PENIELA (Season 1 Ep 20)
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Anitha una hakika umesoma vizuri jina la mtu aliyemo ndani ya chumba hiki? Akauliza Mathew
“Chumba PV 2 – 78 amelazwa mgonjwa anayeitwa John Mwaulaya Albert.Kwani vipi Mathew.Unamfaha
mu mtu huyo?
Mathew akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Yah ! Ninamfahamu.Kama ni kweli aliyemo ndani ya chumba hiki ni John Mwaulaya basi mambo si rahisi kama tunavyofikiri” akasema Mathew kwa sauti ndogo huku akiwa makini akiangalia kila upande kuhakikisha usalama wake kwani alikwisha anza kuhisi hatari eneo lile
“ Mathew who is this guy John Mwaulaya ? Akauliza Anitha
“ Anitha tutaongea baadae.Eneo hili si salama hata kidogo.Please stay in the car and don’t get out” akasema Mathew
“ Mathew whats going on? Akauliza Anitha.Mathew hakujibu kitu .Kuna watu wawili walikuwa wakija kwa kasi.
ENDELEA………………………………..
Mathew alihisi wale jamaa wanamfuata ikamlazimu kuingia katika choo kilichokuwa chumba cha tatu kutoka kile chumba.Wale jamaa wawili waliouwa wakija kwa kasi wakaingia nao katika kile chumba alicholazwa John Mwaulaya.
“ Lazima nipate uhakika kama ni kweli mtu aliyelazwa mle ndani ni John Mwaulaya.Kama kweli ni yeye basi tutakuwa tumeingia katika hatari kubwa.” Akawaza Mathew akiwa amejificha chooni huku macho yake akiwa ameyaelekeza katika kile chumba cha John akitaka kufahamu kila kilichokuwa kikiendelea.
“ Mathew !.akaita Anitha
“ Hallow Anitha” akasema Mathew kwa kunong’ona
“ Say something.Whats going on over there? Akauliza Anitha
“ Anitha endelea kukaa ndani ya gari,bado ninaendelea kuwafuatilia hawa jamaa” akasema Mathew
“ Mathew mbona hutaki kunieleza nini kinachoendelea huko juu?
“ Anitha,nitakueleza lakini si sasa.” Akasema Mathew
Baada ya dakika kama thelathini hivi ,mlango wa kile chumba ukafunguliwa na jamaa wanne wakatoka wakiwa wameongozana na daktari mmoja wa kizungu
“ Anitha,wametoka watu wanne ndani ya kile chumba wameongozana na daktari mmoja wa kizungu.Nadhani wanashuka chini” Mathew akamtaarifu Anitha
“ Ok nitawaona katika kamera watakapofika chini” akasema Anitha
“ Tunamuhitaji Yule daktari wa kizungu.” Akaelekeza Mathew
“ Nimekusoma Mathew” akajibu Anitha
Mathew akatoka mle chooni alimokuwa amejibanza na kutembea kwa kasi akishuka chini kuwawahi wale jamaa.
“ Mathew tayari nimewaona wale jamaa katika kamera.Wako wanne na daktari mmoja wa kizungu.Wale jamaa wameagana na Yule dakatari ambaye kwa sasa anaongea na daktari mwenzake.Namuona Yule daktari ana kitambulisho katika koti lake .Ngoja nimvute karibu nifahamu jina lake” akasema Anitha
“ Ok Anitha.Achana na wale jamaa.Elekeza macho kwa daktari.Mimi niko ghorofa ya pili ninashuka ” akasema Mathew
Baada ya sekunde kadhaa Anitha akasema
“ I’ve got him !”
“ Anaitwa Michael Rodriguerz “
“ Good Job Anitha “ akajibu Mathew tayari akiwa ghorofa ya kwanza
Bado Dr Michael aliendelea kuongea na daktari mwenzake.Mathew akawapita halafu akaenda kusimama nje katika maua
“ Anitha niko hapa nje nikimsubiri atoke” akasema Mathew
“ Mathew , Dr James anatoka nje ya jengo anaelekea upande wa mashariki nadhani ndiko iliko ofisi yake” akasema Anitha
“ Ok Anitha nimekwisha muona,ninamfuatilia” akasema Mathew na kuanza kutembea taratibu akimfuata Dr Michael
“ Mathew nimetafuta kwa haraka haraka taarifa za Dr Michael ni kwamba ana umri wa miaka 53,ni mzaliwa wa Mexico,amesoma nchini Marekani ,Mexico na Urusi.Ni baba wa watoto watatu,Peter,Michael jr na Celine .Mke wake anaitwa Michelle Donalds mzaliwa wa Texas marekani.Dr Michael ni daktari bingwa wa mishipa ya fahamu” akasema Anitha
“ Thank you Anitha.Dr Michael sasa anaingia katika jengo lenye ofisi.Sintoweza tena kuingia mle ndani kwa sababu kuna kibao hapa kinachoonyesha kwamba huruhusiwi kuingia ndani kama si muhusika.Endele
a kumfuatilia kupitia kamera” akasema Mathew na kuanza kurudi mahala walikoegesha gari
“ John Mwaulaya !..” akawaza Mathew na mwili wote ukamsisimka
“ Bado siamini kama kweli ni yeye ndiye aliyelazwa ndani ya chumba kile hadi nitakapomtia machoni ndipo nitaamini” akawaza Mathew huku akitembea kwa kasi .Mara Anitha akaumuita
“ Mathew ,Dr Joshua ametoka,anaelekea katika eneo la kuegesha magari ya madaktari,anaingia katika gari lenye namba BV36P44.Umefika wapi ? akauliza Anitha
“ Tayari nimekwisha fika Anitha” akasema Mathew wakati akilikaribia gari lao.Alitembea kwa haraka akaufungua mlango na kuingia ndani
“ Ameelekea wapi? Akauliza Mathew huku akiwasha gari
“ Ameelekea geti la Mashariki”
“ Ok twende tuondoke tutamuwahi hapo bara bara kuu.” Akasema Mathew na kuwasha gari wakaondoka
Walisimama kwa dakika tatu kusubiri nafasi ya kuingia barabara kuu na mara Anitha akaliona gari la Dr Michael akamuonyesha Mathew
“ Ok.Nimemuona” akasema Mathew na kuingia barabarani akiacha magari matatu kati yao na Dr Michael
“ Hatupaswi kumpoteza.Tunamuhitaji sana” akasema Mathew
“ Mathew whats going on? Who is John mwaulaya? Nimejaribu kutafuta taarifa zake lakini hakuna mahala nimeweza kupata.Who is he? Akauliza Anitha
“ Tutaongea baadae Anitha lakini kwa sasa tuelekeze macho yetu kwa Dr Michael tusije tukampoteza.” akasema Mathew
“ Mathew tunaifanya kazi hii pamoja,na ili tufanikiwe tafadhali naomba uwe muwazi kwangu katika kila jambo ili tusaidiane mawazo nini cha kufanya” akasema Anitha
“ Usihofu Anitha.Kuna mambo mengi sana ambayo unahitaji kuyafahamu lakini kwa sasa tuyaweke pembeni na tuhakikishe hatumpotezi Michael” akasema Mathew.Anitha hakuuliza kitu tena wakaendelea na safari yao ya kumfuatilia Dr Michael.
Baada ya kutoka hospitali,Dr Michael alikwenda moja kwa moja Tanganyika Internationa school akaegesha gari na baada ya dakika kama tatu hivi ,mwanadada mmoja akatokea akiwa amemshika mkono mtoto mdogo .Dr Michael akamkumbatia Yule mtoto na kuwafungulia mlango wakaingia garini halafu wakaondoka.
“ Yule mtoto anaitwa Michael jr.Ni mtoto wa pili wa Dr Michael na Yule mwanadada aliyeongozana nao nadhani ni mtumishi wao” akasema Anitha
Waliendelea kumfuatilia Dr Michael bila ya yeye kufahamu kama anafuatiliwa.Toka pale shuleni Dr Michael hakupita sehemu nyingine ,alielekea moja kwa moja nyumbani kwake.Alipofika kwake alipiga honi akafunguliwa geti na kuingia ndani kisha geti likafungwa
“ Whats next ? akauliza Anitha
“ Najaribu kutafakari nini cha kufanya” akasema Mathew na mara mlango mdogo wa geti ukafunguliwa na Yule mwanadada aliyekuwa ameongozana na Dr Michael toka shuleni akatoka.
“ Yule dada anatoka.Amebeba mkoba wake inaonekana kama vile anaondoka” akasema Anitha
“ Go get her.We can use her .Tunahtaji kumpata Yule mtoto wa Dr Michael na itakuwa rahisi kama tukimtumia yeye” akasema Mathew.Anitha akashuka garini na kutembea kwa haraka akamfuata Yule dada ambaye alikuwa akitembea taratibu huku akiongea na simu.Mara tu alipomaliza kuongea na simu Anitha akamsalimu
“ Habari yako dada”
“ Habari yangu nzuri.Habari yako? Akasema Yule dada ambaye alikuwa na sauti laini ya upole
“ Naitwa Anitha,mwenzangu unaitwa nani? Akasema Anitha hukuakitabasamu
“ Naitwa Lydie Masawe” akasema
“ Nafurahi kukufahmu Lydie.Unaelekea wapi hivi sasa?
“ Naelekea nyumbani lakini nitapita kwanza saluni kurekebisha nywele na kucha”
“ Sawa Lydie,nadhani ni mara ya kwanza mimi na wewe kuonana”
“ Ndiyo ni mara ya kwanza dada Anitha.Sina kumbu kumbu kama tumewahi kuonana” akasema Lydie
“ Ok Lydie.Kama hutajali nina maongezi nawe kidogo kuhusu kazi.Sijui unaweza kuwa na nafasi sasa hivi? Au kama unaelekea uko saluni,nina usafiri wangu tunaweza tukaongozana na tukapata wasaa wa kuzungumza” akasema Anitha.Lydie hakuwa na wasi wasi wakaelekea mahala akina Mathew walikoegesha gari
“ Lydie huyu ni dereva angu anaitwa Mathew” Anitha akafanya utambulisho mfupi baada ya kuingia garini
“ Mathew tupeleke Zulphat beauty salon” akaelekeza Anitha.
Ndani ya gari walikuwa wakiongea mambo mbali mbali yahusuyo urembo kwa ujumla hadi walipowasili Zulphat beauty salon moja kati ya saluni kubwa za akina mama jijini Dar.Lydie alitengenezwa kwa gharama za Anitha kwani saluni hii ni moja kati ya saluni zenye gharama kubwa.Baada ya hapo wakaelekea Ibona hotel kwa ajili ya maongezi
“ Lydie nimekuleta hapa ili tuweze kuongea kwa utulivu na nafasi” akasema Anitha wakiwa katika bustani tulivu
“ Nakusikilza dada Anitha”
“ Lydie umeolewa? Akauliza Anitha ili kutaka kumfahamu vizuri
“ Hapana bado ila nina mtoto mmoja”
“ Hongera.Mwanao yuko wapi? Akauliza Anitha
“ Yuko kwa babu yake huko Moshi”
“ Kwa nini usimchukue ukaishi naye?
“ Natamani sana kufanya hivyo lakini hali ngumu ya maisha inanilazimu nimuache kwa babu zake”
“ Sawa nimekuelewa Lydie.Sasa dada yangu bila kupoteza wakati nimekufuata nina kazi moja ambayo nahitaji unifanyie.Endapo utakubali basi unaweza ukapata pesa ambayo itakusaidia sana katika kuondokana na maisha haya duni na ukaanzisha biashara zako mwenyewe na hutafanya tena kazi kwa mtu na utakuwa na uwezo wa kuishi na mwanao na kumpatia elimu bora ” akasema Anitha
“ Nitashukuru sana dada Anitha kama utanipatia kazi ambayo itaniwezesha niweze kupata mtaji wa kujiajiri mwenyewe.Niambie ni kazi gani unataka nikufanyie? Una mtoto wa kulea?”
“ Hapana sina mtoto bado Lydie lakini kuna kazi nyingine ndogo tu tena ya masaa machache.Kwanza nieleze pale kwa Dr Michael unafanya kazi gani?
“ Kazi yangu ni kumlea Michael Jr.Asubuhi kumuandaa na kumpeleka shule ambako huwa nikishinda huko hadi saa nane mchana.Dereva huja kutuchukua na kuturudisha nyumbani.Saa tisa kamili ndiyo mwisho wangu wa kazi na hurejea nyumbani” akasema Lydie
“ Ok Lydie sasa ni hivi,kuna taarifa muhimu sana tunayoihitaji toka kwa Dr Michael na ambayo hawezi kutupatia hivi hivi,kwa hiyo tunahitaji kutumia njia mbadala kuipata taarifa hiyo.Nahitaji kumtumia mtoto wake Michael kumtisha kidogo ili aweze kunipatia taarifa hiyo” akasema Anitha na kumtazama Lydie
“ Wewe ni polisi? Akauliza Lydie kwa wasi wasi
“ Hapana,mimi si polisi lakini kazi zangu zinafanana kidogo na za polisi.” akajibu Anitha
“ Kwa hiyo unataka kumtumiaje Michael Jr?
“ Nitamtumia kama chambo ili niweze kuipata taarifa ninayoitaka toka kwa Dr Michael.Najua anampenda sana mwanae hivyo akisikia kwamba mtoto wake yuko mikononi mwangu lazima atatoa taarifa hiyo ninayoitaka” akasema Aitha.Lydie akaonekana kuogopa sana
“ Dada Anitha naona siwezi kuifanya hiyo kazi.Ni kazi ya hatari sana na inaweza kunisababishia matatizo.Hilo ni kosa kubwa na endapo nikishikwa na polisi nitaweza hata kufungwa kwa kosa la utekaji na mwanangu akabaki akiteseka.Utanisamehe dada yangu sintoweza”
Anitha akatabasamu kidogo na kusema
“ Usiogope Lydie.Suala hili haliwezi kwenda polisi kwa sababu mimi ninafanya kazi kwa niaba ya polisi kwa hiyo hata kama likifika kwao wananifahamu kwamba niko kazini na lengo langu si kumuumiza mtoto huyo wala Dr Michael,bali ni kupata taarifa hiyo muhimu sana kwa usalama wa taifa.”
“ Pamoja na hayo dada Anitha bado naona sintoweza.Sijawahi kufanya kazi kama hiyo hata mara moja,zaidi ya yote familia ile wananipenda na kunihudumia vizuri ,siwezi kuwafanyia kitendo kama hicho” akasema Lydie.Anitha akamtazama kwa sekunde kadhaa na kumuuliza
“ Lydie unatoka katika mkoa wa Kilimanjaro,si ndiyo?
“ Ndiyo”
“ Ninawafahamu watu wa Kilimanjaro hususani wanawake ni watafutaji wazuri wa pesa.Ni wapambanaji wa kweli katika kutafuta maisha.Wanaitafuta pesa bila kuchoka na hawaogopi changamoto zilizoko mbele yao na hiyo ndiyo siri ya wao kufanikiwa sana.Tunawaona wengi hapa Dar es salaama namna walivyofanikiwa ,namna walivyochangamka kuitafuta pesa,hawakuja hapa mjini kutazama maghorofa au kuza sura zao nzuri,bali wamekuja kutafuta pesa.Ninakupa fursa ya kujikwamua kiuchumi naomba usiipuuze.Please Lydie wake up.This is your chance.Vaa uhusika wa mwanamke wa kichaga asiye ogopa changamoto na ukubali kuifanya kazi hii ndogo lakini yenye maslahi manono.Niambie unahitaji kiasi gani nikupatie? Akauliza Anitha.Lydie akainama akafikiri
“ Ok ngoja nikutajie .Mimi nitakupa Tsh Milioni saba ili uweze kunifanyia kazi hiyo” akasema Anitha na mara Lydie akainua kichwa
“ Kiasi hicho kiko tayari?
“ Ndiyo kipo tayari.Uko tayari kuifanya kazi hii?
“ Kama mtanilipa kiasi hicho cha pesa mimi niko tayari lakini kwa sharti moja tu kwamba mnipatie kwanza kabla sijawafanyia kazi hiyo kwa sababu ninaweza nikahatarisha usalama wangu halafu msinilipe chochote nikawa nimeharibu kazi yangu na maisha yangu”
“ Usihofu kuhusu pesa hata sasa hivi unaweza ukapewa mradi tu ukubali kuifanya hiyo kazi” akasema Anitha
“ Mimi niko tayari kuifanya.Si umesema suala hili haliwezi kufika polisi?
“ Ndiyo haliwezi kufika polisi”
“ Ok nielekeze unataka nifanye nini?
“ Asubuhi utampeleka Michael Jr shule kama kawaida.Saa tano za asubuhi tutakuja na gari na utawaambia waalimu kwamba umepigiwa simu uwahi kurejea nyumbani.Utatukabidhi mtoto na tutakukabidhi mzigo wako na utapotea na huo utakuwa ni mwisho wako kufanya kazi pale kwa Dr Michael.Sisi tutakaa na Yule mtoto kwa masaa machache na Dr Michael atakapotupatia taarifa yetu basi tutampatia mtoto wake.Nakuhakikishia tena kwamba hatuna lengo la kumdhuru mtoto wala mtu yeyote” akasema Anitha.Wakakubaliana na Lydie halafu wakaagana
“ Amekubali japo haikuwa rahisi kumshawishi.Imenilazimu kumtajia dau kubwa ndipo akakubali.Tutamlipa Tsh Milioni saba.” Akasema Anitha baada ya kuachana na Lydie na yeye kurejea garini alikomuacha Mathew
“ Good.Una hakika hawezi kutusumbua au kutuletea matatizo? Akauliza Mathew
“ She wont.She needs money.” Akajibu Anitha
“ Ok Good.Noah amenipigia simu tayari amekwisha wasili.Timu imekamilika” akasema Mathew
“ Wow that’s great.So whats next?
“ Kwa sasa tunatakiwa kuwasiliana na Elibariki ili tumfahamishe kuhusiana na pesa hii ili watupatie au kama hawana basi tutatumia za kwangu na wataturejeshea.Hatuwezi kukwama kwa sababu ya pesa” akasema Mathew
*********
Eugenia Conrad,msaidizi wa Dr Flora Johakim mke wa rais,alitoka mbio ndani ya chumba cha Dr Flora huku akipiga kelele. Walinzi walimkamata na kumuuliza kulikoni kupiga kelele zile
“ Mama Flora !!....Mama Flor……………!!!” hakumaliza sentensi yake akaanguka na kupoteza fahamu.Koplo Winifrida mlinzi wa Dr Flora akakimbia hadi chumbani kuangalia kuna nini,na ghafla akahisi miguu inamuisha nguvu.Dr Flora Johakim mke wa rais alikuwa amelala kitandani huku damu zikimtoka mdomoni na puani.Akajikaza na kukisogelea kitanda na kuita
“ Dr Flora.!!,Dr Flora !!....
Dr Flora hakutikisa hata ukope.Haraka haraka Winifrida akakimbilia katika simu akampigia Captain Amos daktari wa familia ya rais ambaye alifika mara moja na vipimo akampima na kuamuru liitwe gari la wagonjwa haraka.Gari la wagonjwa likafika Dr Flora akapakiwa na kukimbizwa katika hospitali ya jeshi.Pale akapimwa na kukutwa tayari amekwisha fariki.Baada ya kuthibitishwa kwamba amefariki dunia Captain Amos akampigia simu Dr Joshua
“ Hallow Captain” akasema Dr Joshua
“ Mr President its done.She’s dead”
“ Thank you Captain Amos.Niko njiani narejea Dar es salaam” akasema Dr Joshua na kukata simu.Captain Amos alibaki amesimama ameegemea mti.Alikuwa na mawazo mengi sana.
“ I’ve killed the first lady…Please forgive me lord” akawaza Captain Amos
TUKUTANE SEHEMU IJAYO………………
No comments
Post a Comment