RANGI YA SAMAWATI / BLUE
Hello msomaji wangu wa makala hii
Mara nyingi watu hupendelea kuvaa nguo za rangi ya blue wanapoenda kwenye shughuli rasmi au zenye mkusanyiko wa watu wengi. Ushawahi kujiuliza kwanini? Kamata kalamu na karatasi nikushirikishe jambo✍🏿
Blue ni rangi tulivu hivyo inakuongezea kujiamini unapokuwa mbele za watu kwasababu inapunguza attention ya watu katika muonekano wako.
Watafiti mbalimbali pamoja na wanasaikolojia wamekubaliana kuwa rangi ya blue inaongeza ufanisi na uzalishaji (Effectiveness and Productivity) ndo maana ofisi nyingi zinapambwa kwa rangi blue👋🏿Funny fact😀
Kutokana na utulivu wa rangi ya blue huleta picha ya Mamlaka, Msimamo, Amani, Urafiki, Imani, Kujitoa, Kujali, Uwajibikaji, Utiifu, Upole na Heshima.
Watafiti wanatanabaisha kuwa rangi ya blue inasaidia kupunguza stress kwa kuwa inaleta utulivu wa mwili na akili kwa wenye nazo😃 (Jokes).
Rangi ya blue hutumiwa zaidi na makampuni ya Ulinzi katika Sare na matangazo yao kuonyesha ulinzi na usalama.
Kwa kuhitimisha rangi zinategemea zaidi matendo ya mtu (personality) ili kutoa maana inayoakisiwa. Hivyo hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya rangi na matendo ya mtu.
Nakushukuru kwa kuungana nami katika makala hii.
__________________
Mwandishi: RAJABU ATHUMAN (Kibopa)
WhatsApp No: +255715685395
No comments
Post a Comment