PENIELA (Season 1 Ep 28)

 ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

Anitha ambaye alifika mara moja na kompyuta yake,na kuweka chombo fulani karibu na Dr Mathew halafu akamwambia aipokee na aweke sehemu ya kuongelea kwa sauti kubwa ili wote wasikie

“ Hallow”akasema Dr Michael

“ hallow Dr Michael,uko wapi?

“ Nimetoka kazini niko mahala nimepumzika nasubiri maelekezo yenu”

“ ok vizuri.Endelea kusubiri tutakupigia tena baadae kidogo.Nakukumbusha kwamba tunakufuatilia kila unachokifanya,ukithubutu kwenda polisi au kumwambia mtu yeyote Yule basi mkeo hutamuona tena.Tumeelewana Dr Michael?

“ Tumeelewana.Tafadhalini naomba msimdh..” kabla hajamaliza alichotaka kukisema simu ikakatwa

“ Umefanikiwa Anitha? Akauliza Mathew

“ Hapana,simu imewahi sana kukatika ,sijapata chochote”

“ Ok hakuna tatizo tutaendelea kusubiri maelekezo yao.Mmepata chochote katika kamera?

“ Tumegundua kwamba kuna wakati kamera iligeuzwa na kuelekezwa sehemu nyingine.Nadhani walifanya hivi ili waweze kutoka bil akuonekana katika kamera, walipotoka kamera zilirudi kama kawaida .” akasema Anitha

“Team SC41 ni watu hatari sana,muda wote wanafanya mambo yao kwa tahadhari kubwa” akasema Mathew.

ENDELEA……….

Mathew akawaacha wenzake na kuelekea chumbani kwake,akakaa juu ya kitanda akazama mawazoni.

“ Vitani tena na Team SC41” akawaza

“ Bado sijausahau usiku ule walipowaua wenzangu wote .Bado picha ya usiku ule haijafutika kichwani kwangu.Bado picha ya moto ule mkubwa ulioteketeza nyumba na familia yangu inanijia kichwani kila siku,nahisi kama ninasikia vilio vya mke wangu n wanangu wakiteketea katika moto mkubwa.Siku ile furaha yangu yote ya maisha ilipotea.Ni muda sasa wa kulipa kisasi.Damu ya watu wangu inanililia ikitaka niwalipie kisasi.Lazima nilipe kisasi.” Mathew akapatwa na uchungu sana alipoikumbuka picha ya usiku ule mbaya kuliko yote katika maisha yake.

“ Bado najiuliza sana kuhusiana na jambo alilonieleza Jaji Elibariki kuhusu kifo cha mke wa rais.Inawezekana akawa aliuawa? Kama aliuawa ni kwa nini? Na nani alimuua? Akajiuliza

“ Kuna haja ya kufanya uchunguzi wa suala hili ili kufahamu kilichomuua Dr Flora.Lakini ni namna gani tutaweza kuufanya uchunguzi huo? akajiuliza .Akainama akawaza halafu akachukua simu na kuzitafuta namba Fulani akapiga

“ Hallow Neema” akasema Mathew baada ya simu kupokelewa

“ hallow Mathew,habari ya siku nyingi? Mbona umeadimika kiasi hicho?

“ Mimi nipo Ney.Sionekani mara kwa mara nimetingwa sana na kazi.Maisha yanakwendaje?

“ Namshukuru Mungu maisha yanakwenda vizuri sana.”

“ Nafurahi kusikia hivyo.Kuna zawadi yako nimekuletea toka Ufaransa”

“ wow ! ahsante sana Mathew.Kila mara huwa husahau kunikumbuka kwa zawadi.”

“ Siwezi kukusahau Ney.Najua wewe ni mrembo na unapenda vitu vizuri kwa hiyo kila niwapo safarini na kukutana na kitu kizuri huwa nakukumbuka sana”

“ Ahsante sana Mathew,nashukuru.Nikufuate nyumbani nije niichukue zawadi yangu? Akauliza Neema

“ Nitaipeleka ofisini kwako utaikuta pale.” Akasema Mathew

“ Mhh..haya ! akasema Neema.Kikapita kimya kifupi Mathew akasema

“ Neema kuna jambo nataka kukuuliza”

“ Mhh nilijua tu,ukianza mambo ya zwadi lazima utakuwa na shida inayohitaji msaada wangu.haya sema una tatizo gani?

“ Naomba unisaidie kutafuta ni nani daktari mkuu katika hospitali kuu ya jeshi” akasema Mathew

“ Ok Mathew,naomba unipe dakika tatu nitakupigia”akasema Neema na kukata simu

“Neema ni binti ambaye amekuwa akinisaidia sana kupata taarifa mbali mbali,safari hii lazima nimtafutie mkufu wa dhahabu,anapenda sana dhahabu” akawaza Mathew.Baada ya dakika kama tano hivi simu ikaita alikuwa ni Neema

“ Mathew ,daktari mkuu wa hospitali ya jeshi ni Kanali Adolf mubaya.”

Mathew akastuka sana kwa kulisikia jina lile

“ Unasema Kanali Adolf Mubaya? Akauliza

“ Ndiyo.”akajibu Neema.Kikapita kimya kifupi

“ Mathew ,kuna nini kwani? Akauliza Neema

“ naomba unisaidie kufahamu kanali Adolf anaishi wapi?

“ Anaishi katika nyumba za maafisa wa jeshi Kigamboni.Nyumba yake ni namba 54.” Akasema Neema

“ Ok ahsante sana Neema.Nitakutumia mzigo wako baadae”

“ Ahsante sana Mathew.”akajibu Neema na kukata simu

“ Kanali adolf” akasema Mathew baada ya kumaliza kuongea na Neema,akatoka na kuelekea katika chumba walichokuwamo Anitha na Noah

“ Kuna jambo nimelipata sasa hivi.Daktari mkuu wa hospitali kuu ya jeshi ni kanali Adolf Mubaya” akasema

“ Do you know him? Akauliza Anitha

“ Yes I know him” akajibu Mathew

“Who is he? akauliza Noah

“ Simfahamu kiundani sana lakini nilimfahamu wakati nikiwa katika operesheni fulani.Kuna watu nilikuwa nikiwafuatilia ikanilazimu kufanya kazi kama meneja wa baa”

“ hahahaa..! Anitha akacheka

“ Kumbe uliwahi kuwa meneja wa baa?

“ Yah ! Ilinilazimu kuwa meneja wa baa moja maarufu sana.Baa hiyo inamilikiwa na Eva mwabukuku ambaye ni kachero wa siri wa idara ya usalama wa taifa.Wakati nikiwa katika baa ile ndipo nilipomfahamu Kanali Adolf .Alikuwa akifika pale kila siku kuanzia mida ya saa tano na kukaa hadi mida ya saa saba za usiku .Alikuwa akifika pale kufuata wanawake wanaojiuza.Si yeye tu bali hata watu wengine wakubwa wakubwa walikuwa wakifika pale kwa siri wakifuata huduma hiyo.Ninamfahamu Kanali Adolf kwa matumizi makubwa aliyokuwa akiyafanya.Kwa kuwa si yeye niliyekuwa nkimfuatilia sikutaka kumchunguza lakini kwa mujibu wa Eva,Kanali Adolf anajipatia fedha zake kutokana na miradi mbali mbali anayoifanya kwa siri.Kwa muda niliokaa pale niliwafahamu watu wengi hususani viongozi wakubwa waliokuwa wakifika pale kumwaga hela na makahaba.Eva Mwabukuku ni rafiki yangu sana na nimewahi kumsaidia sana huko nyuma ,yeye anawafahamu wakubwa wengi,anazifahamu siri zao nyingi kwani yeye ndiye ambaye huwa anawaunganishiwa wasichana wale makahaba,nina hakika hata kanali Adolf atakuwa akimfahamu kiundani.Nitaka kutafuta jambo ambalo litamfanya Kanali Adolf akubali kuifanya kazi yetu kwa usiku wa leo ”

“ Una hakika huyo Eva anaweza akakubali kukupa siri za Kanali Adolf? Akauliza Noah

“ Eva ni rafiki yangu sana ingawa kwa muda mrefu hatujaonana lakini ninazo namba zake za simu za siri katika kitabu changu cha kumbu kumbu ngoja nikazitafute nimpigie “ akasema Mathew na kurejea chumbani kwake akafungua kabati la ke analohifadhi nyaraka zake muhimu akatoa kitabu fulani ambacho huandika kumbukumbu zake mbali mbali za muhimu na kuzitafuta namba za simu za Eva Mwabukuku akazipata

Haraka haraka akaziandika namba zile katika simu yake akapiga simu ikaita

“ Hallo Zombie,are you back from hell? Ikauliza sauti ya upande wa pili na kumfanya Mathew acheke kicheko kikubwa.

“ I’m back Eva,I’m back” akasema Mathew

“ Welcome back.Umepotea sana Mathew.Its been years.How are you?” Akasema Eva

“ kweli Eva,umekuwa ni muda mrefu sana hatujaonana,maisha yanakwendaje?

“ Maisha yanakwenda vizuri sana .Vipi wewe,unaendeleaje?

“ Ninaendelea vizuri Eva.” Akasema Mathew na kukaa kimya kidogo.

“ Eva ninahitaji kukuona nina shida kidogo nahitaji msaada wako” akasema Mathew

“ Mathew hata mimi nina hamu sana ya kukuona.Uliponipigia simu sikuamini .Umekuja kwa wakati muafaka wakati ambao nakuhitaji sana.Njoo hapa pub utanikuta.” akasema Eva

“ Ok ninakuja hapo muda si mrefu” akasema Mathew na kukata simu halafu akawafuata wenzake

“ Nimeongea na Eva,amesema nimfuate katika baa yake ananisubiri.Nina hakika kwa Eva lazima kuna jambo nitalipata.Yule ana siri nyingi sana za watu wengi.Anitha jiandae twende,Noah utabaki na Dr Michael.” Akasema Mathew halafu akaingia chumbani kwake kujiandaa kisha akamfuata Dr Michale aliyekuwa amejiinamia sebuleni

“ Dr Michael ninatoka kidogo kuna sehemu ninahitaji kwenda ,nitarejea baada ya muda si mrefu sana.kama jamaa wakipiga simu utanifahamisha nini wamesema” akasema Mathew.Dr Michael akaonyesha wasi wasi

“ sasa itakuaje jamaa wakipiga simu na haujarejea? Akauliza Dr Michael.

“ Yupo Noah na chochote watakachosema atanifahamisha.Usihofu kitu Dr Michael kila kitu kitakwenda vizuri.Niamini ninachokwambia tutampata mkeo” Akasema Mathew halafu akaongozana na Anitha wakatoka na kuingia garini safari ya kuelekea kwa Eva ikaanza..

“ Mathew umenifurahisha sana leo,hukuwahi kuniambia kama uliwahi kufanya kazi baa.” Akasema Anitha Mathew akatabasamu na kusema

“ Yah ! hakukuwa na ulazima wowote wa kukueleza.Hiyo ni historia yangu ya zamani sana ambayo nimekwisha isahau.” Akasema Mathew

“ Huyu Eva,una hakika anaweza akatusaidia kupata taarifa za kanali Adolf? Akauliza Anitha

“ Nina uhakika asilimia mia moja .Kama anazo taarifa zozote za kumuhusu Kanali adolf basi atanipatia.Hakuna namna tnayoweza kufanya uchunguzi wa mwili wa Dr flora bila ya kumtumia Adolf.Ile ni hospitali ya kijeshi kwa hiyo kuingia pale na kufanya tunachokitaka si kazi rahisi ingawa tunaweza kufanya hivyo lakini hatuna muda wa kutosha hivyo inatulazimu kutafuta njia ya mkato ya kuweza kulifanikisha suala hili” akasema Mathew

“ na vipi kuhusiana na Team SC41? Bado hujatupa maelekezo yoyote ya nini kinaendelea na nini tufanye.”

“ kwa sasa tunasubiri maelekezo atakayopewa Dr Michael na ndipo tutajua nini cha kufanya.Watu hawa ni hatari kwa hiyo tunatakiwa kuwaendea kwa tahadhari kubwa sana.” Akasema Mathew

“ Mauaji ya Edson ,yanahusiana vipi na Team SC41? Usinielewe vibaya Mathew ila ninauliza hivyo kwa sababu naona kama vile tumehama katika kazi yetu ya msingi na kwa sasa tumehamia kwa team SC41” akauliza Anitha.Mathew akatabasamu na kusema

“ Bado hatujatoka katika shughuli yetu ya msingi Anitha.Bado tunaendelea kuchunguza kifo cha Edson lakini team SC41 wameingia katikati ya uchunguzi wetu baada ya kuonekana nyumbani kwa peniela hivyo lazima tuwachunguze.Tunachunguza Peniela ana mahusiano gani na Team SC41? Tukifahamu mahusiano yao tutajaribu kuangalia kama kuna muunganiko wowote kati ya mauaji ya Edson na Team Sc41” akasema Mathew.

“ Kwa nini tusimchunguze peniela moja kwa moja ili tufahamu mahusianoyake na Team Sc41? Akauliza Anitha

“ Peniela kuna namna yake ya kumchunguza.Tutamfanyia uchunguzi tu lakini ngojakwanza tushughulike na masuala mawili yaliyoko mbele yetu kwanza halafu tutarejea kwa Penny” akasema Mathew.Wakaende

lea na maongezi mengine hadi walipofika katika baa inayomilikiwa na Eva mwabukuku.Mathew akatabasamu baada ya kuiona tena baa ile.

“ Imebadilika sana baa hii.Imeboreshwa mno.” Akawaza huku akitabasamu.Alikumbuka mbali sana.

“ Ndani ya baa hii nimeshuhudia mambo mengi sana yakifanyika na mengi yakiwa ni ya aibu hata kuyasimulia” akawaza huku akifungua mlango na kushuka akampigia simu Eva akamfahamisha kwamba tayari amekwisha fika.Baada ya dakika tatu Eva akatokea.Alikuwa ni mwanamma mwenye umbo la kuvutia mno.Wakakumbatiana kwa furaha ya kutoona kwa muda mrefu

“ Ouh Mathew,karibu sana.” Akasema Eva.Mathew akamtambulisha Anitha kwa Eva halafu wakaongozana kuelekea ndani Anitha akakaribishwa katika meza ya pembeni kabisa akapewa muhudumu wa kumuhudumia,Mathew na Eva wakaelekea ofisini..

“ Mathew siwezi kukuficha nimefurahi sana kukuona tena.Wewe ni mmoja wa watu ambao nilihitaji sana kuwaona.Nimefurahi sana kwa kweli.Umenawiri mno inaonekana mambo yako si mabaya siku hizi” akasema Eva

“ hata mimi nimefurahi sana kukuona tena stone lady.Hata baada ya miaka kadhaa kupita lakini bado umenawiri na unazidi kupendeza.Hongera sana naona baa yetu inaendelea vizuri,imeboreshwa mno siku hizi” akasema Mathew

“ Kwa kweli ninamshukuru sana Mungu kwani ninaendelea vizuri sana na ndiyo maana unaona mabadiliko makubwa.” Akasema Eva

“ Eva nina mambo mengi mno ambayo nahitaji kuongea nawe lakini itahitajika siku nzima.Kwa jioni hii nimekuja kwako ninahitaji msaada wako.” Akasema Mathew

“ Karibu sana Mathew.Hapa kwangu umefika na nitakusaidia chochote unachotaka” akasema Eva

”Nafurahi kusikia hivyo “ akasema Mathew

“ Ni msaada gani unauhitaji Mathew “ akauliza Eva

“ Kuna mwili wa mtu ambao nahitaji kuufanyia uchunguzi kujua sababu za kifo chake.Mwili huo uko katika hospitali kuu ya jeshi na kama unavyojua mahala pale hapaingiliki kirahisi na kuingia pale kwa nguvu unakuwa umetangaza mgogoro na jeshi.Nahitaji kutumia njia rahisi isiyokuwana tatizo wala kuniingiza katika mgogoro wa aina yoyote na chombo hiki cha usalama” akasema Mathew

“ Nimefuatilia nimegundua kwamba kanali Adolf ndiye daktari mkuu wa ile hospitali kwa hiyo ninataka kumtumia yeye.Nimekuja kwako kwa kuwa wewe unawafahamu watu wengi,una siri za watu wengi hasa hawa wakubwa kwa hiyo ninahitaji kupata taarifa Fulani ya kanali Adolf ambayo ninaweza kuitumia kumlazimisha afanye kazi ninayoihitaji ya kuifanyia uchunguzi maiti hiyo.” Akasema Mathew

“ Mathew natamani sana kukusaidia kwa hilo lakini nasikitika kwamba sina taarifa zozote za kumhusu Kanali Adolf” akasema Eva

“ Eva nimekuja kwako kwa kuwa ninafahamu wewe hukosi kitu chochote cha kunisaidia.Tafadhali naomba unisaidie ni muhimu mno kwangu.Please Eva don’t shut me down on this.” Akaomba Mathew.Eva akainama akafikri kidogo kisha akasema

“Mathew wewe ni mtu wangu wa karibu sana.Tumefanya kazi pamoja na tumesaidiana katika mambo mengi kwa hiyo nitakusaidia lakini kwa sharti moja tu.”

“ Sharti gani Eva?

“Kuna kazi ambayo na mimi nitaomba unisaidie”

“ usijali Eva,niko tayari kukusaidia katika kazi hiyo .I give you my word.Tafadhali nisaidie kwanza katika hili”akasema Mathew

“ Ok Mathew nitakusaidia.Kanali Adolf siku hizi hafiki tena hapal,Lakini pamoja na kukata kabisa mguu baada ya mambo yake kuanza kwenda vizuri ninafahamu mambo yake mengi.Moja ninalolifahamu ambalo watu wengi hawalifahamu ni kwamba Kanali Adolf ni mshirikina wa kutupwa na Ili mambo yake yaende vizuri alikwenda kwa mganga na akaambiwa kwamba atafute viungo vya mlemavu wa ngozi.Binti mdogo wa miaka kumi na mitano alitolewa mkoani Geita akaletwa hapa Dar es salaam,akachinjwa na kuchukuliwa viungo vyake na kisha akazikwa katika nyumba yake mpya aliyohamia hivi sasa.Mahala alipozikwa kumepandwa mnazi.Ninayafahamu madhambi yake mengi lakini hilo tu linaweza kumfanya akafanya kila unachokitaka.Mathew nimekwambia siri hii kwa sababu wewe ni mtu wangu wa karibu na ninafahamu umekuja kwangu unahitaji mno msaada.Sasa na mimi ninaomba nikwambie kazi ninayohitaji unisaidie”

“ Sema Eva ni kazi gani unahitaji msaada?

“ Kuna msichana mmoja ambaye amepotea katika mazingira ya kutatanisha sana na mpaka sasa hajulikani alipo.” Akasema Eva.Mathew akatabasamu na kumtania

“ siku hizi umeanza kufanya kazi za polisi Eva? Kutafuta watu waliopotea ni kazi ya jeshi la polisi.” Akasema Mathew

“ Si hivyo Mathew,suala hili liko tofauti.Msichana huyo anaitwa Sabina .Alikuwa akija hapa mara kwa mara akiwa na mzee mmoja hivi aliyekuwa akifanya biashara.Mzee Yule alifariki katika mazingira ya kutatanisha sana na baada ya wiki moja Sabina akapotea.Hakukuwa na taarifa zozote za kupotea kwake.Jana nilipigiwa simu na namba ngeni kabisa nikapokea nikaisikia sauti ya Sabina.Alikuwa akilia na kuniambia kwamba nimsaidie kumuokoa amefungiwa ndani ya chumba kwa miezi saba sasa.Nikamuuliza yuko wapi na ni akina nani waliomfungia ndani ya chumba hicho akaniambia kwamba ametekwa na watu wasiojulikana .Kabla hajaendelea kunieleza zaidi nikasikia amenyang’anywa simu ikazimwa.Sifahamu yuko wapi na kwa nini amekamatwa na watu hao waliomfungia ndani kwa kipindi chote hicho.Nimechang

anyikiwa na sijui ni namna gani nitaweza kumuokoa kwa sababu sielewi yuko wapi .Laiti ningefahamu yuko wapi ingekuwa rahisi kidogo lakini sifahamu mahala aliko na sikuona mtu mwingine wa kumshirikisha katika suala hili ambaye anaweza kunisaidia..Uliponipigia simu nilimshukuru Mungu sana.Mathew please help me I need to save that girl.Najua kuna sababu iliyopelekea msichana Yule akakamatwa na kufungiwa ndani.We need to find her” akasema Eva

“ Ok Eva,nakuahidi nitafanya kila linalowezekana kumtafuta msichana huyo na kumpata ila kwa sasa naomba unisaidie katika suala hili nililokwambia’”

“ Nimekwisha kusaidia Mathew kama ulivyokuwa ukihitaji.Nimekupa tarifa ambayo itamfanya Adolf atii kila utakachomwambia”

“ Nashukuru sana kwa hilo Eva lakini bado naomba unisadie tena kitu kingine”

“Kitu gani Mathew? Akauliza Eva

“ Natumai una mawasiliano na Kanali Adolf.Naomba uwasiliane naye na umuombe mkutane.Najua kwako wewe hawezi kukataa.Mimi kum,pata kwa sasa itanichukua muda mrefu kidogo”

Eva akainama akafikiri kidogo halafu akachukua simu yakena kuzitafuta namba za simu za Kanali Adolf akampigia

“Hallow Adolf,habari yako? Akasema Eva baada ya Kanali Adolf kupokea simu

“ ouh Eva.habari za siku nyingi?

“ habari za siku nyingi nzuri sana,umenikimbia siku hizi.Toka mambo yako yalipokuwa mazuri hata sisi watu wako wa zamani hututaki tena”

“ Si hivyo Eva.Unajua nimetingwa sana na kazi siku hizi na ndiyo maana umeona sifiki mara kwa mara hapo kwako” akasema kanali Adolf

‘ Kanali adolf uko wapi mida hii?

“ kwa sasa niko barabarani kuna sehemu naelekea “

“ Ok ninahitaji kukuona nina shida Fulani”

“ una shida gani we mtoto? Akauliza kanali Adolf

“ Ni shida ambayo siwezi kukueleza simuni.Tafadhali naomba uje hapa ofisini kwangu au nielekeze ulipo nikufuate .Ni muhimu sana”

Kanali Adolf akakaa kimya kidogo halafu akasema

“ Ok ! siko mbali sana na hapo ofisini kwako ,nisubiri kama dakika tano hivi nitakuwa hapo lakini sintakaa sana kuna mahala ninahitajika usiku wa leo” akasema Kanali Adolf

‘ Nashukuru sana Adolf” akasema Eva na kukata simu.

“ Ndani ya dakika tano Adolf atakuwa hapa.sasa niambie utanisaidiaje kumpata msichana Yule ? akauliza Eva

“ Usihofu kuhusu kumpata huyo msichana Eva.Mimi na timu yangu tutampata tu.Tukishamaliza suala hili tutageukia suala lako.I give you my word Eva tutampata huyo msichana aliyepotea” akasema Mathew

“Nitashukuru sana kama utanisaidia kumpata.Msichana Yule anahitaji msaada na hana mtu mwingine wa kumkimbilia zaidi yangu.”akasema Eva na kuchungulia dirishani akaliona gari la kanali Adolf likiingia katika maegesho

“ kanali adolf ameingia kama alivyoahidi.Ni kweli hakuwa mbali na hapa” akasema Eva

“ Ahsante sana Eva.”akasema

Baada ya kama dakika mbili hivi mlango ukagongwa.

“ Its him”akasema Eva huku akiinuka na kwenda kuufungua mlango

“ Ouh Adolf ! karibu sana.” Akasema Eva kwa furaha

“ Ahsante sana Eva.Habari za siku nyingi? naona umefanya mabadiliko makubwa sana “

“ Ndiyo Adolf ni muhimu kufanya mabadiliko ya mara kwa mara.Umepotelea wapi siku hizi?

“ Kazi zimekuwa nyingi sana Eva ndiyo maana unaniona niko kimya sana,lakini hapa ni nyumbani na muda wowote nitakaopata nafasi nitakuja”

“ Ok vizuri.karibu sana.Adolf huyu ni rafiki yangu anaitwa Mathew.Mathew huyu ni kanali Adolf daktari mkuu wa hospitali kuu ya jeshi” Eva akafanya utambulisho.Mathew na Adolf wakapeana mikono.

“ Ndiyo Eva nimefika kama ulivyokuwa umenitaka.Nieleze shida yako kwa sababu kuna mahala ninataka kuwahi”akasema kanali Adolf

“ kanali Adolf,mimi sina shida lakini kuna huyu ndugu yangu hapa ndiye mwenye shida na wewe ya muhimu sana.Nitawaacha ninyi wawili muongee na mkisha malizana nitarejea”akasema Eva huku akiinuka na kutoka .Kanali adolf akabaki akishangaa.

“ halow Mathew,natumai hatujawahi kuonana” akasema Adolf

“Ndiyo kanali Adolf hii ni mara yetu ya kwanza tunaonana”akasema Mathew.

“ Una tatizo gani kijana wangu? Akauliza kanali Adolf

“ kanali Adolf nina tatizo moja ambalo linahitaji sana msaada wako.”

“Sema tu kijana wangu kama litakuwa ndani ya uwezo wangu nitakusaidia”

“ Kanali Adolf,kwa sasa nchi iko katika maombolezo ya kifo cha mke wa rais.Tunaambiwa kwamba kifo chake kilikuwa cha ghafla sana.Wewe kama daktari mkuu wa hospitali iliyothibitisha kifo chake unaweza ukaniambia kwamba nini sababu ya kifo chake?

Kanali Adolf akastushwa sana na swali lile akamkazia macho Mathew

“Kijana mbona sikuelewi? Wewe ni nani? Umetokea wapi?Unahusiana vipi na familia ya rais hata uniulize swali kama hilo?Wanaopaswa kuniuliza swali kaam hilo ni wafiwa na si wewe” Akauliza adolf ambaye alionekana kukerwa na swali lile

“ Naomba usikasirike kanal Adolf,si lazima niwe natokea familia ya rais ndiyo niulize swali kama hili.kama unafahamu kilichosababisha kifo cha Dr Flora tafadhali naomba uniambie”akasema Mathew.Kanali Adolf akainuka

“ I’m not having conversation with idiots”akasema na kukisukuma kiti nyuma ili aweze kupata nafasi ya kuondoka.Mathew akamtolea bastora na kumuelekezea

“kaa chini kanali Adolf..!!akasema kwa ukali Mathew.Adolf hakuogopa akacheka kidogo kana kwamba alikuwa akimdharau Mathew

“ Eva kanifanyia mambo gani haya? Mimi mtu wa kunikutanisha na wahuni kama huyu” akawaza

“ Sema unachotaka kusema kijana,usidhani nitaogopa hiyo bastora.Mimi ni kanali wa jeshi na huwezi kujua nimepitia mambo mangapi hadi hapa nilipofika” akajitapa

“ Nafahamu wewe ni kanali wa jeshi na umepitia mambo mengi sana lakini kuanzia sasa utakaa na kunisikia ninachokwambia” akasema Mathew

“ hahaahaa..vijana wa siku hizi njaa zitawaua.kama sitaki utanifanya nini?

“ I’ll destoy you “ akasema Mathew.Adolf akacheka na kusema

“ Nimekwisha zizoea kauli kama hizo za kihuni.Huna uwezo wa kunitisha mtu kama mimi.Ninaondoka na huna uwezo wa kunifanya chochote na ninakutuma nenda mwambie huyo mwanamke kahaba aliyenileta hapa kwamba mimi si mtu wa kufanyiwa mchezo na wahuni” akasema kanali Adolf huku akipiga hatua kuelekea mlango

“ Stop there Adolf” akapaaza sauti Mathew.Adolf akasimama.

“ Najua huogopi silaha lakini ukijaribu kutoa mguu wako nje ya huo mlango kesho asubuhi vichwa vya habari vya magazeti yote nchini vitapambwa na habari moja tu,ya wewe kumuua Albino ”

Kanali Adolf aligeuka ghafla kama mtu aliyepandwa na wazimu akamtazama Mathew kwa macho makali sana.Uso wake ukakunjamana kwa hasira

“ Kijana anaomba usinijaribu.Hunifahamu mimi ni nani.Nitakuondoa katika hii dunia hata nzi wasifahamu nimekupeleka wapi” akasema Adolf kwa hasira

“ Adolf huwezi kunifanya kitu.Ninakufahamu zaidi ya unavyojifahamu .Ninafahamu kila kitu unachokifanya na kubwa zaidi likiwa ni hili la kumuua mlemavu wa ngozi.Kama hutakuwa tayari kunisikiliza ninachotaka kukwambia usiku huu nitaongozana na kikosi cha askari na waandishi wa habari na kwenda kuwaonyesha mahala ulikofukia mwili wa binti Albino uliyemuiba toka Geita.Sitaki mambo haya yafike huko.”akasema Mathew.Adolf alihisi miguu ikimuisha nguvu akatoa kitambaa akafuta jasho,halafu akaketi kitini.

“ Kijana unatakiwa uwe makini sana na unayoyasema.Una ushahidi wa hayo yote unayoyasema? Ninaweza kukufungulia mashitaka kwa kunikashifu.Mimi kanali Adolf ninaweza kweli kuua mlemavu wa ngozi?



“ Nina kila ushahidi wa kukutia hatiani Adolf.Ninawafahamu vijana uliowatuma kwenda kumteka Albino Geita,ninamfahamu hata mganga aliyekuagiza ufanye hivyo.”akasema Mathew kwa kujiamini

“ Unataka nini kijana? Shida yako ni nini? Adolf akauliza taratibu huku akiendelea kujifuta jasho

“ kanali Adolf naomba tusiyafanye mambo haya yawe makubwa.Naomba unisikilze kwa makini.Mke wa rais Dr Flora Joshua alipofariki aliletwa hospitalini kwenu.Nani aliwazuia msifanye uchunguzi kubaini kifo chake? Mathew akauliza.Adolf hakujibu kitu akabaki kimya

“ kanali Adolf naomba unijibu.Mlipokea simu mkizuiwa kufanya chochote katika mwili wa Dr Flora.Ni nani aliyewapigia simu kuwaambai kwamba msimfanyie uchunguzi?

“ Hiyo ni amri iliyotoka kwa uongozi wa juu”

“ Uongozi wa juu ni nani.Nahitaji jina!!

“ Nilitaarifiwa na katibu wa rais”

“nahitaji Jina”

“ Anaitwa Dr Albert kigomba.”

“ yeye alipewa maagizo hayo na nani?

“ Sifahamu aliambiwa na nani.Sisi ni watendaji tu na tukipokea agizo tunalifanyia kazi” akasema Adolf

“ Ok sasa kilichonifanya nikutafute ni kwamba unatakiwa uufanyie uchunguzi mwili wa Dr Flora na kubaini kilichomuua usiku wa leo”

“ What ?!!...Adolf akashangaa

“ Nataka ufanye uchunguzi wa kubaini kilichomuua Dr Flora usiku wa leo”

“ No ! I cant do that!!..Tumekatazwa kufanya hivyo na siwezi kwenda kinyume na maagizo hayo”

“ Ninasema kwamba utafanya ninavyokuelekeza.Ninataka ufanye uchunguzi wa mwili wa Dr Flora usiku wa leo”

“ No ! Nimesema siwezi kufanya hvyo”

“ Utafanya nimekwambia.Kama ukikataa kufanya hivyo utaozea gerezani kwa maisha yako yote” akasema Mathew.Kanali Adolf akainama akafikiri kwa muda na kusema

“ Kwa nini unataka kufahamu kilichomuua Dr Flora? Wewe ni nani?

“Huna haja ya kufahamu mimi ni nani na kwa nini ninataka kufahamu kilichomuua Dr Flora ,nataka kusikia jibu moja tu ,utafanya au hutafanya?

Adolf akafikri kidogo na kusema

“ ok I’ll do it.Lakini kwa sharti moja “

“ Sharti gani hilo?

“ Hii iwe ni mara ya kwanza na ya mwisho kunitaka nikufanyie kitu cha namna hii.After this we’re done.Sitaki unibughudhi tena.Ukithubutu kunifuata tena I swear I’ll kill you.Do we have a deal?

“ deal “akasema Mathew.

“ Ok itanilazimu vile vile kuwataarifu baadhi ya madaktari ambao nitafanya nao uchunguzi huo siwezi kufanya peke yangu”

“ Huna haja ya kufanya hivyo.Tunaye daktari wetu ambaye utashirikiana naye kufanya huo uchunguzi.”

“ Yuko wapi huyo daktari?

“ Usijali utamuona tu.Twende tuondoke” akasema Mathew.Anitha alikwisha rejea garini akimsubiri Mathew,wakaingia garini na kuondoka.

UCHUNGUZI WA KIFO CHA DR FLORA UTAFANIKIWA? TUKUTANE SEHEMU IJAYO……

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...