SIMULIZI: PENIELA (Season 1 Ep 33)

 ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

Wakati Penny na John Mwaulaya wakiwa ndani Osmund aliyekuwa amesimama nje ya mlango wa Joh Mwaulaya akapigiwa simu.Baada ya kuongea na simu ile akamgeukia mwenzake aliyekuwa amesimama naye pale mlangoni

“ We have a situation.Kuna watu wamevamia mahal tulipomficha mke wa Dr Michael na hivi sasa kuna mapambano yanaendelea .Tuma kikosi haraka sana kwenda kutoa msaada.Hakikisha kwa kila namna hawafanikiwi kumchukua mke wa Dr Michael.Hali ya John inazidi kuwa mbaya na tunamtaka sana Dr Michael amfanyie upasuaji ili kuokoa maisha yake.Bila kuendelea kumshikilia mke wake hataweza kuifanya hiyo operesheni.Tafadhali hakikisheni vijana wanarejea hapa wakiwa na mke wa Dr Michael na wale wote waliojaribu kufanya uvamizi huo” akaamrisha Osmund.


ENDELERA……………………..


Peniela alisimama pembeni ya kitanda cha John Mwaulaya akiwa ameshika lile kasha huku akionekana kuchanganyikiwa asijue afanye nini.Alitamani sana John angemfafanulia kuhusiana na kile alichomweleza.

“ Mr John,…” akaita Penny lakini bado John mwaulaya aliendelea kuyafumba macho yake

“ Mr John,please listen to me…” akasema Penny na John akafumbua macho yake akatabasamu na kusema

“ Peniela come closer,hug me” Penny akamsogelea John pale kitandani akainama na kumkumbatia.Katika macho ya John Mwaulaya kulionekana michirizi ya machozi

“ Sasa ninaweza kwenda kwa amani” akasema John Mwaulaya kwa sauti ndogo

“ Penny you can go now.Siku zote usisahau kwamba ninakupenda sana” akasema John

“ Mr John,..Mr John..!! akaita Penny

“Go Penny…go…!! Akasema John mwaulaya halafu akaupeleka mkono chini ya kitanda chake akabonyeza kitufe Fulani na mlango ukafunguliwa akaingia Osmund kwa haraka na moja kwa moja akamfuata John Mwaulaya pale kitandani.

“ John ..!! akaita

“Ossy nataka uniahidi kitu kimoja” akasema John kwa sauti ya chini sana

“ I need you to take a very good care of Penny after I’m gone.Make sure she’s always safe.” akasema John

“ Usijali John nitamuangalia penny ,na atakuwa alama.”

“ One more thing” akasema John

“ Once this mission is over,please let her go.Give her a chance to start her own life.Can you promise me that? Akauliza John

“ Yes ! I give you my word John.I’ll let her go.I’ll help her” akasema Osmund

“ Thank you Osmund.Now escort her out.I need to be alone for a while” akasema John .Osmund akamuangalia halafu akamfuata Peniela na kumuomba amfuate.

“ Amekwambia nini John?akauliza Osmund wakati wakishuka ngazi.

“ Nothing important,alinieleza tu kuhusiana na operesheni inayoendelea.Alinisisitiza kwamba nijitahidi sana kuhakikisha inamalizika haraka iwezekanavyo.”

“ Good.” Akasema Osmund wakati wakishuka ngazi kuelekea chini

“ Katika hilo kasha kuna nini? Akauliza tena Osmund

“ Ni zawadi amenipa”akajibu Penny

“ He loves you so much” akasema Osmund,Penny hakumjibu kitu akatabasamu

Walielekea moja kwa moja hadi katika maegesho ya magari.

“ Penny ningekupeleka nyumbani lakini kuna tatizo limetokea hapa muda si mrefu ambalo linahitaji kushughulikiwa haraka sana.Vile vile John anahitajika kufanyiwa upasuaji kwani hali yake inazidi kuwa mbaya.Kijana huyu atakupeleka nyumbani kwako na nitawasiliana nawe tena baadae.” Akasema Osmund

“ Will he be ok? Akauliza Penny

“ yes ! He’ll be ok.”

“ Nashukuru sana Osmund kukufahamu na kumfahamu pia John Mwaulaya.Namuombea apate nafuu ya haraka na apone ugonjwa unaomsumbua.” akasema Penny na kuingia katika gari.

“ Hata mimi nimefurahi sana kukufahamu Penny.”

“ Hali yake itakapoboreka ninaweza kupata nafasi ya kuonana naye tena?

“ Usijali Penny,nijakujulisha pindi hali yake itakapoboreka na utapata wasaa wa kuonana naye” akasema Osmund aliyeonekana kuwa na haraka ,akaagana na Penny kisha akakimbilia ghorofani.Gari aliyopanda Penny ikaondoka

“ Bado naona kama ndoto ,kuonana na mtu ambaye nimekuwa nikihitaji sana kuonana naye ili anipe majibu ya maswali yangu mengi.Kwa bahati mbaya sana nimekutana naye katika siku zake za mwisho.Kwa hali aliyonayo sina hakika kama bado ana maisha marefu.Laiti ningepata nafasi ya kuonana naye tena”akawaza Penny akiwa garini akirejeshwa kwake

“ John Mwaulaya amekuwa akiyaongoza maisha yangu toka nikiwa mtoto mdogo.Kila nilichokuwa nikikifanya ni nilikifanya kwa maongozi yake.Nimefurahi sana kumuona lakini pamoja na furaha hiyo bado sijaweza kupata kile nilichokuwa nikikihitaji kukipata toka kwake .Nilihitaji sana anieleze kwa mdomo wakemimi ni nani? Familia yangu iko wapi? Kwa nini nikalelewa katika nyumba ya yatima?Kwa nini aliniingiza katika kazi hii?Akaendelea kujiuliza halafu akalishika lile kasha akalitazama kwa makini

“ Kasha hili ndilo lenye kila kitu kuhusiana na mimi.Kwa mujibu wa John ni kwamba kasha hili haliko peke yake.Kuna mengine matatu kama hili na nikiyapata yote ndipo nitakapoweza kufahamu kila kitu.Mchungaji Edmund Dawson nitampata wapi? Anahusika vipi na team SC41? Mambo haya yanachanganya sana “akainama akazama katika mawazo.

“ Nitalihifahdhi wapi kasha hili sehemu yenye usalama? Kwa mujibu wa john ninatakiwa nilihifadhi sehemu salama sana.Siwezi kulificha kwangu kwa sababu tayari watu wale wanaweza wakafika kwangu muda wowote na wakaingia wakalichukua” akawaza


********


Alipohakikisha Peniela ameondoka ,Osmund akarejea haraka chumbani kwa John.

“ Penny tayari ameondoka” Osmund akamweleza John

“ Thank you Ossy,” akajibu John kwa sauti ya chini

“ Kwa sasa unajisikiaje John?

“Hali yangu si nzuri hata kidogo.I don’t know if I’m going to make it”

“ John don’t worry.You are going to make it.You are going to be ok.Kila kitu kinaandaliwa hivi sasa ”akasema Osmund.John akamfanyia ishara kwamba atoke mle chumbani anahitaji kuwa peke yake.Akafumba macho na kumbu kumbu Fulani ikamjia

“ Its been years…!!! Akanong’ona na kumbu kumbu zikamrejesha tarehe 26 April 1986


26 April 1986

Saa saba za usiku ,mvua kubwa inayesha jijini Dar ,mitaa mingi imefurika maji.Nje ya nyumba moja yenye uzio wa michongoma,gari moja imesimama ikiwa na watu wanne ndani yake. Mtu mmoja aliyekuwa amekaa pembeni ya dereva alikuwa akiongea na simu

“ Frederick ,tayari niko nje ya nyumba ya akina Pamela.Are you sure you want to do this? Akauliza mtu yule

“ John please please you have to do it.Kesho yule msichana na mama yake wanakwenda katika vyombo vya habari na kunitangaza.Tayari nimekwisha taarifiwa na vyanzo vyangu vya habari kwamba kesho Pamela na mama yake wanakutana na waandishi wa habari na wanawaeleza kila kitu.Lengo lao ni kutaka kuniangusha kisiasa.Nina wabaya wangu wengi ambao hawalali wanatafuta namna watakavyoweza kuniangusha.Nimejaribu kutafuta suluhu na Pamela na mama yake lakini hawako tayari kunisikiliza kwani wameahidiwa pesa nyingi sana na wabay wangu kama wakifanikiwa kuniangusha.Sitaki wafike kesho.” Akasema Frederick

John akanyamaza kidogo akafikiri na kuuliza

“ What about the baby?

“ Kill them all” akasema Fred.

“ Ok Fred nitakupigia baada ya dakika ishirini.”akasema John kisha akawageukia vijana wake

“ It’s a go.” Akawaambia vijana wale aliokuwa nao garini wakajifunika nyuso zao kwa kofia na kuacha macho tu,wakavaa gloves na kisha wakachukua silaha zao wakashuka na kupenya uzio wa michongoma wakaingia ndani.Mvua kubwa bado iliendelea kupiga ,hivyo hakuna aliyesikia wakati mlango ukifunguliwa .Waliingia ndani na moja kwa moja wakaanza kukagua chumba kimoja baada ya kingine.Nyumba ile ilikuwa na vyumba vitatu vya kulala.Katika chumba kimoja walimkuta msichana mmoja aliyejitambulisha kama msichana wa kazi,chumba cha pili alikutwa msichana Pamela na mtoto wake mchanga,chumba cha tatu kilikuwa ni cha mama yake Pamela ambaye alikuwa amelala na mdogo wake aliyekuja kumtembelea toka kijijini.Wote walikusanywa sebuleni na kufungwa mikono na miguu na kisha kwa amri ya John wakamiminiwa risasi kutoka katika bastora zenye viwambo vya kuzuia sauti.Yalikuwa ni mauaji ya kinyama sana.

“ Vipi kuhusu mtoto?akauliza mmoja wa wale vijana

“ Don’t kill that baby.Tunaondoka naye” akasema John ambaye alimbeba yule mtoto Walikagua nyumba yote na kujaribu kuchukua kila walichoona kinaweza kufaa kuchukuliwa wakaondoka.Wakiwa garini John akampigia simu Fred

“halo Fred…Kazi imemalizika” akasema John

“Ahsante sana John.Sijui nikulipe kitu gani kwa kuniokoa na janga hili.Ninakuahidi John sintokusahau katika maisha yangu kwa namna ulivyonisaidia.Usihofu kitu makubaliano yetu yako pale pale”akasema Fred

“ Usijali Fred wewe ni mtu wangu wa karibu .Pamoja na hayo ninaomba tuonane usiku huu,kuna jambo la muhimu nataka tuongee”

Fred akakaa kimya kwa sekunde kadhaa halafu akasema

“ Kuna jambo gani John? Kuna jambo halikwenda vizuri?

“ Hapana Fred ,kila kitu kimekwenda vizuri.Kuna kitu nataka nikukabidhi” akasema John

“ Tukutane wapi John?

“ Tukutane daraja la mamba” 

John na vijana wake walielekea hadi katika darajala mto Mamba wakasimamisha kandoni mwa daraja.Eneo lile lilikuwa kimya sana.Mto mamba ulikuwa umefurika maji kutokana na mvua kubwa zlizoendelea kunyesha.Baada ya kama dakika arobaini hivi likatokea gari aina ya Range rover Vogue rangi nyeusi.Gari likazima taa na baada ya dakika tano John akashuka ndani ya gari akaliendea lile range rover vogue.Mlango wa ile range rover Vogue ukafunguliwa akashuka mtu mmoja mnene akiwa na mwavuli.Akamkumbatia kwa furaha John

“ Ahsante sana John kwa msaada wako.”akasema yule jamaa

“ Usijali Fred.kazi imemalizika.Kwa sasa uko huru” akasema John

“ Ahsante sana.Umeniokoa sana John.” Akasema Fred

“ Fred,hatuna muda mwingi wa kukaa hapa.Kuna kitu nataka nikakukabidhi katika gari langu.” akasema John wakaelekea katika gari la John.Akaufungua mlango na kumulika tochi .Fred akapatwa na mshangao mkubwa

“ Mtoto !..akashangaa

“ Yah..”

“ Umemtoa wapo huyu mtoto? Akauliza Fred

“ This is your daughter .”

“ My daughter? Fred akashangaa

“ Yah ! Huyu ni mwanao.Hii ni damu yako”akasema John.Fred akamtazama kwa macho makali.

“ You didn’t kill her? Akauliza

“ Sikumuua”

“ kwa nini John? Nilikwambia wamalize wote.Sitaki aina yoyote ya ushahidi.John suala hili si la kufanyia mchezo hata kidogo.These people will haunt me and make sure the take me down”akasema Fred

“ Fred I cant kill an Innocent baby.Huyu ni malaika asiye na kosa lolote.Siwezi kufanya ukatili mkubwa kiasi hiki.I cant kill her” akasema John.Fred akamtazama kwa hasira

“ So what are you going to do with her? Akauliza

“ I don’t know.But right now this is what I’m going to do” akasema John na kwa kasi ya umeme akachomoa bastora yake na kumchakaza Fred kwa risasi.Akaanguka chini.

“ Siko tayari kumuua mtoto mdogo kama huyu asiye na kosa lolote.Sijawahi kufanya ukatili mkubwa kama huo.” Akasema John kisha akaenda katika gari la Gred akalikagua na kuchukua simu ya fred na vitu vingine kadhaa akaingia katika gari lake na kuondoka



Kumbu kumbu ile ikamfanya John afumbe macho kwa uchungu

“ I saved her.I saved Peniela.Nilimuua mama yake na baba yake hakutaka Penny abaki hai.” Akawaza John.

“ Nimefanya mambo mengi mabaya lakini Mungu anaweza akanisamehe kwa jambo hili jema nililolifanya.Nilimuokoa mtoto malaika asiuawe.Mtoto ambaye alitakiwa kuuawa leo hii ndiye aliyejitolea maisha yake kuifanya nchi hii iwe salama” Akawaza John.


*******


Peniela alifikishwa nyumbani kwake.Baada ya kuingia ndani alisimama sebuleni kwake akiangalia namna vitu vilivyokuwa vimesambaratika kutokana na ugomvi wa akina Jason.Akaenda kuketi sofani.

“ Ilibaki kidogo wanaume wale wangeuana hapa ndani.Niliogopa sana kwa namna walivyokuwa wakirushiana makonde.Natamani kufahamu Jaji Elibariki yuko katika hali gani hivi sasa.Aliumizwa sana chupa aliyopigwa na Jason.Niliogopa nikadhani amekufa ”akawaza.

“ Sijui Jason naye yuko wapi mida hii.Nimefanya jambo baya sana la kuwagombanisha wanaume wale.Wote wawili ni watu wangu muhimu na kwa msaada wao nimeweza kuwa huru tena.Bila wao hivi sasa ningekuwa nikiozea gerezani.Nitawatafuta kila mmoja kwa wakati wake wakati wametulia na hawana tena hasira na nitamalizana nao.Nitawaweka sawa .Nitaendelea na kila mmoja kwa wakati wake kwani bado ninawahitaji lakini sitaki tena wawe marafiki na waendelee na mpango wao wa kuchunguza kifo cha Edson kwani ni hatari kwao.Kitu kikubwa ninachotakiwa kukifikiria kwa sasa hivi ni kuhusiana na jambo lililotokea leo,nimeonana na John Mwaulaya mtu ambaye nimekuwa nikihitaji sana kuonana naye kwa miaka mingi.Sikukipata nilichokuwa nikihitaji toka kwake lakini amenipa hili kasha na kudai kwamba kila kitu ninachohitaji kukifahamu kuhusiana na mimi kipo ndani ya hili kasha na mengine mawili ambayo yako sehemu Fulani.Ninatamani sana kulifungua kasha hili hata leo hii lakini John alisema nilifungue baada tu ya kumaliza operesheni hii. “ akalishika tena lile kasha akalitazama

“Nahitaji sehemu salama nikalihifadhi hili kasha kama alivyosema John.Hapa kwangu si sehemu salama hata kidogo.Watu kama Team SC41 wanaweza wakaingia na kufanya chochote wanachokitaka muda wowote.I need somewhere safe”

“ Kama ningekuwa sijawakorofisha akina Jason ningemuomba mmoja wao anihifadhie hili kasha lakini kwa sasa hakuna hata moja anayeweza kulikubali hilo.” Akajaribu tena kufikiri halafu akapata wazo.Akaenda chumbani kwake akachukua simu ile ambayo huitumia kuwasiliana na rais akaishika mkononi.

“ Dr Joshua Yuko katika wakati mgumu sana hivi sasa,kwa kifo cha mkewe lakini sina namna nyingine nahitaji sana msaada wake kwa sasa.” Akawaza Penny na kumpigia Dr Joshua

“ Hallo Penny” akasema Dr Joshua

“ hallow Dr Joshua.How are you?” akasema Penny

“ Niko katika matatizo Penny lakini nimefarijika sana baada ya kuisikia sauti yako malaika wangu.Unaendeleaje?

“ Ninaendela vizuri sana.Iwish I could be there with you right now” akasema Penny kwa sauti ndogo

“ You don’t have an idea of how much I need you by my side Penny.Kwa nyakati kama hizi ni wewe pekee ambaye unaweza ukanifariji na kuniondolea ukiwa.Uko wapi mida hii?

“ Niko nyumbani nimejipumzisha” akasema Penny

“ Maandalizi ya mazishi yanakwendaje?

“ Tunatarajia kuzika kesho kutwa alasiri kijijini kwao.Kesho kutakuwa na zoezi la kuuaga mwili hapa nyumbani “ akasema

“ Pole sana Dr Joshua”

“Ahsante sana Peniela.Nimekwisha poa.Ni mapenzi ya Mungu .Ninatamani sana baada ya shughuli za msiba kumalizika nipate wasaa wa kukaa nawe tuongee.Tatizo ni kwamba siwezi kufika hapo unapoishi.kwanini lakini ulikataa kuishi katika ile nyumba niliyokupatia penny? akauliza Dr Joshua

“Hiyo ndiyo sababu iliyonifanya nikupigie simu Dr Joshua.Niko tayari kuishi katika ilenyumba.”

“ Unasema kweli Penny?

“kweli Dr Joshua niko tayari kuishi pale ili mradi unihakikishie ni sehemu salama”

“ Penny nimefurahi sana kusikia kwamba uko tayari kuishi pale.Kuhusu usalama usihofu,pale ni sehemu salama mno.Nitakuwekea ulinzi wa kutosha kila sehemu utakayokuwa kwa hiyo usiwe na wasiwasi wowote kuhusiana na usalama wako.”

“ Dr Joshua nitaishi pale lakini kuna jambo moja ninalotaka kukuomba”

“ Omba chochote penny katika dunia hii nitakupatia isipokuwa roho yangu”

“ Sihitaji ulinzi wa aina yoyote.Sihitaji mtu wa kunifuatilia kuhusu maisha yangu.Siku nikigundua kwamba umeniwekawalinzi hata wa siri,Dr Joshua kutakuwa na mgogoro mkubwa kati yangu na wewe”

“ lakini peniela hii ni kwa ajili ya usalama wako.Kama mke wa rais mtarajiwa unahitaji ulinzi .Ok sintakuweka walinzi lakini promise me that we’ll talk about this”

“ Yes Dr Joshua we’ll talk about this ” akasema Penny.

“ Nimefurahi sana Penny kwa jambo hili .Lini unahamia? Akauliza Dr Joshua

“ Kesho” akajibu

“ Kesho?! Akauliza Dr Joshua

“ Ndiyo kesho.Kuna tatizo lolote?

“ Hakuna tatizo Peniela.Nitamkabidhi Kareem jukumu hili atalishughulikia yeye kesho.Wewe usisumbuke na kitu chochote.”

“nashukuru sana Dr Joshua.” Akasema penny

Kimya kikapita halafu Dr Joshua akasema

“ Penny I love you.More than you can imagine”

Penny akatabasamu na kusema

“ I love you too Joshua “ akasema Penny na kukata simu ingawa Dr Joshua alihitaji sana kuendelea kuongea naye


******

Osmund alionekana kuwa na hofu kubwa sana.Kila alipojaribu kupiga simu kwa vijana wake waliokuwa katika mapambano na watu waliokuwa wamekwenda kumkomboa mke wa Dr Michael.Alimuhitaji sana Dr Michael kwa ajili ya kumfanyia upasuaji John Mwaulaya.Hali ya John iliendelea kuwa mbaya na alihitajika daktari kwa haraka na daktari pekee ambaye walimtegemea ni Dr Michael.Aliishika tena simu yake na kupiga

“ hallow bosi” ikasema sauti ya upande wa pili

“ Victor ni kitu gani kinaendelea huko? Kwa nini hampokei simu?

“ Bosi,hali huku ni mbaya sana.Wale jamaa ni hatari sana.Wamefanikiwa kumchukua Yule mwanamke na wameondoka.Watu wetu sita wameuawa lakini na sisi tumefanikiwa kumuua mmoja wao”

Osmund alihisi miguu ikimuisha nguvu akakaa juu ya msingi.


MEK WA DR MICHAEL AMEFANIKIWA KUOKOLEWA NA MTU MMOJA AMEUAWA.NI NANI ALIYEUAWA? NDANI YA KASHA ALILOPEWA PENNY KUNA NINI? USIKOSE SEHEMU IJAYO………

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...