SIMULIZI: PENIELA (Season 1 Ep 34)
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Osmund alionekana kuwa na hofu kubwa sana.Kila alipojaribu kupiga simu kwa vijana wake waliokuwa katika mapambano na watu waliokuwa wamekwenda kumkomboa mke wa Dr Michael.Alimuhitaji sana Dr Michael kwa ajili ya kumfanyia upasuaji John Mwaulaya.Hali ya John iliendelea kuwa mbaya na alihitajika daktari kwa haraka na daktari pekee ambaye walimtegemea ni Dr Michael.Aliishika tena simu yake na kupiga
“ hallow bosi” ikasema sauti ya upande wa pili
“ Victor ni kitu gani kinaendelea huko? Kwa nini hampokei simu?
“ Bosi,hali huku ni mbaya sana.Wale jamaa ni hatari sana.Wamefanikiwa kumchukua Yule mwanamke na wameondoka.Watu wetu sita wameuawa lakini na sisi tumefanikiwa kumuua mmoja wao”
Osmund alihisi miguu ikimuisha nguvu akakaa juu ya msingi.
ENDELEA……………………
“ Whats happening to me? Nimeshika tu uongozi ndiyo mambo yote haya yanaanza kutokea.Ugonjwa wa John Mwaulaya,na hawa watu wanaoanza kutufuatilia” Akajiuliza Osmund akiwa amekaa juu ya jiwe.
“ Lakini watu hawa ni akina nani? Wanatafuta nini kwetu? Wametumwa na nani? Kwanini walikuwa wakimfuatilia John?.Wamefahamuje mahala alipokuwa amefichwa mke wa Dr Michael? Osmund akaendelea kujiuliza maswali mfululizo bila kupata jibu
“ Nina wasi wasi kuna watu kati yetu wanaotoa taarifa zetu.Si rahisi kwa mtu wa kawaida kufahamu mahala tulipokuwa tumemficha mke wa Dr Michael.Inabidi tufanye uchunguzi haraka sana ili tubaini kama kuna yeyote ambaye atakuwa akitoa habari zetu na kuwapa hawa jamaa .Nina hakika lazima kuna mtu ambaye anatoa habari zetu na ndiyo maana hawa jamaa wamekuwa wakifahamu kila tunachokifanya.Nitafanya uchunguzi na kama nikifanikiwa kumpata ninaapa nitatoa somo kwa wengine.” Akawaza Osmund halafu akakumbuka kwamba hakuwa ameikata simu akaiweka tena sikioni
“ Hallow Victor ! akaita
“ Hallow bosi,wale jamaa wameondoka na tunasubiri maelekezo yako”
“ Ondokeni sehemu hiyo haraka sana muda wowote polisi wanaweza wakafika.Hakikisheni hakuna mtu yeyote anayebaki hapo hapo.Hakikisheni miili ya watu wote inarejea hapa.Mtu wao aliyeuawa muacheni hapo hapo lakini kata kidole gumba chakulia ili tuweze kumfahamu ni nani.Chukueni pia simu yake na chochote mnaachoona kinaweza kutusaidia.Nawahitaji hapa haraka sana” akasema Osmund na kukata simu.
“ Ninaanza kuwa na wasiwasi sana na Peniela.Nyendo zake zinanitia shaka sana na nina mashaka labda yeye anaweza akawa ndiye anaye toa taarifa zetu kwa wale watu. Nyendo zake sizielewi kabisa.Siku hizi havai tena kile kifaa cha mawasiliano ambacho kinatuwezesha sisi kuwasiliana naye kwa urahisi kila wakati ambacho ni salama zaidi kuliko kutumia simu.Kuna kila sababu ya kuanza kumchunguza Peniela na kuzifahamu nyendo zake.Tunatakiwa kufahamu anafanya nini,anashirikiana na watu gani na tunaweza kugundua kitu.Nina hakika kabisa kwamba tukimchunguza Pennykuna kitu tutakigundua.Nimekuwa na mashaka naye sana” Akawaza Osmund wakati akipanda ngazi kwa kasi kuelekea chumbani kwa John Mwaulaya.Alifungua mlango na kumfuata John kitandani
“ John……John..”akaita.John mwaulaya akafumbua macho
“ Unajisikiaje hivi sasa?
‘ I’m weak, I’m very weak Ossy.” Akasema John Mwaulaya kwa sauti ndogo.Roho ikamuuma sana Osmund kumuonaJohn Mwaulaya akiwa katika hali ile.Akaenda kuegemea kabati
“ Nitafanya nini kuhusiana na John? Nitamtibu vipi? Hali yake inazidikuwa mbaya.Hapa hakuna namna zaidi ya kuwasiliana na makao makuu niwape taarifa hii kwamba tumeshindwa kumtibu John ili waweze kuona namna ya kumsaidia.Daktari tuliyekuwa tukimtegemea ni Dr Michael pekee lakini naye kwa hivi sasa hatutaweza kumpata tena” Osmund akatoka nje akaingia katika chumba kimoja kilichokuwa na kompyuta kadhaa akawakuta vijana wawili.
“ Stanley wataarifu watu wote tukutane hapo chini haraka sana.Kuna jambo zito la kuwafahamisha” akasema Osmund na kutoka akaelekea chini mahala alikoelekeza wakutane
“ Kwa mara ya kwanza ninahisi mambo kutaka kunishinda.I don’t know what I’m going to do.” Akawaza wakati akishuka ngazi.Mara tu baada ya kupata mwito ule toka kwa Stanley watu wote waliokuwepo pale katika nyumba ya John wakakusanyika chini.
“ Ndugu zangu,nimewaita hapa kwa dharura kuna mambo makubwa matatu ambayo nataka kuwaeleza.Jambo la kwanza ni kuhusiana na afya ya mkuu wetu.Kama sote tunavyofahamu kiongozi wetu anaumwa sana na hali yake inazidi kuwa mbaya.Jitihada za kumfanyia upasuaji ili kuokoa maisha yake zinaonekana kugonga mwamba kwani daktari tuliyekuwa tukimtegemea kwa ajili ya upasuaji huo hatutaweza kumpata tena.Kwa sasa ninajaribu kuwasiliana na makao makuu ili tuone namna tunavyoweza kuokoa maisha ya John.Nimeona niwaeleze kuhusu hili kwa sababu kwa hatua aliyofikia hivi sasa anything can happen so we have to be prepared.” Akanyamaza akameza mate na kuendelea
“ Jambo la pili ninalotaka kuwaeleza ni kwamba kuna watu wanatufuatilia.Bado sijafahamu wana tafuta nini kwetu lakini watu hawa wanaonekana ni watu hatari na wanafahamu kila tunachokifanya.Inaonekana kati yetu kuna mtu anayetoa taarifa zetu kwa hawa jamaa.Ninatoa onyo kwamba kwa yeyote atakayebainika kufanya jambo kama hilo adhabu yake ni kali sana.Kila mmoja wakati akijiunga na Team SC41 aliapa kwamba hatatoa siri za aina yoyote lakini inaonekana kuna mtu au watu waliokiuka kiapo chao na kuanza kutoa siri.Uchunguzi mkali unaendelea ili kwanza kuwafahamu wale watu wanaotufuatilia ni akina nani na vile vile kumfahamu mtu anayetoa taarifa zetu kwa wale jamaa.” Akanyamaza tena akawaangalia watu wake na kuendelea
“ Jambo la tatu ninalotaka kuwaeleza ni kwamba usiku huu yametokea makabiliano kati ya watu wetu na hawa jamaa niliwaeleza kwamba wanatufuatilia na katika mapambano hayo tumewapoteza vijana wetu sita na tumefanikiwa kumuua mmoja wao.Hili ni pigo kubwa kuwahi kutokea katika team SC41 .Ninaahidi kwamba tutawasaka watu hawa na kuwapata wote .Usiku huu tutawazika watu wetu ili kesho tuamkie jambo moja tu.Kuwasaka wavamizi hawa.Miili italetwa hapa na tuatwaaga wenzetu na usiku huu tutawazika” akasema Osmund. Halafu akareja katika chumba walichokuwamo wale vijana wawili na kumuita Stanley nje
“ Stanley wewe ni kijana ambaye ninakuamini sana na sina shaka nawe hata kidogo.Kuna kazi ambayo ninahitaji unisaidie kuifanya.”
“kazi gani mkuu? akauliza Stanley
“ Nadhani umefuatilia niliichokuwa nawaeleza wenzako kule chini.Kuna watu wanatufuatilia na wanapata taarifa zetu.Hili ni jambo hatari sana kwetu na kwa serikali ya Marekani na Tanzania kwa maana hiyo basi ninataka ufanye kazi moja ya muhimu sana.Ninataka umchunguze mtu mmoja mmoja katika Team SC41 ,angalia mawasiliano yao katika siku hii ya leo hii ili tuone kama kuna yeyote anayetoa taarifa zetu kwa watu hawa.Jambo hili sitaki mtu mwingine yeyote alifahamu.This is between us .Can you do that for me? Akauliza Osmund
“ Ndiyo ninaweza kufanya hivyo ingawa inaweza kuchukua muda kidogo lakini nitafanya hivyo.Lakini ninaweza kufanya hivyo kwa kutumia vifaa vilivyopo kule makao makuu .”
“ Ok Stanley go, do it”akasema Osmund na kurejea tena katika chumba cha John mwaulaya.Akamfuata palekitandani
“John…”akaita na John akafumbua macho
“ John,nasikitika upasuaji wako hautaweza kufanyika.Daktari tuliyemtegemea hatutaweza kumpata tena.kwa hivi sasa ninawasiliana na makao yetu makuu ili kuona uwezekano wa kukuhamisha na kukupeleka nje ya nchi kwa matibabu ”akasema Osmund kwa masikitiko.John akamfanyia ishara kwamba akipandishe kitanda.Osmund akabonyeza kitufe ukutani na kitanda kikainuka upande wa juu,na kumuwezesha John kukaa
“ Osmund,listen to me my boy.Tafadhali usiwasiliane na makao makuu.Muda wangu umefika and please dont do anything. Its my time to go on rest now”akasema John
“ No John! Don’t give up.Tunafanya kila linalowezekana ili uweze kupona.Ninakwenda kuongea na makao yetu makuu ili tuone uwezekano wa kupata ndege na ukakimbizwa mara moja Marekani kwa matibabu”
“ Osmund tafadhali usisumbuke kijana wangu.You have done enough.Stop wasting your time.”
‘ John ninakuomba usikate tamaa.Tutakushughulikia na utapona”
John akamtazama Osmund na kumwambia
“ Ossy tafadhali naomba uniache mwenyewe.I need to be alone now”akasema John.Osmund akamtazama halafu akatoka kwa kasi .John Mwaulaya akafumba macho na kuendelea kukumbuka
Mambo yaliyotokea usiku ule .Picha ya mtoto mdogo akiwa amelala katika kiti cha nyuma ya gari ikamjia na kwa mbali akatabasamu
“ She was so cute.I didn’t even know her name that night.” akasema kwa sauti ndogo
27 April 1986
Bado mvua kubwa iliendelea kunyesha.John alikuwa amembeba yule mtoto mdogo ambaye tayari alikuwa amelala.
“ You’ll be safe little angel.You’ll be fine.I’ll do everything I can to make sure that you are safe” akawaza John
“ Bosi tunaelekea wapi? Akauliza mmoja wa vijana wake.John hakujibu kitu akachukua simu yake na kuzitafuta namba fulani za simu akapiga.
“ Hallow Martha.” Akasema John baada ya simu yake kupokelewa
“Hallow John” ikasema sauti ya mwanadada aliyeonekana kujawa na usingizi.
“ Samahni nimekuamsha usiku huu”akasema John
“ Bila samahani John.Una tatizo gani?
“ I need to see you”
“ Now? Akauliza Martha
“ yes.Now” akajibu
“ Uko wapi mida hii?
“ Niko barabarani katika hii njia inayoelekea Mkuse Lodge”
“ Ok,naomba unisubiri pale Eusebio night club, nitafika pale muda si mrefu” akasema Martha na kukata simu.John akamuelekeza dereva aliyekuwa akiendesha gari lile mahala walikokuwa wakielekea.Walifika Eusebio Night club na kuegesha gari,bado mvua kubwa iliendelea kunyesha.Baada ya dakika kama kumi na tano hivi ikatokea gari moja ndogo .John akaitambua gari ile.Akachukua koti la mvua na kumfunika yule mtoto akashuka na kuwaamuru vijana wake waendelee na safari ,yeye akaenda hadi katika lile gari ,akafunguliwa mlango na kuingia
“ John..whats going on? akauliza Martha .John hakujibu kitu akalitoa lile koti la mvua na kumstua Martha baada ya kukiona kitoto kidogo.
‘John !!..akasema Martha kwa mshangao
“ What are you doing with this baby? Akauliza
“ Usiulize maswali mengi sana Martha.Mtoto huyu anahitaji sehemu salama na ya siri.Nahitaji msaada wako katika hili” akasema John.Martha akamtazama yule mtoto mdogo akamshika usoni halafu akawasha gari
“ Mama yangu mdogo rafiki yake anayemiliki kituo cha kulelea watoto yatima.Ngoja niwasiliane naye anipe namba zake za simu nimpigie.” Akasema Martha na kusimamisha gari pembeni ya barabara akachukua simu yake na kumpigia mama yake mdogo wakaongea kwa dakika kama tatu akampatia namba za huyo rafiki yake mwenye kituo cha kulelea yatima.Baada ya kuongea na mama yake mdogo,Martha akampigia simu yule mama mwenye kituo cha kulelea watoto yatima akamtaarifu kwamba anahitaji kuongea naye.Ilikuwa ngumu kidogo kwa mama yule kukubali ombi la Martha hadi alipomtajia jina kwamba ameelekezwa na mama yake mdogo ndipo alipokubali kwani ni rafiki yake mkubwa.Alimuelekeza mahala aliko na bila kupoteza wakati wakachoma mafuta kuelekea huko.
Bi Bernadetha Usuwo mmiliki wa kituo kile cha kulelea watoto yatima akawapokea na kutaka kufahamu shida iliyowapeleka kwake usiku ule.John akamdanganya kwamba mtoto yule aliyekuwa amemshika amezaa na mwanamke mmoja ambaye amekuwa ni mlevi na anakesha katika kumbi za usiku akifanya biashara za kujiuza.Aliendelea kudanganya kwamba alipigiwa simu na majirani wa mwanamke huyo ambao walimtaka aokoe maisha ya mwanae kwa kwenda kumchukua na ndipo alipoamua kwenda kumchukua mwanae na kumleta pale ili aweze kupatiwa uangalizi makini.
“ Ouh Jamani kwa nini wasichana wa siku hizi wamekuwa hivi? Unawezaje kumfanyia mambo kama hayo malaika kama huyu? Mtoto huyu bado mdogo tayari anaanza kuruka ruka katika starehe ! Mwanamke mwenye vitendo kama hivyo hafai kabisa kuachiwa mtoto amlee.Umefanya jambo la maana sana kumchukua mwanao.Hapa atalelewa na kupata malezi anayostahili” akasema Bi Bernadetha
“ Ninashukuru sana mama kwa msaada wako huu mkubwa.Pamoja na hayo kuna jambo lingine ambalo ninataka unisaidie”akasema John
“ Jambo gani hilo?
“ Nataka mtoto huyu alelewe kwa siri.Sitaki watu wafahamu kwamba ni mwanangu na wala sitaki mtoto huyu anijue mimi kama baba yake na wala asifahamu kama ana mama.Nitakulipa fedha nyingi kama utanisaidia katika hilo.”
“ kwa nini unataka iwe hivyo John?
“ Ni kwa ajili ya usalama wa mtoto.Yeyote atakayekuuliza kuhusiana na mtoto huyu sema kwamba aliletwa kutokea huko Singida au sehemu nyingine yeyote mbali kabisa na Dar es salaam.Tafadhali mama nakuomba sana unisaidie katika hilo” akaomba John
“ Hii ni ajabu sana.Kwa nini mtoto asifahamu kuhusu wazazi wake ni akina nani?
“ Mama Bernadetha ni vigumu kukuelewesha kwa sasa lakini naomba unisaidie sana katika hilo.Mimi nitagharamia gharama zote za matunzo na malezi yake na atapata kila kitu kinachotakiwa isipokuwa tu hataniona.Nitakuwa karibu nawe ili kuhakikisha anakua katika malezi mazuri na ninakuahidi ataishi maisha ya raha mustarehe kuliko hata mtoto wa rais lakini kitu kimoja tu atakikosa ambacho ni wazazi.” akasema John..Bi Benrnadetha alijaribu kufikiri kuhusu suala lile lakini kiasi kikubwa cha pesa alichoahidiwa na John kikamfanya akubali kufanya vile anavyotaka John
“ Jina lake nani huyu malkia? Akauliza Bi Bernadetha.John na Martha wakaangaliana.Hakuna aliyekuwa akilfahamu jina la yule mtoto.Mara John akajikuta akitamka
“ Peniela.Her name is Peniela”akatamka John.
********
“ Ahsante Mungu kwa kuturejesha nyumbani salama” akasema Dr Michael baada ya kuwasili nyumbani kwa Mathew.Gari lilisimama lakini hakuna aliyetaka kushuka.Wote walionekana kuwa katika hali ya kutoamini kama ni kweli wamerejea salama.Anitha ambaye naye alikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa baada ya kupoteza mawasiliano na akina Mathew ilipoanza kusikika milio ya risasi mfululizo alikuwa amesimama katika kibaraza akiwa na Jaji Elibariki.Wote walishangazwa kuona sekunde zinasonga mbele na hakuna mtu yeyote aliyeshuka mle garini.Kwa wasi wasi mwingi wakalisogelea lile gari .Ilikuwa vigumu kujua nani alikuwamo ndani kutokana na vioo vyeusi vya gari lile.Jaji Elibariki akagonga katika kioo cha mbele upande wa dereva.Taratibu mlango ukafunguliwa akashuka Mathew akiwa ameloa damu.
“ Ouh my God ! Mathew..”akasema Jaji Elibariki.Anitha alistuka sana akamfuata Mathew
“ Pole sana Mathew. ?akauliza Anitha huku machozi yakimlenga.Mathew alitaka kuongea kitu lakini alihisimaumivu makali. Mlango mwingine ukafunguliwa akashuka Noah naye akiwa katika hali kama aliyokuwa nayo Mathew.Alikuwa amechafuka kwa damu.
“Ouh Mungu wangu ! Noah..” akasema Anitha na kwenda kumkumbatia na kumsaidia kusimama vizuri kwani alionekana kushindwa kusimama.Jaji Elibariki akafika mara moja na kumtegemeza akampeleka ndani.Katika mlango wa kati kati akashuka Dr Michael akifuatiwa na mke wake.
“ Dr Michael !! akasema Anitha na kumkumbatia kwa nguvu
“ Ahsante Anitha.Ahsante sana kwa kila kitu.Umetuokoa ” akasema Dr Michael.Mke wa Dr Michael bado aliendelea kumwaga machozi.Mume wake akamkumbatia na kumtuliza akimuhakikishia kwamba anyamaze kulia kwani tayari alikuwa huru.
Mathew alikuwa ameegemea gari lililokuwa na matundu mengi ya risasi.Anitha akamsogelea
“ Pole sana Mathew.Nashindwa kuelezea wasi wasi niliokuwa nao baada ya kuanza kusikia milio ya risasi na ghafla mkapotea.Sijawahi kuogopa kama leo hii.” Akasema halafu akanyamaza kidogo na kuuliza.
“ Where is A…….” kabla hajamaliza kusema alichotaka kukisema Mathew akamkatisha
“ We lost him….”
Anitha akainama.
Dr Michael akamfuata Anitha na kumuomba ampeleke mke wake ndani halafu akamfuata Mathew
“Mathew ,nina mambo mengi ambayo ninataka kuyasema kwako na timu yako lakini kwa sasa nataka niseme maneno mawili tu ahsante sana.Uliniahidi kunirejeshea mke wangu na umefanya hivyo.Mmepambana kufa na kupona ,mmetukinga kwa risasi mimi na mke wangu na mkajeruhiwa kwa risasi ambazo zilipaswa kutupata sisi na mmeturejesha salama.Ninyi ni mashujaa ambao nchi ya Tanzania imejaaliwa kuwapata.Nchi hii inapaswa kujivunia watu kama ninyi.Papo hapo nawapa pole sana kwa kumpoteza Dr Adolf.Naomba nikiri nimekuwa nikiyatazama matukio kama yale katika filamu na leo nimeshuhudia kwa macho yangu namna watu wanavyobadilishana risasi.Nimeogopa sana.Picha ile haitaweza kamwe kufutika kichwani kwangu.” Akasema Dr Michael huku michirizi ya machozi ikionekana mashavuni pake.
“ Dr Michael ahsante nawe pia kwa ushirikiano wako.Sote tumepambana mpaka tukatoka salama.Katika mapigano kama yale mtu mmoja au timu nzima kufa ni kitu cha kawaida sana” akasema Mathew
“ Mathew jeraha linatoa damu nyingi,tafadhali naomba tuingie ndani ili niweze kuwatibu majeraha haya”akasema Dr Michael halafu Jaji Elibariki akamshika mkono Mathew na kumsaidia kutembea kuelekea ndani.
Ndani ya jumba hili la Mathew kulikuwa na chumba maalum cha matibabu.Aliifahamu vyema kazi yake kwamba imezungukwa na hatari muda wote hivyo akatenga chumba maalum kwa ajili ya matibabu pale anapokuwa ameumia.
“ Mathew umejiandaa sana.Hapa una kila kitu kinachohitajika.Hii ni kama hospitali ndogo”akasema Dr Michael wakati akiviweka sawa vifaa kwa ajili ya kumtibu Mathew aliyepigwa risasi mkono wa kushoto.Mathew akalala kitandani na Dr Michael akaanza kumuhudumia akianzia na jeraha la risasi katika mkono wa kushoto.
“ Una bahati sana Mathew.Risasi ile haikupiga mfupa.Imepita pembeni kidogo.Ingepiga mfupa ingekuwa ni hatari zaidi”akasemaDr Michael wakati akiendelea kulitibu jeraha la Mathew.Baada ya kumaliza kulitibu jeraha la Mathew akaendelea pia kumtibu Noah ambaye alikuwa amepigwa risasi ya paja.Wakati Dr Michael akiendelea kumtibu Noah,Mathew alikuwa sebuleni na Anitha na jaji Elibariki ambao walitaka kufahamu kila kitu kilichotokea katika kumkomboa mke wa Dr Michael.
“ Sikuwa nimetegemea kama mapambano yale yangekuwa makubwa kiasi kile.” Akasema Mathew
“ Maelekezo uliyokuwa ukitupatia yalitufikisha katika kanisa lililokuwa likiendelea kujengwa.Tuliwakuta watu wanne waliokuwa wakimlinda mke wa Dr Michael ambao tulipambana nao na kuwamaliza wote na tukafanikiwa kumuokoa mateka.Ghafla wakati tukijiandaa kuondoka,ziliwasili gari tatu na tukajikuta tumezingirwa.Hapo mapambano yakaibuka upya.Inavyoonekana kuna wenzao waliwapa taarifa kwamba tumevamia na ndiyo maana wakaja kwa kasi namna ile.Mapambano ya kujiokoa yalikuwa makali sana .Watu wale walikuja wakiwa wamejipanga vizuri sana wakiwa na silaha kali.“ akasema Mathew
“ Nakumbuka mara ya mwisho ulinitaarifu kwamba tayari mateka mko naye na mnajiandaa kurudi lakini ghafla nikasikia milio ya risasi nadhani ni hapo ndipo wale jamaa walipowazingira.Mawasiliano yalikata ghafla na sikuweza kuwapata tena.”akasema Anitha
“ Eneo lote lilikuwa giza kwa hiyo yalikuwa ni mapambano makali sana.Wale jamaa walikuwa na kifaa kilichokuwa kikifuatilia masafa tuliyokuwa tukitumia kwa hiyo ilikuwa rahisi kwao kuweza kufahamu mahala tulipokuwa tumejificha na hivyo kutuelekezea mashambulizi hivyo tukalazimika kuvitupa.” Akasema Mathew.
“ Tulipambana sana na tukafanikiwa kupata upenyo wa kukimbia. Wakati tukiingia katika gari kuna mtu mmoja alivurumisha risasi ambazo zilitakiwa kumpata Dr Michael lakini anali Adolf akalazimika kumkinga na risasi zile zikampata na kumuua pale pale.Tulishindwa namna ya kuondoka naye kwa namna risasi zilivyokuwa zikivurumishwa kwetu.” Akasema Mathew
“ Watu hawa ni akina nani?akauliza jaji Elibariki kwa uoga
“ Team SC41 “ akasema Mathew
“ Team SC41? Elibariki akauliza kwa mshangao
“ Ni nani haoTeam SC41? akauliza Elibariki
“ Ni habari ndefu sana nitakueleza baadae kwa sasa bado kuna kazi ya muhimu sana ambayo tunatakiwa kuikamilisha.” Akasema Mathew na kuinuka akamfuata Dr Michael ambaye alikuwa akimalizia kumtibu Noah Jeraha la risasi katika paja lake.
“ Dr Michael tayari nimeitimiza ahadi yako na sasa ni zamu yako kumalizia ile kazi yetu” akasema Mathew.Dr Michael akamgeukia na kumtazama akatabasamu
“ Mathew nilidhani utahitaji muda zaidi wa kupumzika baada ya tuko lile la usiku wa leo na isitoshe jeraha lako lilikuwa linavuja damu nyingi .”akasema Dr Michael
“ Dr Michael,sisi tuko vitani na tunapokuwa vitani tunapambana hadi dakika ya mwisho bila kuchoka,we fight like devils.We never give up.Majeraha ni kitu cha kawaida katika mapambano kama haya kwa hiyo usitishike na jeraha kama hili.Kazi ile lazima imalizike usiku wa leo.”akasema Mathew.Dr Michael akamfunga Noah bandeji halafu akamchoma sindano halafu akamuomba Mathew wasaidiane kumpeleka chumbani kupumzika.Noah aliachwa chumbani akipumzika ,Mathew na Dr Michael wakaelekea sebuleni.
“ Dr Michael kutokana na hali halisi ilivyo hivi sasa wale jamaa wataendelea kukufuatilia kwa karibu sana.Sikushauri uchunguzi wa zile sampuli ukaufanyie pale hospitalini kwako.Hakuna sehemu ambako tunaweza kwenda usiku huu ukafanya uchunguzi huo? Tunahitaji majibu kabla ya jua kuchomoza “ Akasema Mathew.Dr Michael akafikiri kidogo na kusema
“Kuna rafiki yangu mmoja anaitwa Dr Robert yeye anamiliki hospitali yake binafsi.Ana maabara kubwa pale na ninaweza kwenda na kuzifanyia uchunguzi sampuli zile tulizonazo”
“ Vizuri sana Dr Michael.Anitha msaidie Dr Michael awasiliane na rafiki yake kwani simu yake haitakiwi kutumika.Team SC 41 lazima watakuwa wakifuatilia ili wafahamu mahala alipo.” akasemaMathew na kuelekea chumbani kwake.Akaegemea kabati lake kubwa na kuyafuta machozi.Picha ya Kanali adolf akimiminiwa risasi ilimjia akilini na kumuumiza sana.
“I’m so sorry Adolf.Umekufa kishujaa “ akasema Mathew halafu akachukua baadhi ya vifaa vyake na kuwafuata akina Anitha
“ Mathew tayari nimekwisha wasiliana na Dr Robert na ameniambia hakuna tatizo naweza kwenda kuitumia maabara ya hospitali yake.” Akasema Dr Michael.
“ Ok Good.Elibariki wewe utabaki hapa pamoja na Noah na familia ya Dr Michael.Sisi tunaenda kuzifanyia uchunguzi sampuli tulizochukua ili kubaini chanzo cha kifo cha Dr Flora.Tutakaporejea tutakuwa tayari na jibu lenye uhakika nini kilimuua” akasema Mathew na kumfuata Noah.
“Noah endelea kupumzika ,tunakwenda kutafuta majibu ya zile sampuli.Elibariki na familia ya Dr Michael watabaki hapa.Protect them.Anitha tunaondoka naye yeye ndiye atakayetuendesha kwani mkono wangu bado una maumivu makali sana.” akasema Mathew kisha akaongozana na Dr Michael,na Anitha wakaingia garini wakaondoka
“ Nilifahamu toka mapema team SC41 ni watu hatari sana.Kwa mara nyingine tena leo hii nimenusurika toka katika mikono yao.Nitapambana nao.safari hii sintaogopa wala kukata tamaa lazima nihakikishe nimepambana nao na kulipa kisasi cha familia yangu na wenzangu walioteketezwa kikatili.Tukio la leo ni salamu kwao kwamba watu wanaopambana nao kwa sasa si wa kawaida.” Akawaza Mathew wakiwa garini
“ kwa sasa tunahamia kwa Peniela.Kwa sasa inabidi tuanze kumchunguza Peniela.Katika hili itabidi kuwatumia akina Elibariki.Tunatakiwa kuzifuatilia nyendo zake.Siku ile wale watu wa Team SC41 walitokea kwake ndipo wakaelekea hospitali kwa John Mwaulaya.Ninashawishika kuamini kwamba yawezekana kabisa Peniela akawa na mahusiano naTeam SC41.Endapo tutagundua kwamba Penny ana mahusiano na Team SC41 basi nitawaunganisha katika kifo cha Edson.Baada ya hapo tutaanza kuitafuta sababu ya kumuua.Kama ni kweli TeamSC41 walihusika katika mauaji ya Edson it’ll be for something big.very big”akawaza Mathew
TEAM SC41 WANAPATA PIGO LAKWANZA LA KUULIWA KWA VIJANA WAO .WATACHUKUA HATUA GANI? JOHN MWAULAYA NAYE ANAENDELEA KUIKUMBUKA HISTORIA YA PENIELA TOKA UTOTO WAKE HADI HIVI LEO,NI MAMBO GANI YAMO KATIKA HISTORIA YA PENIELA? TUKUTANE TENA KATIKA SEHEMU IJAYO………
No comments
Post a Comment