SIMULIZI: PENIELA (SEASON 1 EP 3)
MTUNZI : PATRICK.CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Ni saa tatu za usiku ,chupa ya mvinyo iliendelea kushuka taratibu.Toka aliporudi nyumbani Jaji Elibariki alikuwa amejifungia chumbani kwake akiendelea kupata mvinyo huku akitazama mpira katika runinga kubwa iliyokuwamo humo chumbani.Kazi kubwa aliyokuwa nayo usiku huu ni kupokea simu toka kwa watu mbali mbali marafiki zake waliokuwa wakimpongeza kwa hukumu ile ya kihistoria.Wakati akiongea na mmoja wa rafiki zake simu nyingine ikaita,akatazama mpigaji alikuwa ni baba mkwe wake,Profesa Joshua Joakim rasi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
“ Kazi imeanza” akawaza na kumuomba samahani Yule rafiki yake aliyekuwa akiongea naye na kuichukua simu ile iliyokuwa ikiita akabonyeza kitufe cha kupokelea.
“ Hallo mzee” akasema Jason.Zikapita kama sekunde kadhaa akasikia sauti ya rais.Haikuwa ile sauti yake aliyoizoea kuisikia.
ENDELEA………………………………………….
“ Hallow mheshimiwa Jaji habari za jioni?
“ Habari nzuri mheshimiwa rais.Pole na majukumu”
“Ahsante sana kijana wangu nimekwisha poa” akasema mheshimiwa rais halafu kimya kifupi kikapita.Rais akauvunja ukimya
“ Elibariki nimekupigia simu kuna jambo nataka tuongee”
“ Ndiyo nakusikiliza mzee”
“ Naomba kwanza nikupongeze kwa kuimaliza kesi ngumu iliyovuta hisia za watu wengi.Pamoja na pongezi hizo, naomba niwe wazi kwako kwamba sijafurahishwa hata kidogo na maamuzi uliyoyafanya.
To ka awali nilikuomba ufanye kila linalowezekana ili shemeji yako Anna aweze kupunguza machungu ya kifo cha mpenzi wake Edson.Alimpenda sana Edson na walikuwa na ndoto nyingi siku za usoni.Sina maana ya kudharau maamuzi yako kama jaji,lakini kitendo cha kumuacha huru muuaji wa mpenzi wa mwanangu kimenifadhaisha sana mimi na familia yangu kwa ujumla.Elibariki umemuoa mwanangu kwa hiyo nakuhesabu nawe ni sehemu ya familia yangu.Kama mwanangu ulitakiwa kusimama upande wa familia yako na kumuadhibu muuaji lakini pamoja na ushahidi wote uliowasilishwa mahakamani bado umeupuuza ukamuachia huru Yule msichana.
Naomba tu ufahamu kwamba maamuzi haya yamenifadhaisha sana mimi na familia yangu kwa ujumla.Ni hayo tu niliyotaka kukwambia usiku huu.Kwa heri Jaji” akasema mheshimiwa rais na kukata simu.Jaji Elibariki alihisi kijasho kikimchuruzika.Akainua glasi yake ya mvinyo na kunywa fundo kubwa.
“ Nilijua tu lazima mambo kama haya yangejitokeza kwani rais na familia yake walitegemea ningefanya kama walivyokuwa wakishinikiza wao kwamba nimpatie Penny adhabu kali.Kwa maamuzi ya kumuachia huru nimekwisha tangaza vita na familia hii na nina hakika maisha yangu yatakuwa magumu sana kuanzia sasa.Lakini vyovyote itakavyokuwa siyajutii maamuzi yangu.Nimetenda haki na siku zote nitasimama katika haki.Nitatenda haki bila kujali uwezo wa mtu na sintokubali kufanya kazi yangu kwa shinikizo toka kwa mtu yeyote .
Si rais wa nchi wala mtu yeyote atanishinikiza nifanye kazi kwa matakwa yake.Ninafanya kazi kwa mujibu wa sheria za nchi.” Akawaza Jaji Elibariki akiwa na hasira na kunywa tena fundo lingine
“ Ndiyo maana ninataka nifanye uchunguzi ili kumbaini muuaji wa Edson.Hapo ndipo nitakapowadhihirishia kwamba maamuzi yangu ya kumuachia Penny yalikuwa sahihi kabisa.Nisipofanya hivyo nitajiweka mahala pabaya na hata Penny maisha yake hayatakuwa na amani na salama.Lazima watamuandama tu.”
Akiwa bado katika mawazo mara mlango ukafunguliwa na akaingia mke wake Flaviana.Bila kumsalimu mumewe akajitupa kitandani .Alionekana mchovu sana na usoni alionekana ni mwenye hasira.Baada ya dakika kama tano hivi za ukimya mle chumbani kitu ambacho hakikuwa cha kawaida kwao Elibariki akaamua kuuvunja ukimya na kumuuliza mke wake
“ Umechelewa wapi?
“ Nilikuwa nyumbani kwa baba nikilia na familia yangu” akajibu Flaviana kwa sauti ya ukali
“ Kwa nini hukunitaarifu kama utachelewa ili nisiwe na wasi wasi kuhusu usalama wako?
Flaviana akacheka kidogo kicheko cha dharau na kusema
“ Sikuona umuhimu wa kukutaarifu.”
Jibu lile likamstua sana Jaji Elibariki.Hata siku moja mke wake hakuwahi kumjibu kijeuri namna ile
“ Hukuona umuhimu wa kunitaarifu mahala uliko? Tabia hii imeanza lini? Akauliza Elibariki
“ Ndiyo sikuona umuhimu huo”
“ Flaviana naomba uwe makini na kauli zako.Mimi ni mumeo na ni lazima nijue kila kitu unachokifanya.
Mimi nina maadui wengi nitajuaje kama umedhurika huko njiani? Nimekaa hapa mawazo tele nikiwazia usalama wako” akasema Jaji Eli
“ Kwa maana hiyo unataka kumaanisha kwamba mimi ni wa muhimu kwako? Akauliza Flaviana
“ Maswali gani hayo unayouliza Flaviana? You are my wife and you are important to me”
“ Save your breath Eli.I’m not important to you at all.I mean nothing to you”
“Una hakika na hayo unayoyasema ? akauliza Eli
“ Ningekuwa ni wa thamani kwako basi ungeithamini na familia yangu pia na usingefanya maamuzi kama uliyoyafanya.Sikutegema kama ungemuachia huru Yule kahaba.
How could you let her go? Kahaba Yule alimuua Edson na kuna kila ushahidi wa kutosha ulikuwepo kumtia hatiani lakini kwa makusudi kabisa umeamua kumuacha huru.You have broken my sister’s heart and mine as well.I’m disappointed,very disappointed” akasema Flaviana kwa hasira.Elibariki akanywa fundo kubwa la mvinyo halafu akazima runinga na kumgeukia mkewe
“ Flaviana naomba iwe ni mwanzo na mwisho wewe na familia yako kuingilia kazi yangu.Mimi ndiye ninayehukumu na si mtu mwingine kwa mantiki hiyo basi hakuna anayeweza kunishinikiza nifanye anavyotaka yeye.Si wewe wala baba yako wala mtu yeyote Yule anayeweza akanifundisha namna ya kuifanya kazi yangu.Halafu naomba iwe ni mara ya kwanza na ya mwisho kumuita Penny kahaba.She’s a respectable woman and you’ll have to respect her” akasema kwa ukali Jaji Elibariki.
“ Huwezi kunizuia kuongea Eli. Nitaongea chochote nikitakacho na hutanifanya kitu.That woman is just a prostitute .Nashangaa unavyosimama na kumtetea kwa nguvu.Who is she to you? Akafoka Flaviana
Maneno yale ya mke wake yakamuumiza sana Jaji Elibariki akamsogelea mkewe
“ Flaviana nakupa onyo la mwisho.Naomba tafadhali usithubutu kunijibu namna hiyo.”
“Usinitishe Elibariki.Huwezi kunifanya lolote” .Flaviana akongea kwa ukali na kwa kujiamini.Elibariki akamshika shingoni kwa hasira
“ I married you because I love you,and not because you’re a president’s daughter so don’t dare disrespect me again.If you do that again I’ll forget that your father is the president and I’ll break your neck.” Akasema Elibariki kwa hasira na kutoka mle chumbani. Pamoja na ujasiri wote aliokuwa Flaviana akajikuta akiogopa ghafla kwani hakuwahi kumuona muwe akiwa amekasirika namna ile .
“ What a stupid husband” akasema kwa sauti ndogo Flaviana baada ya Eli kutoka mle chumbani
“ Sijawahi kudharauliwa kama alivyonidharau Flaviana leo.Lakini nilijua tu mambo kama haya lazima yatakuja.Ninachopaswa kufanya ni kukabiliana nayo,.Huu ni mwanzo tu.Mengi yatakuja makubwa zaidi ya haya.” Akawaza Jaji Elibariki akiwa amekaa sebuleni amefura kwa hasira
***********
Ilipata saa nane na dakika kumi na tatu za usiku kwa mujibu wa saa kubwa ya ukutani,hali ya chumba ikiwa ni ya ubariki uliotokana na kipoza hewa huku kukiwa na mwanga hafifu na muziki laini kwa mbali,msichana mrembo Peniela alikuwa amejilaza kitandani.Baada ya kusota gerezani kwa takribani mwaka mzima hatimaye leo kama ndoto amerejea tena katika chumba chake
Kwa muda wa masaa mawili sasa amekuwa simuni akiongea na wakili wake Jason Patrick
“ Penny muda umekwenda sana nadhani ni wakati sasa wa kukuacha upumzike.Siku ya leo ilikuwa ndefu sana” akasema Jason
“ Ouh C’mon Jason,unadhani ninaweza kupata usingizi leo? Siwezi kabisa kupata usingizi kwa furaha niliyonayo na pili bado niko katika mstuko.Bado siamini kama ni kweli niko huru.Itanichukua siku kadhaa ili niamini kama ni kweli niko huru.” Akasema Penny.Jason akacheka kidogo na kusema
“Penny amini kwamba kesi imekwisha na uko huru.Mahakama imekukuta huna hatia na imekuachia huru”
“ Nakubaliana nawe Jason lakini kwa upande mwingine bado nina wasi wasi sana na maisha yangu.Sina hakika kama maisha yangu yatakuwa sawa tena.”
“ Kwa nini unasema hivyo Penny?
“ Nimewashinda watu wakubwa waliotaka kuniangamiza .Ninaamni jambo hili halitaishia hapa.Wataendele
a kuniandama usiku na mchana hadi wahakikishe kwamba wametimiza lengo lao.Anna mtoto wa rais aliapa kwamba ataniangamiza na ndiyo maana umeshuhudia nguvu kubwa ikitumika katika kuhakikisha ninafungwa gerezani.Uliona wewe mwenyewe ushahidi mzito uliotolewa mahakamani lakini pamoja na jitihada zao zote Mahakama imeniachia huru.Nina hakika mapambano yetu hayatishia hapo tu.
Nitaendelea kuandamwa kokote nitakakokuwa.My life will be a living hell”
“ Penny nashukuru kama umelifahamu hilo.Kitu cha msingi unachotakiwa kufanya ni kujiweka mbali kabisa na mambo yoyote yale yanayoweza kuwafanya wapate sababu ya kufanya lolote juu yako.Najua watatumia uwezo wao kuyafanya maisha yako yawe magumu lakini usihofu wala usiogope.Mimi nipo pamoja nawe siku zote.Vita hii ni yetu na tutashinda sote” akasema Jason
Sijui nikushukuruje Jason kwa msaada wako mkubwa.Hata nikikulipa mamilioni ya pesa ,hayataweza kufikia ukubwa wa msaada ulionisaidia.Dunia nzima ilinitenga baada ya kuaminishwa kwamba mimi ni muuaji lakini wewe pekee ndiye uliyeniamni kwamba sikutenda kosa lile na ukasimama pamoja nami.Ahsante sana Jason “ akasema Penny na kwa mbali machozi yakamlenga akikumbuka namna Jason alivyompigania hadi akawa huru
“Penny toka siku ya kwanza nilipokuona machoni niliamini hukutenda kiosa hilo na ndiyo maana nimepambana kufa na kupona kuhakikisha kwamba binti malaika asiye na hatia anaachiwa huru. Hata hivyo hayo yameshapita na ninachokuomba uyasahu yote na tuangalie mambo ya mbele.Tunatakiwa kuangalia nini kitafuata baada ya wewe kuwa huru.Tutakaa pamoja na kuangalia ni namna gani tutafanya ili uweze kujiweka vizuri kiuchumi..Mwaka mzima uliokaa gerezani najua mambo yako mengi yameyumba lakini usihofu niko pamoja nawe ,nitakusaidia hadi hapo utakapoweza kusimama tena”
“ Ouh Jason,you are so sweet.Ahsante sana kwa kujitolea kunisaidia lakini naomba kwa hili niseme hapana.Jason umenipigania mpaka nimekuwa huru.Sitaki niendelee kuwa mzigo kwako” akasema Penny
“ Penny tafadhali usirudie tena kutamka hilo neno eti wewe ni mzigo kwangu.Ninajiona ni mwenye bahati sana kuwa na rafiki kama wewe.Zaidi ya yote wewe bado ni jukumu langu.Kukusaidia kushinda kesi bado haitoshi lazima nihakikishe kwamba umeweza kujiimarisha kiuchumi .Pesa ni vitu vya kupita kwa hiyo naomba ukubali nikusaidie Penny” akasema Jason.Penny akacheka kidogo na kusema
“ Jason siku zote hutaki kushindwa.Ok tutakaa na kuliongelea suala hili”
“ Ahsante sana Penny.Pumzika sasa tutaonana kesho” akasema Jason wakaagana na kukata simu
“ Afadhali sasa nitaweza kulala usingizi.Kesi ya Penny iliyokuwa ikininyima usingizi imekwisha “ akawaza Jason
“ Nitamsaidia kwa kadiri niwezavyo hadi nihakikishe amerejea katika maisha yake ya awali.Uchumi wake umeyumba sana baada ya kukaa mwaka mzima gerezani.Bado Penny anahitaji sana msaada wangu” Akawaza halafu akastuka baada ya kukumbuka kitu
“ Kuna kitu nimekuwa najiuliza sana kuhusu Penny.Toka nimemfahamu sijawahi kuwaona ndugu zake,wala wazazi wake.Mwaka mzima nimehangaika naye katika kesi na sijawahi kumuona ndugu yake yeyote wala hajawahi kutamka lolote kuhusu ndugu zake.Jambo hili linanifanya nijiulize maswali mengi kuhusiana na maisha yake.Je hana ndugu? Kama anao wako wapi?
Kwa nini walimuacha wakati wa kipindi kigumu alichokuwa nacho?Nadhani ninahitaji kumfahamu Penny kwa undani zaidi.Kuna mambo mengi kumhusu yeye ambayo nahitaji kuyafahamu” akawaza Jason
No comments
Post a Comment