SIMULIZI: PENIELA (Season 1 Ep 6)

 SEASON 1

SEHEMU YA 6

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

“ Nimepigiwa simu na ofisi kuu asubuhi ya leo wakinionya kuhusiana na kutorudiwa tena kwa uzembe mkubwa uliopita kiasi cha kumuacha Penny akaingia katika matatizo makubwa na kuhatarisha mpango wetu wa miaka mingi.Endapo Penny angekutwa na hatia mahakamani na kufungwa ,kila kitu kingefikia mwisho.Juhudi zote za miaka zaidi ya ishirini zingekuwa ni kazi bure. Bila Penny kila kitu kitakwama .Kwa hiyo basi maagizo niliyoyapata toka ofisi kuu ni kwamba tuhakikishe uzembe kama ule haujirudii tena na Penny apewe ulinzi wa kutosha na kumuepusha na mambo yote yanayoweza kumsababishia matatizo na kuhatarisha mpango mzima.


Kazi kubwa imekwisha fanyika na tuko katika hatua za mwishoni.Tunatakiwa kuongeza umakini maradufu.Tunatakiwa tufahamu na tuwepo kila mahala alipo Penny,tufahamu watu anaokutana nao na kwa kuanzia tunatakiwa kumfahamu Jaji Elibariki Chukuswa ambaye anakwenda kuonana na Penny jioni ya leo.” Akasema Yule jamaa


ENDELEA……………………………….


Kwa mara ya kwanza baada ya kukaa gerezani kwa mwaka mzima,Penny alisimama mbele ya kioo kikubwa cha kujitazamia kilichopo chumbani kwake akijitazama namna alivyokuwa amependeza.Alikuwa amevaa gauni refu jekundu maalum kwa kutokea usiku.Alijiangalia na kutabasamu halafu akageuka na nyuma akajiangalia

“ Nothing have changed.I’m still the hot Peniela” akawaza Penny huku akiikoleza rangi ya mdomo.

“ sasa niko tayari kwenda kuonana na Jaji Elibariki” akawaza

Akiwa bado anamalizia kujiremba,kengele ya mlangoni ikalia,akatoka na kwenda kufungua mlango .


Kwa sekunde kadhaa akabaki akitazamana na Jason ambaye hakuamini macho yake

“ Wow ! “ akasema Jason

“ Umependeza mno Penny.Sikuwahi kukuona ukiwa umependeza kama ulivyopendeza leo.Kumbuka Jaji Elibariki ni mtu mwenye ndoa yake kwa hiyo chunga asije akachanganyikiwa na uzuri wako na kubadili mawazo” akasema Jason na wote wakaangua kicheko.


“ Ni muda mrefu sijapendeza Jason ndiyo maana kwa usiku wa leo nimeona nirudie enzi zangu”

Akasema Penny

“ Uko tayari? Akauliza Jason

“ Ndiyo Jason,niko tayari lakini naomba unisubiri dakika mbili kuna kitu nimesahau chumbani.” Akasema Penny na kuelekea chumbani kwake.Wakati akiwa bado chumbani kengele ya mlangoni ikalia .Jason aliyekuwa sebuleni akaenda kuufungua mlango na kukutana na kijana mmoja mrefu mwembaba,aliyevaa suti nzuri nyeusi iliyomkaa vyema.

“ Hallo” akasema Jason

“ Hallo” akajibu Yule jamaa ambaye sura yake ilionyesha mshangao kidogo kwa kumkuta Jason pale ndani

“Karibu ndani” akasema Jason na Yule jamaa akaingia ndani

“ Nimemkuta Penny? Akauliza

“ Ndiyo.


Penny yupo ,anakuja sasa hivi” akasema Jason halafu kikapita kimya kifupi

“ I’m Jason” akasema Jason

“ I’m Kareem” akasema Yule jamaa na kabla maongezi hayajaendelea zaidi Penny akatokea.

“ Kareem!!..akasema Penny kwa furaha

“ Penny..!!” akasema Kareem na kumfuata Penny wakakumbatiana.

“ Welcome back Penny”

“ Ahsante sana Kareem” akajibu Penny

“ Pole sana kwa matatizo.Nilikosa kabisa hata muda wa kuja kukuona.”

“ Usijali Kareem.Ninaelewa ugumu wa kazi zenu.Nashukuru Mungu matatizo yamekwisha”

“ Nashukuru kwa kulitambua hilo.


Vipi uko tayari?

“ Kareem I’m sorry.Leo sintaweza kwenda ,nimepatwa na dharura.Samahani sana kwa usumbufu.Labda siku nyingine” akasema Penny na kumstua Kareem

“ What ?!!!..

“ I’m so sorry Kareemkwa leo sintaweza kwenda”

“ How could you do this Penny? What am I going to tell him? Akauliza Kareem

“ Tell him that I don’t have time today” akasema Penny na kumgeukia Jason

“ Jason can we go?


Jason akainuka na kumfuata wakatoka nje akamfungulia Penny mlango wa gari akaingia halafu wakaondoka na kumuacha Kareem akiwa amesimama mlangoni hajui afanye nni

“ Sorry Peny”

“ Sorry for what?!!..akauliza Peny

“ Nimekuvurugia ratiba zako.Kama ulikuwa na miadi na mtu ungenitaarifu mapema ili tuahirishe kazi yetu”

“ Usijali Jason.Kuna mtu nilikuwa nahitahi kuonana naye jioni ya leo lakini haikuwa na umuhimu mkubwa.

“ Your boyfriend? Akauliza Jason

“ I don’t have a boy friend Jason” akasema Penny na kumfanya Jason atabasamu


Waliwasili Moniz 5 star hotel,wakashuka garini wakapanda lifti hadi ghorofa ya tano wakashuka na kuanza kutembea katika varanda refu huku wakisoma namba za vyumba.Walisimama katika mlango wa chumba namba 204.Jason akabonyeza kengele ya mlangoni na baada ya dakika moja mlango ukafunguliwa na jaji Elibariki akajitokeza.Wakaingia ndani

“ Hallow Penny. habari yako? Akasema jaji Elibariki

“ habari nzuri Jaji Elibariki.Pole na majukumu”

“ Ahsante sana Penny.Vipi unaendeleaje na maisha mapya?

“ Ninaendela vizuri sana jaji.Mwanzo unakuwa mgumu lakini baada ya muda nitazoea na kurudia hali yangu ya kawaida.” Akasema Penny.Jason akapiga simu hotelini na bila kuchelewa muhudumu akafika akiwa na toroli lenye vinywaji akaviweka mezani.


Jason akaomba awaache Jaji Elibariki na Penny yeye kaenda kuendelea na majukumu mengine

“ Penny ni mara ya kwanza mimi na wewe kukutana,lakini utakuwa mi mwanzo wetu pia kufahamiana rasmi” akaanzisha mazungumzo Jaji Elibariki baada ya Jason kuondoka na kuwaacha wao wawili pekee mle chumbani

“ Ni kweli mheshimiwa Jaji,Sikuwa nakufahamu hapo kabla na nilikufahamu tu pale ulipoanza kuisikiliza kesi iliyokuwa inanikabili.Nafurahi sana kukutana nawe ana kwa ana.Nilistuka Jason aliponiambia kwamba unahitaji kuniona,lakini kwa upande mwingine nikafurahi kwa sababu hata mimi nilikuwa na wazo la kukutafuta na kukushukuru kwa kuniachia huru.” Akasema Penny Jaji Elibariki akatabasamu

“ Penny si mimi niliyekuachia huru bali ni Mahakama baada ya kujiridhisha kwamba hukutenda kosa. Na hiyo inatokea si kwako tu bali kwa wote wanaofikishwa mahakamani na kukutwa hawana makosa,mahakama huwaachia huru.” Akasema jaji kikapita kimya cha sekunde kadhaa

“ Penny nadhani Jason amekwisha kueleza kwa ufupi kuhusiana na kilichotufanya tukutane leo hii.” Akasema Elibariki

“ ndiyo,alinieleza kwa ufupi” akajibu Penny

“ Nimeifuatilia kesi hii toka ilipoanza na nikagundua kwamba kuna nguvu kubwa iliyotumika ili kuhakikisha kwamba unapatikana na hatia na hatimaye kufungwa.


Nimejiuliza sana ni kwa nini nguvu kubwa itumike namna hii ikiwa ni pamoja na kuwasilisha kila aina ya ushahidi ambao kama Jaji usipokuwa makini unaweza kabisa kumtia mtu hatiani. Kutokana na mwenendo mzima wa kesi namna ulivyokuwa,nime

shawishika kuamini kwamba kuna kitu kipo nyma ya kesi hii.Kuna kundi la watu ambao walifahamu kabisa kwamba hukutenda lile kosa lakini walisimama imara kuhakikisha kwamba unabambikiwa kesi ile na kukutwa na hatia na hatimaye kuhukumiwa kwa mauaji.Ninachojiuliza,je watu hawa ni akina nani? Kwa nini walitaka ufungwe? Nani alimuua Jason? Akasema jaji Elibariki na kunywa mvinyo kidogo halafu akaendelea

“ Kutokana na maswali hayo ambayo nimekuwa nikijiuliza bila ya kupata majibu,ninalazimika kuamini kwamba pamoja na kukuacha huru lakini bado usalama wako uko mashakani.Watu hawa bado wako nyuma yako na watakuandama usiku na mchana bila kulala hadi wahakikishe kwamba lengo lao limetimia.


Kwa hiyo basi nimekuita hapa kukutaarifu kwamba mimi na wakili wako Jason tumeamua kufanya uchunguzi kisiri siri na kumjua muuaji wa Edson.Ni hiyo tu ndiyo itakuwa salama yako na sisi sote pia.Unaweza ukaona kwamba hali ni shwari lakini naomba nikuhakikishie kwamba hali yetu kiusalama si nzuri hata kidogo.Ninachokiomba toka kwako ni ushirikiano wako ili kwa pamoja tuweze kumtafuta na kumpata muuaji na kumfikisha mbele ya mkono wa sheria.Tukimpata muuaji tutajua sababu ya wewe kubambikiwa kesi ya mauaji.


Tutauweka ukweli wazi ili jina lako lisafishwe katika jamii”

Penny akanywa kinywaji kidogo na kusema

“ Jaji Elibariki,kama nilivyomwambia Jason kwamba nakubaliana na wazo hilo la kufanya uchunguzi wa kumbaini mtu aliyefanya mauaji yale.Niko tayari kutoa ushirikiano wangu wa kila namna ili tuweze kumbaini mtu huyo” akasema penny

“ Nashukuru sana Penny kwa hilo.” Akasema jaji Elibariki na kunywa funda moja la mvinyo



“ Kabla ya kuanza kwa uchunguzi au kuamua nini tufanye,ningependa kwanza kufahamu machache kutoka kwako kuhusiana nanamna tukio lile lilivyotokea na wewe ukajikuta ukitiwa hatiani.Samahani lakini kwa kukukumbusha mambo ambayo unajitahidi kuyasahau.” Akasema jaji Elibariki


Penny akafumba macho na kufikiri kwa muda halafu akasema

“ Ilikuwa ni siku ya Jumamosi,mimi na edson tulipanga tutoke kwa chakula cha jioni.Sikujua anataka kunipeleka sehemu gani kwani alisema angenifanyia surprise.Vile vile alisema kwamba kuna jambo analotaka kunieleza usiku huo” Penny akanyamaza akanywa mvinyo kidogo na kuendelea

“ Alitaka kunipitia nyumbani kwangu lakini nikakataa na kumwambia nitampitia yeye nyumbani kwake na siku hiyo tutatumia gari langu jipya.Saa moja na nusu niliwasili nyumbani kwake na kubonyeza kengele ya getini ambayo iliita kwa dakika kadhaa bila majibu.Nikajaribu kufungua eti na kukuta liko wazi.


Mlango wa kuingilia sebuleni ulikuwa umefungwa kwa funguo nikahisi labda Eddy atakuwa ametoka na kwenda maeneo ya karibu.Nilikuwa na funguo aliyonipa yeye mwenyewe nikafungua na kuingia ndani.Nilikaa sebuleni kwa takribani dakika kumi bila kutokea nikaamua kumpigia simu ambayo iliita bila kupokelewa.Nili

patwa na wasi wasi ikanibidi kupanda ghorofani katika chumba chake cha kulala.Nilipoingia tu ndani nikakutana na picha ambayo sintakuja kuisahau katika maisha yangu.”


Akanyamaza kidogo na kunywa mvinyo halafu akaendelea

“ Nilimkuta Edson akiwa amelala kitandani,huku mwili wake ukiwa umetapakaa damu.Kifuani pake kulikuwa na bastora .Nilipatwa na taharuki nikaenda kuishika bastora ile nikaiweka pembeni na kuanza kumuangalia Eddy kama bado mzima.Nilichanganyikiwa na kutaka kutoka ili nikatafute msaada.Wakati nashuka ngazi nikikimbia kwenda kutafuta msaada nikakutana na watu wanne waliodai kwamba wamesikia mlio wa risasi.Nilishindwa kuongea .Wakanikamata na kudai kwamba nimemuua Eddy.Nilipelekwa polisi na kufunguliwa mashitaka na kilichoendelea baada ya hapo unakifahamu hadi pale uliponiachia huru..”akasema Penny na mara simu yake ikaita..


“ Samahani nilisahau kuizima simu” akasema Penny na kuitoa simu ile akatazama mpigaji na mara sura ikambadilika.Hakuipokea simu ile akaikata na kuizima kabisa.Jaji Elibariki akavuta pumzi ndefu na kusema

“ Pole sana Penny kwa yote yaliyotokea.Lakini kuna jambo moja nataka kulifahamu.Unahisi ni kitu gani Edson alitaka kukueleza?

Penny akafikiri na kusema

“ Hapana sifahamu alitaka kunieleza nini lakini alisema kwamba ana jambo la muhimu la kuniambia usiku huo”

“ Kwa muda gani ulikuwa naye katika uhusiano?

“ Ni zaidi ya mwaka mmoja.Tulianza kwa siri lakini baada ya yeye kuachana na mpenzi wake Anna,tukaamua kuweka wazi mahusiano yetu”

“Hapo kabla uliwahi kuwa na mpenzi ambaye mliachana?

“Hapana ,sijawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi hapo kabla.Edson alikuwa ni mwanaume wangu wa kwanza”

“ Uliwahi kupokea vitisho vyovyote toka kwa mpenzi wa zamani wa Edson au mtu mwingine yeyote?

“ Maneno na vitisho haviwezi kukosekana.Tulikuwa tunatumiana jumbe mbali mbali za kutishana,kutuk

anana na hata kupigiana simu za vitisho”

“ Unadhani Anna anaweza akawa na mkono wake katika kifo cha Edson?

Penny akafikiri kidogo na kusema

“ Hapana ,sidhani kama anaweza kuwa amehusika na kifo kile “

“ kwa nini?

“Kwa sababu alimpenda sana Edson “

“Hufikiri kwamba Anna aliumizwa sana baada ya kuachwa na Edson na hivyo akaamua kumuua ili kulipiza kisasi?

“ Sidhanikama Anna anaweza akafanya hivyo kwa namna alivyompenda Edson.” Akajibu Penny na kimya kidogo kikapita

“ Kama si Anna ,unahisi nani anaweza akawa ni muuaji? 


Akauliza Jaji Elibariki.Penny akainama akafikiri kwa muda na kusema

“ Hapana mheshimiwa sifahamu kabisa nani anaweza kuwa muuaji”

Kimya kifupi kikapita halafu jaji Elibariki akasema

“ Penny kuna jambo lolote ambalo hukuwahi kumueleza mtu yeyote Yule ambalo ungependa kuniambia na linaloweza kutusaidia katika uchunguzi wetu?

Swali lile likamfanya Penny anyamaze kwa muda wa zaidi ya dakika mbili halafu akasema

“ Hapana mheshimiwa,mambo yote nimekwisha yasema.


Hakuna ambalo sijalisema”

Waliendelea kuongea mambo mengi na muda ulipofika Jason akarejea na kumchukua Penny akamrejesha kwake.Akiwa njiani kurejea nyumbani kwake ,Jaji Elibariki akampigia simu

“ Halo jaji” akasema Jason

“ Jason,umemfikisha penny salama?

“ Ndiyo nimemfikisha salama.Niko njiani kuelekea nyumbani “

“ Ok Jason.Nimezungumza mambo mengi na Penny lakini kuna jambo moja nimeligundua toka kwake”

“ jambo gani Jaji?

“ Kuna kitu anakifahamu kuhusiana na kifo cha Edson lakini hayuko tayari kuliweka wazi”

“Are you sure? Akauliza Jason

“ yah ! I’m sure.


Kuna kitu anakifahamu lakini hayuko wazi kukisema.”

“ sasa tutafanya nini?

“ Tutaendela na uchunguzi wetu kimya kmya bila ya kumshirikisha Penny.” Akasema Jaji Elibariki

Jason akafikiri na kusema

“ Ok Jaji.Tutaonana kesho na tutajadili kwa kirefu” akasema Jason na kukata simu


TUKUTANE SEHEMU IJAYO…

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...