PENIELA (Season 1 Ep 30)
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Hatimaye walikata kona na kuingia katika jumba moja kubwa la ghorofa zipatazo nne lililozungukwa na miti mingi.Magari zaidi ya ishirini yalikuwa yameegeshwa katika maegesho kubwa iliyokuwamo ndani ya jumba hili.Kijana mmoja aliyevaa suti nyeusi akafika na kumfungulia mkono Penny na bila kujitambulisha akamuomba amfuate.Penny aliendelea kujiuliza mahala pale ni wapi .Akaendelea kumfuata yule kijana wakaanza kupanda juu ghorofani hadi walipofika ghorofa ya nne.Kote walikopita walikutana na watu kadhaa na wote wakiwa wamevalia suti.Kila mmoja alionyesha heshima kubwa kwa Peniela na kuzidi kumshangaza.Hakuwahi kufika mahala pale wala hakuna aliyemfahamu lakini wao walionekana kumfahamu na kumuheshimu sana.
“ Nimeletwa hapa kufanya nini? Mbona kila mtu ninayekutana naye anatoa heshima kubwa? Akajiuliza na mara Yule kijana aliyeongozana naye akasimama akaongea na mtu mmoja hivi pande la mtu.Mtu Yule akamsalimu penny kwa heshima kubwa halafu akamuomba amfuate.Penny akazidi kushangaa.
ENDELEA……………………
Kikao cha kamati ya kushughukikia mazishi ya Dr Flora kilikuwa kinaendelea katika makazi ya rais .kikao hiki kiliwashirikisha pia viongozi wa juu wa serikali akiwemo Dr Joshua rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.Mazishi ya mke wa rais yalipangwa kufanyika kijijini kwao Itogole mahala alikozaliwa.Wakati kikao kikiendelea katibu wa rais Dr Albert Kigomba akapigiwa simu akasimama na kutoka nje ya chumba na kuipokea.Baada ya kumaliza kuongea na simu ile sura yake ilionyesha wasi wasi mwingi.Akasimama na kufikiri kidogo akavuta pumzi ndefu halafu akamuendea rais.
“ Mheshimiwa rais ninaomba tuongee kidogo” akasema Dk Albert Kigomba .Dr Joshua akaomba samahani kidogo halafu akatoka nje .Wakajificha katika kona Fulani isiyokuwa na watu.
“ What is it Dr Kigomba ?akauliza Dr Joshua
‘ Mheshimiwa nimepokea simu sasa hivi toka kwa Brigedia Abasana anasema kwamba kuna madaktari wameingia katika chumba cha maiti hospitali kuu ya jeshi na mpaka sasa hawajatoka wanaufanyia uchunguzi mwili wa Dr Flora” akasema Dr Albert
“ What ?!!..Dr Joshua akahamaki.
“ Who are they? Akauliza Dr Joshua
“ Haijulikani ni akina nani lakini inasemekana wanaongozwa na kanali Adolf”
“ kanali Adolf?!!..Dr Joshua akashangaa
“Ndiyo kwa mujibu wa vijana waliowekwa kulinda katika kile chumba cha kuhifadhia maiti ha hospitali kuu ya jeshi ,Kanali Adolf aliongozana na madaktari wengine wameingia usiku huu ndani ya chumba cha maiti na wanafanya uchunguzi kwa mwili wa Dr Flora.”
“ Ouh my God !!!..akasema Dr Joshua huku akishika kichwa .Alihisi kuchanganyikiwa.Akainama na kuzama mawazoni
“ What are we going to do Mr President? Akauliza Dr Albert
“ Do something to stop them as quick as possible.Hakikisha wote wamekamatwa na hakuna yeyote atakayefanikiwa kutoroka.” Akaamrisha Dr Joshua na mara moja Dr Albert akasogea pembeni na kuanza kupiga simu.
Wakati Dr Albert akiongea na simu ,hakujua kama katika chumba cha karibu na pale alipokuwa amesimama ,kulikuwa na mtu akisikiliza kila alichokuwa akikiongea.Anna mtoto wa rais alikuwa amejipumzisha ndani ya chumba kile .Alistushwa sana kusikia Dr Albert akimuelekeza mtu kwamba ahakikishe madaktari wote wanaoendelea na uchunguzi kwa mwili wa Dr Flora wanakamatwa haraka sana.
“ Mwili wa mama unafanyiwa uchunguzi halafu madaktari wote wanaofanya uchunguzi huo wanatakiwa kukamatwa? Anna alistuka sana .
“ Kwa nini Dr Kigomba atoe amri ya kukamatwa madaktari wanaofanya uchunguzi kubaini kilichomuua mama? Kuna tatizo lolote katika kufanya uchunguzi huo? Je baba anafahamu kinachoendelea ? Something is going on.I have to see Flaviana” akawaza Anna halafu akaufungua mlango wa kile chumba alichokuwamo akatazama huko na huko kuhakikisha kwambahakuna mtu halafu akatoka na kuelekea katika vyumba vyenye watu kumtafuta dada yake, wakaenda sehemu isiyokuwa na watu
“ Anna kuna tatizo gani? Mbona umeniogopesha? Akauliza Flaviana
“ Sikuwa nikijisikia vizuri na sikutaka kusikia kelele za aina yoyote ile hivyo nikaenda kupumzika katika chumba cha kule mwisho ambacho alikuwa akikaa bibi na kwa sasa hakikaliwi na mtu.Wakati nimejipumzisha kule nikasikia Dr Kigomba akiongea na simu ,alikuwa akitoa maelekezo kwa mtu kwamba ahakikishe madaktari wote wanaofanya uchunguzi kwa mwili wa mama wakamatwe haraka sana kabla hawajaendelea na uchunguzi wao na asitoroke hata mmoja.Nilistushwa sana na maagizo yalenikajiuliza ni kwa nini wakamatwe wakati wanataka kufahamu kilichomuua mama? Flaviana kuna kitu hakiko sawa hapa.” akasema Anna na kumstua sana Flaviana ambaye alishika kichwa kwa mikono yake
“ Elibariki !! ..Flaviana akasema kwa mstuko huku akiichukua simu yake na kuzitafuta namba za simu za Elibariki akapiga.
“ Hallow Flaviana” akasema Elibariki baada ya kupokea simu
“ Elibariki uko wapi? Akauliza Flaviana.Elibariki hakujibu kitu akabaki kimya
“ Elibariki nakuuliza uko wapi mida hii? Bado Elibariki hakujibu kitu
“ C’mon Eli answer me where are you? akauliza Flaviana huku machozi yakimlenga
“ Niko..niko hapa..hospitali” akasema Elibariki kwa wasiwasi akitegemea maswali kutoka kwa mkewe akitaka kujua ni kwa nini alikuwepo pale hospitalini
“ Elibariki get out of there now!!!..” akasema Flaviana akifikiri kwamba mumewe alikuwapo katika hospitali kuu ya jeshi kufuatilia uchunguzi wa mwili wa Dr Flora
“ What ?!... Elibariki akashangaa
“ Eli,please get out of there now !! Achana na kila kitu unachokifanya,get out.Tayari wamekwisha jua mko hapo hospitali” akasema Flaviana kwa ukali
“ Whats going on flaviana” akauliza Elibariki huku akigugumia kwa maumivu aliyokuwa akiyasikia kichwani
“ Kuna amri imetolewa kwamba madaktari wanaoendelea na uchunguzi wa mama wakamatwe wote.Nina hakika uko pamoja nao tafadhali ondokeni mara moja.”akaonya Flaviana
“ Ahsante sana Flaviana kwa tahadhari,tunatoka sasa hivi” akasema Elibariki na kukata simu.Kijasho kikamtoka kwa mbali.Hakutaka kupoteza muda akampigia simu Mathew
“ Hallow Elibariki” akasema Mathew baada ya kupokea simu
“ Mathew uko wapi?
“ Niko hapa hospitalini tunaendelea na uchunguzi.Wewe uko wapi?
“ Mathew,get out of there now.Tayari mmekwisha fahamika mnachokifanya humo.Please you are in great danger” akasema Elibariki
“ Ok Thank you Eli” akajibu Mathew na kukata simu akawageukia wenzake.
“Guys we haveto stop everything,they know we’re here and the’re after us.Lets get out of here now !!” akasema Mathew.Wote mle ndani wakastuka sana.
“Please let’s get out of here.!! “akasema Mathew kwa ukali.
Kwa haraka Dr Michael akakata kipande kidogo cha ini akakiweka katika kimfuko kidogo cha nailoni halafu akachukua tena na sampuli za vitu alivyokuwa akivihitaji akaviweka katika vifuko vidogo vidogo .
“ Are we going to leave her like this? Akauliza Anitha
“ Lets go. We don’t have much time here ” akasema Mathew huku akitoa bastora moja na kumrushia Anitha .Yeye alikuwa na bastora mbili mkononi.Kwa tahadhari kubwa akaufungua mlango na kuchungulia nje hakukuwa na mtu yeyote .
“ Its clear ,lets go’ akawataarifu wenzake wakatoka .Kwa kupitia kioo kidogo cha dirishani Mathew akachungulia nje na kuwaona wale wanajeshi wawili waliokuwa wakilinda nje ya chumba cha maiti.Akamfanyia ishara kanali Adolf atangulie nje akaongee nao.Kanali Adolf akafungua mlango na kutoka nje.Akawaita wale wanajeshi wawili akaanza kuongea nao.Walionekana kama wanabishana kitu Fulani
“ It’s our chance now” akasema Mathew na kisha akamfanyia ishara Anitha ailenge kwa risasi taa kubwa iliyokuwa ikimulika eneo lile ili kupafanya mahala pale pawe na giza.Anitha akafungua mlango kidogo na kuilenga ile taa kwa kutumia bastora yenye kiwambo cha kuzuia sauti .Eneo lote likawa giza.Kitendo kile cha taa kuzimika ghafla kikawastua sana wale wanajeshi.Wakati wakishangaa kilichotokea, Ghafla Mathew na Anitha wakatokea na ndani ya sekunde kadhaa wanajeshi wale walikuwa wamelala chini hawakuwa na fahamu.Kanali Adolf alibaki akishangaa kwa namna wanajeshi wale walivyopigwa na kupoteza fahamu ghafla namna ile.
“ Hakuna muda wa kupoteza ,twendeni tuondoke.” Akaamrisha Mathew wakaanza kutembea kwa kasi .Walifika katika maegesho ya magari wakaingia katika gari la kanali Adolf na kuondoka kwa kasi.
“ Tunaelekea wapi? Akauliza kanali Adolf
“ Some where safe” akasema Mathew na kumuelekeza sehemu wanakoelekea.Umbali wa mita kadhaa wakakutana na gari tatu za jeshi zilizojaa wanajeshi.
“ Tungechelewa kidogo sana wangetukuta.Thanx to Elibariki” Akasema Mathew
“ Ulijuaje kama wanajeshi wanakuja? Akauliza Kanali Adolf
“ Tunapofanya kazi tunafanya kama timu” akasema Mathew
“ Who are you guys” akauliza Adolf .Hakuna aliyemjibu,safari ikaendelea.
*******
Bado Flaviana alikuwa ameiweka mikono kifuani kwa woga,alikuwa na mawazo mengi sana kuhusiana na usalama wa mume wake .
“ Flaviana ni kitu gani kinaendelea hapa? Shemeji Elibariki yuko wapi? Mbona hutaki kunieleza chochote? Akahoji Anna.Bado Flaviana alikuwa ameiweka mikono yake kifuani akimuomba Mungu amsaidie mume wake.
“ Ngoja kwanza Anna,nitakueleza kila kitu.” Akasema Flaviana huku akitazama simu yake kana kwamba kuna simu anasubiri apigiwe.Dakika zilizdi kwenda ikamlazimu azitafute namba za simu za Elibariki akampigia
“ Hallow Flaviana ,” akasema Elibariki
“ Elibariki mmeshaondoka hapo hospitali? Akauliza
“ Flaviana naomba unisubiri kidogo nitakupigia” akasema Elibariki na kukata simu
“ Flaviana, Elibariki anafanya nini huko hospitali? Kuna nini kinaendelea? Naomba unieleze tafadhali
“Ok Anna nitakwambia.” Akasema Flaviana halafu akafikiri kidogo na kusema
“ mama alifariki ghafla kabla hajatueleza jambo alilotaka kutueleza na mpaka sasa bado hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kuhusiana na nini kilisababisha kifo chake.Niliwasil
iana na daktari mmoja wa pale hospitali kuu ya jeshi ili kumuuliza nini sababu ya mama yangu kufariki ghafla akaniambia kwamba hawawezi kufanya uchungzui kubaini kitu gani kilimuua mama kwa sababu wamekatazwa kufanya hivyo.Hakuniambia ni nani aliyezuia uchunguzi ule usifanyike.Baada ya kufikiri sana nililazimika kumuomba Elibariki anisaidie kutafuta ukweli wa nini kilichomuua mama.Elibariki yeye ana watu wengi anaowafahamu ambao wanaweza kumsaidia kuutafuta ukweli.Aliondoka hapa jioni akaniambia kwamba anakwenda kushughulikia suala hilo.Nadhani walionekana na ndiyo maana taarifa zikafika hapa haraka na hivyo kutumwa kikosi kwenda kuwakamata.Anna kuna kitu kinaendela hapa ambacho kinafichwa kuhusiana na kifo cha mama”akasema Flaviana na kumstua sana mdogo wake
“ Ahsante sana Flaviana kwa kunifumbua macho.Unajua mimi sikuwa nikifikria kabisa kitu kama hicho.Ninafahamu mama alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu na niliamini ndicho kilichomuua.Taarifa hii uliyonipa imenistua sana.”
“ Ni kweli Anna,mama alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu na nisingekuwa na tatizo lolote kama kusingetolewa amri ya kuzuia mwili wake kufanyiwa uchunguzi kufahamu kilichosababisha afariki ghalfa namna ile.Ukumbuke kwamba kuna jambo ambalo alitaka kutueleza jioni ya siku ile.Ni kwa nini sababu ya kifo chake isijulikane? Kwa nini uchunguzi wa kifo chake unazuiwa? Kuna nini kinafichwa?akauliza Flaviana.Anna akainama akafikiri kwa muda na kusema
“ Ninakubaliana nawe Flaviana.Kama ni shinikizo la damu ndilo lililomuua basi hakuna sababu ya kuficha.Lakini kuzuai kabisa mwili wake kufanyiwa uchunguzi kubaini kilichosababisha kifo chake inatia shaka sana.Inaonekana wazi sababu ya kifo chake haitakiwi kujulikana.kwa nini isifahamike?
“ Hilo ndilo swali ambalo tunatakiwa tujiulize,ni kwa nini sababu ya kifo cha mama inafichwa?.Sisi ni watoto wake na tuna haki ya kufahamu kilichosababisha kifo cha mama yetu” akasema Flaviana
“Kwa hiyo Flaviana unafikiri nini?mama aliuawa? akauliza Anna
“Siwezi kusema moja kwa moja kwamba aliuawa lakini kwa mazingira yaliyopo yanajenga hisia hizo .Hii ni sababu iliyonifanya nimuombe Elibariki anisaidie kuufahamu ukweli wa jambo hili ili niweze kuondokana na duku duku nililonalo.Baad
a ya kupatikana kwa taarifa ya nini kilisababisha kifo cha mama,tutajua kama aliuawa ama kulikuwa na uzembe wa aina yoyote wa madaktari na wasaidizi wake.Mungu amsaidie Elibariki aweze kutoka salama na tuone kama anaweza kuwa amefanikiwa kupata chochote” akasema Flaviana
“ Flaviana umemuingiza shemeji Elibariki katika hatari kubwa.Endapo akikutwa huko hospitali lazima atafanyiwa kitu kibaya sana.”
“ Ni kweli Anna.Najutia uamuzi wangu wa kumtaka anisaidie kuutafuta ukweli.Nimemuweka mume wangu katika hatari kubwa sana.Lolote baya linaweza kumkuta” Akasema Flaviana kwa uchungu mwingi
“Flaviana unadhani baba atakuwa anafahamu chochote kuhusiana na suala hili? Akauliza Anna
“ Sina hakika kama analifahamu kwa sababu wakati mama anafariki dunia yeye alikuwa mkutanoni jijini Arusha na alipofika hapa tayari mama alikwisha pelekwa hospitali.” Akasema Flaviana
“ kwa maana hiyo haya mambo yalifanyika wakati baba akiwa hayupo,namaanisha taarifa hiyo ilitolewa wakati hata baba hajafika.Ninadhani kuna ulazima wa kumueleza baba ukweli wa hili jambo.Inawezekana akawa hafahamu chochote kinachoendelea.Yawezekana akawa amepewa taarifa zisizo za kweli” akashauri Anna.Flaviana akafikiri kwa muda na kusema.
“ Unashauri tumweleze baba?
“ Ndiyo.Ninadhani litakuwa ni jambo la busara kumueleza baba kuhusiana na kinachoendelea ili afahamu mambo yanayofanywa na watu wake wa karibu na ikiwezekana achukue hatua kulichunguza suala hili.Na hii inaweza kuwa njia nzuri ya kumsaidia Elibariki.Unaonaje kuhusu jambo hili?
“ Si vibaya ingawa nilipenda sana kulifanya jambo hili kwa siri lakini tufanye kama ulivyoshauri.Twende tukamuone baba tumueleze kuhusiana na suala hili” akasema Flaviana.
“ Ni mapema sana kufikiria hivyo lakini katika sehemu kama hizi kila kitu kinawezekana.Kwa muda wa miaka sita nimekaa ikulu na nimejifunza kitu kimoja kikubwa , kuutoa uhai wa mtu kwa ajili ya kulinda maslahi Fulani ya wakubwa au ya nchi ni kitu kidogo sana kwa hiyo japokuwa silipi uzito mkubwa suala la mama kuuawa lakini linawezekana kabisa kutokea na kama ikitokea ni hivyo,itakuwa ni kwa sababu nzito” akasema Flaviana.Baada ya kushauriana wakaondoka wakamfuata baba yao.Flaviana akaongea na mmoja wa walinzi wa rais akamuomba awaitie baba yao aliyekuwa ndani ya kikao.Mlinzi Yule akaingia ndani ya kile chumba ambacho kulikuwa na kikao kinachohusiana na mazishi ya Dr Flora akamtaarifu rais kwamba wanae wanahitaji kumuona.Dr Joshua akawaomba radhi wanakamati akatoka na kwenda kuonana na binti zake
“ Flaviana ,Anna kuna tatizo gani? Akauliza
“ Baba tunajua una mambo mengi kwa sasa lakini kuna suala la muhimu ambalo tumekuitia na tunaomba tukaliongelee katika chumba cha maongezi” akasema Flaviana .Dr Joshua akaongozana na wanae hadi katika chumba cha maongezi
“ Kuna tatizo gani Flaviana? Akauliza Dr Joshua
“ Baba kuna tatizo.Ni kuhusu kifo cha mama” akasema Flaviana na Dr Joshua akatikisa kichwa
“ Baba ,tumekuwa tukijiuliza maswali mengi sana kuhusiana na kifo cha ghafla cha mama ..Mpaka sasa hatuelewi nini kilisabisha kifo chake,hatujui kama ni shinikizo la damu ambalo lilikuwa likimsumbua kwa muda mrefu au ni kitu kingine. Mpaka sasa hatujapata ripoti yoyote kuhusiana na suala hilo.Kuna daktari mmoja pale katika hospitali kuu ya jeshi ninafahamiana naye ,nilimuuliza kama wanafahamu nini kilisababisha kifo cha mama alisema kwamba hawafahamu chochote kwa sababu walizuiliwa kutokufanya uchunguzi wowote katika mwili wa mama.Binafsi nilistushwa sana na taarifa hizo ingawa hakunieleza ni nani aliyetoa amri hiyo.Baada ya kufikiri sana nikaamua kutumia njia zangu mwenyewe kuutafuta ukweli wa suala hili na ndipo niliposhirikiana na Elibariki kutaka kujua nini sababu ya kifo cha mama.Baba tumegundua kwamba wasaidizi wako wanakuzunguka.Kuna mambo ambayo huyafahamu kuhusia na kifo cha mama.Kuna mambo ambayo hujawekwa wazi.Usiku huu katibu wako Dr Kigomba amesikika akitoa amri kwamba madaktari walioko katika uchunguzi wa kifo cha mama wakamatwe na washughulikiwe haraka sana.Miongoni mwa watu waliomo ndani ya chumba hicho cha uchunguzi ni mume wangu Elibariki ambaye tunashirikiana naye kuutafuta ukweli.Kwa nini wazuiwe kufanya uchunguzi wa kifo cha mama? Tumeona tukuite na tukufahamishe kuhusiana na suala hili ili kwanza uwazuie watu waliotumwa kuwakamata madaktari aho ambao miongoni mwao yumo Elibariki na waachwe waendelee na uchunguzi wao na pili suala hili ulifanyie uchunguzi wa kina ” akasema Flaviana.Dr Joshua akainama akafikiri kwa muda na kusema
“ Nawashukuruni sana wanangu kwa taarifa hizi ambazo hata mimi zimenistua sana.Sikuwa nikifahamu chochote kilichokuwa kinaendelea .Kama ulivyosema Flaviana ni kweli yawezekana nimefichwa mambo mengi.Niachieni suala hili nilifanyie uchunguzi.Kuhusu sababu ya kifo cha mama yenu nimekwisha zungumza na madaktari wa kutoka hospitali kuu ya taifa na wataufanyia uchunguzi mwili wa mama yenu kesho asubuhi na tutapewa ripoti ya nini kilisababisha kifo chake.Kuhusu uchunguzi huo ulioufanya kwa siri ni jambo zuri lakini ulitakiwa kunifahamisha mapema ili nifahamu na pengine tungeweza kushirikiana kuutafuta ukweli.Kumuacha Elibariki kwenda peke yake kufanya uchunguzi wa jambo hili ni hatari kubwa.Lazima atakuwa hatarini na hata taarifa anayoweza kuipata inaweza isiwe sahihi na ndiyo maana nimeomba timu ya wataalamu kutoka hospitali kuu ya taifa wakafanye uchunguzi na kutupa ripoti sahihi.Msiwe na wasi wasi wanangu kesho tutafahamu kila kitu kuhusiana na nini kilimuua mama yenu.Kuhusu Elibariki nitawasiliana na wakuu wa jeshi ili kufahamu kinachoendelea hapo hospitali na kama atakuwa amekamatwa nitaamuru aachiwe.kwa sasa naombeni mkapumzike na mniachie suala hili nilifanyie kazi.Nina njia nyingi za kuupata ukweli na kama kuna jambo lolote ambalo limefanywa na watendaji wangu nitawaeleza .Ila nawashukuru sana kwa taarifa mlizonipa.Ninafurahi sana kwa kujaaliwa watoto wenye akili nyingi kama nyie.” Akasema Dr Joshua .Flaviana na Anna wakaondoka
Dr Joshua akavuta pumzi ndefu baada ya wanae kutoka mle chumbani.Alibaki ameegemea kiti chake akiwaza.mambo aliyoambiwa na watoto wake yalimstua sana
“ Tayari wameanza kuhisi kitu.This is too dangerous.We have to act so quick to stop any suspicious.Dr Kigomba is very stupid.Suala hili amelifanya kizembe sana hadi watu wameanza kustuka..” Akawaza Dr Joshua.
“ Nimestuka sana ,sikutegemea kabisa kamaFlaviana na Anna wanaweza wakahisi chochte kuhusiana na kifo cha mama yao.Mambo yameanza kuharibika na endapo Elibariki na timu yake watakuwa wamefanikiwa kugundua lolote I’m finished.lazima atamweleza mke wake na wanangu wakigundua kama mama yao aliuawa sijui nitawaeleza kitu gani” akawaza Dr Joshua na kuchukua simu yake akampigia simu Captain Amos daktari mkuu wa familia pamoja na katibu wake Dr Kigomba akawaomba wakutane mara moja ofisini kwake.Aliwataka radhi watu waliokuwa kikaoni kwamba amepatwa na dharura na moja kwa moja akaelekea ofisini kwake..Kichwa chake kilijaa mawazo mengi.Suala aliloambiwa na wanae lilimstua mno
Baada ya kuachana na baba yao Flaviana akampigia simu mumewe Elibariki lakini simu yake haikuwa ikipatikana.Hofu ikamjaa
“ Nina wasi wasi sana na usalama wa Elibariki.Sina hakika kama waliwahi kutoka mle ndani kabla wanajeshi hawajawakuta.If anything happens to him I’ll never forgive myself.Mimi ndiye chanzo cha haya yote.Ee Mungu mlinde mume wangu asipatwe na jambo lolote baya na arejee salama” akaomba Flaviana akiwa amejifungia chumbani akilia machozi.
Dr Joshua aliwasili ofisini kwake na kuwakuta tayari Kaptain Amos na Dr Kigomba wamekwisha fika.Bila kuchelewa kikao kikaanza
“ Dr Kigomba kuna ripoti yoyote kutoka hospitali? Akauliza Dr Joshua
“ Nimepokea taarifa wakati nakuja huku ofisini kwamba hawakufanikiwa kumkamata mtu yeyote.Askari waliokuwa wakilinda eneo lile wamekutwa wakiwa hawana fahamu,vile vile mwili wa Dr Flora umekutwa ukiwa katika chumba cha uchunguzi,na inaonekana watu waliokuwa wakifanya uchunguzi ule walipewa taarifa na mtu aliyeko nje na kwa haraka wakaacha kazi ile waliyokuwa wakiifanya wakakimbia.Lakini hakuna uhakika kama wamepata walichokuwa wanakitafuta kwa sababu shughuli ile ilihitaji muda wa kutosha na wao walikimbia wakati kazi bado haijamalizika.Hata hivyo bado msako unaendelea kumsaka Kanali Adolf ambaye inasemekana ndiye aliyeongoza kundi hilo la madaktari waliojaribu kufanya uchunguzi huo.” Akasema Dr Kigomba .Dr Joshua akakuna upara wake
“ Sasa ndugu zangu sikilizeni,kuna mambo ambayo yanahitajika kufanywa kwa haraka sana.Kaptain Amos you did your job well lakini kazi yako inataka kuharibiwa na uzembe unaofanywa na Dr Kigomba .” Dr Joshua akamgeukia Dr Kigomba
“ Kigomba how could you do such a stupid things ? Unafahamu kabisa jambo hili ni nyeti na la hatari lakini bado hauko makini.Umesikika usiku huu ukipiga simu na kutoa amri kuwa madaktari wakamatwe,bila kujali mahala ulikokuwa umesimama kuna mtu anakusikilza.Mambo kama haya ni ya siri na unatakiwa ufanye kwa siri kubwa.Sasa hata watoto wangu wameanza kuhoji kuhusu nini kimemuua mama yao.Wanataka kupata ripoti ya daktari .Katika watu waliokuwamo mle wakifanya uchunguzi na mume wa mwanangu alikuwemo pia.Hii ilitokana na kuingiwa na shaka .Sina hakika kama watakuwa wamefanikiwa kufahamu kilichomuua Flora lakini endapo wakifanikiwa kujua,litakuwa ni anguko letu vinginevyo itatulazimu kufanya maamuzi magumu sana ili tuendelee kubaki salama.Kwa kuwa bado hatujui ni kitu gani wamekigundua hao madaktari kuna mambo ambayo lazima tuyafanye.Kwanza kesho asubuhi Kaptain Amos utashughulikia ripoti ya uongo ya kuhusu kifo cha Flora ripoti ambayo nitawaonyesha wanangu ili waridhike kwani nimewadanganya kwamba uchunguzi utafanyika kesho.Pili Mwanangu Flaviana anatakiwa aanze kuchunguzwa sana nyendo zake.Yeye ndiye atakayetupeleka mahala aliko mumewe Elibariki na tukimpata Elibariki tutakuwa tumewapata wengine wote walioshiriki katika jambo hili.Nataka mpaka kufika kesho asubuhi niwe nimepata ripoti kuhusiana na jambo hili.Kwa hiyo kuanzia sasa hakutakuwa na kulala.We’re going to work day and night to make sure we’re safe.You’ve messed it now you’ll have to fix it.!! Akasema kwa ukali Dr Joshua
TUKUTANE SEHEMU IJAYO……………
No comments
Post a Comment