PENIELA (Season 1 Ep 22)

 PENIELA

SEHEMU YA 22

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

“ Nini kimesababisha kifo cha mama? Akauliza jaji Elibariki

“ Mpaka sasa hivi hatufahamu chochote kuhusiana na nini kimemuua.Madkatari bado hawajasema chochote lakini daktari wa familia Captain Amos anasema ni shinikizo la damu.Eli,inaniuma sana kumpoteza mama yangu.Jana usiku nimeongea naye akanipigia simu na kuniambia kwamba leo anahitaji kuonana nasi mimi na Anna kuna jambo la maana mno anataka kutueleza lakini kabla ya kuonana naye amefariki dunia ghafla.Inauma sana Eli.Ninaumia mno”

“ Pole sana Flaviana” akasema Jaji Elibariki na kuendelea kumbembeleza mkewe.

“ Jambo gani alilotaka kuwaambia?

“ Sifahamu Eli,sijui alitaka kutuambia nini lakini alisisitiza mno.Inaonekana alikuwa na jambo kubwa la kutueleza.” Akasema Flaviana na kuendelea kulia

“ Kifo cha ghafla cha Dr Flora hata mimi kinanipa mashaka mno.Alitaka kuwaeleza nini wanae? Kwa nini afariki ghafla kabla hajakutana na wanae? Kuna maswali mengi sana ya kujiuliza kuhusiana na kifo hiki” akawaza Jaji Elibariki

ENDELEA…………………………………

Mathew na Anitha walirejea nyumbani na kukutana na Noah aliyekuwa amewasili kitambo akiwasubiri.

“ Welcome home Noah” akasema Mathew

“ Nimekwisha karibia kaka.Poleni na kazi”

“ Ahsante sana “ wakajibu Mathew na Anitha

“ Mtanisamehe kwa kuchelewa.Kuna kazi ambayo nimelazimika kuiacha ili kuja kuungana nanyi katika kazi hii.Mmefikia wapi mpaka hivi sasa? Mmekwishaianza kazi? Akauliza Noah

“ Usihofu Noah wala haujachelewa sana.Mpaka sasa hatujapiga hatua kubwa sana lakini kidogo kuna mwanga Fulani ingawa kadiri tunavyozidi kulichimba suala hili tunagundua kwamba suala hili haliko kama tulivyolitazamia.Suala hili ni zaidi ya mauaji ya Edson.Tunatakiwa tuzidi kulichimba zaidi lakini naomba niwaweke wazi ndugu zangu kwamba kadiri tunavyolichimba suala hili ndivyo tutakavyozidi kukutana na mambo mazito na ya hatari.Please guyz, no matter how danger we’ll be facing,don’t ever give up.Lets fight till the end.Sitaki kuwaficha ndugu zangu kazi hii ni ya hatari kuliko zote tulizowahi kuzifanya kwa hiyo naomba kabla hatujaenda mbali sana kila mmoja atafakari na afanye maamuzi .” Akasema Mathew

Dakika moja ikapita ya ukimya,kila mmoja alikuwa akitafakari.Anitha ndiye aliyekuwa wa kwanza kuuvunja ukimya

“ Mathew,wewe umekuwa ni mshirika wangu,tumekuwa kama mapacha,nimefanya nawe kazi nyingi na za hatari lakini mara zote tunapokuwa pamoja hakuna kazi imewahi kutushinda.Nikiwa pamoja nawe,sina wasi wasi hata kidogo na jambo lolote lile.Uliponieleza kwamba kuna kazi ambayo tunatakiwa tuifanye sikujiuliza mara mbili,niliachana na kazi ambayo nilikuwa nimeitwa nikaifanye nchini Brazili ,kazi yenye pesa nyingi sana ,nikaja kuungana nawe.Kwa moyo mmoja natamka kwamba niko tayari kwa lolote.I’m in” 

“ Ahsante sana Anitha.Vipi kuhusu wewe Noah? Akauliza Mathew

“ Me also.I’m in” akasema Noah

“ Ok good.We’re team now.Naomba nisiwaogopeshe lakini tambueni tu kwamba tunakwenda kukutana na mambo mazito na tunatakiwa tusimame imara tusitetereke.This is war and we as soldiers we have to fight” 

“ Mathew kama tulivyokueleza ni kwamba tuko tayari kwa mapambano.Siku zote hatuogopi kitu .Nielezeni mmefikia wapi mpaka sasa hivi? Akasema Noah

“ Tumeanza kwanza kumchunguza Edson alikuwa ni mtu wa namna gani.Tumegundua kwamba Edson alikuwa na mahusiano na dada mmoja aliyeitwa Brigita ambaye walikuwa wakiwasiliana kwa siri.Tumeipata laini ya simu ambayo Edson alikuwa akiitumia kuwasiliana na Brigita . Tumegundua kwamba Brigita alikuwa pia na mahusiano ya kimapenzi na mzee mmoja aliyeitwa mzee Matiku.Mzee huyu ndiye mmiliki wa hoteli aliyokuwa akifanyia kazi Brigita na ndiye aliyemuwezesha kwa kila kitu.Alimjengea nyumba,akamnunulia gari na kila kitu.Kwa mujibu wa Subira ambaye alikuwa rafiki wa karibu sana na Brigita alisema kwamba Brigita alikuwa na mpango wa kumtoroka mzee huyo kwani hakuwa na mapenzi naye bali alimpendea pesa zake.Brigita alimweleza Subira kwamba alikuwa akitegemea kupata pesa nyingi kutoka katika biashara aliyoifanya na Edson ambayo hakuwahi kumueleza ni biashara gani ,pesa ambayo ingemuwezesha hata kwenda kuishi nje ya nchi.Hapa ninahisi walikuwa na mategemeo ya kupata pesa nyingi sana kutoka katika hiyo biashara.Subira alitueleza kwamba kuna siku Brigita alikuwa na wasi wasi sana na akamwambia kwamba kuna kitu amekichukua kwa mzee Matiku na ana wasi wasi endapo akigundua anaweza akamletea shida.Hakumueleza Subira ni kitu gani hicho na baada ya siku kadhaa akafariki dunia katika ajali ya moto.Inasemekana kwamba mtungi wa gesi ulilipuka na kusababisha nyumba ya Brigita kuteketea na kuwateketeza watu wote waliokuwamo ndani yake.Hii ilitokea wiki mbili tu baada ya Edson kuuawa.Wiki kadhaa baada ya Brigita kufariki dunia mzee Matiku naye alijiua kwa kujipiga risasi ya kichwa.Hadithi ya Edson,Brigita na Matiku ikaishia hapo kwa sababu hatufahamu ni biashara gani ambayo Edson na Brigita walikuwa wanaifanya na ambayo kupitia kwayo walitegemea kupata pesa nyingi . Hatuelewi pia ni kitu gani ambacho Brigita alikichukua kwa mzee Matiku .Picha tunayoipata hapa ni kwamba kuna kitu kilichokuwa kikiendelea baina ya watu hawa watatu.Watu hawa walikuwa na mahusiano na wote wamekufa tena vifo vya utata na ambavyo havikupishana katika kutokea sana.Alianza Edson akauawa kwa risasi,akaja Brigita akafa kwa moto,na mwisho akamalizia mzee Matiku ambaye alijipiga risasi. Lazima hapa kuna sababu iliyopelekea vifo vya hawa watu watatu.Tunatakiwa tuchunguze sababu hiyo ni ipi.” Akasema Mathew akanyamaza kidogo na kuendelea

“ Huo ulikuwa ni upande mmoja tulioanza kuuchunguza.Upande mwingine ni msichana ambaye aliangushiwa tuhuma za mauaji ya Edson aitwaye Peniela .Huyu alikuwa na mahusiano ya wazi ya kimapenzi na Edson .Pamoja na kila aina ya ushahidi kutolewa mahakamani ukimuhusisha Penny na kumuua mpenzi wake ,bado jaji wa mahakama kuu aliyekuwa akiisikilza kesi ile Jaji Elibariki hakuridhika kwamba Penny alitenda kosa na akaamua kumuachia huru.Baada ya kumuachia huru ndipo alipoamua kufanya uchunguzi wa suala hili ili kuufahamu ukweli.Aliungana na Jason wakili aliyekuwa akimtetea Penny mahakamani na kwa pamoja wakaamua kunipa kazi hiyo mimi kwa kuwa wao hawana taaluma yoyote ya kufanya uchunguzi.Bado sijakutana na Peniela na kuongea naye kwa sababu toka nimeanza kazi hii hajaonekana na hajulikani yuko wapi lakini atakapoonekana ni lazima tutamuhoji na kufahamu vitu kadhaa .Nilipata wazo la kutaka kumchunguza Penny hivyo nikaenda nyumbani kwake nikatega butterfly camera na jioni niliporudi nikaona kitu cha kushangaza kidogo.Watu wawili waliingia ndani mwa Penny na kutega camera katika mlango wa kuingilia sebuleni.Sifahamu ni kwa madhumuni gani walitega kamera ile lakini kwa picha ya haraka haraka ilionyesha wazi kwamba walikuwa wakitaka kufuatilia nyendo za Penny.Iwapo wangekuwa ni watu wenye nia njema basi wasingeingia wakati mwenyewe hayupo. Hiyo ilikuwa ni jana.Leo asubuhi tulipomaliza kuongea na Subira watu wengine wawili walinaswa na kamera yetu wakiingia nyumbani kwa Penny.Hatufahamu walikuwa wakihitaji nini ndani mwa Penny lakini baada ya kutoka tuliwafuatilia wale jamaa wakatufikisha Miseko hospitali.Tuliwafuatilia kila sehemu waliyokwenda na kila walichokuwa wakikifanya na tukagundua kwamba walikwenda kumuona mtu aliyelazwa katika chumba PV 2 – 78 .Anitha aliingia katika mfumo wa kompyuta wa hospitali ile na kugundua kwamba aliyekuwa amelazwa katika chumba kile ni John Mwaulaya Albert.” Mathew akanyamaza akafikiri kidogo na kuendelea

“ Baadae tulimfuatilia pia daktari ambaye alikuwa na wale jamaa ndani ya chumba cha John Mwaulaya ,daktari huyu anaitwa Michael Rodriguerz .Tumegundua kwamba ana mtoto wake mmoja anaitwa Michael Jr anasoma katika shule ya kimataifa ya Tanganyika na kila siku huwa anaongozana na mfanyakazi wake aitwaye Lydie masawe kwenda na kurudi shuleni.Tayari tumekwisha ongea na Lydie na amekubali kufanya kazi yetu kwa malipo ya Tsh million saba.Kesho tutamteka mtoto wa Dr Michael na yeye ndiye atakayetupa taarifa zote kuhusiana na mgonjwa Yule aliyelazwa ndani ya kile chumba.Ninataka tupate uhakika kama kweli mgonjwa huyo ni John Mwaulaya ninayemfahamu.Kama ni mwenyewe,we’ll be dealing with something big…” kengele ya mlangoni ikalia.Akasitisha alichotaka kukisema akainuka na kwenda kuufungua akakutana na mlinzi ambaye alimweleza kwamba kuna mtu getini anaitwa .Mathew akamfuata Jason getini na kumkaribisha ndani

“ Hallow Jason,Karibu sana” Mathew akamkaribisha Jason ndani

“ Ahsante sana Mathew” akajibu Jason kisha wakaelekea ndani

“ Jason kutana na Anitha na Noah wale watu niliowataarifu kwamba nitashirikiana nao katika operesheni hii.” Mathew akafanya utambulisho mfupi.Jason akasalimiana na akina Anitha halafu akaketi

“ Nilimtegemea Jaji Elibariki jioni hii” akasema Mathew

“ Ndiyo.Ni Jaji Elibariki aliyetakiwa kufika hapa jioni hii lakini amepatwa na matatizo kidogo na hivyo kunilazimu mimi kusitisha shughuli zangu na kuja badala yake”

“Amepatwa na matatizo gani? akauliza Mathew

“ Mama mkwe wake amefariki dunia.Mke wa rais Dr Flora amefariki dunia leo alasiri”

“ Mke wa rais amefariki?!..Mathew akashangaa

“ Ndiyo amefariki”

“ Nini kimesababisha kifo chake?

“ Hakuna taarifa rasmi mpaka sasa hivi kwani madaktari wanaendelea na uchunguzi wao kubaini kilichomuua lakini kwa mujibu wa daktari wa familia ya rais anadai kilichomuua ni shinikizo la damu”

“ Dah ! mpe pole sana Jaji Elibariki” akasema Mathew halafu kikapita kimya kifupi 

“ Mathew Jaji Elibariki alinielekeza kwamba kuna mzigo unatakiwa”

“ Ndiyo Jason.Tumekwisha ianza rasmi kazi na kuna taarifa Fulani ya muhimu ambayo tunaihitaji.Mtu ambaye atatusaidia ili tuipate taarifa hiyo anahitaji kiasi hicho cha pesa nilichomtaarifu Jaji Elibariki” akasema Mathew.

“ Mmefikia wapi mpaka hivi sasa? Kuna mwangaza wowote? Akauliza Jason

“ Kwa sasa ni mapema mno kusema chochote lakini kazi inakwenda vizuri na baada ya siku kadhaa tutakuwa na cha kusema kuhusiana na uchunguzi wetu lakini kwa sasa hatuwezi sema chochote.Tuachieni kwanza tuendelee kuchunguza.Timu hii unayoiona hapa huwa hishindwi na kitu chochote.Tutalichimba suala hili hadi mzizi wake na mtakipata kile mnachokihitaji” akasema Mathew

“ Ahsante sana Mathew.Basi kama ni hivyo mimi sintakuwa mkaaji sana,nimewapitishia mzigo mliokuwa mkiuhitaji.” Akasema Jason na kufungua begi lake akatoa pesa na kumpatia Mathew

“ Milioni nane hizo.” Akasema

“ Ahsante sana Jason.” Akasema Mathew.Jason ambaye alionekana kuwa na haraka akainuka ishara ya kutaka kuondoka

“ By the way,umepata taarifa zozote za Peniela? Akauliza Mathew

“ Ndiyo.Penny amenipigia simu alasiri ya leo,tayari amekwisha rejea.”

“ Alikwambia alikwenda wapi?

“ Hapana hajanieleza chochote bado”

“ Ok Good.Anafahamu chochote kuhusiana na uchunguzi unaoendelea?

“ Tulimdokeza awali kwamba tunataka kufanya uchunguzi kuhusiana na kifo cha Edson lakini kuhusu kuwakabidhi ninyi jukumu hilo bado hana taarifa zozote”

“ That’s great.Msimueleze chochote kwa sasa.Hatakiwi kufahamu chochote kuhusiana na uchunguzi unaoendelea hivi sasa.Tumuache kwanza apumzike ametoka katika matatizo makubwa” Akasema Mathew na kuagana na Jason

“ Kwa nini Jason alichagua kuwa mwanasheria? Akauliza Anitha baada ya Mathew kurudi akitoka kumsindikiza Jason

“ Kwani kuna ubaya gani akiwa mwanasheria? Akauliza Noah

“ He’s too handsome to be a lawyer” akasema Anitha

“ Kijana mzuri kama Yule alitakiwa awe rubani au meneja kama wa benki au kazi yoyote nyingine kubwa kubwa .” akasema Anitha

“ Hiyo ndiyo kazi ambayo yeye anaipenda na kwa taarifa yako Jason ni wakili mahiri sana hapa nchini ambaye hajawahi kushindwa na kesi.Alipenda kuwa wakili na anaifanya kazi yake kwa moyo mmoja” akasema Mathew

“ Pamoja na hayo bado sikubaliani na yeye kufanya kazi hii ya uwakili.Haimfai hata kidogo.Hapendezi kuwa wakili” 

“ Kwani mawakili wakoje hadi Jason asipendeze akiwa wakili?

“ They have ugly faces because they are always angry” akasema Anitha na wote mle ndani wakaangua kicheko kikubwa.

“ Ok guyz lets get back to business.Kuna jambo ambalo toka mchana nimekuwa nikimuuliza Mathew na akaniahidi kunieleza tutakapo pata wasaa.Nataka kufahamu John Mwaulaya Albert ni nani? Akauliza Anitha.Mathew hakujibu akaenda katika friji akachukua vipande vya barafu akaweka katika glasi halafu akamimina mvinyo ndani yake akanywa.


********************


“ Mhh ! Anitha amenisisimua sana na macho yake.Ni mwanamke mzuri mno.Amenifanya nishindwe kukaa kwa muda mrefu pale ndani kwa jinsi alivyokuwa akinitazama.Macho yake mazuri ya kimalaika yanasisimua akikutazama” akawaza Jason akiwa ndani ya gari baada ya kuondoka nyumbani kwa Mathew

“ Kwa nini Anitha ameamua kuacha kazi zote na kuamua kuifanya kazi hii ya hatari ? Binti mzuri kama Yule hakupaswa kujihusisha kwa namna yoyote ile na kazi kama hizi za hatari.Gosh she’s so pretty.Lakini hawezi kuwa mzuri kumshinda Peniela” Akawaza Jason

“ Kwa sasa ngoja nielekee kwa Peniela.Sijamuona kwa siku kadhaa lazima nikaonane naye jioni hii.Lazima nimuulize alikwenda wapi? Na kwa nini hakuniaga? Dah ! Peniela ameniingia sana akilini.Haipiti saa bila ya kumuwaza.Ninampenda Peniela na kwa hilo siwezi kulificha.Kwa muda wa mwaka mzima nimekuwa na Peniela nikihangaika naye katika kesi na ninaamini nimemfahamu vyema.Nimejiridhisha kwamba ni mwanamke mwenye kunifaa kabisa katika maisha yangu.Ni mwanamke mzuri mwenye kila sifa.Ni mzuri kwa nje na ndani pia nadhani hii ndiyo sababu iliyomfanya hata Edson kuamua kumuacha binti wa rais na kumfuata Penny.Sitakiwi kuendelea kupoteza muda kumueleza ukweli wa moyo wangu kwani chelewa chelewa utakuta mwana si wako.Natakiwa nianze kuchukua hatua kuanzia sasa.Peniela anatakiwa afahamu kwamba ninampenda na niko tayari kufunga naye ndoa na kumsahaulisha mateso na maumivu yote aliyoyapata” akawaza Jason.

Saa mbili kasori dakika kumi na nne za usiku akawasili nyumbani kwa Penny.Akabonyeza kengele ya getini ikaita bila majibu.Takribani dakika tano aliendelea kubaki nje akibonyeza kengele bila geti kufunguliwa.Akachukua simu yake na kumpigia Penny akamfahamisha kwamba yuko pale nje.Hazikupita dakika mbili geti likafunguliwa

“ I’m so sorry Jason.Sikujua kama ni wewe ndiye uliyekuwa ukigonga.Sikuwa nikimtegemea mgeni yeyote Yule jioni hii” akasema Penny 

“ Usijali Penny.Mimi ndiye mwenye makosa kwa kutokutaarifu kwamba nitakuja .Utanisamehe sana kwa kuingilia ratiba zako lakini nisingeweza kulala usiku wa leo bila kuja kukuona na kuhakikisha umerejea salama” akasema Jason

“ Usijali Jason.Hapa ni nyumbani kwako huna haja ya kunitaarifu kwamba unakuja.Muda wowote unakaribishwa” akasema Penny na kumfanya Jason atabasamu.Mezani kulikuwa na chupa kubwa ya whysky.Penny akauliza

“ Unatumia kinywaji gani Jason?

“ Wine” akasema Jason

“ Ouh Jason,tonight why cant you change? Try some whisky.I feel like I want something strong tonight.Join me” akasema Penny.Jason akatabasamu na kusema

“ Ok Penny lets have fun “ akasema Jason.Penny akammiminia whysky katika glasi wakaanza kunywa

“ Jason kwanza kabisa naomba samahani sana kwa kutokutaarifu kwamba sintakuwepo kwa siku kadhaa.” Akasema Penny

“ Usijali kuhusu hilo Penny.Nilifika hapa kwako na kukutana n makufuli.Nilipatwa na wasi wasi sana kuhusiana na usalama wako kwani hata simu yako haikuwa ikipatikana.Siku hizi zote nilikuwa nikiishi kwa wasi wasi mkubwa .Thanks God you are back” akasema Jason

“ Vipi wewe unaendeleaje ? akauliza Penny

“ Ninaendelea vizuri Penny.Just mised you”

“ I missed you too Jason.Naomba nikwambie ukweli Jason huko nilikokuwa hazikupita dakika mbili bila kukuwaza” akasema Penny.Jason akatabasamu

“ Kwani ulikwenda wapi Penny? Umerejea umebadilika sana.Umekuwa mrembo mno tofauti na Penny Yule niliyemzoea.Kama si sauti yako ningeweza hata kukupotea” akasema Jason na kumfanya Penny acheke kicheko kikubwa

“ Nilikwenda kufuatilia masuala yangu ya biashara.And you ? ,leo umetoka wapi kwa sababu umependeza mno tofauti na nilivyokuzoea ukiwa katika suti kila siku.Dont tell me you had a date” akasema Penny ambaye usiku huu alikuwa amechangamka sana

“ No ! I had to meet a friend.It wasn’t a date” akasema Jason.Penny akanywa funda moja na kuuliza

“ Jason kuna kitu nimekuwa nikitaka kukuuliza kila siku lakini sikuweza kutokana na kutingwa na kesi lakini kwa sasa kwa vile mambo yamekwisha naomba nikuulize” 

“ Uliza Penny” 

“ Where is your wife? Sijawahi kukusikia hata siku moja ukizungumizia masuala ya familia”

Jason akatabasamu na kusema

“ Sina mke wala familia”

“ What ?!..Huna mke? ..

“ Ndiyo sina mke.Mbona umeshangaa sana Penny?”

“ Nimeshangaa sana kwa sababu kwa kijana mzuri kama wewe tena msomi uliyebobea katka sheria huna mke.What are you waiting for Jason? Akauliza Penny.Jason akanywa funda moja la whysky akatabasamu na kusema

“ Ni kweli Peniela sina mke mpaka sasa lakini sababu kubwa iliyonifanya niwe hivi mpaka leo ni kutokana na kutingwa mno na kazi na hata kujisahau kwamba na mimi ninahitaji kuwa na maisha kama wengine.Kingine kikubwa ni kwamba bado sikuwa nimefanikiwa kumpata mwanamke Yule ambaye ataufanya moyo wangu usimame,ambaye atanifaa kuwa mke” akasema Jason .Penny akanywa funda la mvinyo na kusema



“ I’m curious.Why a handsome guy like you, you are still single up to now? Be honest with me Jason.Are you a gay? Akauliza Penny.Jason akastushwa sana kwa swali lile akashindwa kujibu akabaki amemtazama Penny .Walitazamana kwa sekunde kadhaa halafu Penny akanywa funda la whysky na kusema

“ Mbona hunijibu Jason? Is it true? Akauliza Penny.Bado Jason hakumjibu kitu.Penny akainuka toka katika sofa alilokuwa amekaa akamfuata Jason na kukaa karibu naye.

“ Jason tell me the truth.” Penny akamnong’oneza Jason sikioni.Mapigo ya moyo ya Jason yakaanza kwenda kasi baada ya Penny kumpumulia sikioni.Penny akamtazama usoni na kuwaza

“ There is only one way to find the truth” 

Taratibu Penny akaupeleka mkono wake hadi katika maeneo nyeti ya Jason na ghafla akahisi kushika kitu kigumu

“ Gosh ! its serious” akasema huku akicheka.Jason hakuwa akicheka.mapigo ya moyo yalikuwa yakimuenda mbio.Penny akaendelea kuchezea maeneo nyeti ya Jason yaliyokuwa yamefura.

“ Sorry Jason nilikufikiria vibaya.Umezidi kuwa mzuri” akasema Penny kwa sauti ya kunong’ona

“ what are you doing Penny ? What do you want? Akauliza Jason

“ Please Jason,make my night beautiful” akasema Peniela.Kwa kasi ya ajabu Jason akamvuta Peniela na kuanza kumwagia mabusu mazita mazito huku akimtoa nguo

“ Jason I need you..I need you Ja…!!..” akasema Penny

“ I’ve been waiting for so long for this chance.Leo utaongea lugha kumi na mbili” akasema Jason huku akivua nguo yake ya ndani

TUKUTANE SEHEMU IJAYO……………………………

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...