SHIRIKI MAFUNZO YA KIFEDHA
Utanufaika Na Haya Kama Utashiriki Mafunzo Ya Kufanyika Kazi Malengo Ya Kifedha 2022
Rafiki yangu, kwa asili sisi binadamu ni viumbe wa kujifunza, kwa sababu tunapozaliwa ubongo wetu wa juu huwa mweupe kama karatasi. Ubongo huu unakuwa tayari kupokea kila taarifa na maarifa mapya kila siku. Hii ina maana kwamba hakuna binadamu anayezaliwa akiwa anajua kitu chochote. Nafahamu unatamani uwe kama watu wenye mafanikio ya kifedha kwenye jamii inayokuzunguka.
Unachotakiwa kufahamu watu hao wana maarifa na hatua wanazochukua tofauti na wewe. Maarifa na hatua wanazochukua wamejifunza, hawakuzaliwa wakiwa wanajua chochote. Mwanafalsafa wa kale aliyeitwa Socrates aliwahi kuulizwa kwa nini una hekima sana, alijibu kuwa katika maisha yake yote huwa anachojua ni hajui kitu chochote, hivyo alikuwa na fursa ya kujifunza mara zote na hakuna siku aliyoweza kusema ameshajua kila kitu. Sasa unaweza kujiuliza mwenyewe kama mtu mwenye hekima kama huyu alijifunza kila siku, kwa nini wewe unaishi kwa mazoea?
Hivyo hapo ulipo una fursa kubwa ya kuendelea kujifunza na ukawa kama hao unaowatamani. Usijidanganye unajua, haujui vitu vingi ndio maana upo kwenye hali hiyo. Hali uliyonayo ni matokeo ya maarifa, taarifa na fikra ulizozijenga huko nyuma. Kama unataka kubadilisha hali hii, unatakiwa kujifunza maarifa mapya na kujenga fikra mpya.
Kumbuka ubongo wako wa juu jinsi ulivyoumbwa unakupa fursa ya kujifunza kila siku mpaka mwisho wa maisha yako, hauna ukomo wa kupokea maarifa na taarifa. Utafiti uliofanyika hivi karibuni kuhusu ubongo wa binadamu ni kuwa hutumika kwa asilimia mia moja kila siku tofauti na tafiti za miaka iliyopita kuwa unatumika kwa asilimia kumi.
Hapa unachotakiwa kujifunza ni kwamba unaweza kutumia asilimia mia moja ya ubongo wako kupokea maarifa na taarifa zenye tija kwenye maisha yako au zisizo na tija kwa maisha yako, hapo ni swala la maamuzi yako mwenyewe. Ubongo wako unafanya kazi kila siku na kwa asilimia mia moja, hivyo kwako wewe ni muhimu ujifanyie tathmini ya jinsi unavyotumia ubongo wako.
Baada ya kujifanyia tathmini na kugundua ubongo wako unatumika kwenye mambo yasiyo na tija. Kuanzia leo anza kutumia rasilimali hii ya ubongo wa juu kujifunza kuhusu fedha, utajiri na uhuru wa kifedha ili uweze kutimiza malengo yako ya kifedha 2022. Kupitia kujifunza utaweza kujenga tabia mpya zitakazokusaidia kuchukua hatua kila siku mpaka kufikia lengo lako la kifedha 2022.
Ili uweze kuanza kutumia vizuri ubongo wako nakualika ushiriki mafunzo ya kufanyia kazi malengo ya kifedha mwaka 2022. Kwenye mafunzo haya utajenga fikra mpya kuhusu fedha, utajiri na uhuru wa kifedha. Utajifunza kuongeza kipato chako kwa shughuli unayofanya sasa na kuanzisha shughuli mpya kuanzia hapo ulipo. Utajifunza namna ya kupunguza na kudhibiti matumizi yako. Utajifunza jinsi ya kuweka akiba na kama umeshaanza kuweka akiba utaboresha zaidi.
Utajifunza kuhusu uwekezaji na uwekezaji rahisi kuanza nao mara moja. Utajifunza jinsi ya kukokotoa utajiri wako na jinsi ya kuuongeza zaidi. Utajifunza kuondokana na madeni mabaya na kuacha kuingia kabisa kwenye madeni hayo. Utajifunza jinsi ya kukuza thamani yako na shughuli unayofanya.
Hakika mafunzo haya kwako ni ukombozi kutoka kwenye giza nene ulilokuwepo kuhusu fedha, utajiri na uhuru wa kifedha. Kama unajitambua na upo makini na maisha yako hakikisha haukosi mafunzo haya muhimu.
Mafunzo haya yatafanyika kwa njia ya WATSAPP kuanzia tarehe 15.01.2022 mpaka tarehe 15.02.2021. Kujiunga na kundi hilo la mafunzo fungua link hii; https://chat.whatsapp.com/ICuMnwtYizYLqTUaW84Obj
Jinsi ya kushiriki mafunzo haya, tuma meseji kwenye watsapp namba 0762331555 ili nikuunge. Pia jiunge kwenye mtandao huu wa uhuru wa kifedha kwa kusajili jina lako, email yako na namba yako ya simu fungua hapa, www.uhuruwakifedha.co.tz Utakapojiunga utaunganishwa moja kwa moja kwenye group la watsapp la UHURU WA KIFEDHA. Huduma hii ya mafunzo kwa siku 10 za kwanza itakuwa bure ila baada ya hapo unatakiwa kulipia kiasi cha shilling 10,000 kama ada ya ushiriki kupitia mpesa namba 0762331555.
Baada ya mafunzo haya utapatiwa zawadi ya MUONGOZO WA HATUA 100 ZA KUCHUKUA ili ufikie uhuru wa kifedha. Kwenye mwongozo huu utajifunza hatua za vitendo na sio nadharia kufikia uhuru wa kifedha.
No comments
Post a Comment