SIMULIZI: PENIELA (Season 1 Ep 31)
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Hii ilitokana na kuingiwa na shaka .Sina hakika kama watakuwa wamefanikiwa kufahamu kilichomuua Flora lakini endapo wakifanikiwa kujua,litakuwa ni anguko letu vinginevyo itatulazimu kufanya maamuzi magumu sana ili tuendelee kubaki salama.Kwa kuwa bado hatujui ni kitu gani wamekigundua hao madaktari kuna mambo ambayo lazima tuyafanye.Kwanza kesho asubuhi Kaptain Amos utashughulikia ripoti ya uongo ya kuhusu kifo cha Flora ripoti ambayo nitawaonyesha wanangu ili waridhike kwani nimewadanganya kwamba uchunguzi utafanyika kesho.Pili Mwanangu Flaviana anatakiwa aanze kuchunguzwa sana nyendo zake.Yeye ndiye atakayetupeleka mahala aliko mumewe Elibariki na tukimpata Elibariki tutakuwa tumewapata wengine wote walioshiriki katika jambo hili.Nataka mpaka kufika kesho asubuhi niwe nimepata ripoti kuhusiana na jambo hili.Kwa hiyo kuanzia sasa hakutakuwa na kulala.We’re going to work day and night to make sure we’re safe.You’ve messed it now you’ll have to fix it.!! Akasema kwa ukali Dr Joshua
ENDELEA………………….
Jaji Elibariki alikuwa amepumzishwa kwa muda baada ya kushonwa jeraha lake alilokuwa amepigwa na chupa kichwani.Alikuwa ametundikiwa chupa ya damu kwani ilionekana amepoteza damu nyingi.Akiwa amelala kitandani mawazo yake yote yalikuwa kwa akina Mathew kama walifanikiwa kutoka salama.Kingine kilichomuumiza kichwa ni namna gani angemueleza mkewe kuhusiana na jeraha lile .
“ Nimekwisha pata jawabu.Nitamueleza kwamba niliumia katika harakati za kutoroka hospitali.Ninadhani kwa uetetezi huo atanielewa.” Akawaza halafu picha ya tukio zima lililotokea nyumbani kwa Peniela ikamjia kichwani
“ Bastard !!..akasema kwa hasira na kutaka kuinuka lakini akahisi maumivu makali sehemu yenye jeraha akajilaza tena
“ Kilichotokea nyumbani kwa penny ni kitendo cha aibu sana.Ninashukuru sehemu ile si sehemu yenye mkusanyiko mkubwa wa watu kumetulia na hakuna watu wengi.Endapo kungekuwa ni sehemu zenye watu wengi sijui ni aibu gani ningeipata.Mtu ninayeheshimika kama mimi,jaji wa mahamakama kuu ninagombana kwa sababu ya mwanamke ni aibu kubwa sana.Ingekuwa sehemu zile zlizojaa wadaku sijui ningeuwekawapi uso wangukwani picha zangu zingesambaa katika kila gazeti la kesho.Ingekuwa ni aibu kubwa kwa sababu Yule mshenzi amenikuta nikiwa mtupu kabisa ” Akawaza Elibariki na kuuma meno kwa hasira
“ Kuna klitu ambacho ninajiuliza na sipati jibu.Peniela na Jason walikuwa na mahusiano? Ninahisi hivyo kwa sababu Jason alikuwa akijitapa kwamba Peniela ni mwanamke wake.Aliongea kwa kujiamini sana..Kama walikuwa katika mahusiano kwa nini basi peniela akubali kuanzisha mahusiano na mimi? Nakumbuka Peniela ndiye aliyenishawishi hadi tukafanya mapenzi.Yeye ndiye aliyeniita kwake akidai ana shida kubwa lakini nilipofika kwake akaniambia shida yake ilikuwa ni kufanya mapenzi na mimi kwani alinitamanisiku nyingi.Iweje anitamkie manenohayo na wakatyi huo huo akawa na mahusiano na Jason wakati anaelewa kabisa kwamba mimina Jason ni washirika? Hili suala linanichanganya sana.Peniela lazima anipe maelezo kwa nini ametufanyia hivi .Kwa atuchezee kiasi hiki? “ akawaza na picha mbali mbali za Penny zikamjia kichwani.
“ Lakini pamoja nayote yaliyotokea bado ninampenda penny.Bado yuko moyoni mwangu na siko tayari kumuona akiwa nayule kijana.Jason ni kijana mshenzi sana na asiye na adabu hata kidogo.Ninaapa nitamuonyesha kazi mimi ni nani hapa mjini.Ninataka nimfunze adabu ili siku nyingine asizoee kuingilia mali za watu.Mimi ndiye ninayestahili kuwa na Peniela kwa sababu ndiye niliyemuachia huru.Anajua ni mambo gani nimeyapitia hadi Peniela akawa huru? Nitamuonyesha kwamba nchi hii ina wenyewe .Nataka amuone pen……………” akastuliwa toka mawazoni na simu.Akaichukua na kutazama mpigaji alikuwa ni Mathew
“Hallow Mathew,nipe habari.Mmefanikiwa kuwahi kutoka?akauliza
“ Ndiyo Eli,tumefanikiwa kuwahi kutoka .Wewe uko wapi?akauliza Mathew na jaji Elibariki akabaki kimya
“ Elibariki uko wapi ? akauliza tena Mathew
“ Niko hapa Brahmaputra hospital”
“ Unafanya nini hapo hospitali?
“ Nimekuja kutibiwa jeraha nililoumia.Mmefanikiwa lile zoezi?”
“ Eli,ninakuja hapo hospitali.I need to talk to you.”akasema Mathew na kukata simu
“ Ahsante Mungu Mathew na timu yake wamefanikiwa kutoka salama.Lakini Flaviana amepataje taarifa hizi za kutaka kuwakamata madaktari wanaofanya uchunguzi ? Akajiuliza
“ Mambo haya yanazidi kunichanganya.Inaonekana wazi kwamba sababu ya ya kifo cha Dr Flora haitakiwi kujulikana.Ni kitu gani kinafichwa? Nadhani Flaviana alikuwa sahihi,kuna kitu hakiko sawa kuhusiana na kifo cha Dr Flora.Ninaanza kuhisi yawezekana Dr Flora akawa aliuawa.Kama ni hivyo ni nani aliyefanya hivyo na kwa nini? Akajiuliza na kushindwa kupata jibu.
Nusu saa toka Elibariki awasiliane na Mathew,mlango wa chumba alimolazwa ukafunguliwa akaingia daktari akiw ameongozanana Mathew na Anitha
“ hallo Eli.Pole sana.Nini tatizo? akauliza Mathew
“ Ah ! Mathew nilipata jeraha kidogo.”
“Ulifanya nini?akauliza Mathew
“ Nilikuwa naamulia ugomvi sehemu fulani basi ikarushwa chupa na kunipata kichwani.I’m ok now.Vipi kuhusu nyie mmefanikiwa kupata chochote?akauliza Elibariki
“ Eli hatuwezi kuongea sasa hivi,naomba uinuke tuondoke.” Akasema Mathew na kumgeukia daktari
“ Daktari naomba uchomoe chupa hiyo ya damu kwa mgonjwa wetu tunaondoka naye sasa hivi” akasema Mathew na kumfanya daktari Yule mwenye asili ya India abaki akishangaa
“ Usishangae daktari ,chomoa huo mpira wa damu,tunaondoka na mgonjwa wetu” akaamuru Mathew.
“Mgonjwa bado anahitaji kupatiwa huduma.Jeraha lake limesababisha akapoteza damu nyingi kwa hiyo anatakiwa kuongezewa damu mwilini.Mkimchukua kwa haraka namna hii inaweza kuwa ni hatari kwa mgonjwa”
“ Daktari nimesema chomoa huo mpira wa damu sasa hivi.Hatuna muda wa kuendelea kusubiri hapa”akasema Mathew.Daktari Yule akaogopa na kuisimamisha damu ile aliyokuwa ametundikiwa jaji Elibariki.Wakati akifanya hivyo simu ya jaji Elibariki ikaita,alikuwa ni mkewe Flaviana.Mathew akamsaidia kubonyeza kitufe cha kupokelea na kumuwekea sikioni
“ Hallow Flaviana”akasema Elibariki
“ Hallo Eli.Uko wapi? Uko salama?
“ Niko salama mke wangu,ninaendelea vizuri usihofu”
Flaviana akavuta pumzi nefu baada ya mumewe kumuhakikishia kwamba yuko salama.
“ Kwa hiyo ukowapi Eli? I need to see you” akasema Flaviana
“ kwa sasa niko mbali kidogo lakini baadae nitakuelekeza mahala tunakoweza kuonana.Nini kinaendelea hapo? Kuna taarifa gani?
“ Usihofu Eli,nimeongea na baba na kumfahamisha kila kitu kuhusiana na kinachoendelea na mlichokuwa mnakifanya.Inaonekana kuna watendaji wake waliokuwa wakimzunguka na kufanya mambo bila ya yeye kufahamu.Ameahidi kulishughulikia suala hili kwa hiyo usiogope tafadhali,babat ayari anafahamu mlichokuwa mnakifanya na ameshukuru,ila ameahidi kwamba kesho asubuhi kuna timu ya madaktari kutoka hospitali kuu ya taifa wanakwenda kufanya uchunguzi kufahamu chanzo cha kifo cha mama.”akasemaFlaviana.Mathew akamfanyia ishara akate simu ili waondoke
“Flaviana I have to go now.I’ll talk to you later”akasema Elibariki na kukata simu.Tayari daktari alikwisha maliza kazi yake akamuomba waongozane hadi katika dirisha la dawa ili akamuandikie dawa ambazo angeendelea kuzitumia.Jaii Elibariki akapatiwa dawa na kisha wakaingia katika gari wakaondoka.Safari ilikuwa ya kimya hadi walipowasili nyumbani kwa Mathew.Mara tu baada ya kuingia ndani Dr Michael akamshika mkono Mathew na kumvuta pembeni
“ Mathew tayari nimefanya kila ulichotaka kukifanya.Ni zamu yako sasa kumtafuta mke wangu yuko wapi.”akasema Dr Michael
“ Dr Michael nakushukuru sana kwa msaada wako .Nilikuahidi kwamba mke wako atapatikana.Niamni ninavyokwambia kwamba mkeo atapatikana.kwa sasa tuangalie namna tutakavyoweza kumalizia ile kazi tuliyokwenda kuifanya kule hospitali.”
“ Nina sampuli kadhaa hapa ambazo zinatakiwa zifanyiwe uchunguzi,lakini sintaendelea na kazi hii mpaka hapo nitakapompata mke wangu.” Akasema Dr Michael
“ Dr Michael nilikupa ahadi hiyo na lazima nitaitimiza lakini kwanza nahitaji kuimaliza kazi tuliyokwenda kuifanya.Ni muhimu sana.”
“ Mathew nimekwisha kueleza kwamba sintofanya kazi yoyote ile hadi mke wangu atakapopatikana.” Akasema Dr Michael.Mathew akamtazama na kugundua kwamba hakuwa akitania.
“ Ok Dr Michael tutamtafuta mkeo.Nipe muda nikae na timu yangu.”akasema Mathew na kuingia ndani.Ile ametia mguu sebuleni akakutana na Kanali adolf
“ Nini kinaendelea hapa? Ninafanya nini hapa? Kazi yenu nimekwisha imaliza na sina deni tena kwako.I need to go back.I need to clean my mess” akasema Adolf.Mathew akamshika mkono na kumsogeza pembeni
“ Adolf,kwa sasa huna sehemu nyingine ya kwenda.Hapa ni sehemu pekee ya wewe kuwepo kwa sasa.Utaendelea kukaa hapa hadi tutakapokamilisha uchunguzi tuliokwenda kuufanya na baada ya hapo nitashughulikia suala lako.Niamini Adolf,nitalimaliza suala hili na utarejea tenakazini kwako lakinikwa sasa utaendela kubaki hapa ” akasema mathew
“ Uchunguzi wetu uliingiliwa kati kati na hakuna namna tutakayoweza kujua nini kilimuua Dr Flora.”
“ hapanaAdolf,bado uchunguzi wetu unaendelea.Kabla ya kuondoka mle ndani,Dr Michael alichukua sampuli kadhaa za kufanyia uchunguzi.Yeye anafanya kazi katika hospitali kubwa hapa nchini kwa hiyo tutaitumia maabara ya hospitali hiyo anakofanyia kazi kufanya uchunguzi wa sampuli zile alizochukua.Kwa sasa kuna kazi ambayo tunatakiwa kuifanya ili aweze kumalizia uchunguzi .Tunatakiwa kumpata mkewake aliyetekwa”
“ Mke wake ametekwa? Akashangaa Adolf
“ndiyo ametekwa”
“Ametekwa na akina nani?
“ Hatuna uhakika ni akina nani mpaka sasa hivi.”
“ Kitu gani kinaendelea hapa nchini? Ninyi ni akina nani? Akauliza Kanali Adolf
“Adolf kaa upumzike na utuache tufanye kazi,tutaongea zaidi baade”akasema Mathew na kumfuata Anitha
“ Anitha nenda kaweke sawa mitambo yako tunaanza zoezi la kumtafuta mke wa Dr Michael”
Anitha akaelekea chumba cha mawasiliano halafu Mathew akamuendea Jaji Elibariki
“ Elibariki,kuna mambo ambayo yanaendelea ambayo nimeona nikufahamishe.Kwanza usistuke kuona kuna watu tuko nao hapa.Yule mzungu anaitwa Dr Michael na Yule mwingine anaitwa kanali adolf ambaye ni daktari mkuu wa hospitali kuu ya jeshi.Kwa pamoja wote wako hapa kwa sababu maalum.Siwezi kukueleza kila kitu hapa kwa kuwa hatuna muda wa kutosha. Kikubwa ninachotaka kukueleza nikwamba tumefanikiwa kuufanyia uchunguzi mwili wa Dr Flora lakiniwakati tukiwa katikati ya uchunguzi ndipo ulipotupigia simu na kutupa ile taarifa ikatulazimu kuondoka haraka sana.Pamoja na hayo lakini tumefanikiwa kuondoka na sampuli kadhaa ambazo Dr Michael ataendelea kuzifanyia uchunguzi lakini ni baada ya mke wake kupatikana.”
“ Mke wake yuko wapi? akauliza Elibariki
“Mke wake ametekwa na watu wasiojulikana na kwa sasa tunaingia katika zoezi la kumtafuta.Tukishampata mke wake Dr Michael ataendelea na uchunguzi.Tukimpata majibu ya uchunguzi huo tutajua nini kilimuua Dr Flora.Ninachotaka kufahamu toka kwako ni nani aliyekupa taarifa za kwamba tumegundulika tunafanya uchunguzi?
“Ni mke wangu Flaviana ndiye aliyenipigia simu na kunipa taarifa hizo”akasema Elibariki
“ Alikwambia ni wapi alizipata taarifa hizo?
“ Hapana sijaongea naye lolote kuhusiana na suala hilo “
“ Ok itakubidi umpigiie simu umuulize alizipataje taarifa hizo za sisi kuwapo mle ndani.Tukifahamu tutajua nini cha kufanya.Vilevile anatakiwa awe makini sana.Mwambie achukue tahadhari kubwa kwa kila anachokifanya kuanzia sasa hadi hapo tutakapojua ninikilichomuua mama yake”
“ Kwa niniunasema hivyo mathew?
“Ni kutokana na hali halisi ilivyo.Kuna kila dalili zinazoonyesha kwamba kuna jambo lilsilo la kawaida linaloendelea hapa.Mpaka tulifahamu ni jambo gani mnatakiwa mchukue tahadhari kubwa.”
“ Kuna uwezekano Dr Flora akawa aliuawa? Akauliza Elibariki
“ Kuna uwezekano huo kutokana na hali ya mambo ilivyo.Kuna juhudi kubwa za kujaribu kuficha chanzo cha kifo chake kwahiyo inashawishi kuamini kwamba Dr Flora aliuawa lakini tusubiri kwanza majibu ya vipimo yatatuambia nini” akasema Mathew na kumuacha jaji Elibariki ameduwaa.Akachukua simu na kumpigia mkewe.
“ Hallo Elibariki” akasema Flaviana baada ya kupokea simu
“ Flaviana uko wapi?
“ Niko hapa msibani,kuna nini Elibariki? Akauliza Flaviana
“ Kuna watu hapo karibu ambaowanasikia unachoongea simuni?
‘ Hapana niko chumbani peke yangu nimejifungia”
“ Ok vizuri,kuna jambo nahitaji kulifahamu.Nahitaji kufahamu namna ulivyozipata zile taarifa “
Flavina akamueleza mumewe kila kitu kilichotokea
“ Kwahiyo hapa inaonekana Dr Kigomba ndiye aliyetoa amri ya kuzuia mwili wa Dr Flora usifanyiwe uchunguzi”
“ Inaonekana hivyo kwa sababu Anna amemsikia kwa masikio yake akielekeza kwamba madaktari wanaoendela na uchunguzi wakamatwe haraka sana.”
“ Ok ahsante sana nashukuru ,lakini kuna jambo moja nataka kukuonya.Kuanzia sasa kuwa makini sana na kila unachokifanya.Kuha jambo linaloendelea hapo ikulu ambalo tunatakiwa tulifahamu.Kesho tunaweza kupata majibu ya uchunguzi wa kifo cha Dr Flora lakini mpaka wakati huo kuwa makini sana.Nitakupigia tena simu baadae” akasema Elibariki ina kukata simu kisha akamfuata Mathew
“ Mathew nimeongea na mke wangu anasema kwamba aliyesikika akitoa amri ya kukamatwa kwa madaktari wanaofanya uchunguzi wa kifo cha Dr Flora ni Dr Albert Kigomba katibu wa rais.
‘unasema Dr Kigomba? Akauliza Mathew kwa mshangao
“ Ndiyo .Dr Kigomba ndiye aliyetoa amri hiyo”
“ Kwa mujibu wa kanali adolf Dr Kigomba ndiye aliyetoa amri kwamba mwili wa Dr Flora usifanyiwe uchunguzi na leo hii ni yeye ambaye anatoa tena amri kuwakamata madaktari wanaofanya uchunguzi wa kifo cha Dr Flora.Kuna jambo hapa si bure” akawaza Mathew halafu akawageukia Anitha na Noah
“ Guys tumepata tena mtu mwingine tunayetakiwa kumchunguza.Dr Albert Kigomba anaingia rasmi katika mikono yetu.Tunatakiwa kuchunguza uhusika wake katika kifo cha Dr Flora.Tutalifanya hili baadae lakini kwanza tuelekeze nguvu kumpata mke wa Dr Michael ili aweze kumaliza kufanya uchunguzi na baada ya hapo tutajua nini cha kufanya.Anitha umefikia wapi?
‘ Kila ktu kiko tayari.Naombeni simu ya Dr Michale ili niiunganishe na kompyuta yangu “
Dr Michaela kaitwa mle chumbani ,simu yake ikachukuliwa ,Anitha akaichomeka katika kifaa Fulani kilichounganishwa na kompyuta yake halafu akaendelea kubonyeza bonyeza namba kadhaa na baada ya muda akawageukia akina Mathew
“ mambo tayari.Nitaipiga simu ya mkewa Dr Michael na kama haijazima basi tutaonyeshwa mara moja yuko sehemu gani.Lakini hata kama imezimwa basi tutaitafuta kwa njia nyingine ” akasema Anitha na kisha akabonyeza kitufe cha kupigia simu kilichoonekana katika kompyuta yake.Katika runinga kubwa iliyokuwa ukutani kukaonekana kitu Fulani mfano wa taa ndogo ikiwaka na kuzima.
“Simu yake inaita.Haijazimwa.Tusubiri sekunde kadhaa tutajua mahala alipo.” Akasema Anitha .Watu wote walikuwa kimya.Baada ya sekunde kadhaa kile kitaa chekundu kilichokuwa kinawaka na kuzima kikabadilika rangina kuwa cha kijani halafu kukatokea picha fulani mithili ya ramani..
“ Done.Tayari nimejua mahala alipo mke wa Dr Michael.”akasema Anitha halafu akaanza kubonyeza kompyuta yake baada ya dakika mbili akaenda katika runinga ilena kuikuza ile picha picha iliyokuwa inaonekana
“ .Simu ya mke wa Dr Michael inaita toka katika jengo hili “ akasema Anitha na kuwalekeza akina Mathew
“Good Job Anitha .Noah jiandae tundoke.” Akasema Mathew
“Na mimi ninawafuata” akasema Dr Michael
“ Hapana Dr Michael utabaki hapa.Ni hatari sana kuongozana nasi .”
“ Mathew huyu ni mke wangu na ninatakiwa nishiriki katika kumuokoa.Hebu pata picha ingekuaje angekuwa ni mke wako ndiye aliyetekwa? Ungeweza kukaa hapa na kusubri wakati mkeo yuko katika hatari? Akauliza Dr Michael.Mathew akainama akafikiri na kusema
“ Hapana.Nisingeweza kufanya hivyo”
“ Kama ni hivyo na mimi naungana nanyi.Ninaweza kulenga shabaha vizuri,naninajua kutumia bastora.Ninaweza kupambana” akasema Dr Michael.
Mathew akaenda chumbani kwake akachukua silaha na vitu vingine ambavvo aliona vitamsaidia katika kazi ile halafu akampatia Dr Michael fulana ya kuzuia risasi pamoja na bastora moja na kisha akaenda sebuleni na kumrushia Kanali Adolf bastora
“ we’re going out.”
“ Out where?
“ To rescue a woman.get ready ” akasema Mathew na kumfuata Anitha
“ Anitha tunakwenda kumchukua mke wa Dr Michael.Tunakutegema sana wewe katika operesheni hii.I promised to get his wife back and that’s what we’re going to do..” Akasema Mathew na kuchomeka sikioni kifaa cha mawasiliano akajaribisha na kuona kiko sawa
“ Usihofu Mathew kila kitu kimekaa sawa.Nitaona kila kitu kutokea hapa kwa kutumia satellite.” Akasema Anitha
Mathew,Noah ,Dr Michael na kanali Adolf wakaingia garini na kuondoka .
OPERESHENI YA KUMUOKOA MKE WA DR MICHAEL ITAFANIKIWA? PENIELA YUKO WAPI? NA JE JIBU LA NINI KILIMUUA DR FLORA MKE WA RAIS LITAPATIKANA ? TUKUTANE TENA SIKU YA JUMATATU KWA MWENDELEZO WA SIMULIZI HII
No comments
Post a Comment