ONGEZA IMANI YAKO

ONGEZA IMANI YAKO KWA MUNGU UTENDE MAKUU



Hello msomaji wangu. Nakukaribisha na leo kuungana nami.

Mathayo 21:18-22

18 Hata asubuhi alipokuwa akienda mjini, aliona njaa.

19 Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele. Mtini ukanyauka mara.

20 Wanafunzi walipoona, walistaajabu, wakisema, Jinsi gani mtini umenyauka mara?

21 Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng?oka, ukatupwe baharini, litatendeka.

Bwana Yesu asifiwe mtu wa Mungu.

Maandiko tuliyosoma hapo juu yanatukumbusha kuchochea iman zetu.

Mtu wa Mungu hiki kipindi nikipindi cha kuiweka iman mbele, nikipindi cha kumtegemea sana Mungu na kumpa nafasi yakutenda katika kila kila jambo lililo mbele yetu

Tujikumbushe maana ya Iman

 " Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana." Ebrania 11:1,


Iman ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, mambo yasiyoonekana,

Maana yake kuna vitu vipo kichwan mwetu havionekan vinataka iman ili vidhihilike katika ulimwengu wa mwili, 



Tatizo watu wengi wanaamini lakini iman yao ni mfu, haifanyi kazi, maana yake watu wanaiman ya mdomon,


Wakati huo Neno linatuambia Iman pasipo matendo imekufa Yakobo 26:2.


Mtu wa Mungu Yesu anawambia wanafunzi ' Amin nawambia mkiwa na iman msipokua na shaka mtafanya si hilo tu la mtini tu, lakin hata mkiuambia mlima huu Ng'oka ukatupwe baharini litatendeka.


Mashaka, hofu, wasiwasi, kusikiliza wazee walifanya vile wakashindwa na yeye anaogopa kushindwa vinawasumbua watu wengi


Mtu wa Mungu Yesu aliona mashaka kwa wanafunzi, yale mashaka ndio kikwazo kwa watu wengi


Jiulize wewe nimmoja ambao wanasumbuliwa na mashaka katika kuamua mambo au katika kufanya mambo? Jiulize 


Ili uwe na wokovu imara na wokovu wako uwe na matokeo weka iman yako kwa Mungu katika yote unayoyafanya na unayoomba,


Huwa nawaambia watu yaamini maombi yako pia liamini Neno la Mungu.


Ukiyaamini maombi yako na Neno umemshinda adui, kwakua adui anaachilia mashaka kwa mtu akijua mtu mwenye mashaka Mungu hampendi na majibu yake hapokei toka kwa Mungu


Tuone Yakobo 1:6

6 Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.


Ukitaka uwe na nguvu za rohon usiwe mtu wa kuyumba yumba kwenye maamuzi, mtu mwingine anapanga kufunga siku 7 au siku 30 anafika kati anaacha kwanini sababu anayumba hana msimamo, ukiamua kufanya jambo lifanye kwa nguvu hata kama ndani yako zinasikika sauti zakukuvunja moyo songa mbele,


Ukiamua kukua kiroho chukua hatua sema naamua kuwa mfungaji kuwa muombaji nitasimama katika maombi Neno ndani ya hii miez sita iliyobaki.


Hakika katika jina la Yesu maisha yako yatabadilika tu kwakua umedhamilia na unafanya kwa bidii.


Omba kwa jina la Yesu kukataa roho za mashaka wasiwasi na hofu ndani yako, ng'oa kama pando ukiomba vizuri utakua jasiri katika maamuzi yako, watu watakuona watofauti vile utakavyokua unayakabiri mambo.


Omba kuongeza iman yako kwa Mungu katika jina la Yesu, Luka 17:5


Mungu akubariki sana.


Kama umebarikiwa na ujumbe huu share kwa ndugu jamaa na rafiki zako popote pale facebook na kwenye magroup ya Whatsup hutaachwa hivyo hivyo bali utabarikiwa kwa kuitangaza injili kwa kushare. Pia like Facebook Page yetu ya Nyumba ya Sala kwa Mataifa Yote kwa masomo mengi zaidi.


Ukipenda kutumiwa masomo ya Neno la Mungu kila siku kwa Whatsup tuma majina yako mawili inbox, whatsup kwa namba ya Tigo 0657 048393 kuomba kuunganishwa kupewa masomo kila siku na utatumiwa, pia kwa ushauri na maombi piga namba zilizopo hapo chini, na Mungu wambinguni akubariki sana.


Merito Tagalile

~0657 048393

~0625 610925

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...