilikuwa ni kujua mahala walikokuwa wakielekea.
“ Tunamfuata huyu jamaa aliyeingia na gari sasa hivi”
“ Arnold? Akauliza Yule mlinzi
“ Ndiyo tunamfuata Arnold.Tumeongozana naye” akasema Mathew na Yule mlinzi akawaruhusu wapite na kuwalekeza sehemu ya kuegesha piki piki.
“ Hizi ni ofisi za kampuni gani? akauliza akauliza Anitha wakati wakishuka katika piki piki yao.
“ hata mimi sifahamu .We’ll find out soon” akasema Mathew halafu wakaanza kupiga hatua kuelekea nsdani ya jengo lile
Walifika katika sehemu ya mapokezi na kumkuta mwanadada mmoja mrembo aliyewasalimu kwa heshima huku uso wake ukpambwa na tabasamu mwanana.Naye alitaka kufahamu ni ofisi gani ya lile jengo akina Mathew walikuwa wanaelekea.
“ Tunaelekea katika ofisi ya Arnold” akasema Mathew huku akitabasamu na mara Arnold akaonekana akishuka ngazi..Mathew akatabasamu na kusema
“ Ouh mtu mwenyewe tuliyekuwa tunamfuata ndiye huyo anashuka”
“ Hallow Atnmold” akasema Mathew huku akimpa mkono kana kwamba anamfahamu vizuri.
“ Hallow “ akasema Arnold huku akitoa tabasamu lenye mshangao kidogo kwani ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuonana na Mathew.
“ Arnold nina shida nawe ya kiofisi.Unatoka? akauliza Mathew
“ Yah ! ninatoka kidogo.Una shida gani? Akauliza Arnold
“Kama unatoka tunaweza tukaongelea hata nje” akasema Mathew kisha yeye na Anitha wakatangulia nje na kumuacha Arnold akitoa maelekezo Fulani kwa yule mwanadada wa mapokezi kisha akatoka na kuwafuata akina Mathew
“ Una shuda gani kaka? Halafu bado hatujafahamiana.Umetokea wapi?akauliza Arnold huku akionekana ni mwenye haraka sana ya kutaka kuwahi sehemu
“ Ninaitwa Mathew na yule dada anaitwa Anitha”
“ Ndiyo Mathew nikusaidie nini?akauliza Arnold
“ Arnold kwa kuwa una haraka can we talk in your car? Kuna kitu nataka kukuonyesha ” akasema Mathew huku akiingiza mkono mfukoni kana kwamba kuna kitu anataka kutoa.Arnold alisita kidogo lakini kwa kuwa alikuwa na haraka akaongozana na Mathew katika gari lake.Akafungua mlango na kungia garini
“Mathew nieleze shida yako.Nina haraka sana kuna mahala ninawahi” akasema Arnold huku akiwasha gari
“ Ghafla kwa kasi ya umeme ,Mathew akachomoa bastora toka katika mfuko wa koti na kumuwekea Arnold tumboni.Jicho likamtoka hakuamini alichokiona
“ Usithubutu kupiga kelele ndesha gari twende” akaamuru Mathew.Arnold alikuwa akitetemeka mikono akakanyaga mafuta na gari ikaanza kuondoka.Anitha akawasha pikipiki na kuwafuata.
******
Taarifa za Falviana kukimbizwa hospitali zilimfikia jaji Elibariki na kumstua sana.Bila kuaga mtu yeyote akaingia garini na kuondoka kuwahi hospitali
“ Flaviana alikuwa mzima kabisa na hakuonekana kuwa na tatizo lolote,nini kimemtokea na kusababisha akimbizwe hospitali? Akajiuliza Elibariki akiwa garini kuelekea hospitali
“ Inawezekana akawa alizidiwa baada ya kuona mwili wa mama yake? Lakini kama ni fahamu angepoteza kule hospitali tulipokwenda kuuchukua mwili na yeye na Anna wakapewa nafasi ya kutosha ya kuuaga mwili wa mama yao na aliweza kuhimili iweje aje apoteze fahamu huku uwanjani? Nitakwenda kufahamu huko huko hosspitali ,nini kimemtokea” akawaza Elibariki akiwa katika mwendo mkali akiwahi hospitali.Alipofika alipelekwa moja kwa moja katika chumba alichokuwa amelazwa Flaviana
“ Flaviana ..!! akasema Eli mara tu alipoingia mle chumbani na kumkuta mke wake akiwa amelala kitandani
“ Eli .!!! akasema Flaviana .Elibariki akamsogelea na kumbusu
“ Pole sana.Nini kimetokea?akauliza
“ Hata mimi sifahamu Eli.Sielewi nini kimetokea.Ninachokumbuka…..!!” akanyamaza kidogo na kusema
“Unakumbuka nini? Akauliza Elibariki
“Ninachokumbuka tukiwa pale uwanjani shughuli ikiendelea,alinifuata dada mmoja na kumiambia kwamba kuna mtu anahitaji kuniona katika gari la wagonjwa.Dada yule simfahamu lakini alikuwa amejitanda sare zilizovaliwa na akina mama pale msibani.Nikaongozana naye hadi tulipolikaribia gari la wagonjwa lililokuwa limeegeshwa pembeni ya uwanja mara nikahisi kizunguzungu na miguu ikaishiwa nguvu na macho yakashindwa kuona tena.Ninachokumbuka ni kwamba nilitaka kudondoka chini na watu Fulani wakanidaka na nilipozinduka nimejikuta hapa hospitali.Sielewi ni kitu gani kilinitokea na kunisababishia hali ile lakini nilikuwa mzima kabisa na sikuwa na tatizo lolote ”akasema Flaviana
“Pole sana mke wangu.Kwa sasa unajisikiaje?akauliza Elibariki
“Kwa sasa ninajisikia vizuri na madaktari wamesema hakuna tatizo hali yangu inaendelea vizuri na baadae nitaruhusiwa kurejea nyumbani nikapumzike” akasema Flaviana na mara daktari akaingia.Jaji Elibariki akamuuliza kuhusiana na kilichosababisha mke wake kupoteza fahamu ghafla
“ Tumempima lakini hatujaona tatizo lolote kila kitu kinafanya kazi vizuri.Inawezekana hali hii ikawa ilisababishwa na vitu vingine kama vile uchovu mwingi,msongo wa mawazo,n.k.Anatakiwa apate muda mwingi wa kupumzika .” akasema daktari na kuendelea kumpima Flaviana na alipohakikisha kila kitu kiko vizuri akatoka
“ Flaviana dada huyo aliyekwambia kwamba unahitajika katika gari la wagonjwa unaweza kumkumbuka ukimuona?
“ Ndiyo ! nikimuona lazima nitamkumbuka”
“ Alikueleza ni nani aliyekuwa anakuhitaji katika gari hilo la wagonjwa?
“ Hapana hakunieleza nilikuwa naitwa na nani lakini nilimuamini kutokana na na muonekano wake.”akasema Flaviana .Jaji Elibariki aliyekuwa amekaa kitandani pembeni ya mkewe akamtazama na kusema
“ Kuanzia sasa tafadhali usimuamini mtu yeyote yule ambaye humjui.Hata wale ambao unawafahamu kuwa nao makini sana.Dr Flora amefariki katika mazingira yenye utata mkubwa na mpaka hapo tutakapobaini ni akina nani waliosababisha kifo chake tunatakiwa tuwe makini sana”akasema Jaji Elibariki
“Unayoyasema ni ya kweli kabisa.Inanibidi kuwa makini sana “akasema Flaviana
“Ni nani lakini aliyekuwa anataka kuonana na Flaviana? Akajiuliza jaji Elibariki
“Suala hili linanipa mashaka sana.Nina wasiwasi sana na maisha ya mke wangu.Watu waliomuua Dr Flora wako ndani ya ikulu na hawatasita kufanya kila linalowezekana ili kujilinda wasijulikane.We’re in great danger.I have to talk to Mathew about this ”akawaza Elibariki akachukua simu yake na kumpigia Mathew lakini simu ikaita bila kupokelewa,akapiga tena bado haikupokelewa
********
John Mwaulaya alikuwa ameiweka mikono kifuani pake.Alionekana kuwa katika mawazo mengi
“Hali yangu inazidi kuwa dhaifu na ninafahamu kwamba sintopona ugonjwa huu lakini siko tayari kuja kuuliwa na mkono wa Dr Burke.Nina hakika Josh atafanikiwa kumuwahi kabla hajaniwahi. Nilifanya makosa makubwa kumpendekeza Osmund katika nafasi kubwa na kuwaacha vijana watiifu kama Josh.Endapo atafanikiwa kumuondoa Burke ,nitajitahidi kwa kila niwezavyo kabla pumzi zangu hazijakata kuhakikisha Josh anakuwa katika nafasi za juu kabisa ndani ya Team SC41”akawaza John na kumbukumbu zake zikamrejesha mbali
“ Bado naikumbuka siku ile nilipomuua seneta Joe Burke na yule rafiki yake mwanasiasa Elisante.Ni miaka mingi imepita lakini nahisi ni kama jana .” akawaza John Mwaulaya akafumba macho na kuikumbuka siku aliyofanya mauajiya seneta Joe Burke baba yake na Dr Burke
Kiza kimenza kutanda jijini Dar es salaam .Pilika pilika za jioni watu wakishughulika na usafiri wa kuwarejesha makwao ziliendelea kama kawaida.Katika hoteli ya Salama Spring hali ilikuwa ni ya utulivu mkubwa.Watu waliendelea kupata vinywaji chakula na kuburudika na muziki wa bendi
Saa mbili kasoro dakika nane ,gari moja aina ya Nissan Patrol ikapita katika geti la kuingilia hotelini hapo na kuelekea moja kwa moja katika maegesho.Haraka haraka mlango ukafunguliwa akashuka kijana mmoja na kuwahi kuufungua mlango wa mbele.Mtu mmoja mzee wa makamo akashuka na kuongozana na yule kijana kuelekea ndani ya hoteli.Huyu alikuwa ni Mr Elkisante kiongozi wa chama kikubwa cha siasa nchini ambaye amefika katika hoteli hii kukutana na seneta Joe Burke toka chama cha Republican cha nchini Marekani
Wakati Dr Elisante akiingia hotelini hapo hakuwa na habari kwamba kuna watu wanne waliokuwa wakimfuatilia.Akiwa ameongozana na mlinzi wake mmoja walielekea hadi katika chumba cha Seneta Burke
“ He’s in” John Mwaulaya akiwa amekaa katika sehemu ya baa akipata kinywaji akiwa amezungukwa na warembo wawili ,alitaarifiwa na kijana wake aliyekuwa amekaa ghorofa ya kwanza kuhusiana na kuwasili kwa Dr Elisante.Mara tu alipoipokea taarifa iIe John akainuka na kuwaomba wasichana wale waendelee kupata kinywaji na angerejea baada ya muda mfupi,kisha akatoka
Mara tu baada ya kuachana na wale warembo John akatoa simu na kumpigia mmoja wa vijana wake na bila kuchelewa kijana Yule akampa maelekezo
“ John ,nenda ghorofa ya pili ingia chumba namba 108,utakuta kila kitu tayari kimeandaliwa .Chumba cha Seneta Burke ni namba 123 ghorofa ya nne” akasema Scola muhudumu wa hoteli hii ambaye ni mmoja kati ya vijana wa John mwaulaya na ndiye alifanikisha mpango huu kwa kiasi kikubwa
Kwa mwendo wa kujiamini John akatembelea hadi chumba alichoelekezwa,akaangaza kama kuna mtu yeyote ambaye alikuwa anamfuatilia kisha akajitoma ndani ya ile chumba ambacho mlango wake ulikuwa wazi.Juu ya kitanda kuliwekwa suti nyeusi ,shati jeupe na tai nyekundu mavazi ambayo huvaliwa na wahudumu wa kiume wa hoteli hii.Haraka haraka akavua nguo zake na kuvaa zile sare za wahudumu akajitazama katika kioo alionekana kama kweli muhudumu wa hoteli .Ndani ya chumba kile kulikuwa na torori la kubebea vyakula na vinywaji lililokuwa na chupa kadhaa za vinywaji.Akaiweka bastora yake yenye kiwambo cha sauti chini ya kitambaa cheupe kilichofunika lile torori na kuanza kulisukuma akatoka na kupanda hadi ghorofa ya nne.Kila aliyekutana naye hakumtilia shaka hata kidogo kama si muhudumu wa hoteli ile.
John mwaulaya akafika hadi katika mlango wa chumba cha Seneta Burke akagonga na mlango ukafunguliwa na mlinzi wa Dr Elisante
“ Halow’ John akamsalimu yule muhudumu
“ Hallow ,nikuidie nini? Akauliza yule mlinzi
“ Nimeelekezwa nilete vinywaji katika chumba hiki” akasema John
“ Umeelekezwa na nani?
“ Kuna simu imepigwa na kuagiza vinywaji viletwe “ akasemaJohn. Mlinzi yule akamtazama John kwa makini na kumuomba asubiri palepale ili akamuulize bosi wake kama ni kweli vinywaji vimeagizwa.Kitendo cha kumpa mgongo John ni kosa kubwa alilolifanya yule mlinzi.Hazikupita hata sekunde tano kwa kasi ya ajabu John akaichukua bastora yake na kumiminia risasi mfululizo yule mlinzi ,ambaye alianguka chini .Haraka haraka John akaliingiza ndani lile torori la vinywaji na kufunga mlango.Chumba alichopanga seneta Burke kilikuwa na vyumba vitatu yaani sebule chumba cha chakula na chumba cha kulala.Sauti za watu wakijadiliana jambo zilisikika katika chumba cha kulia chakula.Hakutaka kupoteza muda akaufungua mlango ule kwa kasi na kujitoma ndani.Kitendo kile kiliwastua sana wazee wale waliokuwemo mle ndani.Kufumba na kufumbua bila hata kutamka neneo moja John akaanza kuifanya kazi iliyompeleka mle,aliwamiminia risasi wazee wale ,Seneta Joe Burke na DrElisante wakaanguka chini hawakuwa na uhai tena,Risasi nyingi zilizotoka katika bastora mbili za John zilizokuwa na viwambo vya sauti ziliwasambaratisha na kuwaharibu vibaya.Bila kupoteza hata sekunde moja John akakusanya makaratasi yote yaliyokuwapo pale mezani,akayapakia katika sanduku dogo akaenda chumbani na kuchukua kompyuta ndogo ya seneta Burke pamoja na kila kitu ambacho alikiona kinafaa kuchukuliwa halafu akaufunga mlango na kurejea katika chumba kile alichoacha mavazi yake akavua zile nguo za wahudumu wa hoteli akaziweka katika sanduku dogo na kuondoka.
“That’s how I killed seneta Burke.Baada ya miaka mingi kupita mwanae anakuja kulipiza kisasi,he’s coming to kill me”
Akawaza John Mwaulaya
TUKUTANE SEHEMU IJAYO……
No comments
Post a Comment