SABABU ZINAZOPELEKEA WATU WENGI (HASA VIJANA) KUKATA TAMAA -1

Habari za wakati huu ndugu yangu, natumaini ni mzima wa afya njema. Ni imani yangu mafundisho haya yatakutoa mahali na kukupeleka mahali palipo bora zaidi.
Kumetokea wimbi kubwa sana la watu (hasa vijana) unapoongea nao unapata picha ya kuwa wamekata tamaa. Iwe ni kwenye biashara, kazi, mahusiano, miradi n.k. Hii siyo sio ishara nzuri pale ambapo tunategemea vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa wao kupoteza mwelekeo na kukosa tumaini.
Hivyo kwa pamoja naomba tutazame taratibu sababu zinazofanya watu wakate tamaa kisha tutatazama nini tufanye kutatua changamoto hii inayotukabili.


1. KUSHINDWA KUFIKIA MALENGO.
Vijana wengi wamekata tamaa baada ya kupata matokeo (uhalisia) ambao ni tofauti sana na matarajio aliyokuwa amejiwekea awali.
Kabla ya kuanza biashara matarajio ya kijana huyu yalikuwa ni kupata faida nzuri lakini matokeo yake amepata hasara na inawezekana na kapoteza na mtaji wenyewe. Hapa ndio huja kauli/maamuzi ya SITAKI KABISA KUSIKIA MAMBO YA BIASHARA.
Kabla ya mradi wa kilimo alishapiga faida atakayoipata baada ya kuvuna matokeo yake mvua haikunyesha, au ilinyesha iliyopitiliza, au wafugaji waliingiza ng'ombe shambani na kula mazao mwishoni matarajio yake yalikuwa tofauti sana na uhalisia. Hapa huja kauli/ maamuzi SITAKI KABISA KUSIKIA MAMBO YA KILIMO.
Ulitarajia siku unamaliza chuo basi unachukua cv yako na matokeo yako unapeleka kwenye ofisi na kuajiriwa ila mpaka sasa ni miaka kadhaa imepita hata interview hujawahi kuitwa umekata tamaa hata kutuma maombi tena.
Hali ndio ipo hvyo hvyo kila eneo, hata kwenye mahusiano ulitarajia awe hvyi uhalisia wake ni tofauti kabisa na vile ulivyotegemea. Hatimaye unajikatia tamaa hata ya kuwa na mahusiano imara/kuoa/kuolewa.
Maumivu pia huongezeka pale unapokutana na maneno kutoka kwa watu walio kuzunguka na tena hata wakiwa ni watu wa familia, ndugu, marafiki au majirani.
"Tulijua haufiki mbali, kiko wapi sasa?"
"Wewe ulikurupuka"
"Una kula na kujaza choo tu hapa hufanyi lolote"
Maumivu haya huleta msongo wa mawazo na unaweza pelekea mtu kuchukua maamuzi fulani. Asipopata mtu wa kuzungumza naye na kumtia moyo mara nyingi watu walio wengi huchukua maamuzi mabaya kwa sababu mbele haoni mwanga bali kiza, hakuna wa kumshika mkono wote wanamkandamiza shimoni.

Nini unapaswa ufanye unapopitia katika hali kama hii?
Itaendelea........
Arnold Dominic
0717 580 790
Fb: Arnold Dominic
Insta: don_arnold2
Email: adominic63@gmail.com

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...