SIMULIZI: PENIELA (Season 2 Ep 15)
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Kitu gani kilipeleka ukabadili sura yako ? akauliza Peniela
“ Penny kuna mambo mengi sana ambayo huyafahamu na ninatamani sana kukueleza lakini ninashindwa kwa sababu Team SC41 si sehemu sahihi unayostahili kuwepo.”
Peniela akamtazama John na kusema
“ Bado hujanieleza ni kwa nini team Sc41 wameshindwa kukupatia matibabu?akauliza tena Penny
“ Its because I’m dead “
“ You are dead? Akauliza Penny kwa mshangao
“ Yes I’m dead” akasema
“ Ninashindwa kuelewa baba John umekufa vipi?
“ Ngoja niliweke hivi ili unielewe.Ni kwamba kwa miaka kadhaa sasa hivi ninajulikana kwamba nimekwisha fariki.Mimi ni mtu niliyekuwa nikitafutwa sana na serikali mbalimbali duniani kwa hiyo nililazimika kutumia njia hii ya kutengeneza kifo changu ili nisiendelee kutafutwa na ndiyo maana kuna ugumu mkubwa kwa mimi kutibiwa hapa nchini na nje ya nchi”akasema John
“ Kitu gani kilisababisha utafutwe? Akauliza Peniela
“ Nilifanya jambo kubwa sana ambalo sintaweza kukueleza” akasema John
ENDELEA…………………..
Peniela alimuangalia John Mwaulaya na kusema
“ Ni jambo gani baba ambalo huwezi kunieleza? Akauliza Peniela
“ Peniela kuna mambo mengi sana ambayo siwezi kukueleza.Itakuwa vyema endapo hutayafahamu” akasema John na kufumba macho akakumbuka tukio moja kubwa alilowahi kulifanya na ambalo lilisababisha abadilishe sura yake kwa mara ya pili.
Ni siku ya jumanne asubuhi John akiwa ofisini kwake ukaingia ujumbe katika anuani yake ya barua pepe.Ujumbe ule ulitoka katika makao makuu ya Team SC41 Marekani.Katika ujumbe ule alitaarifiwa kwamba kuna kiongozi mmoja wa kidini kutoka nchini Uingereza anakuja Tanzania kwa ziara ya kidini.Ziara ya kiongozi huyo wa kidini imebeba ajenda kubwa nyuma yake kwani anakuja kuzungumza na serikali ya Tanzania kuhusiana na kutoruhusu uwekezaji wowote wa marekani katika madini ya Uranium.Kwani kwa siku za karibuni Marekani imeonyesha kutaka kufanya uwekezaji mkubwa sana katika uchimbaji wa madini ya Uranium nchini Tanzania.Taarifa ile ilimtaka John na Team SC41 wahakikishe kwamba kiongozi yule wa kidini anauawa kabla hajaonana na rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mazungumzo ya faragha.
John mwaulaya aliusoma tena ujumbe ule kwa makini,akaurudia tena na tena na kuuelewa.
“ Ninatakiwa kumuua kiongozi wa kidini ! akasema kwa sauti ndogo
“ Hii si kazi rahisi hata kidogo.Ni jambo zito ambalo sikuwahi kulifanya toka kujiunga na Team SC41.” Akawaza John na kuegemea kiti chake akafikiri sana na baada ya kama nusu saa hivi akawaita vijana wake katika chumba cha mikutano
“ Nimepokea maelekezo toka makao makuu kwamba kuna kiongozi mmoja wa kidini anatoka nchini Uingereza atafanya ziara ya kichungaji nchini Tanzania.Ziara hiyo imebeba ajenda kubwa nyuma yake.Katika ziara hiyo kiongozi huyo mkuu wa kidini anataka kuja kuishawishi serikali ya Tanzania kutoruhusu uwekezaji wowote wa madini ya Uranium unataka kufanywa na Marekani.Kwa kuwekeza katika kuchimba madini ya Uranium Marekani itakuwa imekiuka makualiano yaliyofikiwa kati ya mataifa yenye nguvu za kinyuklia duniani kwamba waendelee kupunguza matumizi ya nishati hii ya nyuklia lakini Marekani imeonekana kutaka kuongeza idadi ya vinu vya nyuklia katika kuzalisha nishati ya umeme.Makao makuu wanahitaji kiogozi huyu wa kidini auawe kabla hajaonana na rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.” Akasema John na kuwatazama vijana wake.
“ Jambo hili ni kubwa na kumuua kiongozi mkubwa kama huyu si kazi rahisi lakini kwa kuwa tnfanya kazi kwa maslahi ya Marekani lazima tuifanye.Ilitufanikiwe lazima tubuni mkakati mzito sana utakaotuwezesha kumuua kiongozi huyo.Mkakati nilioubuni nikwamba itaabidi mmoja wetu ajifanye ni mchungaji na ajumuike pamoja na wachugaji wengine katika kumpokea kiongozi huyo toka Uingereza.Hili ni jambo zito na linalohitaji umakini mkubwa kwa hiyo nitasimama mimi mwenyewe katika kuifanya shughuli hii kwani hakutakiwi kosa lolote hapa.Nitakachokifanya ni kwamba nitakuwa na pete mkononi ambayo itakuwa imepakwa sumu na katika pete hiyo kuna kisindano kidogo sana ambacho si rahisi kusikia kama kimekuchoma.Nikishikana mkono tu na kiogozi huyo na kisindano kile kikifanikiwa kumchoma basi sumu ile kali husambaa haraka sana mwilini atakufa ndani ya dakika kumi na tano tu.Kuhusu changamoto ya ulinzi ni kweli ulinzi utakuwepo lakini hautakuwa ni ulinzi mkubwa sana kwani huyu si kiongozi wa kiserikali japokuwa ni kiongozi mwenye heshima kubwa sana nchini mwao.” John Mwaulaya akawaambia vijana wake na kisha wakaanza mikakati kabambe ya maandalizi ya mpango ule .
Siku ya siku ikawadia ambapo askofu Wilbert young Jr akitokea nchini Uingereza akawasili nchini na kupokewa na viongozi kadhaa wa dhehebu lake na kisha msafara wake ukaelekea katika kanisa kuu la dhehebu lake .Katika njia ya kuelekea ofisi kuu viongozi zaidi ya ishirini toka katika madhehebu mbali mbali walikuwa wamejipanga kwa ajili ya kuonyesha mshikamano wao kwa kiongozi huyu mkubwa ambaye alikuwa akisalimiana na mmoja mmoja.Miongoni mwa watu waliokuwemo katika mstari ule wa kusalimiana na kiongozi yule alikuwepo mtu mmoja aliyevalia mavazi nadhfu ya kichungani na alionekana kama mchungaji kijana sana.Hakuna aliyeweza kudhani kwamba mtu yule aliyekuwa miongoni mwao akiwa na sura yenye tabasamu la kichungaji alikuwa ni mtu hatari sana.Huyu alikuwa John Mwaulaya kiongozi wa team SC41.Kiongozi yule wa kidini alishikana mkono na John Mwaulaya wakasalimiana na alionyesha kufurahi sana kukutana na mchungaji kijana kama John na kumtaka azidi kumtumaini Mungu nasiku moja atafika mbali katika kazi yake ya utumishi.Katika viongozi wote waliokuwe popale ,ni John peke yake ambaye alionekana kuchukua muda kidogo kuzungumza na Askofu Wilbert.Zoezi la kusalimiana na wachungaji wengine na maaskofu liliendelea halafu askofu Wilbert akakaribishwa kuingia ofisi kuu ambako kulikuwa na kikao kifupi cha ukaribisho kabla ya kuendelea na ratiba nyingne alizopangiwa .Wakati askofu mkuu wa Tanzania akitoa maeneno ya kumkaribisha askofu Wilbert alianza kujisikia vibaya akaomba apatiwe maji ya akanywa lakini akazidi kujisikia vibaya na ghafla akajikuta akiishiwa ngucvu na kuanguka chini.Kizaa zaa kikaibuka na gari la wagonjwa likaitwa haraka sana wakampakia askofu Wilbert wakamkimbiza hospitali lakini hawakufanikiwa kufika askofu Wilbert akafariki.
Taarifa za kifo cha askofu Wilbert ziliistua sana serikali ya Uingereza na raia wake kwani askofu yule ni mtu aliyekuwa anaheshima kubwa ndani ya nchi ya Uingereza.Mstuko haukuwa kwa serikali ya Uingereza peke bali kwa serikali nyingi duniani zilistuswa sana na tuko lile ikiwemo serikali ya Tanzania.
Kufuatia tukio lile serikali ya Tanzania ikishirkiana na seriakali ya Uingereza walianzisha uchunguzi mkubwa ili kufahamu ni nani hasa waliofanya kitendo kile kwani ilithibitika kwamba Askofu Wilbert aliuawa kwa sumu.Ilimlazimu John mwaulaya kufanyiwa upasuaji wa kuibadili sura yake ili kupoteza kila aina ya ushahidi kwani taarifa kulikuwa na kila dalili za kugundulika kwamba ndiye aliyefanya mauaji yale.Pamoja na kumbadili John Mwaulaya sura lakini iliwalazimu pia kutengeneza kifo chake na baada ya miezi sita kupita ya uchunguzi wa kifo cha askofu Wilbert taarifa ilitoka na kubainisha kwamba aliyemuua ni mtu mwenye uraia wa Tanzania na marekani lakini taarifa ikaonyesha kwamba mtu yule ambaye alifahamika kwa jina la bandia la Moses Lupakise na taarifa zake zote zikasambazwa kila mahala duniani ili atakapoonekana akamatwe lakini baadae tayari ikatolewa kwamba Moses alikwisha fariki dunia.Hiyo ni sababu kubwa iliyowafanya team SC 41 kushindwa kumpeleka John nchini marekani kwa matibabu.
“ John ! ..Peniela akamstua John aliyekuwa amefumba macho akikumbuka mbali sana.
“Peniela samahani nilikuwa mbali sana kimawazo.Umenifanya nikumbuke mambo mengi sana makubwa” akasema John .Peniela akamtazama na kusema
“ Samahani kwa kukukumbusha mambo ambayo umekwisha yasahau”
“ Usijali Peniela.Kichwa changu kimejaa kumbukumbu nyingi mbaya ambazo najaribu sana kuzisahau lakini ninashindwa.”
“ Usiwaze sana kuhusiana na mambo yaliyopita.Kitu kikubwa kwa sasa ni kushughulika na afya yako ,utibiwe na upone uendelee na maisha yako ya kawaida.Niambie ni kitu gani ninachoweza kukifanya ili kukutibu?
“ Peniela ahsante kwa kunijali lakini kwa sasa sina hakika kama nitapona tena.Hali yangu japokuwa inaimarika lakini ninajua kwamba sina muda mrefu wa kuishi kwa hiyo hakuna haja ya kupoteza nguvu kunihudumia.Its my time to face death”
“usiseme hivyo John,ninakuhitaji sana katika maisha yangu.Wewe bado ni mtumuhimu sana katika maisha yangu.Umenihudumia angali nikiwa mdogo na ni wakati wangu sasa kukuhudumia na kuhakikisha kwamba unapona .Wewe ndiye baba ninayekufahamu ,kwa hiyo naomba uniruhusu nikuhudumie upone.I need to spend much time with you.I don’t want you to die” akasema Peniela huku machozi yakimtoka.John akamuonea huruma sana binti yule akamfanyia ishara amsogelee.Penny akaketi katka kitanda cha John
“ kwa mara ya kwanza leo hii umenifanya nibadili msimamo wangu.Ninataka kuendelea kuishi tena kwa sababu yako.Nataka niyatengeneze maisha yako upya kwani ni mimi niliyeyaharibu kwa kukuingiza huku Team SC41.” Akasema John.
“ Nashukuru sana John kwa kuendelea kunithamini .Nashukuru sana kwa kukubali kutibiwa” akasema Peniela.John Mwaulaya akafumba macho akafikri kidogo na kusema
“ Kuna daktari mmoja ambaye nitakupa mawasiliano yake anaitwa ni rafiki yangu sana utawasiliana naye na utamfahamisha hali yangu na halafu tatakupa jibu nini anaweza akafanya.Huyu ni daktari ambaye nina hakika anaweza akanitibu”
“ Kama ulikuwa na daktari mtaalamu kama huyu kwa nini hukumtafuta mapema toka awali na ukasubiri hadi hali yako imefikia hapa ? Akauliza Peniela
“ Sikuwa nikihitaji kuishi .Nilikata tamaa na maisha yangu kwani sikuona tena thamani ya kuendelea kuishi kutokana na mambo mengi mabaya niliyoyafanya “
“ Ndiyo maana ninataka utibiwe upone .You deserve a second chance.”
“ Second chance? Akauliza
“ Yes you deserve a second chance .Pengine ni mpango wa Mungu ili uweze kuyabadili maisha yako” akasema Peniela.John akamtazama na kusema
“ Do you believe in God? Peniela Akakaa kimya
“ Una fikiri Mungu anaweza akanisamehe makosa yote niliyoyatenda? Akauliza John.
“ John kwa sasa tunachotaka kushughulika nacho ni afya yako na baada ya hapo haya mambo mengine ya kiimani kama unahitaji ushauri wao utawaona viongozi wa dini lakini kwa sasa unatakiwa kwanza upone” akasema Peniela.John akamuelekeza amletee kitabu alichoandika namba mbalimbali za simu akampatia mawasilano ya daktari rafiki yake.
Baada ya kupewa namba zile Peniela hakutaka kuendelea kupoteza wakati akamuaga John na kuondoka.Hakutaka kupoteza muda mwingi pale kwa John kwani alimuacha jaji Elibariki peke yake nyumbani
*******
Ilikuwa ni siku ndefu sana iliyoambatana na matukio mengi.Wakati bado watu wakiendelea kutafakari mahala alipo jaji Elibariki na sababu ya gari lake kushambuliwa ,watu wawili walikutwa wamekufa kwa kupigwa risasi katika chumba cha hoteli ambao mmoja alikuwa raia wa Marekani na mwingine raia wa Tanzania.
Saa kumi na mbili za jioni Dr Joshua alirejea nyumbani akitokea kijijini alikozaliwa mke wake Dr Flora walikoenda kumzika.Mara tu baada ya kuwasili nyumbani Flaviana akamfuata baba yake na kumuuliza kama kuna taarifa zozote amezipata kuhusiana na uchunguzi unaoendelea ili kuwabaini walioshambulia gari la mumewe na mahala aliko Elibariki.
“Mpaka sasa hivi sijapokea taarifa zozote za kuhusiana na tukio lile.Naomba unipe muda kidogo ili niwasiliane na watu wangu nijue wamefikia wapi” akasema Dr Joshua.
Bila kupoteza muda Dr Joshua akawaita Dr Kigomba na captain Amos ambao ni washirika wake wa karibu na kutaka kupata ripoti ya kinachoendelea kuhusiana na kumtafuta Elibariki
“ Mpaka jioni hii Elibariki hajaonekana na hajulikani yuko wapi.Hakuna uhakika kama alitoka hai katika shambulio lile ama alikuwa mzima.Na hata kama alikuwa mzima basi nina uhakika mkubwa sana kwamba lazima atakuwa amejeruhiwa.Vijana wamekuwa wakizungukia hospitali zote kubwa na zahanati ili kutaka kufahamu kama kuna mgonjwa alifika kutibiwa akiwa na majeraha ya risasi lakini hakuna hata hospitali moja iliyothibitisha kumtibu mgonjwa mwenye jeraha la risasi.”akasema Dr Kigomba
“ Kwa hiyo unataka tuamini vipi? Kwamba Elibariki amefariki dunia ? akauliza Dr Joshua
“ Sina hakika sana kama alikufa ama bado yuko hai.Ili kufahamu kama Elibariki mzima au alikufa inatubidi kwanza tumfahamu mtu ambaye alikuwa akipambana na vijana wetu.Bado mpaka sasa hivi hatujafanikiwa kumfahamu mtu huyo ni nani .Lakini ni wazi kwamba mtu yule alikuwa akipambana kumsaidia Elibariki na nina hakika ni huyu ndiye aliyemtoa alibariki pale na kumpeleka mafichoni kwa hiyo kama tunataka kufahamu mahala alipo Elibariki na kama ni mzima ama alikufa basi tunatakiwa kumfahamu huyu mtu ni nani” akasema Dr Kigomba
“ Kuna ugumu gani wa kumfahamu mtu huyo? Sisi ndio tulioishika nchi hii na kila kitu kiko chini yetu kwa hiyo tunatakiwa tutumie kila aina ya mbinu ili kuweza kumpata huyo mtu ambaye nina hakika kabisa kwamba tayari anafahamu kila kitu kuhusiana na sisi na amekuwa akitufuatilia.Nina uhakika kabisa kwamba siri yetu tayari imekwisha julikana .Lakini kuna jambo ambalo nimelifikiria sana siku ya leo” akasema Dr Joshua
“ Jambo gani hilo? Akauliza Captain Amos
“ Tulianza vizuri mpango wetu na tumekwenda viuri sana lakini hapa karibu na kufika mwisho kumeanza kutokea mambo ambayo yanahatarisha kuharibika kabisa kwa mpango wote.Na kama tusipokuwa makini basi tunaweza kujikuta tukipoteza kila kitu na kushindwa kufikia malengo yetu.Mtu wa kwanza ambaye aliapa kuharibu kila kitu alikuwa ni Frola ambaye tayari tumekwisha muondoa.Baada ya Flora kumeibuka tena kikwazo kingine ambacho ni Elibariki na huyo mtu aliyemsaidia jana.Elibariki amefahamu kilichomuua Flora na kama atakuwa amenusurika katika ajali basi lazima atataka kulichimba kwa undani suala hili .Tusimpe nafasi ya kufanya hivyo.Kwa ajili hiyo basi nimefikiria sana na kuona kwamba kuna umuhimu wa kumaliza kila kitu haraka sana,kwa sababu endapo tukiendelea kuvuta muda tutajikuta tukishindwa kabisa kufikia mwisho kwa hiyo basi ninataka kuanza mawasiliano na wale jamaa zetu ili ndani ya wiki mbili wawe wamejikamilisha na kutupatia fedha zetu ili tuwape mzigo wao.Hakuna haja ya kuendelea kuogopa na hatuwezi kuziachia trilioni hizi nyingi za fedha ambazo watatumia hadi vitukuu vyetu kwa maana hiyo basi kwa sasa endeleeni kuhakikisha kwamba hakuna jambo lolote litakalojitokeza kuharibu mpango wetu na tukifanikiwa kumaliza salama hatutakuwa na wasi wasi tena na Elibariki wala huyo mwenzake” akasema Dr Joshua
“ Hilo ni wazo zuri sana Dr Joshua.Ni kweli hakuna haja ya kuendelea kulivuta sana suala hili kwa hiyo kuimaliza biashara hii ndani ya muda mfupi ujao itakuwa vizuri sana kwani kadiri siku zinavyozidi kwenda yanazidi kuibuka mambo mapya kila siku” akasema Captain Amos
“ Ok jamani shughulikieni suala hilo la kuwatafuta Elibariki na huyo mwenzake na mimi nitawasiliana na watu wetu na kuwafahamisha kwamba tumeamua kufanya biashara hii haraka iwezekanavyo”akasema Dr Joshua kisha wakaondoka.
“nadhani kulimaliza suala hili kwa haraka ndilo jambola msingi kwa sasa.Nimeanza kuingiwa na wasiwasi kwamba kuna hatari ya kuyakosa yale matrilioni ya fedha.Karibu nitamaliza muda wangu wa uongozi na kwa hiyo ninataka baada ya kumaliza muda wangu wa kuongoza nimchukue Peniela niondoke naye nikaishi naye mbali kabisa maisha ya kifalme nikifurahia uzee wangu.Nimemkumbuka sana huyu binti ngoja nimpigie simu.Peniela ni mwanamke ambaye ananifanya nijione kama kijana wa miaka thelathini nikiwa naye.Ningefanya kosa kubwa sana kama ningekubali peniela akafungwa gerezani.Nitamfanyia mambo makubwa binti yule na hatawafikiria tena vijana ambao hawawezi kumpa chochote.” Akawaza Dr Joshua na kuchuk ua simu yake akampiga simu Peniela
“ Hallow Peniela” akasema Dr Joshua baada ya Peniela kupokea simu
“ hallow Dr Joshua habari yako?Umeshindaje leo? Tayari umekwisha rejea?akauliza Peniela ambaye alikuwa ametoka nje kuongea na Dr Joshua akiogopa jaji Elibariki kusikia maongezi yale
“ Nimerudi salama na tumemaliza salama kumzika Flora.Umeshinda salama?
“Mimi nimeshinda salama Dr Joshua.Niliyekuwa nakuhofia ni wewe tu”
“ Hata mimi nilikuwa nakuwaza sana Peniela.Natamani hata muda huu ningekuja nikuone kama ungekuwa katika ile nyumba niliyokupa.” Akasema dr Joshua
“ usijali Dr Joshua nikishamaliza shughuli yangu huku nitahamia katika ile nyumba.Hata mimi sipendi kukaa mbali nawe.”
“ Nashukuru sana Peniela kusikia hata wewe unaniwaza.Ninakupenda zaidi ya unavvoweza kufikiri na nitakufanyia mambo makubwa sana ambayo sijawahi kumfanyia mtu yeyote.Utaishi maisha zaidi ya malkia yote haya yatawezekana tu kama ukiniahidi kitu kimoja”
“Kitu gani Dr Joshua?
“Nataka uniahidi kwamba hautaingia katika mahusiano yoyote na hawa vijana na kwamba utakuwa na mimi tu”
“ Dr Joshua kwa sasa kwa vile uko huru basi siwezi kuwa na mahusiano na kijana mwingine yeyote” akasema Peniela na kumfurahisha Dr Joshua
“ Umenifurahisha sana Peniela na ninapenda kukumbusha kwamba ahadi yangu iko pale pale”
“ ahadi gani Dr Joshua?
“ kukuoa” akasema Dr Joshua na kumfanya Peniela atabasamu
“NI mapema sana Dr Joshua kuzungumza kuhusiana na masuala hayo ya kuoana.Bado tuna mambo mengi sana ya ufanya kabla ya kufikia maamuzi hayo makubwa”akasema Peniela
“ Hakuna muda wa kusubiri sana peniela.Ngoja ngoja yaumiza matumbo.Mimi ninakupenda na kwa sasa hakuna kizuizi chochote kinachonifanya nisifunge nawe ndoa.Flora tayari amekwisha kwenda kwa hiyo nina uhuru wa kufanya kila ninachokitaka” akasema Dr Joshua
“ Dr Joshua ni mapema sana kuanza kufikiria masuala kama hayo.Lakini usijali tutapata wasaa mzuri tutaongea na kuyaweka sawa” akasema Peniela.
“ Ok peniela nitakupigia tena baadae ili tuongee kwa undani zaidi kuhusu suala hili”
“ Hapana usinipigie baadae Dr Joshua nimechoka sana leo na ninahitaji kupumzika”akasema peniela wakaagana na dr Joshua akakata simu
“ Huyu mzee anaonekana kifo cha mkewehakijamgusa kabisa.Hainiingii akilini eti hata mkewe hajamaliza siku moja kaburini tayari ameanza kufikiria masuala ya kuioa.laiti angenijua wala asingeongea upuuzi ule .Lakini mbona ninaanza kuingiwa na shaka sana kuhusiana na kauli hizi za Dr Joshua? Toka kipindi kile hata mkewe bado hajafariki alikuwa akinitamkia kwamba mke wake atakufa hivi karibuni na mimi nitakuwa first lady.Ninapatwa na wasiwasi kwamba ya wezekana kifo cha dr Flora kikawa ni cha kupangwa ili mambo anayoyataka Dr Joshua yaweze kutimia” akawaza peniela wakati aiingia chumbani.Akaiweka simu mezani na kupanda kitandani akajilaza pembeni ya jaji Elibariki
“ Elibariki kuna kitu nataka kukuuliza” akasema Peniela
“Uliza Penny”akasema Elibariki
“ Nini kilimuua Dr Flora? Akauliza Peniela na kumstua sana Elibariki
” kwa nini unauliza hivyo Penny?
“ Ninahitaji tu kufahamu” akasema Penny
“ Dr Flora alikufa kwa shinikizo la damu”
“ Are you sure? Akauliza penny
‘ yes I’m sure” akajibu jaji Elibariki na kuendelea kushangaa kwa nini Peniela alimuuliza maswali kama yale.
NI BIASHARA GANI AMBAYO DR JOSHUA NA WENZAKE WANATAKA KUIFANYA? TUKUTANE SEHEMU IJAYO……
No comments
Post a Comment