PENIELA (Season 1 Ep 16)

 ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

“ Tafadhali usilie Penny.Usilie malaika wangu.Kuna mambo mengi ambayo yametokea kitu cha kwanza ninachokihitaji toka kwako ni msamaha wako.Ni kweli nilikuacha ukaingia katika matatizo makubwa na sikusimama pamoja nawe.Penny please forgive me my angel.We have so many to talk” akasema Dr Joshua.Penny akainua kichwa akamtazama na kusema

“ Nimekwisha kusamehe Dr Joshua na ndiyo maana niko hapa.Umesema tuna mambo mengi ya kuongea hata mimi nina mengi ya kuuliza lakini kwanza nataka unieleze kwa nini Edson aliuawa? Akauliza Penny.Dr Joshua akachukua kitambaa na kujifuta jasho,akainuka na kwenda mezani akajimiminia mvinyo na kupiga funda kubwa.

ENDELEA………………………………….

“ Kwa nini unataka kufahamu Penny? Akauliza Dr Joshua

“ Edson was my friend and my lover so I need to know why you ordered him killed” akasema Penny

“ He was your lover ! akasema Dr Joshua kwa sauti ya juu.Penny hakujibu kitu akakaa kimya

“ You cheated on me !

“ I loved him..He was such a gentleman” akasema Penny na Dr Joshua akakaa kimya akazunguka chumbani halafu akasema

“ Unataka kuufahamu ukweli?

“ Ndiyo nahitaji kuufahamu ukweli “ akasema Penny.Dr Joshua akamsogelea akamshika mkono na kusema

“ Ni wivu ndio ulionifanya nitoe maamuzi yale.Ninakupenda mno Peniela na nilipogundua kwamba unanisaliti kwa kutembea na Yule kijana nilikasirika sana.Penny wewe ni wangu peke yangu na sitaki unichanganye na mtu yeyote hususani hawa vijana wadogo.Kijana Yule hakuwa na kitu chochote cha kukupatia .Nilikuahidi kukupa kila fahari ya dunia hii lakini bado ukanisaliti.Penny I’m a powerful man in the country so I can do anything when I’m angry.Nakupa uhuru nieleze kitu chochote na kila unachokitaka nitakupatia lakini ubaki kuwa wangu peke yangu na usije ukanichanganya na mtu mwingine.” Akasema Dr Joshua

Penny akafuta machozi na kumtazama Dr Joshua kwa macho makali

“ Hukutakiwa kufanya vile.Hutakiwi kuwa na wivu na mimi,wewe ni mtu mwenye familia yako.You cant control me.You cant give me all that I want.You cant be there all the time when I need you.I’m a human Dr Joshua and I have needs” akasema penny kwa sauti ya juu

“ Penny mara ngapi nikwambie kwamba wewe ni kila kitu kwangu? Unataka niende katika luninga na kuutangazia ulimwengu kwamba ninakupenda? Niko tayari kufanya hivyo kama hiyo itakufanya uufungue moyo wako na kuniruhusu niingie ndani.Nipe nafasi ya kukuonyesha ni namna gani ninakupenda Penny.Forget that I’m married and I have a family.Not all marriages are real.Some are in papers. Kama ukinipa nafasi ndani ya moyo wako ,nitakuweka katika nafasi ya juu kuliko wanawake wote wa nchi hii.You’ll be the first lady.So why cant we skip the past and talk about our bright future? Akasema Dr Joshua Penny akamuangalia na kusema

“ Najaribu kukubaliana nawe lakini bado moyo wangu na maswali mengi ambayo yanahitaji majibu sahihi Dr Joshua.”

“ Just one question Penny.One question only” akasema Dr Joshua

“ Kwa nini kesi ile ya mauaji ya Edson iliniangukia mimi na ukakubali kuniona nikinusurika kuangamia wakati ukijua kabisa kwamba sikutenda kosa? Kwa nini hukufanya lolote kunisaidia kama kweli unanipenda?

“ Hayo ni maswali mawili Penny.Nitajibu swali moja tu” akasema Dr Joshua ,akanywa funda moja la mvinyo na kusema

“ I was angry” akasema na kunyamaza

“ I was angry for what you did to me and I wanted to destroy you.Nilitaka ufutike kabisa katika dunia hii,nilidhani kwamba ile ilikuwa ni njia muafaka ya kuweza kukusahau,but I was wrong.Penny naomba uelewe kwamba tayari umeniingia katika kila mshipa wa mwili wangu na siwezi kukutoa tena.Ninaomba utambue kwamba nilipata wakati mgumu sana kwa maamuzi yale na hilo ndilo jambo ambalo nitaendelea kulijutia hadi siku ninaingia kaburini.Tafadhali naomba utafute ndani ya moyo wako unisamehe na tuendelee na mapenzi yetu kama zamani.Nilifanya kosa kutaka kukupoteza mara ya kwanza safari hii sitaki tena kurudia kosa .Please lets not talk about the past .Lets not ruin our lovely night.Lets open new chapter in our book.” Akasema Dr Joshua kwa sauti ya kubembeleza,akamvuta Penny na kumkumbatia akambusu

“ Nimekwisha kusamehe Dr Joshua kwa sababu ninakupenda na ndiyo maana niko hapa ila tafadhali nakuomba usifanye tena jambo kama lile.Kama kuna tatizo kati yetu tafadhali naomba uniadhibu mimi na si watu wengine wasiokuwa na hatia.Please don’t hurt people that I love”

“ Siwezi kufanya hivyo tena kama utanihakikishia kwamba hautakuwa na mahusiano na mtu mwingine zaidi yangu. Niambie chochote kile nitakupatia Penny.I have power ,money and everything to make you live like a queen”

‘ Dr Joshua I’m still young and you are getting old.You have a family,you have a wife on bed,you have huge responsibilities and you cant be there all the time that I need you……………..” Penny hakumaliza sentensi yake Dr Joshua akamkatisha

“ I’ll be there ! Anytime you need me just call me and I’ll be there.Kwako sintakuwa na neno la hapana.Niambie chochote unachokitaka nitakutimizia” akasema Dr Joshua na kumfanya Penny atabasamu

“ This is the moment I’ve been waiting .Tayari ameingia mwenyewe katika nyavu na kilichobaki sasa ni kumvua tu.Ni wakati wangu sasa kumaliza kazi yangu” akawaza Penny

“ Dr Joshua kabla ya yote kuna jambo ambalo nataka nikuombe”akasema penny

“ Omba chochote Peniela.Kila kitu katika nchi hii kipo chini yangu” akasema Dr Joshua

“ Ninao watu wangu wawili ambao ni zaidi ya marafiki.Niko nao karibu sana watu hawa.Naomba kwa namna yoyote ile watu hawa wasije wakadhurika.Wana mchango mkubwa sana katika maisha yangu.Can you give me your word that you wont hurt them?” akasema Penny.Dr Joshua akatabasamu na kusema

“ I give you my word Penny.Who are they?

“ Wakili wangu Jason pamoja na Jaji Elibariki”

Dr Joshua akastuka kidogo baada ya kusikia jina la jaji Elibariki likitajwa

“ Usihofu Penny.Jaji Elibariki ni mwanangu.Amemuoa binti yangu. Ni kijana makini na mchapakazi na ndiyo maana nikamchagua kuwa jaji wa mahakama kuu.Nafahamu wewe na yeye ni marafiki na baada tu ya kumalizika kwa kesi mlikutana kwa chakula cha usiku.Nadhani ulikwenda kumshukuru kwa kukuachia huru” akasema Dr Joshua huku akicheka

“ Kwa hiyo umeweka watu wa kunifuatilia maisha yangu? Akauliza Penny

“ Ni kwa sababu ya usalama wako Penny.

“ Tafadhali naomba uwaondoe watu wako wasiendelee kunichunguza.I can defend myself.Siku nikigundua kwamba bado watu wako wanaendelea kunfuatilia it’ll be the end of us”

“ Ok Penny nitawaondoa kama ndivyo unavyotaka lakini ukumbuke kwamba wewe ni mke mtarajiwa wa rais kwa hiyo unahitaji ulinzi.Sema kingine unachokitaka” Penny akatabasamu na kusema

“ Kwa sasa kingine ninachokihitaji ni hiki” akasema na kulivuta taulo alilojifunga Dr Joshua na kumsukuma kitandani halafu akaanza tena kumfanyia utundu na baada ya dakika kadhaa wakaingia tena katika mzunguko mwingine.Ulikuwa ni usiku wa aina yake kwa Dr Joshua.

***********

Kengele ya mlangoni ililia kuashiria kwamba kuna mtu mlangoni.Mathew akainuka na kwenda kuufungua.

“ Anitha the devil ..!! akasema kwa furaha Mathew baada ya kuufungua mlango na kukutana na Anitha

“ Welcome my dear.Welcome home” akasema Mathew huku akikumbatiana na Anitha

“ Thank you so much Mathew.” Akasema Anitha

“ Ungenitaarifu muda ambao utatua ili nije nikupokee “ akasema Mathew

“ Usijali Mathew,hapa ni nyumbani na hauna haja ya kupoteza muda wa kufanya mambo mengine kwa kuja kunipokea.Npe habari kazi inaendeleaje? Akauliza huku akifungua friji na kutoa chupa ya mvinyo akajimiminia katika glasi.

“ Hautaki hata kupumzika Anitha? Pumzika kwanza halafu mambo ya kazi yatafuata baadae” akasema Mathew na kumfanya Anitha acheke kidogo

“ Mathew you know me,I work like a devil. Nimekuja kikazi kwa hiyo tufanye kazi na mambo mengine yatafuata baadae” akasema Anitha.Mathew akatasamu na kusema

“ Kazi tayari imeanza na mpaka sasa hakuna hatua kubwa iliyopigwa japo kuna mwangaza kidogo tayari nimeupata” akasema Mathew.Anitha akageuza kichwa na kumtazama Mathew akasema

“ Nilipata kazi ya pesa nyingi nchini Brazil ambayo nilitakiwa nikaifanye wiki hii lakini nimelazimika kuweka pembeni kwanza ile kazi na kuja kuimaliza kwanza kazi uliyoniitia. Nipe taarifa za kina kuhusiana na kazi hii” akasema Anitha huku akiifungua mizigo yake na kutoa zana zake za kazi

“ Ahsante sana Anitha kwa kuahirisha mambo yako mengine na kuja kuungana nami.Hata mimi pia nimelazimika ksimamisha baadhi ya shughuli zangu kwa ajili ya shughuli hii. Si kazi yenye malipo makubwa lakini ni muhimu sana kwa rafiki zangu” akasema Mathew



“ Kuna kijana mmoja aitwaye Edson,ambaye alikuwa mfanyakzi wa kitengo cha mawasiliano ikulu,aliuawa na watu wasiofahamika na kesi hiyo kumuangukia msichana mmoja aitwaye Peniela . Jaji Elibariki ambaye alikuwa akiisikiliza kesi ile aligundua kwamba msichana Yule aliyekuwa akituhumiwa hakutenda kosa hivyo akalazimika kumuachia huru.Baada ya kesi kumalizika alishawishika kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na kesi ile kutokana na sintofahamu kadhaa alizozigundua wakati wa usikilizwaji wa kesi.Aliungana na wakili Jason aliyekuwa anamtetea mtuhumiwa na kwa pamoja wakaamua kunipa kazi hii kutokana na kwamba wao hawana taaluma ya uchunguzi.Kwa hiyo naomba ufahamu kwamba tunaifanya kazi hii kuitafuta haki na vile vile kuwasaidia rafiki zetu” akasema Mathew

“ Kesi hii inafanana na ile ya Justine Abangiza wa Rwanda” akasema Anitha huku akiunganisha vifaa vyake

“ Yah ! zinashabihiana sana ingawa hii ya Edson ina utofauti kidogo” akasema Mathew

“ Nimeongea na wazazi wake jioni ya leo .Nilitaka tu kufahamu mtoto wao alikuwa ni mtu wa namna gani.Kabla ya hapo mchana wa leo nilikwenda nyumbani kwa Peniela,msichana aliyetuhumiwa kumuua Edson, na kutega kamera mbili ,niliporudi nimekutana na picha hizi” akasema Mathew na kumuonyesha Anitha zile picha za wale watu walionaswa katika kamera nyumbani kwa Penny

“ They look so professional “ akasema Anitha

“ Yah ! Wanaonekana wazoefu sana .Ninachojiuliza ni kwa nini wametega kamera mlangoni kwa Penny?

“ Jibu ni jepesi Mathew,Wanataka kuangalia kila kinachoendelea nyumbani kwa Penny.Cha kujiuliza ni kwa nini wanataka kutazama kila kinachoendelea nyumbani kwa Penny?Kwa nini Peniela anachunguzwa? Au watu hawa yawezekana wakawa ni walinzi binafsi wa Peniela? Akauliza Anitha

“ Sina hakika kama watu wale ni walinzi wa Peniela kutokana na namna walivyoingia.Wanaonekana wazi kufahamu kwamba muda ule Peniela hakuwepo nyumbami ndiyo maana waliingia kwa kunyata na kuweka ile kamera nadhani kwa lengo la kutaka kufahamu mienendo ya Penny.Tunachotakiwa kufahamu watu hawa ni akina nani na nini lengo lao la kumchunguza Penny.Tayari tuna sehemu nzuri sana ya kuanzia uchunguzi wetu.Sehemu nyingine ya kufanyia uchunguzi ni katika laini ya simu ya Edson. Wauaji waliondoka na simu na pamoja na kompyuta zake zote.Inaonekana wazi kwamba kuna kitu kilichokuwa kinafichwa na ndiyo maana wauaji wale hawakuwa na shida na pesa na wakaondoka na vitu hivyo tu.Wakati wa kuhamisha vifaa vyake,ilipatikana laini ya simu ikiwa imefichwa katika chungu cha maua.Sielewi ni kwa nini aliificha laini hii ya simu lakini nina imani hakutaka ionekane kwa sababu maalum.Inaweza ikawa na msaada kwetu.Tunatakiwa tuichunguze laini hii pia” akasema Mathew.Anitha hakujibu kitu aliendelea na kazi yake ya kuunganisha mitambo yake. Nusu saa baadae alimaliza kuunganisha mitambo yake akaiwasha na kujaribu

“ Everything is in position.We can start our job now” akasema Anitha

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...