WEWE NI SHUJAA WA BWANA

 WEWE NISHUJAA WA BWANA

Hello msomaji wetu wa makala zetu. Karibu Sana kuungana nami katika somo la leo.

Kutoka 3:11

11 Musa akamwambia Mungu, Mimi ni nani, hata niende kwa Farao, nikawatoe wana wa Israeli watoke Misri?


Musa alimuuliza Mungu wakati anatumwa kwenda kuwaokoa wana wa Israel utumwan misri


Musa alijiona kwamba yeye nimdogo Sana, alijiona yeye nidhaifu Sana, namzungumzia Musa alikua akijilinganisha na mfalme farao wa misri anaona ni vitu viwili tofauti


Hofu ya Musa nikwamba anazijua nguvu na uwezo wa farao mfalme wa misri lakini alikua hajui anatumwa na nani


Musa huyu huyu ndani yake alikua na uchungu ndani yake wa kuwasaidia Ndugu zake waebrania kiasi cha kutoka kuishi kwenye nyumba ya mfalme nakuamua kwenda kuishi na Ndugu zake hata kumuua mmisri na kumfukia kwenye mchanga, Matendo 7:23-25


Alifanya yote haya nguvu za Mungu zikimfatilia na pasipo kujua kuwa anafuatiliwa na Mungu na pasipo kujua kuwa ni Mungu ndie alie msaidia hata asikamatwe alipomuua mmisri anakuja kumuuliza Mungu "Mimi ni nani hata niende kwa farao, nikawatoe wana wa Israel watoke misri"



Upo mahali unajisikia uchungu miaka na miaka familia haina mwelekeo,


Ndugu zako wako utumwan, Ndugu zako wengine wamekufa vifo vyakutatanisha, ndani yako kuna mzigo umeshindwa kuutua, umebaki kusema namuachia Mungu, umebaki kusema Mungu ndie mgawaji wa riziki kama kunipa atanipa tu umeridhika na huo umasikini na taabu zako, na familia ukiitazama huon mbele wala nyuma


Nimetumwa kukutangazia wewe ndie shujaa aliesubiwa kwa muda mrefu aiokoe familia yako, aokoe Ndugu zako waliopotea, waliofungwa kwenye mashimo.


Hebu ona Yeremia 1:10, "angalia nimekuweka Leo juu ya mataifa na juu ya falme"


Wewe ni uko juu ya Kila tatizo unaloliona nikubwa, 

Roho mtakatifu akusaidie kuelewa, wewe ni mkuu sana, kuliko unavyojiona, una nguvu za ajabu Sana kuliko unavyojifikilia


Ukitamka tu inakua, sasa kazi ni kwako nikipi unachoona kimekuzuia kitamkie kiondoe kwenye maisha yako, kitamkie kiondoke kwenye familia yako,


Hata kama nikwamachozi wewe tamka kwa nguvu kitakuachia, haijalishi kimekukamataje 


Mungu alimuuliza Musa unanini mkononi Kutoka 4:2, Musa akajibu Fimbo akaambiwa aitupe chini


Sikia mwana wa Mungu, Musa hakujua kuwa ameshika siraha kuu ambayo anaweza kuitumia na kumuanganiza farao


Wewe unasiraha kubwa zaidi, una damu ya Yesu, una jina la Yesu, una moto wa Yesu


Angalia niwapi hapako sawa, tumia hizo siraha kuteketeza na kuharibu,


Watoto wengi wa Mungu wanakandamizwa na matatizo na mambo mbali mbali pasipo kujua kuwa wana mamlaka kuu.


Badilika mwana wa Mungu, hebu Leo amua tu kufulumusha vyote vilishoshukilia maisha yako, vilivyoshikilia mtaa wako na nchi yako


Isaya 42:22 Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.


Wakurudisha si mwingine mwana wa Mungu niwewe, ninakuombea Mungu akutie nguvu uweze kurudisha vyote vilivyoshikiliwa na adui zako


Mungu Baba katika jina la Yesu namleta mtoto wako huyu anaesoma ujumbe huu kwa majina yake, naomba rehema na msamaha kwaajili yake katika jina la Yesu, Yesu Kristo kama ulivyo nituma nimemletea ujumbe kama ulivyo, nakuomba umjaze nguvu ujasiri wakufungua alipofungwa, ilipofungwa familia yake, yalipofungwa maisha yake popote pale, Baba mpe ufahamu na akili ya kujua nimahali gani pakufungua na kufunga katika jina la Yesu nimeomba na kuamini nakupokea amen.


Mungu akubariki, nakutakia siku njema ya Maombi mazito ya kufungua na kutoka kwenye Kila kilichokushikilia katika jina la Yesu.


Kama umebarikiwa na ujumbe huu share kwa ndugu jamaa na rafiki zako popote pale facebook na kwenye magroup ya Whatsup hutaachwa hivyo hivyo bali utabarikiwa kwa kuitangaza injili kwa kushare. Pia like Facebook Page yetu ya Nyumba ya Sala kwa Mataifa Yote kwa masomo mengi zaidi.


Ukipenda kutumiwa masomo ya Neno la Mungu kila siku kwa Whatsup tuma majina yako mawili inbox, whatsup kwa namba ya Tigo 0657 048393 kuomba kuunganishwa kupewa masomo kila siku na utatumiwa, pia kwa ushauri na maombi piga namba zilizopo hapo chini, na Mungu wambinguni akubariki sana.


Merito Tagalile

~0657 048393

~0625 610925

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...