SIMULIZI: PENIELA (Season 2 Ep 13)

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

“ Unaongea na Peniela” ikasema sauti ya upande wa pili.Yule mwanamke akamgeukia jaji Elibariki

“ Anasema anaitwa Peniela ndiye rafiki yako? Akauliza

“ Ndiyo”

“ Do you trust her? Akauliza tena

“ Ndiyo ninamuamini sana” akasema jaji Elibariki

“ Ok ongea naye” akasema Yule mwanamke na kumpatia Elibariki simu

“ Hallow Peniela Elibariki hapa ninaongea”

“Elibariki?

“Ndiyo ni mimi?

“ Mbona unanishangaza Elibariki? Mbona unanipigia kwa kutumia simu nyingine? Uko wapi ? Uko na nani?

“ Niko katika gari na ….” Elibariki akasita.Yule mwanamke aliyekuwa akiendesha gari akaachia usukani wa gari na kumnyang’anya Elibariki simu

“ Hallow Peniela.Una gari? Akauliza

“ Ndiyo ninalo”

“ Ok vizuri basi washa gari lako sasa hivi na uje pale Kisulo restaurant uje umchukue rafiki yako .He’s in trouble na anahitaji sehemu salama.Tafadhali usimwambie mtu yeyote kuhusiana na jambo hilina uwe na uhakika hakuna mtu anayekufuatilia” Akasema Yule mwanamke na kukata simu.


ENDELEA…………………

Kisulo Restaurant ni moja ya hoteli kubwa na nzuri jijini Dar es salaam ambayo kwa masaa yote huwa imejaa watu kutokana na huduma nzuri wanazozitoa pamoja na chakula kizuri kinachopika hapa.Kila aina ya chakula unachokihitaji basi unaweza ukakipata hapa.Eneo la maegesho la hoteli hii ni kubwa kutokana na idadi kubwa ya watu wanaofika hapa.Gari alilokuwa amepanda jaji Elibariki lililokuwa linaendehshwa na mwanamke ambaye hakumfahamu lilivuka hoteli kidogo na kwenda kusimama mbele yake,yule mwanamke akalizima akatoa bastora yake na kuiweka tayari.Alikuwa na wasiwasi sana yawezekana walikuwa wakifuatiliwa.

“Peniela ! do you trust her? Akarudia tena kuuliza yule mwanamke

“ Yes I do “ akasema Jaji Elibariki

“ kwa nini unaniuliza hivyo? Akaulizia

‘ Ninakuuliza hivyo kwa sababu maisha yako ya sasa hivi yanategemea sana watu unaowaamini.” Akasema yule mwanamke

“ kwani wewe ni nani? Umenifahamuje? Kwa nini umeniokoa? Unawafahamu waliotaka kuniua? Akauliza jaji Elibariki

“ Eliariki nimekwisha kwambia kwamba usitake kunifahamu.Kukuweka sehemu salama ni jukumu langu la kwanza .Nitakutafuta tena baadae.Ila ninachokuonya ni kwamba hutakiwi kabisa kuonekana kwa sasa.Hutakiwi kutoka hadi hapo nitakapokuamuru.” Akasema yule mwanamke.Jaji Elibariki akamtazama na kusema

“ Ninashukuru sana kwa kuniokoa lakini bado ninashauku kubwa ya kutaka kukufahamu wewe ni nani ,na kwa nini umeniokoa? Akauliza .Yule mwanamke hakujibu kitu akatoa simu yake na kuzitafuta namba za simu za Peniela akampigia

“ Hallow Peniela umefika wapi?

“ Nimekaribia sana kufika.” Akajibu Peniela

“ Ok good.Ukifika utalifuata gari Fulani limeegeshwa mbele ya kibanda kile cha kuuza vocha za simu .” akasema Yule mwanamke na kukata simu

“ Elibariki are you sure you’ll be in safe hands? Akauliza yule mwanamke

“ Yes I’m sure” akasema Elibariki

“ Kitu kingine usithubutu kumpigia simu mtu yeyote yule na kumweleza kwamba uko hai na mahala uliko.Si mke wako wala yeyote unayemfahamu mpaka hapo nitakapokuruhusu kufanya hivyo.Tumeelewana Elibariki?

“ Tumeelewana”akajibu jaji Elibariki ambaye bado kila kitu kilichotokea kwake ilikuwa ni kama sinema

“ This woman Peniela ,who is she to you? Akauliza yule mwanamke

“ What ? akauliza jaji Elibariki ambaye alionekana kuwa mbali sana kimawazo

“ nakuuliza huyu Peniela ni nani wako?Ndugu yako,rafiki yako au ni nani wako?

“ Ni rafiki yangu.” Akajibu Jaji Elibariki

“ Unamfahamu? Akauliza jaji Elibariki

“ Hapana simfahamu ila ninahitaji kumfahamu ili nihakikishe kwamba niko katika mikono salama”akasema yule mwanamama

“ Kwa nini umeniokoa? Kwa nini unataka kuhakikisha kwamba niko katika mikono salama? Akauliza jaji Elibariki na mara gari moja ndogo nyeusi ikawapita na kwenda kusimama mbele yao akashuka msichana mmoja ambaye jaji Elibariki akamtambua

“ Thats Peniela” akasema

“ wow she’s so beautiful” akasema yule mwanamke huku akitabasamu na kufungua mlango wa gari akashuka

“ Peniela ! akaita yule mwanamke na Peniela akamsogelea.Alikuwa na wasi wasi mwingi

“ Habari yako” yule mwanamke akamsalimu Peniela

“Nzuri .Elibariki yuko wapi? Is he ok? Akauliza Peniela akiwa na hamu ya kutaka kujua hali ya Elibariki 

“ Usihofu Elbariki ni mzima na anaendelea vizuri .Kumefanyika shambulio usiku huu kuna watu waliotaka kumuua lakini nimefanikiwa kumuokoa. Elibariki anatafutwa auawe kwa hiyo anatakiwa apate sehemu ya kujificha hadi hapo mambo yatakapokaa vizuri Kwa sasa wewe pekee ndiye mtu ambaye anakuamini na anaamini katika mikono yako atakuwa salama.”akasema yule mwanamke

“ Ni akina nani wanaotaka kumuua? Akauliza Peniela akiwa na wasi wasi mwingi

“ Ni mapema mno kusema ni akina nani lakini naomba tu ufahamu hilo kwamba roho ya Elibariki inatafutwa kwa gharama yoyote ile kwa hiyo basi hakikisha kwa kila namna utakavyoweza Elibariki anakuwa salama.Muda wowote ule ukihisi hatari yoyote ile utanipigia simu yangu na kunifahamisha na nitakusaidia.”akasema yule mwanamke



“ kwani wewe ni nani? Akauliza Peniela lakini yule mwanamama hakujibu akaufungua mlango wa gari na kumtoa Jaji Elibariki kwa haraka haraka akaingia katika gari la Peniela kisha yule mwanamke akaondoa gari lake kwa kasi.Kwa muda wa sekunde kadhaa jaji Elibariki na Peniela walibaki wanaangaliana.Peniela aliogopa sana kwa namna Elibariki alivyokuwa ameloa damu

“ Pole sana Elibariki” akasema Penny

“ Ahsante sana Penny”

“ Umeumia mahala kokote?akauliza Peniela

“ Nina jereha hapa katika mkono wa kulia nahisi nimekwaruzwa na risasi na katika mguu ninahisi kuna maumivu makali”

“ Pole sana Elibariki.Nani lakini waliofanya kitu hiki? Unaweza kuwafahamu? Akauliza Peniela

“ Hapana Penny siwezi kuwafahamu ni akina nani lakini nia yao ilikuwa ni kuniua” akasema Elibariki.Penny akawasah gari wakaondoka

“ Nani ametaka kumuua Elibariki? Yawezekana akawa ni Jason akitaka kulipiza kisasi ? Ninaanza kuwa na wasi wasi sana yawezekana kabisa akawa ni Jason huyu ndiye aliyepanga njama hizi.Jason alichukia sana siku ile na nilimuona kabisa kwamba alikuwa na dhamira ya kuua na ndiyo maana alimpiga Elibariki na chupa kichwani.Sioni mwingine anayeweza kufanya jambo kama hili zaidi yake.” Akawaza Peniela

“ Kwa mujibu wa yule mwanamke Elibariki yuko katika hatari kubwa sana ya kuuawa.Lazima nitafute sehemu salama ya kwenda kumuweka.Sehemu ipi ni salama zaidi kumuweka kwa sasa?akajiuliza Peny

“Nyumbani kwangu sina hakika kama ni salama na nina ogopa anaweza akajulikana .Katika ile nyumba mpya niliyohamia leo ni sehemu salama na anaweza akaishi pale muda mrefu bila ya mtu yeyote kufahamu lakini tataizo ni kwamba lengo la rais kunitaka nikaishi pale ni ili awe na uwezo wa kufika muda wowote anaotaka .Itakuwaje iwapo atakuja na kumkuta Elibariki yuko pale? Hapana sehemu ile si muafaka kumuweka Elibariki.Itanibidi nimpeleke nyumbani kwangu halafu kesho nitaangalia namna nzuri ya kufanya. Lazima nipate sehemu salama kabisa ya Elibariki kuishi kwa muda wowote anaoutaka” akawaza Peniela

“ Nimefurahi kwa Elibariki kutua tena katika mikono yangu.Nilikuwa naitafuta sana nafasi hii ya kuweza kuutengeneza upya uhusiano wangu na Elibariki.Ni mtu ambaye amenisaida sana katika kuniweka huru .Lazima na mimi nimsaidie katika kipinid hiki ambacho anahitaji sana msaada ” akawaza Peniela na hawakuongea kitu chochote hadi walipofika nyumbani kwake akashuka na kufungua geti akaingiza gari ndani halafu akaufungua mlango wa gereji na kuliingiza gari katika gereji na ndipo alipomruhusu Jaji Elibariki kushuka.Akamsaidia kutembea hadi sebuleni akamkalisha sofani.Bado jeraha alilokuwa amelipata jaji Elibariki katika mkono wake liliendelea kutoa damu.Peniela akaenda chumbani kwake na kurejea na kiboksi chenye vifaa vya huduma ya kwanza na kulisafisha jeraha lile na kisha kupata dawa na kulifunga ili lisiendelee kutoa damu.

“ Pole sana Elibariki,usijali hapa uko sehemu salama na nitafanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba unakuwa salama.Kwa sasa ngoja nizuie hii damu halafu nitamuita daktari atakuja kukuangalia “ akasema Peniela na Elibariki akaonyesha wasi wasi Fulani

“usiogope Elibariki.Daktari huyo ni rafiki yangu mkubwa tumesoma wote toka shule ya msingi “ akasema Peniela.Baada ya kumfunga jeraha lile akamshika mkono na kumuongoza hadi bafuni ambako alimsaidia kuoga halafu akampeleka kitandani .

“ Peniela nashukuru sana “ akasema Jaji Elibariki

“ Usijali Elibariki.Wewe ni mtu wa muhimu sana kwangu kwa hiyo nitafanya kila linalotakiwa kufanywa kuhakikisha kwamba uko salama.” Akasema Peniela wakatazamana kwa muda halafu Peniela akasema

“ Elibariki ninaomba samahani sana kwa jambo lililotokea siku ile.Ni jambo la aibu sana lakini naomba tusahau yote yaliyotokea.Najua ulikasirika sana kwa tukio lile lakini nina hakika tutakaa na kuliongelea “ akasema Peniela .Jaji Elibariki akatabasamu kidogo na kusema

“Peniela naomba kwa sasa usiwaze kuhusiana na mambo hayo.Yamekwisha pita na kwa sasa tuko katika mambo mengine kabisa.Tushughulike na lili liko mbele yetu yaliyopita yamekwisha pita tusihangaike nayo.Tell me anything and I believe you”akasema jaji Elibariki na kumfanya Peniela atabasamu

“ Nashukuru sana Elibariki.Ngoja kwanza niwasiliane na daktari” akasema Penny na kumpigia daktari rafiki yake waliongea kwa dakika kama mbili hivi halafu akamfuata Elibariki

“ Daktari anakuja muda si mrefu” akasema

“ nashukuru sana Penny.Ahsante sana kwa kunijali ” akasema Elibariki na Penny akatabasamu na kusema

“ Elibariki nilistuka sana uliponipigia simu.Baada ya tuko lile la siku ile nilikuwa naogopa hata kukupigia simu na kukujulia hali yako.Kila nilipotaka kukupigia nilijikuta nikishindwa.Uliponipigia leo nilistuka sana na kujiuliza ni kwa nini mimi? Kwa nini katika watu wote hawa waliokuzunguka ukanichagua mimi? Am I that important to you?akauliza Peniela .Jaji Elibariki akamtazama na kusema

“ Peniela ,jina lako lilikuwa la kwanza kulifikiria mara tu nilipofikiria kama kuna sehemu salama ninaweza kwenda kukaa kwa usiku huu.Sikuwaza mtu mwingine yeyote zaidi yako kwa hiyo nina amini kwamba hapa niko sehemu sahihi “ akasema jaji Elibariki. 

“ Mkeo ana taarifa ya kilichotokea? Akauliza Peniela

“ Nina hakika lazima atakuwa na taarifa mpaka hivi sasa.Siku hizi taarifa hazichelewi kusambaa.Nina hakika baada ya kuzipata taarifa hizi atakuwa katika wakati mgumu sana ”

“ Elibariki najua bado uko katika mstuko lakini unaweza ukanieleza hasa nini kilitokea? Akaulizia Peniela

Jaji Elibariki akafumba macho na kuvuta picha ya tukio lile kisha akasema

“ Usiku huu mke wangu alinipigia simu na kunitaka niende nikaonane naye kuna suala ambalo alitaka kunieleza.Siwezi kukuficha Peny kwa siku za hivi karibuni mimi na mke wangu tumekuwa katika mikwaruzano kidogo.Hata usiku huu tulipoonana tulishindwa kuelewana ikanilazimu kuondoka kwani nilikuwa na miadi ya kuonana na rafiki yangu mmoja anaitwa Mathew.Kabla sijafungua mlango wa gari langu nilipigiwa simu na mtu ambaye simfahamu.Alikuwa ni mwanamke na akaniambia kwamba nisiingie katika gari.Nikamuuliza yeye ni Nani na kwa nini nisiingie katika gari langu akaniambia kwamba kuna mpango wa kuniua.Nikampuuza na kuingia garini.Nilikuwa na mtu mmoja anaitwa Noah ambaye ndiye aliyekuwa akiendesha gari langu usiku huu.Tuliendelea na safari hadi tulipofika katika makutano ya barabara za Mkwavinyika na Kilimanjaro pale kwenye taa za kuongozea magari tukakuta kuna msururu mrefu wa magari.Wakati tukisubiri taa ziwake ghafla zilitokea piki piki mbili na kuanza kutuvurumishia risasi.Yule jamaa niliyekuwa naye garini Noah aliniwahi na kunikinga na zile risasi zikampata yeye na kumuua pale pale.Bila Noah hivi sasa tayari ningekuwa nimekufa.Alijitolea hai wake kwa ajili yangu” akasema jaji Elibariki

“ Pole sana Elibariki.Pole sana” akasema Peniela na kumfuta machozi yaliyokuwa yakimtoka.

“ Ahsante sana Peniela.”

“ Lakini ni akina nani waliotaka kufanya jambo hili? Ni kwa nini walitaka kukuua? Akauliza Peniela huku naye machozi yakimtoka

“ Sifahamu Peniela.Sifahamu ni akina nani wanaoitafuta roho yangu .Kwa sasa baada ya kunusurika inanibidi nichukue tahadhari kubwa sana kwani watu hawa wakijua wamenikosa hawatalala usingizi wataendelea kunisaka usiku na mchana hadi wahakikishe wametimiza lengo lao.lakini nakuhkikishia Peniela kwamba lazima watu hawa watapatikana tu” ” akasema jaji Elibariki na Kengele ya getini ikalia kuashiria kwamba kuna mtu.

“Huyo atakuwa ni daktari wangu” akasema Peniela na kuinuka akaelekea getini.Ni kweli alikuwa ni daktari aliyemuita Dr Jonesia.Peniela akampokea na kumpeleka moja kwa moja hadi chumbani kwake ambako alikuwepo jaji Elibariki.Dr Jonesia akasalimiana na jaji Elibariki halafu akaanza kumuangalia mahala alikoumia.Alimchunguza kwa muda wa kama nusu saa hivi kila sehemu ya mwili ambayo kulionekana kuwa na damu halafu akasema

“ Mungu ni mkubwa majeraha haya yote ni ya michubuko tu na hakuna risasi hata moja iliyoingia mwilini mwake” akasema Dr Jonesia na kuyatibu majeraha yote ya jaji Elibariki halafu akamchoma sindano na kumtaka apumzike.Peniela akamshukuru na kumsindikiza akaondoka

“ Peniela nashukuru tena kwa mara nyingine kwa msaada wako .Kama nilivyosema awali kwamba sikukosea kabisa kuja hapa.Ninaamini nimefika sehemu sahihi ninakotakiwa kuwapo kwa sasa”akasema jaji Elibariki na Penny akatabasamu kidogo

“Usijali Elibariki nitafanya kila linalowezekana kwa ajili yako “ akasema Peniela na mara simu ambayo huwa anaitumia kuwasiliana na Dr Joshua ikaita

“ Sorry Elibariki I need to take this call in Private .Its important’akasema Peniela na kuichukua simu ile akatoka mle chumbani

“hallow Dr Joshua’akasemaPeniela

“hallow Peniela,hujambo? habari za makazi mapya? Kareem aliniambia kwamba ila kitu kimekwenda vizuri kama ulivyotaka”

“Ndiyo Dr Joshua kila kitu kimekwenda vizuri na ninashukuru sana.Vipi wewe unaendeleaje? Akauliza Penny

“Hata mimi ninaendlea vizuri sana Penielea.Leo tulikuwa na zoezi la kuuaga mwili wa Flora na kesho tunalekea kijijini alikozaliwa kwa ajili ya mazishi.”

“ Pole sana Dr Joshua.” Akasema Peniela

‘ Ahsante sana Peniela.lakini yote hii ni mipango ya Mungu .Yeye ndiye mwenye kupanga mambo yote yatokee na hata kwa hili ana makusudi yake kwa nini litokee sasa.Nadhani ana mpango mkubwa wa nchi kumpata first lady mpya” akasema Dr Joshua huku akicheka kidogo

“Dr Joshua achana na mawazo hayo kwanza.Subiri kwanza hadi mkeo atakapozikwa”

“ Hahaha Peniela unanifurahisha sana,Flora is gone and she’ll never come back.Maisha lazima yaendelee “akasema Dr Joshua akatulia kidogo halafu akaendelea

“ Peniela nimekupiga simu kukutakia tu usiku mwema na kukumbusha ni namna gani ninavyokupenda.Endapo kama kusingekuwa na watu wengi hapa msibani nigekuja sasa hivi kujaku kuangalia na kupata faraja.Wewe ndiye furaha yangu”

“ Dr Joshua kwa sasa siko katika ile nyumba mpya .Nimerejea kwanza nyumbani kwangu kwa muda.” Akasema Penny na kumstua Dr Joshua

“kwa nini penny? Kuna tatizo lolote?akauliza Dr Joshua

“hapana Dr Joshua hakuna tatizo lolote ila kuna mambo ambayo nataka niyaweke sawa kwanza kabla ya kuanza kuishi katika nyumba mpya.” Akasema Peniela

“ Sawa Peniela tutaongea vizuri nikisharudi kesho.Endapo kuna kitu chochote unakihitaji utawasiliana na Kareem moja kwa moja” akasema Dr Joshua

“ Usiku mwema Dr Joshua”

“ Usiku mwema Peniela.I love you”akasema Dr Joshua na kukata simu

“ Huyu mzee hana akili nzuri.Yaani hata mke wake bado hajazikwa tayari amekwisha anza kuwaza mambo mengine kabisa.Laiti angenifahamu wala asingethubutu kunitamkia maneno yale ya kipuuzi.” Akawaza peniela na kurejea tena chumbani.

“ Peniela kuna jambo nataka nikuombe”

“ Omba chochote Elibariki”akasema Peniela

“Kuna mtu wa muhimu sana ambaye nataka niwasiliane naye”

“ Mke wako? Akauliza Peniela

“hapa sitaki kuwasiliana na mke wangu.Ni rafiki yangu tu ila ni wa muhimu mno ” akasema jaji Elibariki.Peniela akachukua simu yake na kuziandika namba alizotajiwa na Elibariki halafu akapiga.

“ Simu inaita”akasema Penny na kumpatia Elibariki simu

‘ Hallow” ikasema sauti ya upande wa pili

“ Hallow Mathew.Elibariki hapa ninaongea” akasema

“ Elibariki ? ! ..Mathew akastuka

“Ndiyo Mathew ni mimi”

“ Uko wapi Elibariki ? akauliza Mathew

“ Niko sehemu salama kwa sasa.Tayari mmepata taarifa za kilichotokea?

“ Ndiyo Elibariki.Tayari tumekwisha zipata taarifa na muda si mrefu tumetoka hospitali kuutambua mwili wa Noah.Pole sana kwa kilichotokea.”

“ Ahsante sana Mathew.Kwa kweli lilikuwa ni tukio baya sana na sikuwahi kutegemea kama siku moja tukio kama lile linaweza kunitokea.Ilikuwa nife lakini Noah ameniokoa .Amekufa kishujaa .He saved me.He saved my life” akasema Jaji Elibariki huku akilengwa na machozi

“ Kifo cha Noah kimeniumiza sana Elibariki.Lakini hatuna namna ya kufanya imeshatokea imetokea.Kwa sasa uko wapi? Akauliza Mathew

“ Kuna sehemu nimejificha”

“ Is it a safe place? Are you sure you are safe? Akauliza Mathew

“ Yes I’m sure.I’m safe”

“ Ok good.Endelea kujificha hapo hapo .Kwa sasa tunashughulikia msiba wa Noah.Nimewasiliana na wazazi wake tayari nchini Zimbabwe na wamesema kwamba tutawasiliana tena asubuhi ili wanitaarifu kuhusiana na walichokipanga.Noah alikuwa ni kama mdogo wangu kwa hiyo nitaweka kila kitu pembeni kwa sasa na baada tu ya kumzika ndipo nitaanza tena kazi.Ninakuahidi kwamba yeyote aliyehusika katika tukio hili hatabaki salama.Nitakaporejea utashuhudia nitakachokifanya.Kila risasi iliyoingia mwilini mwa Noah italipwa.Kwa sasa endelea kukaa hapo hapo hadi nitakaporejea.Endapokukiwa na tatizo lolote unitaarifu mara moja.Lakini mpaka hapo tutakapoonana tena please stay safe” akasema Mathew na kukata simu


TUKUTANE SEHEMU IJAYO…

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...