PENIELA (Season 1 Ep 8)
SEHEMU ILIPOISHIA........
“ Penny nitakuwa na safari ya kwenda Arusha wiki ijayo kwa hiyo jiandae nawe utakwenda Arusha.Kareem atashughulikia kila kitu kuhusu safari hiyo.Kwa heri Penny” akasema Dr Joshua na kukata simu.Penny alihisi jasho likimchuruzika .
“ I’m back to a living hell.!..Nayachukia sana maisha haya lakini sina namna tena tayari nimenaswa.Endapo nitaenda kinyume na huyu mzee kuna uwezekano yakanifika makubwa .Nimeponea chupu chupu kesi ya mauaji na safari hii lazima niwe makini sana kwa kila ninachokifanya.” akawaza Penny huku kijasho kikimchuruzika na mara simu yake ikaita,akatazama mpigani na kubonyeza kitufe cha kupokelea
“ Hallow” akasema
“ Penny don’t say No to Mr president.Fanya kila atakachokuamuru ufanye.We’re so close” ikasema sauti ile na kukata simu.Penny akahisi kuchanganyikiwa.
ENDELEA………………………
Penny alikaa kitandani akazama katika tafakari nzito.Simu mbili toka kwa watu wawili tofauti alioongea nao muda mfupi uliopita zilimchanganya sana.
“Sijui nini itakuwa hatima ya maisha yangu.Sijui nitaendelea na maisha haya hadi lini? Nimechoka sasa na maisha haya na ninahitaji kuwa huru na mimi niishi maisha ya kawaida.Nimepewa amri ya kuendeleza mahusiano na Dr Joshua japokuwa moyo wangu hautaki kabisa.Kamuua Edson kijana ambaye nilimpenda kwa moyo wangu wote.
I was deeply in love with him.Kama haitoshi nikaangushiwa kesi ile kubwa ya mauaji ambayo nusura inipeleke maisha gerezani.Yote hii ni kwa sababu ya wivu wa Dr Joshua.He’s a powerfull man and he can do anything.Sikuwa nataka kuwa na mahusiano naye ya namna yoyote ile baada ya kuachiwa huru lakini najikuta nikilazimishwa kukubali kuendeleza mahusiano naye ili kuikamilisha kazi .
I hate that bastard.” Akawaza Penny huku akijifuta jasho
“ Lakini kwa sasa ngoja niwe mpole na niendelee kumkubalia kwa kila anachotaka lakini iko siku moja atalia na kuomboleza. Kitendo alichokifanya cha kumuua Edson kimeniumiza mno na iko siku atalipia uovu huu.Ninachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kuhakikisha kwamba Jason na Jaji Elibariki wanaachana na kutafuta muuaji wa Edson.
Wanajiweka katika hatari kubwa sana bila wao wenyewe kujua.Hawa ni watu wangu wa muhimu sana na sintokubali kuona kwa namna yoyote ile mmoja wao yakimpata kama yaliyompata Edson.” Akawaza Penny na kuinuka akaelekea bafuni kuoga kwani jasho jingi lilikuwa linamtiririka
“ kuna nyakati huwa siamini kama ni kweli nimeweza kufanikiwa kumchanganya mkuu wa nchi,mtu anayeheshimika ndani na nje ya nchi, kwa kumpa penzi la kiwango cha juu .Mzee Yule amechanganyikiwa kiasi cha kumuombea mke wake anayesumbuliwa na saratani afariki mapema ili aweze kuwa na uhuru na mimi anioe na anifanye first lady.Hahaha laiti angejua angeyafuta kabisa mawazo yake.Ngoja nivumilie na kujifanya mjinga na kumsikiliza kila atakachokisema kwa sababu kimebaki kipindi kifupi sana kukamilisha kazi yangu” akawaza Penny akiendelea kuoga.
********
Saa mbili za asubuhi Jaji Elibariki aliondoka nyumbani kwake na kuelekea ofisini .Si kawaida yake kuondoka mapema hivi lakini kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri na mke wake Flaviana ilimlazimu kuwahi kuondoka.
“ Siku ya pili sasa mimi na Flaviana hatuongei.Nimechoshwa na maisha haya ya mikwaruzano kila siku.Flaviana ni mwanamke ambaye anataka kuwa na sauti ndani ya nyumba na maamuzi yake yawe ndiyo ya mwisho.Yote hii ni kwa sababu yeye ni mtoto wa rais.
Siko tayari kuendelea kuvumilia dharau zake.Siko tayari kuendelea kuishi maisha yasiyokuwa na furaha hata kidogo eti kwa sababu ya kiapo cha ndoa. “Akawaza jaji Elibariki na mara sura ya Penny ikamjia
“ Sura ya Penny toka niliponana naye jana hainitoki kichwani.Ninamuwaza kila dakika.Yawezekana ni kutokana na uzuri wake.Ni mtoto mzuri mno.Ameumbwa akaumbika.
Ana uzuri wa kipekee mno ambao sijui nimfananishe na nani.Jana nilipomuona namna alivyokuwa amependeza niliogopa na kudhani labda ni malaika.Hakuwa Penny Yule ambaye nilizoea kumuona mahakamani ” akawaza Jaji Elibariki wakati akikata kona kuingia Lavenda Restaurant kupata kifungua kinywa kwani aliondoka nyumbani bila kupata mlo wa asubuhi.
“ Katika maongezi yangu na penny jana usiku sijaweza kugundua chochote cha kuweza kunipa mwanga kuhusu wapi nitaanzia uchunguzi wangu.Nilivyomsoma penny ni kama vile hataki tena kujihusisha na masuala yoyote yanayohusiana na kifo cha Edson.Nadhani anajitahidi kujisahaulisha yaliyopita lakini pamoja na hayo kuna kitu nimekiona katika macho yake ambacho kinanifanya niamni kwamba kuna kitu anakifahamu lakini hayuko wazi kukisema. Siwezi kumlazimisha kusema kila kitu anachokifahamu .Kama kuna kitu hataki kuniambia basi nitakifahamu kwa njia nyingine.Ninaapa nitalichimba suala hili hadi mzizi wa mwisho.Nataka nimdhihirishie rais na familia yake kwamba ninapofanya maamuzi huwa sikurupuki tu.
Lazima nimpate muuaji ” akawaza jaji Elibariki halafu akampigia simu Jason na kumfahamisha kwamba wakutane mahala walikokutana jana asubuhi
Kisha maliza kupata kifungua kinywa,akaondoka na kuelekea moja kwa moja katika sehemu waliyopanga wakutane na Jason.
Dakika kumi na mbili toka awasili mahala walikopanga kukutana,Jason akawasili.Wakasalimiana na bila kupoteza wakati wakaanza kujadili kile kilichowakutanisha pale
“ Vipi kuhusu jana,mambo yalikwendaje? Akauliza Jason.
“ Jana mambo yalikwenda vizuri ingawa si vizuri sana lakini si mbaya kwa kuanzia.Niliongea mambo mengi na Peniela na alikubali kushiriiana nasi ili kumbaini nani muuaji wa Edson.Alinieleza kwa ufupi tu namna mahusiano yake na Edson yalivyokuwa na hadi siku mauaji yalipotokea.Hakuna kitu kipya katika maelezo yake.Maneno aliyoniambia jana ndiyo yale yale ambayo aliyasema mahakamani.Lakini hata hivyo kuna kitu nilikigundua baada ya kuongea naye.Kuna kitu anakifahamu lakini hayuko tayari kukisema.Hiyo nayo inazidi kunipa mshawasha wa kutaka kufahamu kwa undani zaidi kuhusiana na jambo hili.” Akasema Jaji Elibariki.Jason akafikiri kidogo na kusema
“ Penny ni rafiki yangu na nimekuwa nikiisimamia kesi yake kwa muda wa mwaka mzima na ninakubaliana nawe kwamba Penny ni msiri sana.Ana ambo mengi ambayo hajawahi kuyaweka wazi na huwa hataki kabisa kuyaongelea.Kwanza ni kuhusiana na familia yake.Kwa muda wa mwaka mzima sijawahi kuiona familia yake au ndugu yake yeyote Yule .Najiuliza mara kwa mara ndugu zake wako wapi? Sijapata nafasi ya kumuuliza kuhusu suala hilo na wala hajawahi kunieleza chochote.Nakubaliana nawe kabisa kwamba kuna mambo ambayo penny anayafahamu lakini hayuko tayari kuyaweka wazi.”
“ Kama ni hivyo basi” akasema jaji Elibariki
“ itatubidi tufanye mambo mawili.Kwanza inatubidi tumfahamu huyu Edson alikuwa mtu wa namna gani.Tuyafahamu maisha yake alikuwa akiishi vipi,marafiki aliokuwa akiambatana nao,tutachunguza pia nyumbani kwake na mwisho tutafuatilia mawasiliano yake na watu mbali mbali ambao alikuwa akiwasiliana nao na hasa wale aliowasiliana nao siku tatu kabla ya kifo chake vile vile tutaipitia tena taarifa ya uchunguzi toka jeshi la polisi .Tunatakiwa tufahamu kila kitu kuhusiana na Edson.” Akasema Jaji Elibariki akanyamaza kidogo halafu akaendelea.
“ Jambo la pili ambalo tunatakiwa tulifanye ni kumchunguza Penny” akanyamaza na kumtazama Jason
“ Lazima tumfahamu Penny lakini ni baada ya kumfahamu Edson” akasema Jaji Elibariki.
Waliendelea na majadiliano na baadae wakaondoka kila mmoja akaelekea ofisini kwake .
Baada ya kuachana na Jaji Elibariki,Jason aliamua kuelekea nyumbani kwa Peniela.Hakuwa ameongea naye toka asubuhi hivyo akaamua kwenda kuonana naye kabla hajaendelea na mambo mengine .
“ Ninakubaliana na Jaji Elibariki kwamba Penny ni mwanamke msiri sana.Ninaamini hakumuua Edson lakini nina imani kuna mambo ambayo anayafahamu kuhusiana na kifo cha Edson lakini hayuko tayari kuyaweka wazi.Anyway tutachunguza na tutapata jibu” akawaza Jason akiwa njiani kuelekea kwa Penny
Ilimchukua dakika thelathini kuwasili katika makazi ya Penny.Katika geti la kuingilia ndani kulikuwa na makufuli makubwa manne kuashiria kwamba hakukuwa na mtu ndani.Jason akatoa simu yake na kumpigia lakini hata simu yake haikuwa ikipatikana.Jason akaingiwa na wasi wasi mkubwa.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO
No comments
Post a Comment