FANYA KILA JAMBO KWA WAKATI
Hello ndugu msomaji wetu.
Watu wengi wanafanya kazi au biashara zao wakiwa “interested” na hawako “committed”,hii ni sababu mojawapo ya kupata matokeo ya wastani katika mambo mengi sana.
Kuna tofauti kubwa sana unapofanya kitu kwa sababu UNAJISIKIA kufanya na kufanya kitu kwa sababu UMEJIWEKEA dhamira ya dhati kufanya.Watu wengi kila mwaka wanakuwa na malengo ila kwa mujibu wa chuo kikuu cha Scranton ni 8% ya malengo ya watu ya kila mwaka ndio huwa inafanikiwa,sababu kubwa ikiwa ni wengi hawana “Commitment “.
Mtu mwenye “Commitment” huwa hasubiri kujisikia vizuri ili afanye alichoamua,anafanya katika hali yoyote ile.Mtu wa namna hii huwa hatoi visingizio vilivyozoeleka-“Sina sapoti”,”sina mtaji”,”wananichukia”,”sina connection”,”sina muda” n.k
“Commitment “ maana yake ni kutoruhusu changamoto yoyote izuie kile unachotaka kukipata katika maisha.Mfano:Simba akitokea ghafla hapo ulipo,utakuwa na “Commitment” ya kuokoa maisha yako:Hautaanza kutoa visingizio vya kuwa wewe ni mnene huwezi kukimbia ama hukujiandaa-Utashangaa unampita kila mtu na unakimbia kwa kasi ambayo hukuwahi kujua kama unayo.Hiyo ndiyo “commitment”
Usisubiri uwe kwenye “mood” ili kufanya,fanya kwa sababu umeamua.Jitofautishe kwenye maisha yako leo.Je,wewe uko “committed” katika unachokifanya?
See You At The Top
@joelnanauka_
#TIMIZAMALENGOYAKO
No comments
Post a Comment