PENIELA (Season 1 Ep 10)
SEHEMU ILIYOPITA
“ Hallo Mathew” akasema Jaji Elibariki
“ hallo jaji.habari za siku? Leo umenikumbuka ndugu yangu lazima utakuwa na tatizo.”
“ Ni kweli nina shida ndugu yangu nahitaji kukuona” akasema Elibariki
“ Unataka tuonane saa ngapi?
“ sasa hivi.Uko wapi?
“ Niko nyumbani kwangu”
“ Ok njoo utanikuta lakini tafadhali naomba uje peke yako.Sitaki uwe umeambatana na mlinzi yeyote”
‘ Nitakuja mimi mwenyewe.dereva wangu ana matatizo ya kifamilia na nimempa likizo ya muda” akasema Elibariki
“ Good” akajibu Mathew na kukata simu.jaji Elibariki akainuka akavaa koti lake na kutoka
“ It’s time for action now” akasema jaji Elibariki huku akiingia garini.
“Mbivu na mbichi lazimazijulikane katika kipindi kifupi” akasema kwa sauti ndogo
ENDELEA…………………………………..
Jaji Elibariki waliwasili katika jumba moja kubwa lililozungushiwa ukuta mkubwa.Alipiga honi mara tatu na toka katika mlango mdogo wa geti akatokeza mlinzi akiwa na mbwa mkubwa akamfuata Elibariki katika gari
“ habari yako mkuu” Akasema Yule mlinzi aliyevalia sare za ulinzi za kampuni binafsi ya ulinzi
“ Habari nzuri.Nina miadi na ndugu Mathew” akasema jaji Elibariki
“ Wewe ndiye Elibariki? Akauliza Mlinzi
“Ndiye mimi”
“ Ok.taarifa zako ninazo” akasema Yule mlinzi huku akiingia ndani na kufungua geti.Jaji elibariki akaingia .
Mbwa watatu wakubwa wakalizingira gari lile na kuanza kubweka kwa nguvu.jaji Elibariki akaogopa kushuka ndani ya gari kwa namna mbwa wale walivyokuwa wakubwa.Mlinzi akafika mara moja na kuwatuliza akawapeleka katika nyumba yao.Elibariki akashuka na kuongozwa na mlinzi hadi ndani.Akakaribishwa sebuleni.Ilikuwa ni sebule kubwa yenye vitu vingi vya thamani.Baada ya dakika kama nne hivi Mathew akatokea.Ni mtu mmoja mfupi mwenye mwiliwa wastani.
“ Mheshimiwa jaji.habari za siku ndugu yangu?
“ habari nzuri Mathew.Maisha yanakwendaje?
“ maisha yanakwenda vizuri.Mungu ananiwezesha.Vipi wewe mambo yako yanakwendaje?
“ Mambo yangu yanakwenda vizuri lakinisi vizuri sana.”
‘Nini tatizo Elibariki? Mpaka uje kwangu lazima ni tatizo kubwa.Niambie nini tatizo? Niko tayari kukusaidia.Wewe ni rafiki yangu mkubwa.Hukuniacha wakati nina matatizo .” akasema Mathew huku akiwasha sigara yake na kuvuta
“ Mathew,kuna kijana mmoja anaitwa Edson alikuwa akifanya kazi katika idara ya mawasiliano ikulu,aliuawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake.Baada ya mauaji hayo mpenzi wake alituhumiwa kwamba ndiye muuaji na kufunguliwa mashtaka.
Kesi imeendeshwa kwa muda wa mwaka mzima na wiki hii nimetoa hukumu na kumuachia huru Yule msichana.Hakuwa na kosa lolote.Hakumuua Edson lakini nguvu kubwa ilitumika kushinikiza mahakama imkute na hatia na hatimaye afungwe maisha gerezani.Shinikizo kubwa lilitoka ndani ya familia ya rais kwani kijana huyo Edson aliwahi kuwa na mahusiano na binti wa rais kabla ya kuachana naye na kuingia katika mahusiano na Penny. Kwa hivi sasa hali si shwari ndani ya ndoa yangu.Mke wangu na ndugu zake wananichukia sana kwa maamuzi niliyoyafanya ya kumuachia huru Penny .Wao wanaamini kwamba penny ndiye aliyemuua Edson.Nimekuwa nikidharauliwa mno na watu hawa kutokana tu na kutenda haki. Baada y kutafakari sana nimeamua kufanya jambo moja la muhimu.
Kumtafuta mtu aliyemuua Edson ili kwanza kuudhihirishia umma wa watanzania kwamba sikukurupuka katika kufanya maamuzi yale na pili kumlinda Penny.Watu ambao walitaka akutwe na hatia na hatimaye apewe adhabu hawatamuacha hivi hivi.Lazima watamuandama na kuhakikisha wanamuondoa kwa namna nyingine.Mathew nimekuja kwako sina msaada mwingine,sina mtu mwingine ambaye anaweza akanisaidia katika jambo hili “ akasema jaji Elibariki.Mathew akainuka na kuelekea katika kabati kubwa akalifungua na kuchukua chupa kubwa ya mvinyo akamimina katika glasi mbili na moja akampatia Elibariki.Akagugumia pombe yote iliyoko katika glasi halafu akavuta mikupuo miwii ya sigara na kupuliza moshi mwingi hewani kisha akasema
“ This is a serious issue than I thought” akasema Mathew kwa sauti ndogo.
“ Si suala dogo hili Mathew na ndiyo maana nimekuja kwako ili unisaidia.Wewe umebobea katika masuala haya ya uchunguzi,umekwisha fanaya kazi katikaidara ya ujasusi ya taifa na una uzoefu mkubwa wa masuala kama haya.Naomba unisaidie kumbaini nani muuaji wa Edson na kwa nini alimuua.Tukifanikiwa katika hilo kila kitu kitakuwa shwari kabisa” akasema Elibariki.Mathew akainama akafikiri tena na kusema
“This girl ..Pe.. Jina lake nani ? Limenitoka kidogo” akasema Mathew
“ Anaitwa penny”
“ Good.This girl Penny who is she to you? Swali lile likamchanganya kidogo jaji Elibariki akafikiri na kusema
“ She’s just an Innocent girl.
Ni mtuhumiwa ambaye hakuwa na kosa na ndiyo maana nikamuachia huru”
“ Eli haujajibu swali langu.Ninafahamu alikuwa mtuhumiwa na hakuwa na kosa .Ninachotaka kufahamu ni mahusiano yako na msichana huyu.Ni ndugu yako,rafiki yako au mpenziwako.Usiogope kuwa muwazi kwangu.” Akasema Mathew
“ Hatukuwahi kufahamiana hapo kabla hadi nilipoanza kuisikiliza kesi yake.Hatukuwahi kuwa na urafiki lakini kwa sasa naweza kusema kwamba tumekuwa marafiki.”
“ Urafiki wa namna gani? Wa mtu na mpenzi wake au urafiki wa kawaida? Akauliza Mathew
“ Ni urafikiwa kawaida tu .” Mathew akavuta sigara na kupuliza moshi halafu akasema
“ Eli nakufahamu vyema,usingeweza kupoteza wakati wako kulishughulikia suala hili kama msichana huyu hana maana yoyote kwako.Please be honnest with me.
I want to help you” “ Ok Mathew,umetaka niwe muwazi na ninakuwa muwazi.Ni kweli msichana huyu ametokea kunivutia sana na tayari nimeanza kuwa na hisia za kimapenzi kwake na ndiyo maana ninajitahidi kufanya kila linalowezekana ili kumlinda”
“ Sawa Eli,ahsante kwa kuwa muwazi.Nitakusaidia.” akasema Mathew halafu akavuta mikupuo miwili ya sigara na kuizima akatoa nyingine katika pakiti akaiwasha.
“ Kwanza naomba ufahamu kwamba hili si suala rahisi kama unavyolichukulia. Ni suala zito na la hatari kubwa.Lakini nakuhakikishia kwamba tutamtafuta muuaji wa huyo kijana kokote alipo na nitahakikisha ninampata.Sikuwa nikitaka kufanya kazi yoyote ya hapa nchini lakini nitaifanya kazi hii kwa sababu yako” akasema Mathew huku akivuta sigara na kupuliza moshi mwingi hewani
“Mathew ninashukuru sana kukubali kunisaidia katika suala hili.Hata hivyo siko peke yangu katika suala hili.Nina mwenzangu aitwaye Jason ambaye ni wakili wa Penny.Ndiye aliyemsimamia Penny katika kesi hii.”
“ Sawa nimekuelewa Elibariki.Mimi niko tayari kufanya kazi hiyo kwa kutumia uwezo wangu wote.
Naomba unipe muda kidogo wa kutafakari namna nitakavyoweza kuifanya kazi hii.Naomba nionane nanyi kesho asubuhi ili niwape mchakato mzima namna nitakavyoifanya hii kazi. Akasema Mathew halafu wakaendelea na maongezi mawili matatu Jaji Elibariki akaondoka
*********
Saa moja na nusu za jioni,jiji ni Arusha bado mvua za manyunyu zinaendelea.Katika hoteli ya kifahari ya Kobe Village Peniela yuko chumban kwake amejilaza..Pembeni ya kitanda chake kulikuwa na meza ndogo iliyokuwa na chupa kubwa ya mvinyo akiendelea kunywa tarataibu huku akifurahia muziki katika runinga.Kengele ya mlangoni ikalia kuashiria kwamba kulikuwa na mtu.Akainuka na kwenda kufungua mlango akakutana na muhudumu aliyevaa suti nzuri nyeusi akiwa na kifurushi mkononi
“ madam kuna mzigo wako umeletwa”akasema Yule muhudumu huku akimpa Penny karatasi ya kusaini kwamba amepokea mzigo.Akasaini karatasi ile na kujifungia chumbani akakifungua kile kifurushi kilichofungwa vizuri.
“ Lazima mzigo huu utakuwa umetoka kwa Kareem” akawaza Penny wakati akikifungua.Ndani ya boksi lile kulikuwa na simu nzuri sana ya gharama kubwa
“ Wow ! what a nice phone” akasema Penny huku akitabasamu.Toka ndani ya lile boksi kulikuwa na kikaratasi kidogo kilichomuelekeza penny aiwashe simu ile.Akaiwasha na kuichunguza ndani,hakukuwa na namba yoyote ya simu iliyoandikwamo.Wakati akitafakari ikapigwa simu akaipokea.Aliitambua sauti ya mpigaji,alikuwa ni Kareem.
“ Hallo Penny” akasema kareem
“ Hi Kareem.”
“ Habari za Arusha?akauliza kareem
“ habari nzuri ila kuna baridi sana huku.?
“ Ok.Usizime hii simu.Mzee atazungumza nawe baada ya dakika chache.” Akasema Kareem na kukata simu.Baada ya dakika kama nne hivi simu ikaita tena kwa namba nyingine tofauti na zile za mwanzo,akabonyeza kitufe cha kupokelea
“ Hallo Penny” ikasema sauti ya upande wa pili ambayo Penny aliitambua ilikuwa ni ya mheshimiwa rais Dr Joshua.
“ Hallo Dr Joshua. Habari yako ? akasema Penny kwa sauti laini “ Habari yangu nzuri.habari za Arusha?
“ huku Arusha kwema kabisa .Habari za Dare s salaam?
“ Huku ni kawaida tu” akasema Dr Joshua
“ Penny mimi ninakuja huo kesho kutwa jioni kwa ajili ya mkutano wa marais wa afrika mashariki utakaofanyika kwa siku tatu kuanzia jumatatu ijayo.Katika siku hizo zote tatu nitakuwa nikionana nawe baada ya kumaliza shughuli zangu.
Nina mambo mengi sana ambayo nataka kuzungumza nawe na zadi ya yote ukumbuke ni mwaka mzima umepita sasa na sitapata ile raha ya aina yake toka kwako.Nataka unipe raha ,nifurahi “
“ Usijali Dr Joshua.Utapata kila unachokihitaji.Nimefurahishwa sana na namna unavyonijali na kunitunza.Nimeamini kwamba ni kweli umedhamiria kuufungua ukurasa mpya kati yetu.” Akasema Penny na kumfanya Dr Joshua acheke kidogo.
“ Ni furaha yangu kama umeridhika na huduma unayoipata Penny.Wewe ni malaika wangu tumia kitu chochote ukitakacho bila kujali gharama.Omba chochote ukitakacho nitakutimizia’ akasema Dr Joshua
“ Ahsante Dr Joshua.Mambo mengi tutaongea ukishakuja huku”
“ Ok Penny .Endelea kupumzika ,tutakuwa wote kesho kutwa.Nimefurahi kuongea na wewe” akasema Dr Joshua na kukata simu. Baada ya Dr Joshua kukata simu ikaingia tena simu nyingine toka kwa kareem
“ Halloo kareem” akasema Penny
“ Penny kuna jambo nimeona nikukumbushe.Simu hiyo ni maalum tu kwa ajili ya kuwasiliana na rais na mimi pekee.Usije ukathubutu kumpigia mtu mwingine yeyote.Isitoshe ukumbuke tulivyokubaliana hakuna kumpigia simu mtu yeyote Yule na kumweleza kwamba uko Arusha.Umenielewa penny?
“ Ndiyo kareem nimekuelewa” akasema Penny na kareem akakata simu
“ mambo yangu yote yanakwenda vizuri sana.Kila kitu kimekaa katika mstari na kinachofuatia sasa ni kuicheza karata yangu ya mwisho.Sitaki kufanya makosa safari hii.Hiki ndicho kipindi cha lala salama” akawaza Penny.
**********
Jaji Elibariki alirejea nyumbani kwake saa tatu za usiku na kumkuta mke wake Flaviana amekaa sebuleni akitazama filamu.Hakumsalimu akapita moja kwa moja hadi chumbani kwake akabadili nguo na kuingia bafuni akaoga halafu akajitupa kitandanina kuanza kusoma kitabu cha hadithi .Baada ya dakika kama ishirini hivi mke wake akaingia mle chumbani na kusimama pembeni ya kitanda.Alionekana wazi alikuwa na hasira
“ Eli ni tabia gani hiyo umeianza ya kuingia ndani bila hata salamu? Akauliza Flaviana.Jaji Elibariki akajifanya kama vile hajasikia akaendelea kujisomea kitabu chake cha hadithi
“Nakuuliza Eli ni tabia gani hiyo ya kuingia ndani bila hata ya kutoa salamu? Nini kinakupa kiburi siku hizi? Au ni hao wanawake unaowakingia kifua ndio wanaokupa kiburi siku hizi? akauliza kwa dharau Flaviana.Taratibu bila kuongea chochote Jaji Elibariki akainuka na kumfuata mkewe na kumzaba kibao kikali kinachomfanya apepesuke na kuangukia kitandani
“ Na iwe ni mwisho kunidharau nakunitolea maneno ya kashfa.Nimechoshoshwa na dharau zako .Nilikwisha kuonya kuhusiana na tabia hii ya dharau hukutaka kunisikia.”akasema kwa hasira Elibariki huku penny akiendelea kulia kwa nguvu.Ni mara ya kwanza toka wameoana Jaji Elibariki kumpiga kofi mke wake.
“ Ahsante Elibariki..ahsante sana..Wewe si mtu wa kunipiga mimi !...” akalia kwa uchungu Flaviana.
“ Toka nimezaliwa hata baba yangu hajawahi kunipiga kofi sembuse wewe ng’ombe ! ..Kauli ile ikampandisha hasira Elibariki na kuanza kumshushia mke wake kipigo kikali kilichomfanya apige ukelele mkubwa .Jaji Elibariki hakujali kelele zile akaendelea kumpa kipigo mkewe.Hadi anamuachia Flaviana alikuwa anavuja damu.
“ Siku nyingine usithubutu kabisa kunidharau paka wewe ..! akasema jaji Elibariki huku akitweta kwa hasira Huku akilia,Flaviana akaingia bafuni na kujifuta damu zilizotoka katika majeraha yaliyotokana na kipigo kikali
“ Eli umenipiga hadi kunitoa damu.Sasa nitakuonyesha mimi na wewe nani mwenye nguvu.I swear in heaven and earth lazima nikuonyeshe kazi na hautanisahau mpaka unaingia kaburini”akasema kwa hasira flaviana na kutoka kwa kasi akaingia katika gari lake na kuondoka kwa kasi
“ Nimechoshwa na dharau za familia hii.Yote hii ni kwa sababu baba yao ni rais .Hapana hawawezi kunitisha hata kidogo,hakuna aliye juu ya sheria.” Akasema jaji Elibariki kwa hasira.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO…
No comments
Post a Comment