PENIELA (Season 1 Ep 13)
MTUNZI : PATRICK .CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Dah ! pole sana kaka.Kama unamuongelea huyo kijana aliyekuwa akifanya kazi ikulu ni kweli alikuwa akiishi hapa lakini inasemekena aliuawa na ndiyo maana wazazi wake wakaamua kuiuza nyumba hii”
Mathew akaonyesha mstuko mkubwa.
“ Dah sikuwa na taarifa hizo.Ahsante sana kwa taarifa hizo ndugu yangu.Nitakwenda kuwapa pole wazazi wake” akasema Mathew na kurejea garini.
“ Wazazi wa Edson wamekwisha iuza nyumba hii .Kwa maan hiyo vitu vyote vya Edson viliondolewa hapa na nina hakika vilipelekwa nyumbani kwa wazazi wake.Nahitaji kukagua vitu vyake.Nahitaji kuikagua simu aliyokuwa akiitumia na kompyuta yake kama bado vipo“ akasema Mathew
“ Kama ni hivyo itatulazimu kwenda nyumbani kwa wazazi wake na kuonana nao na kuwaomba kupitia vitu hivyo” akasema Jason
“ Hiyo ndiyo hatua inayofuata.Unafahamu mahala wanakoishi wazazi wake?” Akasema Mathew.
“ Ndiyo ninapafahamu.Baba yake ni mtu maarufu sana hapa mjini..” akasema Jason..
“ Ok.Tunaweza kupata japo sehemu ya kuanzia.” Akasema Mathew.
ENDELEA………………………………………………….
Jason na Mathew wakawasili katika makazi ya wazazi wa Edson.Lilikuwa ni jumba kubwa la kifahari lililozungukwa na ukuta mkubwa.
“ Wow ! inaonekana wazazi wake ni watu wenye kujiweza sana kiuchumi” akasema Mathew
“ Ndiyo.Wanamiliki biashara kadhaa kubwa kubwa hapa mjini.Ni watu wenye kujiweza sana” akasema Jason huku wakishuka na kuelekea katika geti.Mathew akabonyeza kengele ya getini na mlinzi aliyekuwa amevaa sare za kampuni binafsi ya ulinzi akafungua mlango mdogo wa geti
“ Habari zenu jamani” akawasabahi
“ Habari zetu nzuri.Habari za hapa?
“ Za hapa nzuri.Niwasaidie nini? Akauliza Yule mlinzi
“ Tuna hitaji kuonana na mzee Robinson Kobe”
“ Mzee si rahisi kumpata mida hii.Yuko katika shughuli zake.”
“ Vipi kuhusu mama? Yeye tunaweza kumpata? Akauliza Mathew
“ Hata mama naye ametoka “
“ Unaweza kutuelekeza mahala tunakoweza kumpata mama au mzee?
“ naweza kuwaelekeza ofisi ya mama ilipo lakini mzee ni mtu mwenye mizunguko mingi sana na kumpata si rahisi hata kidogo” akasema mlinzi na kuwaelekeza katika ofisi ya Bi Hellen Kobe mama wa Edson.Bila kupoteza muda Mathew na Jason wakaingia garini na kuelekea Kobe Shopping mall ambao ndiko iliko ofisi ya Bi Hellen.
Waliwasili Kobe’s shopping mall wakaegesha gari na kushuka wakaingia ndani ya jengo.Watu walikuwa wengi sana wakifanya manunuzi ndani ya jengo hili lililokuwa na biashara nyingi ndani yake
Kwa kutumia Lifti wakapanda hadi ghorofa ya tano iliko ofisi ya Bi Hellen Kobe mama wa Edson
“ Sina hakika kama Bi Hellen atakubali kuongea nasi endapo ataniona” akasema Jason
“ Kwa nini? Akauliza Mathew
“ Ananifahamu .Tumekuwa tukionana mahakamani wakati wa kesi na ananifahamu mimi ndiye wakili niliyemtetea mtuhumiwa wanayeamini kwamba ndiye alimuua mtoto wao.Lazima atakuwa na hasira nami” akasema Jason
“ Usijali Jason.Ataongea tu” akasema Mathew kwa kujiamini
Kabla ya kuingia katika ofisi ya Bi Hellen Kobe iliwalazimu waonane kwanza na katibu muhtasi wake ambaye aliwasiliana naye na kuwaruhusu waingie wakaonane naye.Wakati wakiingia ndani ya ofisi Bi Hellen,alikuwa anaongea na simu na mara tu alipokutanisha macho na Jason,mkono wa simu ukamponyoka na kuanguka mezani.Alistuka sana.
“ Ouh my gosh ! This is unbelievable !!..akasema Bi Hellen
“ You again….!!..Umeamua kunifuata hadi huku..!! akafoka Bi Hellen
Jason na Mathew hawakusema kitu wakaingia mle ofisini na kusimama mbele ya meza.
“ Shikamoo mama” akasema Mathew.Bi Hellen hakujibu kitu akainua mkono wa simu na kumpigia katibu muhtasi wake
“ Irene naomba tafadhali watoe watu hawa ofisini kwangu haraka sana.” Akasema kwa ukali Bi Hellen.Mathew akamnong’oneza kitu Jason ,akatoka mle ofisini.Bado Bi Hellen aliendelea kumuangalia Mathew kwa jicho kali hata baada ya Jason kutoka.Katibu muhtasi wa Bi Hellen akaingia mle ndani kwa ajili ya kumtoa Mathew ,huku akitabasamu Mathew akamwambia
“ Its ok Irene.Nina maongezi kidogo na mama ya muhimu sana.Naomba dakika tatu halafu nitatoka.We’re not here for trouble” Irene akamtazama Bi Hellen ambaye alimtazama Mathew usoni kwa sekunde kadhaa halafu akamfanyia ishara aketi kitini.
“ mama naomba nikusalimu tena shikamoo” akasema Mathew baada ya kuketi
“ Marahaba kijana.Una shida gani manake Yule mwenzako tayari amekwisha niharibia siku yangu.Simpendi na sitaki hata kumtia machoni”
“ Mama utanisamehe kwa kuongozana naye lakini ilinilazimu kufanya hivyo kwa sababu jambo lililonileta hapa hata yeye linamhusu vile vile” akasema Mathew
“ Ni jambo gani hilo lililowaleta? Akauliza Bi Hellen
“ Ni kuhusiana na mwanao Edson”
Bi Hellen akastuka kidogo
“ Edson?!
“ Ndiyo mama”
“ Unataka kunieleza nini kuhusu Edson?
“ Mama ,mimi naitwa Mathew ni mtu ninayefanya kazi za kiuchunguzi na kwa sasa ninafanya uchunguzi kuhusiana na kifo cha mwanao Edson” akasema Mathew
Bi Hellen akavuta pumzi ndefu ,akaweka kalamu yake mezani na kusema
“ Sikuelewi una maanisha nini unaposema unafanya uchunguzi wa kifo cha mwanangu.Tayari uchunguzi ulikwisha fanyika na muuaji akapatikana,akapandishwa kizimbani lakini kwa sababu wanazozijua wao mahakama ikamuachia huru,sasa unanishangaza unaposema kwamba unafanya uchunguzi wa kifo cha Edson” akasema Bi Hellen
“ Mama ,ninatamani sana tuongee jambo hili kwa upana wake lakini hapa si mahala pake.Naomba kama utakuwa tayari tuonane jioni ya leo nyumbani kwako ukiwa wewe na mzee na tutaongea kwa kina kuhusiana na jambo hili” akasema Mathew
“Mathew naona unanipotezea muda wangu wa kufanya kazi.Hakuna haja ya kufanya uchunguzi tena wakati kila kitu kiko wazi na muuaji alikwisha patikana lakini akaachiwa huru.Sisi tumekwisha muachia Mungu”
Mathew akamtazama Bi Hellen kwa makini na kusema
“ Mama ,mtu mnayeamini kwamba ndiye aliyemuua mwanenu siye.Peniela hakumuua Edson” akasema Mathew huku akiinuka.
“ Saa moja jioni ya leo nitakuja kuzungumza nanyi.Hakikisha mzee naye yupo ili tuzungumze sote kwa pamoja” akasema Mathew na kuondoka.Moja kwa moja akaelekea mahala walikoegesha gari ambako alimkuta Jason akimsubiri garini
“ Nilifahamu toka mwanzo Yule mama asingekubali kuongea nasi pindi akiniona.She hates me” akasema Jason
“ Usijali Jason.Jukumu letu ni kuwahakikishia kwa vitendo kwamba Penny hakumuua kijana wao.Si rahisi kukuamini kwa sasa lakini itafika wakati ambao wataamini tu. Jason nipeleke nyumbani kwa Penny” akasema Mathew.
“ Nyumbani kwa penny? Jason akashangaa kidogo
“ Yah ! nataka kwenda nyumbani kwa Penny”
“ Penny hayupo nyumbani kwake na hakuna anayeelewa yuko wapi”
“ Usijali Jason.Take me there” akasema Mathew huku akiendelea kuipekua kompyuta yake ndogo.
Baada ya Mathew kutoka mle ofisini ,Bi Hellen alimuita katibu muhtasi wake na kumuomba ampatie dawa zake kwani tayari alianza kujisikia vibaya.Maneno aliyoambiwa na Mathew yalimchanganya sana.
“ Yule kijana ni nani? Akawaza
“ Nani kamtuma afanye uchunguzi huo wakati uchunguzi wa awali ulikwisha fanyika na muuaji akapatikana? Kwa nini aliongozana na Yule wakili aliyemtetea muuaji wa mwanangu? Akawazza Bi Hellen akiwa amekiegemeza kichwa chake kitini.Hakujisikia tena kutaka kufanya kazi yoyote
“ No! hakuna mtu mwingine aliyemuua mwanangu zaidi ya Yule kahaba Peniela.Yeye ndiye aliyekutwa eneo la tukio na kuna kila ushahidi unaoonyesha kwamba ndiye aliyermuua Edson.Simuelewi huyu kijana anaposema kwamba anataka kufanya uachunguzi wakati uchunguzi ulikwisha fanyika na Mahakama ikamuachia mtuhumiwa” akaendelea kuwaza Bi Hellen na kuhisi mwili wake kuanza kutokwa na jasho jingi,akamuita dereva wake na kumuomba amrejeshe nyumbani
“ Yule kijana Mathew amenichanganya sana.Nashindwa nimuamini ama vipi.Amekitonesha kidonda changu kinachojaribu kupona” akawaza Bi Hellen akiwa garini kurejea nyumbani
*********
Jason na Mathew waliwasili nyumbani kwa Peniela.
“ Nisubiri humu humu garini” akasema Mathew huku akivaa glovu na kushuka akaenda getini,akatoa kidude Fulani toka katika koti lake na kulifungua kufuli lililofungiwa mlango mdogo wa geti akaufungua na kuingia ndani.
“ Huyu Mathew anaenda kufanya nini nyumbani kwa Penny wakati mwenyewe hayupo? Itakuaje iwapo Penny atagundua kwamba tumeingia ndani mwake wakati hayupo? Nina hakika akigundua hilo hataniamini tena na kuna hatari hata ukaribu mimi na yeye utapungua. I cant let that happen kwa sababu nina mipango mikubwa kuhusu Penny. Sijapendezwa na namna anavyoifanya kazi yake huyu jamaa” akawaza Jason akiwa garini
Ukuta ulioizunguka nyumba ya Peniela uliwekwa vipande vidogo vidogo vya chupa kwa juu.Mathew akapanda juu ya pipa tupu na kuweka kidude Fulani kati kati ya chupa zile akashuka na kuelekea katika majani mazuri yaliyooteshwa mbele ya nyumba ile ,akaufungua mkoba wake na kutoa kitu fulani mfano wa kipepeo akakibonyeza na kukirusha katikati ya majani yale.Yeyote ambaye angekiona angejua moja kwa moja yule ni kipepeo halisi. Kisha maliza kuviweka vitu vile akatoka akafunga geti na kurejea garini.
“ We can go now” akasema Mathew.Jason akavuta pumzi ndefu na kuliondoa gari maeneo yale.
*********
Katika jengo moja pembeni kidogo ya jiji la Dare s salaam,watu nane wameizunguka meza kubwa ya duara.Ni saa ya pili sasa wako katika kikao kizito.Mtu mmoja mwembamba mrefu ambaye uso wake ulikuwa umekunjana kwa hasira alikuwa akiongea kwa sauti kubwa
“Narudia kusema kwamba sitauvumilia tena uzembe kama huu mlioufanya.Haiwezekani siku ya pili leo msijue mahala aliko Penny.Amekwenda wapi? Mmempoteza vipi katika mitambo yenu wakati mlipaswa kumfuatilia saa ishirini na nne ? Naomba nirudie tena kuwaweka wazi kwamba Peniela ndiye dira yetu. Bila yeye hakuna kitu kinachoweza kufanyika.Operesheni 26B haiwezi kufanikiwa bila yeye.Kwa mwaka mzima ambao alikuwa gerezani akituhumiwa kila kitu kilisimama,na kwa sasa wakati amerejea na kila kitu kimeanza kwenda upya mnafanya tena uzembe.Ninaapa kwa mbingu na nchi kwamba sintouvuilia uzembe wa aina yoyote ile kuanzia sasa.Peniela anatakiwa afuatiliwe kwa saa ishirini na nne. Hamtakiwi kumuacha hata dakika moja.Nawaweka wazi kwamba endapo operesheni 26B itashindwa kufanikiwa kwa sababu ya uzembe tu wa watu basi tujihesabu sisi sote ni marehemu.I want to live,I don’t want to die so I cant lost my soul because of one stupid.If you mess again you’ll die first” akasema kwa ukali Yule jamaa.Watu wote walikuwa kimya wakimsikiliza na walionekana kuingiwa na woga mwingi.Kijana mmoja aliyevalia suti nyeusi na shati jekundu akakohoa kidogo na kusema
“Captain,tulijitahidi kumfuatilia Penny kwa karibu lakini kifaa ambacho huwa anatumia kwa ajili ya mawasiliano nasi kilizimwa usiku wa manane.Tulipokwenda asubuhi nyumbani kwake kufanya uchunguzi tulikutana na makufuli,Penny hakuwepo.Toka amemaliza kesi iliyokuwa ikimkabili Penny anaonekana hataki tena kushirikiana nasi.Hatoi ushirikiano wa aina yoyote.Sina hakika kama yuko tayari kuendelea na operesheni hii” akasema Yule kijana na kumfanya Captain agonge meza kwa hasira
“ Kwa nini mlienda asubuhi?? Ilitakiwa muda ule ule ambao mmeona tukio lile la kukatika kwa mawasiliano mngenitaarifu mara moja ili nijue nini cha kufanya.Uzembe wenu unatugharimu sisi sote.Narudia tena kwamba hili ni onyo la mwisho.Kuhusu Penny kutotoa ushirikiano hilo niachieni mimi.Atake asitake lazima afanye tunavyotaka sisi na si vinginevyo.” Akanyamaza kidogo halafu akaendelea.
“ Leo usiku nina kikao na wakuu cha kujadili kuhusu operesheni 26B ambayo inatakiwa kuzinduliwa rasmi upya.Kabla sijaelekea kikaoni usiku wa leo nahitaji kupata taarifa kwamba tayari mmekwisha fahamu mahala alipo Penny.Kuanzia sasa nendeni tena katika vifaa vyenu,fungueni kompyuta zenu,nendeni katika satellite na mjue wapi aliko Penny.Mna kila kitu kinachotakiwa kwa hiyo ifanyeni kazi na kabla ya saa mbili usiku wa leo nataka ripoti.” Akasema kwa ukali Captain na kutoka mle katika chumba cha mikutano akaingia ofisini kwake akajifungia.Alihisi kichwa kizito kwa mawazo.
TUKUTANE TENA SEHEMU IJAYO……
No comments
Post a Comment