PENIELA (Season 2 Ep 5)
SEASON 2
SEHEMU YA 5
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
ENDELEA………………………
Shughuli ya kuizika miili ya vijana sita waliopoteza maisha katika shambulio la kumuokoa mke wa Dr Michael ilimalizika saa kumi na moja na dakika ishirini na tatu.Mtu wa mwisho ambaye ni Aron mkibala alizikwa katika makaburi ya mkoroshini.Baada ya shughuli ile kukamilika vijana wote wa Team SC41 walitakiwa wakutane makao makuu
Wakati yote haya yakiendelea ,Josh kijana ambaye kwa muda mrefu amekuwa mlinzi wa John Mwaulaya alikuwa katika ofisi ya Osmund akikitafuta kile alichotumiwa na John.Si rahisi kuingia katika ofisi ya Osmund lakini Josh alifanikiwa kuingia katika ofisi hiyo kwa msaada mkubwa wa John Mwaulaya aliyempatia kadi maalum ya kufungulia mlangowa ofisi hiyo pamoja na namba za siri za kufungulia kompyuta ya Osmund.Baada ya kupata kile alichokuwa anakitafuta ,akatoka na kurejea katika makazi ya John mwaulaya
“ Mzee nimefanikiwa ulichonituma.Nimekwisha pata taarifa zote kuhusiana na Dr Burke kwa hiyo usijali nitaifanya kazi yako kikamilifu” akasema Josh
“ Ahsante sana Josh.Ahsante sana kwa kuendelea kuwa mtiifu.Nitakufanyia jambo kubwa kabla ya pumzi zangu kukatika” akasema John
“ Mzee tafadhali usiwaze kuhusiana na masuala hayo ya kifo.Be strong John.You can fight this”akasema Josh
“ I was as strong as a lion but now I’m very weak and I cant fight anymore.I cant fight this Josh .I’m going to die soon.” Akasema John Mwaulaya na kufumba macho na kwa mbali michirizi ya machozi ikaonekana machoni pake.Josh akamuonea huruma mzee yule aliyekuwa amelala pale kitandani ambaye ndiye aliyemuingiza katika Team SC41
“ John what can I do for you? Akauliza Josh
“ Leave me alone for now” akasema John na Josh akatoka mle chumbani na kumuacha John peke yake
“ Nilizoea kuzitoa roho za watu.Sikujua kama siku moja na mimi nitakufa.I’m so scared of death”akawaza John
“ Nimefanya mambo mengi sana mabaya katika kipindi chote cha masha yangu na zaidi baada ya kujiung a na TeamSC41 .Nimeua watu wengi,nimetesa watu wengi lakini ni kitu kimoja tu ambacho nina uhakika nilikifanya sawa.Sikumuua Peniela.Alikuwa mtoto mdogo na hakuwa na kosa lolote” akaendelea kuwaza John na sura ya Peniela ikamjia akatabasamu
“ Ni msichana mzuri sana lakini kuna kitu kimoja nimekikosea .Nilikosea sana kumuingza katika Team SC41.Japokuwa anapata kila kitu anachokihitaji lakini hana furaha ya maisha .Siku nilipomuingiza Team SC41 niliyaharibu maisha na ndoto zake zote.Peniela amekuwa akitumika katika mambo mengi ya hatari na hivyo kuhatarisha usalama wa maisha yake.Kinachonisikitisha zaidi ni kwamba mwili wake mzuri umekuwa ukitumika kama silaha ya Team SC41 katika kufanikisha mambo mengi.Inaniuma sana kuyaharibu maisha yake namna hii” John akauma meno kwa uchungu
“ It’s not too late.kabla sijakata pumzi lazima nihakikishe kwamba Peniela amekuwa na maisha ya kawaida kama wasichana wengine.lazima nimuondoe katika Team SC41 .Lazima nihakikshe anaishi maisha ya kawaida.” Akawaza John na kumbukumbu zikamrejesha mbali siku Peniela alipomaliza elimu yake ya msingi
Ni siku ya mahafali ya darasa la saba katika shule ya St Patrick shule ambayo husoma watoto wa matajiri ..Peniela akiwa ni miongoni mwa wahitimu alikuwa na furaha isiyo kifani.Katika miaka yote saba aliyoitumia katika elimu yake ya msingi Peniela amekuwa ni mmoja kati ya wanafunzi hodari sana na mwenye kutiliwa mfano katika bidii ya masomo darasani,michezo,tabia njema na hata usafi.Kwa upande wa maisha ,japokuwa ni mtoto yatima lakini alikuwa akiisha maisha mazuri mno..Aliwezeshwa kupata kila alichokihitaji .sKulikuwa na gari maalum ya kumpeleka shuleni kila siku asubuhi nakumrejesha nyumbani,alipelekwa kila mahala alikotaka kwenda.Watu wengi hawakuamini kama Peniela ni mtoto yatima kutokana na maisha aliyokuwa akiishi.Peniela alitamani sana siku moja akutane na mtu yule ambaye amekuwa akimuwezesha kuishi maisha ya namna ile.Alijiona ni mtoto mwenye bahati kubwa kumpata mfadhili wa aina ile ambaye alimuwezesha kuishi maisha ya hali ya juu kiasi kile.Kila siku alikuwa akimlilia mama Bernadetha amuwezeshe kumkutanisha na huyo mfadhili wake ili aonane naye na amfahamu kwa sura lakini hadi anamaliza darasa la saba hakuwa amefanikiwa kukutana naye
Saa nne za asubuhi John Mwaulaya akiwa katika gari lake la kifahari aliwasili St Patrick school ili kuhudhuria sherehe za mahafali.Alikuwa na furaha usiyo kifani kwa Peniela kumaliza elimu yake ya msingi
“ She’s growing up so fast.Ni juzi tu alianza darasa la kwanza na leo tayari amemamliza darasa la saba ,Dah ! miaka inakimbia sana” akawaza John akishuka katika gari lake la kifahari na kuungana na watu wengine waliokuwa wamekuja katika mahafali haya
Sherehe zilikwenda vizuri na kabla ya sherehe kumalizika Bi Bernadetha akamuomba Peniela waongozane kuelekea sehemu Fulani kuna kitu anataka akamuonyeshe.Peniela aliingia katika gari wakaondoka bila kujua walikuwa wanaelekea wapi.
Safari yao iliwafikisha katika jumba moja kubwa lenye uzuri wa kipekee.Mlinzi alifungua geti wakaingia ndani.Uso wa Peniela ukapambwa na tabasamu la mshangao baada ya kuishuhudia mandhari ya kuvutia sana iliyokuwemo mle ndani.
Watu wanne walikuwa wamesimama katika mlango wa kuingilia sebuleni.Wote walikuwa na nyuso zenye tabasamu.
“ mama Bernadetha hapa ni wapi? Nani anaishi hapaauni hoteli ? Akauliza Peniela
“ Peniela sikuwa nimekwambai toka mwanzo nilitaka nikushangaze kidogo.Hi si hoteli mwanagu.Hii ni nyumba ya kuishi.Kuanzia dakika hii ni nyumba hii ni yako.Mfadhili wako amekuzawadia i kama zawadi yake kwako kwa kuhitimu elimu ya msingi na kuanzia le o utaishi hapa.Leo utayaanza maisha mapya Penny.” Akasema Bi Bernadetha na kumuacha Peniela akiwa na mshangao
“ mama Bernadetha ! akasema Penny kwa mshangao
“ Peniala najua umestuka sana na hata mimi nilistuka sana lakini na nimeumia sana kwamba hatutakuwa pamoja ,kwani wewe ni mtoto ambaye nimekuzoea sana na ninakupenda mno lakini haya ni matakwa ya mfadhili wako kwamba anataka aanze kukujengea maisha ya kujitegemea.Pamojana hayo naomba usijali Penny mimi bado nitaendelea kuwa mama yako na nitaendelea kuwa karibu nawe kwani nafahamu bado unahitaji sana msaada wangu” akasema Bi Bernadetha kisha wakakumbatiana na Peniela.
Walishuka katika gari na kuelekea ndani ,Bi Bernadetha akamtambulisha Peniela kwa watumishi ambao watakuwa wakimsaidia katika maisha yake ndani ya jumba lile.Alikuwepo mtumishi wa kazi za ndani,mpishi,na mtumishi mwingine ni wa kumsaidia peniela katika kazi zake ndongondogo na vile vile alikuwepo pia dereva wake maalum.Wote walifurahi kukutana na Peniela.Wakamzungusha Penny katika jumba lote na alifurahi sana
“ Mama bernadetha huyu mfadhili wangu anayenifanyia mambo haya makubwa ni nani? Kwa nini hutaki kunikutanisha naye ili nimfahamu na kumshukuru? Watu wa namna hii ni nadra sana kupatikana siku hizi.” Akasema Peniela baada ya kumaliza kutembezwa katika jumba lote
“ Peniela usijali siku moja utakunana na mfadhili wako na utamfahamu.Hata naye ana hamu sana ya kukutana nawe lakini ni mwingi wa safari za nje ya nchi” akasema Bi Bernadetha.
Peniela aliyaanza maisha mapya ndaniya jumba lile kubwa .Alijiona ni kama malkia.Saa tatu za usiku akiwa amejilaza katika kitanda kikubwa chumbani kwake simu iliyokuwa mezani ikaita akainuka na kuipokea.
“ Halow” akasema
“ hallow Peniela” ikasema sauti nzito ya kiume upande wa pili wa simu
“ Ninaongea na nani? Akauliza Peniela
“ Unaongea na John.Mimi ndiye mfadhili wako.”
Peniela akapatwa na furaha ya ajabu sana kwa kuisikia sauti ya mtu ambaye amekuwa akitamani kumuona kwa miaka mingi.
“ Baba John nakushukuru sana kwa kila kitu ulichonifanyia.Sina neno zuri la kuweza kukushukru ila ninakuombea kwa Mungu akupe Baraka nyingi na mafanikio katika shughuli zako” akasema Penny huku akilengwa na machozi kwa hisia kali
“ Peniela nashukuru kwa Baraka zako lakini naomba tu ufahamu kwamba kukosa wazazi si kigezo cha kukufanya uishi maisha ya shida.Unastahili kuishi maisha mazuri kama watoto wengine na hicho ndicho ninachojitahidi kukifanya kuhakikisha kwamba maisha yako yanakuwa mazuri.Umeionaje nyumba yako? Inakufaa?
“ baba John,sina cha kusema ,kila kitu ni kizuri .Siamini kama hata mimi yatima leo hii ninaweza kuishi ndaniya jumba kubwa na zuri kama hili.Mungu akubariki sana baba” akasema Penny
“ Penny kuna picha moja kubwa ya bahari ukutani umeiona?
“ Ndiyo baba nimeiona”
“ Ok nenda kaitoe ile picha na nyuma yake utakuta kuna kasiki lina namba kisha lifungue kasiki hilo kwa namba hizi” akasema John na kumtajia Peniela namba za kufungulia kasiki lile.Peniela akafanya kama alivyoelekezwa
“ Tayari baba nimelifungua”
“ Ok Vizuri .Ndani ya kasiki hilo kuna hati ya nyumba na kadi ya gari ,kadi ya benki na nyaraka nyinginezo .Kila kitu kina jina lako.” Akasema John
“ Baba ahsante sana lakini nina kitu kimoja bado kinanisumbua sana akili yangu”
“ Kitugani Peniela?
“ Ninataka kukuona.Moyo wangu utakuwa na furaha kubwa kama nikikuona.Tafadhali baba naomba uniruhusu nikuone, walau niione sura yako” akaomba Peniela.John akacheka kidogo nakusema
“Usijali Peniela siku moja tutaonana.Nitakuwa nikiwasiliana nawe kila siku kujua maendeleo yako.Kwa heri peniela” John akakata simu
Kumbu kumbu ile ikayafanya macho ya John yaloe machozi.
“ She was so beautiful na maisha yake yalikuwa na furaha sana .Lazima nimrudishie furaha yake aliyokuwa nayo wakati ule.Lazima nimuondoe teamSC 41” Akawaza John
******
Mathew,Anitha na Noah walikuwa katika chumba chao cha kazi.Pamoja nao alikuwepo mtaalamu wa program za kompyuta Arnold ambaye walikuwa wakimshikilia .Wote macho yao yalikuwa katika simu iliyokuwepo mezani wakisubiri simu kutoka kwa watu ambao walitakiwa kukutana na Arnold jioni ile.Simu nyingi zilikuwa zikipigwa na kila simu iliyopigwa Arnold alidai haikuwa yenyewe
“ Arnold una hakika hao jamaa watapiga? Akauliza Mathew baada ya kuona muda unazidi kuyoyoma na hakuna simu yoyote iliyopigwa
“ Watapiga tu,makubalinao yetu ni kwamba leo hii lazima niwapatie mzigo wao na wao wanilipe fedha zangu zilizobaki.Kama nilivyowaambia kwamba tulikubaliana kukutana kuanzia saa moja za jioni leo “
Waliendelea kusubiri na ilipotimu saa kumi na mbili na dakika ishirini na tatu simu ikapigwa na Arnold akaitambua kwamba ,ni ya wale jamaa.Wote wakatega masikio .Arnold akabonyeza kitufe cha kupokelea
“ Hallow “ akasema
“ Arnold .Kila kitu kiko tayari? Ikauliza sautiya upande wa pili
“ Ndiyo kila kitu kiko tayari.Ninasubiri maelekezo yenu”akasema Arnold
“ Ok Vizuri .Tukutane Triple S casino ghorofa ya tatu kaunta C.Jitahidi hadi saa moja na robo uwe umewasili ”akasema yule jamaa
“sawa nitafika kabla ya muda huo” akajibu Arnold na simu ikakatwa
“haya kumekucha “ akasema Mathew
“ sasa tunaelekea tena kazini.Noah wewe kwa kuwa bado haujapona vizuri jeraha lako utabaki hapa na nitaongozana na Anitha.”
“ sawa hakuna shida Mathew” akajibu Noah
“ Anitha kila kitu ulikiweka sawa katika ile tablet? Akauliza Mathew
“ Kila kitu kiko tayari.”akasema Anitha kisha Mathew akamgeukia Arnold
“ Arnold tunakwenda sote huko Casino na utawakabidhi hao jamaa kifaa chao lakini nakuonya tutakuwa karibu tukifuatilia kila kinachoendelea kwa hiyo usijaribu kwa namna yoyote ile kuwatamkia kitu chochote kwamba tunawafuatilia.Wakabidhi kifaa chao kisha utatuachia sisi kazi ya kuendelea kuwafuatilia.Ukienda kinyume na tunachokuamuru fahamu kwamba jua la kesho hutaliona.Tumeelewana Arnold? Akauliza Mathew kwa ukali
“Tumeelewana ndugu zangu.Ntafanya kama mlivyoniamuru lakini kuna mambo bado nahitaji kuyafahamu,ninyi ni akina nani? Na hawa jamaa walionipa hii kazi mnawafahamu? Akauliza Arnold
“ Watu hawa waliokupa hii kazi hatuwafahamu lakini tunahitaji k uwafahamu ni akina nani na ndiyo maana tunawafuatilia Ili tuwafahamu na vile vile tufahamu ni kitu gani wnachokitafuta kwa Eva.”akasema Mathew
“Nina wasi wasi kama hawa jamaa ni watu wabaya wanaweza wakanifanyia kitu kibaya au hata kuniua mara tu nitakapowakabidhi kifaa chao “akasema Arnold
“Usijali Arnold sisi tutakuwepo karibu tunakufuatilia na tutakulinda” akasema Mathew
Noah akamchukua Arnold na kumpeleka bafuni akaoga kisha akapewa suti moja ya Mathew akavaa na kujiweka tayari kwa safari ya kuelekea Triple S casino.Baada ya dakika kumi wote walikuwa tayari wakaingia garini na kuondoka wakimuacha Noah peke yake nyumbani
Dakika kumi tu toka akina Mathew waondoke jaji Elibariki akawasili na kumkuta Noah peke yake .
“ Mathew ametoka kuna mahala amekwenda ila amesema hatachelewa sana kurudi na amesema ukifika umsubiri” akasema Noah Jaji Elibariki akajiegemeza katika sofa na kuvuta pumzi ndefu. Alionekana ni mchovu na mwingi wa mawazo
“ Bado sielewi ni kwa nini rais anakubali kudanganywa na wasaidizi wake kiasi hiki ? Kwa nini amekataa kuikubali taarifa yangu ya ukweli? Kitu gani kinaendelea ndani ya Ikulu? Lazima tufanye uchunguzi wa kina tubaini kinachoendelea ndani ya jengo lile.” Jaji Elibariki akastuliwa toka mawazo nina simu yake iliyokuwa ikiita.Akaichomoa toka mfuko wa koti na kutazama mpigaji alikuwa ni mkewe Flaviana
“ Hallow Flaviana”akasema
“Eli uko wapi? Mbona sikuoni hapa? Nimetuma watu wakutafute lakini wamekukosa.Ninakuhitaji kukuona” akasema Flaviana.Elibariki akafikiri kidogo na kusema
“ Flaviana nimetoka kidogo .Mzee amenichefua sana leo”
“ Unaweza ukaja kidogo tukaonana Eli?
“ Niko mbali kdogo.Kunanini?
“ Nataka tuongee kuhusiana na lile suala”
“ Hakuna cha kuongea Flaviana.Hakuna kati yenu anayetaka kuniamini .Hakuna anayetaka kuiamini taarifa niliyowapa.Nyote mnakubaliana na alichokisema baba yenu”
“ Eli si kwamba hatukuamini lakini mambo haya yanachanganya sana .Hapa nilipo nimechanganyikiwa na sijui nielekee upande upi”
“ Flavina ni wewe ndiye uliyeniambia nikusaidie kutafuta kilichomuua mama yako na nilifanya ulivyoniomba.Hujui ni mambo gani yaliyotokea hadi taarifa ile ikapatikana.lakini pamoja na hayo sikulazimishi wewe wala yeyote katika familia yenu akubaliane na mimi lakini siku moja ukweli utadhihiri” akasema jaji Elibariki
“ Eli tafadhali naomba tuachane na hili suala kwani limekuwa gumu sana.Vyovyote vile itakavyokuwa mama yangu amekwisha fariki na hatafufuka.Jambo la msingi nililoamua mimi ni kuachana kabisa na suala hili.Kama mama aliuawa basi waliofanya hivyo siku moja watahukumiwa mbele za haki.” Akasema Flaviana
“ Flaviana mimi ni jaji wa Mahakama kuu na siku zote kazi yangu ni kuhakikisha haki imetendeka.Siwezi kuliacha suala hili hadi nifike nalo mwisho na ukweli lazima ujulikane” akasema jaji Elibariki
“ Eli tafadhali nakuomba usiliendeleze tena suala hili kwani tayari baba amekwisha lifunga. .Liache kama lilivyo”
“ Hapana Flavina siwezi kuliacha hivi hivi.Baba yako amenidharau sana na kuniona kama kitu kisicho na thamani yoyote.Nataka nimdhihirishie kwamba siku zote huwa na simama katika haki na ukweli.Sintalala usingizi hadi nimdhihirishie kwamba nilikuwa sahihi na siku zote huwa niko sahihi”akasema jaji Elibariki
“Eli tafadhali naomba kabla hujafanya chochote naomba kwanza tuonane.Please Eli “ akasema Flaviana
“ Ok ninakuja” akasema Elibariki na kukata simu
Wakati Flavina na jaji Elibariki wakiongea simuni,maongezi yao yalikuwa yanasikika katika gari moja jeusi aina ya Ford lililokuwa na watu watatu ndani, kupitia katika chombo Fulani kilichokuwa kimeunagnishwa na simu ya Flaviana bila ya yeye kujua wakati alipopoteza fahamu mchana na kupakiwa katika gari la wagonjwa na kukimbizwa hospitali.Flaviana hakufahamu chochote kuhusiana na simu yake kuunganishwa na chombo maalum ambacho kingeweza kunasa maongezi yoyote ambayo angeongea kupitia simu yake.Mara tu simu ilipokatwa mmoja wa wale jamaa watatu akachukua simu na kuzitafuta namba za Dr Kigomba akapiga
“ Hallow Austin.Kuna habari gani? Ikauliza sauti ya upande wa pili ya Dr Kigomba
“Dr Kigomba tumefanikiwa kunasa maongezi kati ya Flaviana na mumewe.Nina kutumia sasa hivi uyasikilize halafu utuambie nini cha kufanya” akasema Austin na kisha akamtumia Dr Kigomba maongezi yale ya Flaviana na Jaji Elibariki ambayo tayari yalikwisha rekodiwa katika kompyuta.
Dr Kigomba aliyasikiliza kwa makini maongezi yale kati ya Flaviana na mumewe akayarudia kuyasikiliza tena halafu akampigia simu Dr Joshua na kumuomba waonane.Baada ya dakika kumi wakakutana.
“Kuna nini Kigomba? Akauliza Dr Joshua.Dr Kigomba akatoa simu yake na kumpa Dr Joshua asikilize maongezi yale.Akasikiliza na kuyarudia tena kisha akamgeukia Dr Kigomba
“ Dr Kigomba nilikueleza toka mapema kwamba huyu jamaa ni hatari sana.Kama alivyomwambia mkewe kwamba hatalala hadi ahakikishe ametulipua.” akasema Dr Joshua
“ Unashauri nini Dr Joshua” akauliza Dr Kigomba
“ Muondoeni haraka iwezekanavyo.Ila kumbuka kwamba umakini mkubwa unahitajika katika jambo hili ili kuwafanya watu wasiwe na aina yoyote ya shaka.”akasema Dr Kigomba
“ What about an accident? akauliza Dr Kigomba
“ Yes ! do it.Make it looks like real” akasema Dr Joshua
“ Ok Mr President.Hivi sasa Elibariki yuko njiani anakuja na kazi itafanyika usiku wa leo” akasema Dr Kigomba
TUKUTANE TENA SEHEMU IJAYO…
No comments
Post a Comment