SIMULIZI: PENIELA (Season 2 Ep 12)
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Noah karudi ? akauliza Mathew
“ Hapana bado.Inawezekana kuna mahala wamepita” akasema Anitha
“ Ok good muache asafishe macho na yule jamaa mwingine anaendeleaje?
“ Amepewa dawa amelala”
“ Ok good.Kuna taarifa nyingine umezipata kuhusia na Habib?
“ bado ninaendelea kutafuta taarifa zake lakini hakuna taarifa zozote mbaya za kumuhusu yeye.Taarifa zake nyingi ni za utumiaji mbaya wa fedha ” Akasema Anitha
“ Ok keep searching.”akasema mathew
“Mmefanikiwa kupata kitu gani huko mlikotoka? Akauliza Anitha.Mathew akakitoa kile kiboksi katika ule mfuko akakiweka mezani
“A box? Anitha naye akashangaa
“Ndiyo ni huu mzigo ambao Sabina aliuficha kwa bibi yake
“ Watu wote hawa wamekufa kwa sababu ya hiki kiboksi? Akauliza Anitha
“ Hata mimi nilistuka kidogo lakini ngoja kwanza tukifungue tujue ndani yake kuna nini” akasema Mathew na kutoka ,halafu akarejea na kifaa cha kukatia chuma na kuanza kukikata kile kiboksi kwa kuwa hawakuwa na funguo.
ENDELEA……………………………….
Mahew na Anitha wote walionekana kuwa na shauku kubwa ya kutaka kufahamu ndani ya kile kiboksi kulikuwa na kitu gani.Alikikata kiungalifu sana ili asije haribu kilichokuwamo mle ndani.Baada ya kufanikiwa kukifungua wote wakapigwa na mshangao kwa walichokikuta ndani.Kulikuwa na bahasha.Akaitoa bahasha ile na kufungua ndani yake kulikuwa na karatasi nne ambazo zilionekana kuchorwa chorwa vitu kama vya kisayansi .Mathew na Anitha wakabaki wanaangaliana.
“ So what’s this? Akauliza Anitha baada ya kuziangalia karatasi zile na kushindwa kufahamu kilichokuwa kimeandikwa
“ Hata mimi sifahamu ni kitu gani hiki” akasema Mathew halafu akachukua tena zile karatasi akaanza kuziangalia
“ Zinaonekana ni kama formula za kisayansi lakini sina uhakika.” Akasema Mathew
“ Kwa hiyo listi yote ile ya watu wamekufa kwa sababu ya karatasi hizi? Akauliza Anitha
“Inashangaza sana lakini nina hakika lazima kuna kitu ndani ya karatasi hizi ambacho hatukifahamu na ndiyo maana kukawa na mlolongo wa vifo” akasema Mathew
“ Mathew nataka kukubaliana na wewe lakini ninasita.Ninahisi kuna kitu kingine walichokuwa wanahitaji kukiuza na si hizi karatasi.Hainiingii akilini kabisa kwamba karatasi hizi zisababishe idadi ile watu kuuawa.Edson,mpenzi wake brigita,mzee Matiku,mzee KItwana wote hawa wamekufa kwa sababu ya hizi karatasi? Ninahisi bado kuna kitu kingine kimefichwa ambacho tunatakiwa tukipate.” Akasema Anitha
“ Anitha mzigo huu tumeutoa kwa bibi yake Sabina ambao alikuwa ameuficha mbali.Sabina alipewa mzigo huu na mzee Kitwana kwamba aufiche.Nina hakika kuna kitu ndani ya karatasi hizi ambacho tunatakiwa tukifahamu.Usikate tama mapema” akasema Mathew
“Mathew una hakika kwamba hakuna kitu kingine tofauti na hizi karatasi? Unajua hainiingii akilini eti watu wote wale wafe kwa sababu tu ya hizi karatasi.Na ukumbuke kwamba hii ilikuwa ni biashara ambayo ilitakiwa kuwapatia watu hawa wote mamilioni ya fedha sasa ninashindwa kuamini kama karatasi hizi ndizo zingewaingizia watu wale millions of money.I think there is something else” akasema Anitha
“ Anitha Karatasi hizi ziliibwa toka ikulu na Edson na walipanga waziuze kwa mamilioni ya fedha kwa Habib Soud ambaye nilikwambia utafute taarifa zake .Kama ni hivyo lazima karatasi hizi zina kitu kizito ndani yake.Karatasi kama hivi kuuzwa kwa mamilioni ya fedha si kitu rahisi ,kwa hiyo basi tunachitakiwa kukifanya kwa sasa ni kujaribu kufahamu karatasi hizi ni za nini na umuhimu wake.” Akasema Mathew
“ Nani ambaye atatueleza kuhusiana na karatasi hizi? Mbona maandishi yake ni ya ajabu ajabu tu? Akauliza Anitha
“ Karatasi hizi zimeibwa toka ikulu na ili kufahamu ni za nini tunatakiwa kumpata mtu toka ndani ya Ikulu ambaye anaweza akatueleza kuhusu nini kilichomo ndani ya karatasi hizi.Zimeandikwa kisayansi sana na sisi si wanasayansi.Hakuna chochote tunachoweza kuambua ndani ya karatasi hizi” Akasema Mathew
“ Ni nani ndani ya ikulu ambaye anaweza akatusaidia Mathew? Huoni kwa kufanya hivyo tunaweza kuwa tunajitafutia matatizo mengine kwa sababu karatasi hizi zimeibwa toka ikulu?” Akasema Anitha.Mathew akafikiri kwa muda halafu akasema
“ Mr President”
“ President? Anitha akashangaa
“ Ndiyo ,tukimfuata na karatasi hizi anaweza akatusaidia kufahamu kilichomo ndani yake na umuhimu wake na kwa nini ziliibwa na kutaka kuuzwa kwa mamilioni ya fedha.Kama zimetoka ndaniya ikulu basi lazima atakuwa anafahamu ni za nini.Hakuna mwingine tunayeweza kumuanini zaidi yake” akasema Mathew
“ Kwa hiyo tutamueleza ukweli sisi ni akina nani ? akaulzia Anitha
“ Kama tubna nyaraka kama hii lazima tumueleze ukweli ili atuamini”
“ How can we meet with President? Akauliza Anitha
“ Through Elibariki.Yeye ni mkwe wake na atatusaidia sisi kuweza kuonana naye kwa urahisi.Jambo hili si la kuchelewa tunatakiwa tulifahamu vizuri na kwa haraka “ akasema Mathew na kuchukua simu yake akazitafuta namba za jaji Elibariki akapiga lakini simu ya jaji Elibariki haikuwa ikipatikana
“ Elibariki yuko wapi? Kwa nini ameizima simu yake? Akauliza Mathew
“ Nilikwambia yawezekana Noah akawa amemshawishi wakapitia sehemu Fulani kupooza koo si unajua tena Noah anavyopenda starehe” akasema Anitha
“ Ok ngoja tuwasubiri lakini ingekuwa vyema kama angewahi kuja ili tuweze kuongea naye kuhusiana na suala hili na atusadie kuweza kulipatia ufumbuzi ” Akasema Mathew na kuzishika tena zile karatasi akaanza kuziangalia
“ Dah ! pamoja na ufahamu wangu wa vitu vingi lakini kwa hili nimegonga mwamba.Nimeshindwa kuambua kitu chochote hapa.Namna vitu vilivyoandikwa andikwa inachanganya sana.” Akasema Mathew
“ Mathew unadhani labda inawezekana kuna kitu kinafichwa ndani ya maandishi haya ili kisijulikane? Yawezekana ni siri Fulani?
“ Kwa namna nilivyoziona hizi ni formula za kisayansi.Kuna mahesabu mengi ya kisayansi humu ndani kwa hiyo inatakiwa tumpate mtu ambaye anaweza akatufafanulia kuhusiana na formula hizi.Usijali Anitha tutafahamu tu ni kitu gani lakini lazima tujue kwamba kilichomo ndani ya karatasi hizi ni kitu kikubwa na ndiyo maana kimegharimu uhai wa watu.Na hata hivyo tunatak…………….” Mathew akakatishwa na simu yake ya mkononi iliyokuwa ikiita.Alikuwa ni Jason
“ Hallo Jason” akasema Mathew
“Mathew samahani kwa kuwasumbua mida hii lakini nataka kuwahamisha kuhusiana na shambulio lililotokea usiku huu”
“ Shambulio ? Mathew akastuka
“ Shambulio gani Jason?
“ Ina maana hamjapata taarifa zozote za kuhusiana na shambulio lililotokea? Akauliza Jason
“ Hapana hatuna taarifa zozote.Ni shambulio gani? akauliza Mathew kwa mshangao
“ Gari la jaji Elibariki limeshambuliwa na watu wasiojulikana usiku huu na inasemekana kuna tu ameuawa” akasema Jason.Taarifa zile zikamstua mno Mathew
“ Shambulio hilo limetokea saa ngapi?
“ Usiku huu Mathew na inasemekana kuna mtu mmoja ameuawa katika shambulio hilo”
“ Ouh my God ! “ akasema Mathew na kushindwa la kusema .Midomo yake ilikuwa inamcheza.
“ What happened Mathew? Akauliza Anitha.Mathew akashinda kuongea
“ C’mon Mathew tell me what happened? Akauliza Anitha
“ Elibariki ameshambuliwa na watu wasiojulikana” akasema Mathew huku sauti ikimtetemeka
“ Don’t tell me he’s dead” akasema Anitha na macho yake yalishindwa kuonyesha mstuko aliokuwa ameupata
“ Jason ! akaita Mathew
“ Mtu aliyekutwa amekufa ndani ya gari ni jaji Elibariki au ni nani ? Kwa sababu Elibariki alikuwa ameongozana na Noah usiku huu” Akauliza Mathew
“ Alikuwa na Noah? Akauliza Jason
“ Ndiyo alikuwa na Noah “ akajibu Mathew
“Mpaka sasa hakuna taarifa kamili kwamba aliyekutwa amekufa ndani ya gari hilo ni nani lakini taarifa zinadai kwamba ni mtu mmojandiye aliyekutwa amekufa.Hivi sasa ninaelekea katika hospitali kuu ya taifa kwa ajili ya kwenda kumtambua kama ni Elibariki ama vipi.” Akasema Mathew
“Jason ahsante sana hata sisi tunaelekea huko sasa hivi” akasema Mathew na kukata simu.Alihisi mwili wake kukosa nguvu
“ Jason anasemaje? Akauliza Anitha
“ Hakuna mpaka sasa taarifa kamili iliyotoka kama aliyekufa ni jaji Elibariki ama si yeye.Kwa sasa Jason anaelekea hospitali kuu ya Taifa ili kwenda kuutambua mwili wa mtu huyo aliyekutwa amekufa ndani ya gari la jaji Elibariki” akasema Mathew
“ Mathew I’m so scared.Elibariki alikuwa na Noah ndani ya gari.Una hakika Noah yuko salama? Akauliza Anitha
“ Siwezi kuwa na uhakika kama aliyefariki takuwa nani lakini lazima tujiandae kwa lolote.Tunaelekea hospitali tukathibitishe.” Akasema Mathew na kuingia chumbani kwake akabadili mavazi halafu wakaingia garini na kuanza safari ya kuelekea hospitali kuu ya taifa kwa ajili ya kwenda kuutambua mwili wa mtu aliyeuaa kwa risasi ndani ya gari la jaji Elibariki.
“ Mathew unadhani ni nani ambaye anaweza kuwa amefanya shambulio hili ? Akauliza Anitha kwa sauti yenye kitetemeshi.
“ hapana siwezi kujua kwa sasa.Ni vigumu kufahamu kwa sababu majaji huwa ni watu wenye maadui wengi.Inawezekana wakawa ni watu ambao hawakuridhishwa na mojawapo ya maamuzi yake kwa hiyo wakaamua kulipiza kisasi.”akasema Mathew ambaye alionekana kuwa na mawazo mengi sana.Anitha alikuwa ameifunga mikono yake na kuiweka kifuani akiomba kimoyo moyo.
“Mungu wangu ninaomba Noah awe mzima kwa sababu naye alikuwamo ndani ya gari la jaji Elibariki.”
Waliwasili katika hospitali kuu ya taifa na kuelekea moja kwa moja katika chumba cha kuhifadhia maiti .Nje ya jengo lile wakakutana na Jason ambaye tayari alikwisha fika
“ Jason tupe taarifa.Umefanikiwa kumtambua mtu huyo? Akauliza Mathew
“ Nimefanikiwa kumuona lakini si jaji Elibariki..” akasema Jason na huku akionekana kuogopa .Anitha alikuwa ameiweka mikono kichwani aliogopa sana.Mathew Anitha na Jason wakaingia ndani ya chumba cha maiti kwa ajili ya kuitambua maiti ya mtu Yule.Anitha akaanguka na kupoteza fahamu baada ya kugunudua kwamba mtu Yule aliyekuwa amefariki ni Noah.Mathew na Jason wakisaidiana na watu wengine waliokuwapo pale wakambeba na kumtoa nje kwa ajili ya kumsadia ili aweze kurejewa na fahamu zake.Alipatwa na mstuko mkubwa sana.Wakati Anitha akiendelea kupatiwa huduma ya kwanza Mathew alisogea pembeni akatoa kitambaa na kujifuta machozi.Aliumizwa sana na tukio lile.
“ Ni nani lakini aliyefanya jambo kama hili? Ni nani aliyemuua Noah? Akajiuliza huku machozi yakiendelea kumtoka
“ Masikini Noah amekufa bado kijana mdogo tu.Nitawaeleza nini familia yake? Bado Mathew aliendelea kuangusha machozi na mara akashikwa bega na Jason
“ Mathew ,Anitha ameamka” akasema Jason
“Jason I’m deeply hurt.Sijawahi kuumia namna hii kwa miaka mingi.Machozi ya mwisho niliyatoa wakati familia yangu ilipoteketea kwa moto lakini leo nimeshindwa kujizuia na kuangusha machozi.Nimeumia sana Jason kwa kifo hiki cha Noah.Nimemfahamu Noah kwa muda mrefu na ni mimi niliyemjenga hadi hapa alipofika.Nilimuita aje anisaidie katika kazi mliyotukabnidhiya kumtafuta muuaji wa Edson na sikjua kama nilikuwa namuita aje kufa.Laiti kama ningejua kijana Yule anakuja kufa wala nisingemuita aje anisaidie kazi” akasema Mathew na kushindwa kujizuia kudondosha chozi
“ Pole sana Mathew.Pole sana” akasema Jason
“ Ahsante sana Jason.Japokuwa kifo tumeumbiwa wanadamu lakini kwa kweli nimeumizwa mno na mauaji haya ya kikatili ya Noah.Sikutegenmea hata siku moja kama Noah angeweza kuawa kikatili namna hii” akasema Mathew kwa ucungu
“ Ilikuwaje Noah akawa katika gari la jaji Elibariki? Akauliza Jason.Mathew akafuta machozi na kusema
“ Noah alikuwa anajeraha katika mguu wake kwa hiyo tulimuacha nyumbani wakati sisi tukielekea katika kazi Fulani usiku huu.Wakati hatupo alifika Elibariki kwa kuwa nilihitaji kuonana naye usiku wa leo.Aliponikosa aliamua kuondoka na kwenda kuonana na mke wake halafu arejee.Alinipiga simu na kunitaarifu kwamba atarejea baada ya muda na anaongozana na Noah ambaye alisema kwamba anataka kwenda kuufanyisha mazoezi mguu wake na alikuwa ameboreka pale ndani peke yake.Ningejua kama anakwenda kufa wala nisingemruhusu aondoke pale nyumbani” akasema Mathew na kufuta machozi.Kikapita kimya cha sekunde kadhaa Jason akauliza
“ Jaji Elibariki yuko wapi? Si umesema kwamba walikuwa wote ndani ya gari? Akauliza Jason
“ Ni kweli walikuwa wote ndani ya gari lakini hata mimi sifahamu Elibariki yuko wapi “ akasema Mathew
“ Hili ni jambo la kushangaza sana kama walikua wote garini yeye yuko wapi? Kwa nini afariki Noah peke yake? Ina maana wakati shambulio hilo linafanyika Elibariki hakuwamo garini? Akauliza Jason
“ Jason jambo hili linashangaza sana.Hata mimi nashindwa kuelewa kwamba ndani ya hilo gari alikuwepo Noah peke yake? Kuna maswali mengi ya kujiuliza hapa lakini kwa sasa inatubidi tuachane kwanza na hayo ili tushughulikie suala la msiba wa Noah.Siwezi kufanya jambo lolote kwa sasa hadi kwanza akili yangu itakapotulia .Elibariki yuko wapi ,amekufa ama hajafa ni suala ambalo nitalishughulikia baadae.” Akasema Mathew ambaye ni wazi alionekana kuchanganyikiwa
“Sawa Mathew ,basi tuanze taratibu zinazotakiwa ili tuweze kukabidhiwa mwili wa Noah.Niachie mimi nitalishughulikia suala hili .Kwani Noah ni mtu wa wapi? Ndugu zake wako wapi?
“Kwa sasa familia yake inaishi jijini Harare Zimbabwe.Mama yake ni mtanzania na baba yake ni raia wa Zimbabwe.Nitafanya utaratibu wa kuwasiliana na familia yake na kuwataarifu kuhusiana na msiba huu na kwa pamoja tujadiliane namna ya kufanya kama Noah azikwe hapa Tanzania au asafiriswe kwenda Zimbabwe.” akasema Mathew
“ Sawa Mathew mimi nitalishughulikia suala hilo .Kwa sasa unaweza kwenda kupumzika mimi nitalishuhulikia jambo hili kwa sababu lina taratibu zake na nitakupa majibu kesho asubuhi.” Akasema Jason .
Tayari Anitha alikwisha rejewa na fahamu zake lakini hakuwa na nguvu kabisa.Machozi mengi yalikuwa yanamtoka.Jason akamshika mkono akamsaidia kutembea hadi katika gari akiwa ameongozana na Mathew
“ Mathew are you sure you can drive? Akauliza Jason
“ Yes I can.Shughulikia suala hilo na nitakufahamisha baada ya kuwasiliana na familia ya Noah” akasema Mathew na kuwasha gari kisha wakaondoka.Anitha alikuwa ameinama akilia.Mathew naye alikuwa akiendesha gari huku machozi yakimtiririka.Kifo cha Noah kilimuumiza sana.
Walifika numbani na Anitha akajitupa sofani akaendelea kulia
“ Anitha najua ni kwa namna gani kifo cha Noah kimekuumiza,hata mimi nimeumia sana na siwezi kueleza ni kwa namna gani ninaumia moyoni lakini pamoja na maumivu yote tuliyonayo kwa sasa tunatakiwa tusimame imara katika suala hili hadi hapo tutakapo hakikisha kwamba Noah amepumzishwa.Sisi ndiyo ndugu zake wa karibu na tunatakiwa tuwe na nguvu na ujasiri tuubebe msiba huu hadi mwisho .Tafadhali Anitha nakuhitaji sana katika hili.Nahitaji sana ushirikiano wako” akasema Mathew
“ Mathew I’m sorry I cant…Ninashindwa kabisa kujizuia kulia.NImeumia sana..Ouh Noah !..Anitha akashindwa kujiuzia na kuangua kilio.Mathew akamfuata akamkumbatia na kumfuta machozi.
“ We need to be strong for him” akasema Mathew halafu akainuka na kwenda chumbani kwake akakaa kitandani nz kuanza kulia.Baada ya kama dakika kumi hivi za kulia akainuka na kujifuta machozi halafu akafungua kabati lake na kutoa kitabu Fulani ambacho huwa anaandika kumbu kumbu kadhaa.Akazitafuta namba Fulani akaziandika katika simu yake na kupiga lakini namba zile hazikuwa zikipatikana.Akaandika tena namba nyingine na kupiga.Simu ikaanza kuita.Mathew alikuwa anampigia simu dada wa Noah anayefanya kazi katika benki moja nchini Zimbabwe.Baada ya kuzipata taarifa zile dada wa Noah akaumuunganisha Mathew na wazazi wake akawataarifu kuhusiana na kilichotokea.Kila aliyeipata taarifa ile alipatwa na mstuko mkubwa sana.Baba wa Noah akamuahidi Mathew kumpigia simu asubuhi ili kumtaarifu ni kitu gani watakuwa wameamua kuhusiana na mazishi ya mtoto wao
Mathew alikaa tena kitandani an kukumbuka mbali sana toka alipokutana na Noah na kujenga urafiki na hatimaye akamtoa katika kazi aliyokuwa anaifanya na kumuingiza katika kufanya kazi binafsi na ambazo zilimletea mafanikio makubwa .
“ Alikuwa ni kijana mchapa kazi na ambaye alikuwa uwezo ajabu.Nimekwisha fanya naye kazi nyingi na kila kazi niliyofanya naye ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa.Yeye na Anitha hawakuwa tu ni marafiki zangu bali ndugu zangu” akawaza Mathew
“ Yeyote aliyefanya kitendo hiki nitamtafuta hadi nimpate.Kila risasi iliyoingia mwilini mwa Noah haitakwenda bure lazima itaondoka na mtu. I swear in heaven and earth yeyote aliyefanya ukatili huu hawezi kujificha sehemu yoyote nisimtambua.Nitawasaka kila mahala na nitawapata.” Akawaza Mathew akiwa na hasira kali
*******
Mwili wa jaji Elibariki ulikuwa umeloa damu na alikuwa na jeraha katika mkono wake wa kulia lililokua linatoa damu.Alikuwa amekaa ndani ya gari huku pembeni yake kukiwa na mwanamke aliyekuwa anaendesha gari kwa umahiri mkubwa sana.Mwili wote bado ulikuwa unamteteteka.Alikumbuka kilichotokea muda mfupi uliopita akaogopa sana.
“ Wamemuua Noah !! akawaza huku machzi yakimtoka
“ Ni akina nani wale waliofanya kitendo kile cha kinyama? Nilifanya kosa kubwa sana kulipuuza onyo lile nililopewa na Yule mwanamke aliyenipigia simu na kunitaka nisiingie katika gari.Inaonekana kuna mpango ulikuwa umekwisha pangwa ili niuawe.Lakini kwa nini watake kuniua? Ni nani wanaotaka kuniua? Mwanamke Yule aliyenipigia simu na kunipa onyo ni nani? Ni huyu pembeni yangu ama ni nani? Huyu mwanamke naye ni nani? Amenifahamuje? Mbona mimi simfahamu? Ananipeleka wapi? Akajiuliza Jaji Elibariki maswali mfululizo bila kupata majibu
“Mpaka sasa hivi sifahamu nimeponaje katika lile shambulio.Dah ! Toka nimezaliwa sijawahi kushuhudia shambulio baya kama lile.Risasi zilikuwa zinavuma kama vitani.Nimeponyoka toka mdomoni mwa kifo.” Akawaza Jaji Elibariki na kuvuta kumbu kumbu kuhusiana na namna tukio lile llilivyotokea.Alikumbuka namna Noah alivyoruka na kumkinga na risasi akaumia sana na machozi yakamtoka
“ Noah aliniokoa.Bila yeye hivi sasa ningekuwa tayari marehemu.Shambulio lile lilinilenga mimi na amekufa kifo nilichostahili kufa mimi.Ninaamini haikuwa ni mipango ya Mungu nifariki leo.Nadhani Mungu ana makusudi yake kwa nini nimepona leo hii.” Akawaza Jaji Elibariki halafu akajaribu kunyoosha mkono akagugumia kwa maumvu makali
“ Elibariki ! akaita Yule mwanamke ambaye alikuwa makini sana katika usukani.Elibariki akageuza shingo na kumtazama.Hakuwa na kumbu kumbu kama amewahi kumuona sehemu mwanamke sehemu yoyote.
“Unajisikiaje? Akauliza Yule mwanamke
“ Sijielewi elewi bado.I feel like I’m dead” akasema Elibariki na Yule mwanamke akatabsamu na kusema
“ You are not dead Elibarki .You are alive.Kuna sehemu yoyote umeumia? Akauliza
“ Ninasikia maumivu makali hapa katika mkono wa kulia na chini ya mguu wa kushoto” akasema Elibariki
“ Pole sana.” Akasema Yule mwanamke
“ Wewe ni nani? Akauliza Elibariki.Yule mwanamke akatabasamu na kusema
“ Mtu ambaye hupaswi kumfahamu”
“ Mtu ambaye sipaswi kukufahamu? Una maana gani kusema hivyo? Wewe ndiye uliyenipigia simu? Akauliza Elibariki
“ Elibariki kitu cha msingi cha kushukuru kwa sasa ni kwamba uko salama.”
“ Nani waliotaka kuniua? Unawafahamu? Akauliza jaji Elibariki
“ Elibariki huu si muda wa maswali mengi” akasema Yule mwanamama.Elibariki akakaa kimya kidogo halafu akauliza
“ Unanipeleka wapi?
“ Somewhere safe.Kuna sehemu yoyote ambayo unahisi inaweza kuwa salama kwa sasa kwa wewe kwenda kujificha? Kwa sababu hutakiwi kabisa kuonekana.”Akauliza Yule mwanamama.Jaji Elibariki akafikiri kwa muda halafu akasema
“ Ndiyo”
“ Ni wapi nikupeleke ? Akauliza Yule mwanamke
“ Kwa rafiki yangu”
“ Unafahamu anakokaa? Akauliza
“ Ndiyo ninapafahamu”
“ Unazifahamu namba zake za simu kwa kichwa ? kwa sababu sitaki uwashe simu yako” Akauliza
“ Ninazikumbuka “ akasema jaji Elibariki na kumtajia Yule mwanamke akaziandika katika simu yake akapiga na simu ikaanza kuita
“ Hallow” akasema Yule mwanamke baada ya simu kupokelewa
“ Hallow” ikasema sauti ya upande wa pili
“ Samahani ninaongea na nani?
“ Unaongea na Peniela” ikasema sauti ya upande wa pili.Yule mwanamke akamgeukia jaji Elibariki
“ Anasema anaitwa Peniela ndiye rafiki yako? Akauliza
“ Ndiyo”
“ Do you trust her? Akauliza tena
“ Ndiyo ninamuamini sana” akasema jaji Elibariki
“ Ok ongea naye” akasema Yule mwanamke na kumpatia Elibariki simu
“ Hallow Peniela Elibariki hapa ninaongea”
“Elibariki?
“Ndiyo ni mimi?
“ Mbona unanishangaza Elibariki? Mbona unanipigia kwa kutumia simu nyingine? Uko wapi ? Uko na nani?
“ Niko katika gari na ….” Elibariki akasita.Yule mwanamke aliyekuwa akiendesha gari akaachia usukani wa gari na kumnyang’anya Elibariki simu
“ Hallow Peniela.Una gari? Akauliza
“ Ndiyo ninalo”
“ Ok vizuri basi washa gari lako sasa hivi na uje pale Kisulo restaurant uje umchukue rafiki yako .He’s in trouble na anahitaji sehemu salama.Tafadhali usimwambie mtu yeyote kuhusiana na jambo hilina uwe na uhakika hakuna mtu anayekufuatilia” Akasema Yule mwanamke na kukata simu.
KARATASI WALIZOZPATA AKINA MATHEW ZIMEANDIKWA KITU GANI? MWANAMKE ALIYEMUOKOA JAJI ELIBARIKI NI NANi? TUKUTANE SEHEMU IJAYO……
No comments
Post a Comment