SIMULIZI: PENIELA (Season 2 Ep 14)

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

“ Kifo cha Noah kimeniumiza sana Elibariki.Lakini hatuna namna ya kufanya imeshatokea imetokea.Kwa sasa uko wapi? Akauliza Mathew

“ Kuna sehemu nimejificha”


“ Is it a safe place? Are you sure you are safe? Akauliza Mathew

“ Yes I’m sure.I’m safe”

“ Ok good.Endelea kujificha hapo hapo .Kwa sasa tunashughulikia msiba wa Noah.Nimewasiliana na wazazi wake tayari nchini Zimbabwe na wamesema kwamba tutawasiliana tena asubuhi ili wanitaarifu kuhusiana na walichokipanga.Noah alikuwa ni kama mdogo wangu kwa hiyo nitaweka kila kitu pembeni kwa sasa na baada tu ya kumzika ndipo nitaanza tena kazi.Ninakuahidi kwamba yeyote aliyehusika katika tukio hili hatabaki salama.Nitakaporejea utashuhudia nitakachokifanya.Kila risasi iliyoingia mwilini mwa Noah italipwa.Kwa sasa endelea kukaa hapo hapo hadi nitakaporejea.Endapokukiwa na tatizo lolote unitaarifu mara moja.Lakini mpaka hapo tutakapoonana tena please stay safe” akasema Mathew na kukata simu


ENDELEA………………………..


“ Mathew ameumizwa sana na kifo cha Noah .Nimeisikia sauti yake na anaonekana wazi kwamba ana nia ya dhati ya kulipiza kisasi.Hata mimi ninamuunga mkono kwa hilo.Lazima watu wote waliofanya kitendo kile wapatikane .Watu wale walikuwa na lengo la kuniua lazima niwafahamu ni akina nani kwa nini wanataka kuniua? Akawaza jaji Elibariki.Mawazo mengi yakamjia kichwani kutafakari kuhusiana na tukio lile .


“ Ama kweli maisha ya mwanadamu ni mafupi sana.Dakika chache zilizopita nilikuwa naongea na kucheka na Noah lakini ghafla tu watu wameukatili uhai wake.Tukio lile litaendelea kukaa katika kumbukumbu zangu kwa miaka mingi sana .Ni tukio baya sana kuwahi kunitokea lakini kwa msaada wa Mathew nina hakika nitawafahamu waliofanya tukio lile.” Akawaza na kukumbuka toka alipopigiwa simu na Yule mwanamke na kumzuia asiingie katika gari


“ Mawazo yananijia kwamba yawezekana kabisa sababu ya kutaka kuniua chanzo chake kikawa ni kifo cha Dr Flora ambaye akifo chake kimetawaliwa na utata mwingi. Nilifanikiwa kuufahamu ukweli wa kilichomuua Dr Flora lakini nilishangaa baadaya taarifa yangu kutupwa mbali kwamba ni taarifa ya uongo na ya kuunga unga.Ninamuamini Mathew na hawezi kunipa taarifa ya uongo.Ninahisi kitendo changu cha kuufahamu ukweli wa kifo cha Dr Flora kimewapa mashaka sana watu waliomuua na hivyo ili kuendelea kuificha siri hii wakaona njia bora ni kuniua na mimi pia.Ni akina nani watu hawa? Kwa nni walimuua Dr Flora? Kuna mambo mengi hapa ya kujiuliza na kuyatafutia majibu “ akawaza na taratibu kijiusingizi kikaanza kumpitia kutokana na dawa alizokuwa amepewa .Peniela akamfunika vizuri na kulala pembeni yake.

“ Lini na mimi nitampata mwanaume wa kulala naye kitandani kama hivi ambaye nitakuwa na uhakika kwamba ni mwanaume wangu? Nitakuwa nikilala na wanaume wa wenzangu hadi lini? Nimekwisha anza kuchoshwa na maisha haya.Sitaki tena kuwa sehemu ya Team SC41.Nataka niishi maisha ya kawaida kama wanawake wenzangu.Lakini yote haya mwisho wake umekaribia sana.Nikishaikamilisha operesheni 26B lazima nirejee katika maisha ya kawaida.” akawaza Peniela akiwa ameuweka mkono wake kifuani kwa jaji Elibariki


********


Kumepambazuka na nchi ikia imeamshwa na taarifa kubwa ya kushambuliwa kwa jai wa mahakama kuu.Vyombo vyote vya habari hii ndiyo ilikuwa habari yao kubwa siku hii.Hakuna aliyeweza kufahamu mahal aliko jaji Elibariki japokua kulikuwa na juhudi kubwa za jeshi la polisi katikakumtafuta mahala aliko.Flaviana Hakuweza kabisa kupata usingizi kutokana na hofu aliyokuwa nayo.Mpaka kunapambazuka hakuwa amepata taarifa zzote kuhusiana na wapi alipo mume wake.Akampigia smu baba yake na kumuuliza kama kuna taarifa zzote za kuhsu mahala aliko mume wake lakini mheshimiwa rais akamuhakikishia kwamba vypmbo vya uslama vinaendelea kmtafuta kila mahala .

“Nakuomba baba tafadhali fanya kila linalowezekana ili mume wangu aweze kupatikana.” Kasema Flaviana

“ Flaviana nimekwisha kuahidfi kwamba nitafanay akila linalowezekana ilikuhakkisha kwamba Elibariki anapatikana tena akiwa hai” akasema DrJoshua na kuwaomba wajiandae kwa ajiliya safari ya kueleka mazishini kijijini alikozaliwa mama yao


*******


Mlio wa simu ukamstua Mathew aliyekuwa amejilaza sofani.Akainuka na kuichukua simu yake.Alikuwa ni baba yake Noah ambaye alimfahamisha kwamba wamekaa kikao cha familia na wameafikiana kwamba Noah azikwe jijini Dar es salaam kwa hiyo familia nzima itakuja jijini Dar kwa mazishi.Baada ya kuongea na baba yake Noah Mathew akampigia simu Jason na kumfahamisha mambo aliyoongea na baba yake Noah.Hakumueleza chochote kuhusiana na Ebariki.Kisha ongea na Jason akaenda kumgongea Anitha ambaye macho yake yalikuwa yamevimba kwa kulia akamfahamisha kilichokuwa kinaendelea


“ Anitha there is one more thing” akasema Mathew

“ Kitu gani Mathew?


“ Nimeongea na Elibariki jana usiku”

“ Elibariki?! Anitha akastuka


“ Ndiyo nimeongea naye jana usiku “


“ Kwa nini hukuniambia usiku ule kama uliongea na Elibariki ili nisiwe na mawazo kama amekufa?


“ Usingeweza kunisikia kwa namna ulivyokuwa na uchungu ” akasema Mathew

“ Yuko wapi ? Is he ok? Is he safe? Akauliza Anitha


“ Hakuniambia kama yuko wapi lakini alinihakikishia kwamba yuko salama.”


“ Are you sure he’s safe? Akauliza Anitha


“ Sina hakika sana kama yuko salama lakini yeye mweyewe alinihakikishia kwamba yuko salama”


“ Nina wasi wasi asije kuwa ametekwa na watu na wakamlazimisha apige simu ili kuwaondoa watu wasi wasi” akasema Anitha


“ Hilo linawezekana kabisa .Unajua kwa wakati ule hata mimi kichwa changu hakikuwa sawa.Nilikuwa na mambo mengi sana” akasema Mathew

“ Namba alizokupigia unazo? Akauliza

“ Ndiyo ninazo “ akasema Mathew


“ Tunatakiwa tuzifuatilie namba hizo tuzifahamu ni za nani ili tujue ni wapi tunaweza kuanza kumtafutia jaji Elibariki.We need to find him Mathew.We need to bring him here.This is the only place we can be sure he’s safe” akasema Anitha. Mathew akamtajia namba alizotumia jaji Elibarki kumpigia simu usiku ,Anitha akainuka na kuchukua kompyuta yake ndogo akafungua program Fulani na kuziandika zile namba alizotumia Elibariki kumpigia Mathew.Baada ya kama sekunde ishirini hivi akamgeukia Mathew


“ What ! Umegundua nini? Akauliza Mathew


“ Peniela !..


“ Peniela? Akauliza Mathew


“ Ndiyo.Namba aliyoitumia Elibariki jana kukupigia ni namba ya simu ya Peniela”


“ Are you sure? Akauliza Mathew


“ Yes I’m sure.Ni namba ya Peniela.Are you sure he’s safe there?

“ I think he’s safe.” Akasema Mathew


“ Amefikaje kwa Peniela? Akauliza Anitha


“ Hata mimi sifahamu bado amefikaje lakini nina hakika ni sehemu ambayo amechagua kuwepo kwa sasa.Ukumbuke niliwaambia mapema kwamba Elibariki na Peniela wana mahusiano kwa hiyo atakuwa ameamua kwenda kujificha kule”

“ What about Team SC41? Akauliza Anitha


“ Anitha kwa sasa kilichopo mbele yetu ni kwanza kushughulika na msiba wa Noah na baada ya hapo tutarejea tena kazini na safari hii tutakuwa na kazi kubwa ya kuweza kuwatafuta wale wote waliomuua Noah ,vile vile tuna kazi kubwa ya kufahamu kuhusiana na zile karatasi,na mwisho tuna kazi kubwa ya …” Mathew akasita

“ Kazi kubwa ya nini? Akauliza Anitha


“ Ouh sorry forget about that.Inuka ujiandae leo tuna siku ndefu sana” akasema Mathew na kutoka.

“ Kazi yangu ya mwisho ni kupambana na Team SC41.Sikutaka Anitha afahamu hili kwa sababu hiki ni kisasi changu peke yangu na sitaki yeyote ahatarishe maisha yake kwa sababu ya kazi hii.Nitapambana peke yangu” akawaza Mathew na kuingia chumbani kwake.


********


Miale ya jua ilipenya ndani ya chumba cha Peniela.Sauti za mbwa wa jirani waliokuwa wakibweka ndizo zilizomstua jaji libariki akafumbua macho.

“ Kumekucha” akasema na macho yake yakatua katika saa kubwa ya ukutani ambayo ilionyesha ni saa mbili kasoro za asubuhi.Kitandani alikuwa mwenyewe Peniela hakuwepo


“ Pamoja na matatizo niliyonayo lakini nimelala usingizi mzuri sana japokuwa ulitawaliwa na ndoto mbaya za tukio la jana.Nilisikia raha ya ajabu kulala nikiwa nimekumbatiwa na Peniela.” Akawaza jaji Elibariki na kujitazama majeraha yake akajaribu kusimama hakuwa akisikia maumivu makali kama aliyokuwa akiyasikia usiku

“Ninaendelea vizuri sana.Sisikii maumivu kama yale ya jana usiku” akawaza jaji Elibariki akijaribu kuunyoosha mguu wake ambao ulikuwa na maumivu makali jana na mara mlango ukafunguliwa akaingia Peniela akiwa na sinia lililokuwa na mlo wa asubuhi


“ Elibariki umekwisha amka? Unajisikiaje? Akauliza penny

“ Ninajisikia vizuri sana na sisikii maumivu kama yale niliyokuwa nikiyasikia jana .Nashukuru sana usiku wangu ulikuwa mzuri mno zaidi ya nilivyotegemea japokuwa picha ya tukio lile la jana bado inaendelea kunijia kila mara” akasema Elibariki

“ Ok ni muda wa kupata kifungua kinywa.Leo utapata kifungua kinywa kitandani kwa sababu sitaki utoke kabisa chumbani.Unatakiwa upate mapumziko ya kutosha.Daktari atakuja baadae kuja kukuangalia unaendeleaje pamoja na kukuchoma sindano” akasema Peniela na jaji Elibariki hakusema kitu alibaki anatabasamu akapanda kitandani .

“ Peniela nashukuru sana.” Akasema jaji Elibariki

“ Unashukuru kwa lipi? Akauliza Peniela


“ Kwa kila kitu kwa namna ulivyonipokea na kwa namna unavyonijali.Nashukuru sana na ndiyo maana nilisema kwamba niko sehemu sahihi ninakotakiwa kuwepo” akasema jaji Elibariki .Peniela akatoa tabasamu pana sana na kusema


“ Wewe ni mtu wangu wa muhimu sana na lazima nikuhudumie.Bila wewe hivi sasa ningekuwa nimekwisha anza kuyazoea maisha ya jela.Mimi ndiye ninayepaswa kukushukuru sana kwa kila kitu ulichonifanyia” akasema Peniela na kumnywesha Elibariki uji halafu akauliza

“Nina hakika mkeo atakuwa katika wakati mgumu sana hivi sasa baada ya kupata taarifa za kilichotokea jana na hajui uko wapi.Kwa nini usimtaarifu kwamba uko sehemu salama ili asiwe na wasi wasi?

“ Usihofu kuhusu hilo Peniela na wala sihitaji ajue niko wapi.”


“ Kwa nini Elibariki? Yeye ni mke wako na anapaswa kufahamu kila kinachokutokea”

“ Sitaki tu afahamu chochote kuhusiana na mahala nilipo.Kubwa ni kwa sababu za kiusalama.Unajua sifahamu ni nani aliyefanya shambulio lile kwa hiyo nahitaji kukaa mafichoni kwa muda .Katika jambo hili ninakuamini wewe tu” akasema jaji Elibariki na mara simu ya Peniela ikaita.Akainuka na kwenda kuipokea


“ Hallow Osmund habari yako? Akasema Penny

“ Habari yangu nzuri.Peniela niliongea na John nikamtaarifu kuhusiana na ombi lako la kutaka kumuona akakubali na akasema kwamba uonane naye jioni ya leo lakini kwa jioni ya leo sina hakika kama itawezekana kwa sababu hivi sasa naelekea uwanja wa ndege kumpokea Dr Burke anatoka Marekani kuja kuangalia afya ya John kwa hiyo basi nitamtuma kijana aje akuchukue asubuhi hii ukaonane na John ili jioni ya leo awe na daktari akifanyiwa uchunguzi.Uko tayari kwenda kuonana naye asubuhi hii? Akauliza Osmund.Peniela akafikiri kidogo na kusema

“ Ndiyo niko tayari Osmund.Nitakwenda kuonana naye” akajibu Penny


“ Ok vizuri basi kuna kijana nimemuelekeza atakuja kukuchukua hapo nyumbani na atakupeleka kwa John “


“ Ahsante sana Osmund kwa msaada wako huo” akasema Peniela

“Peniela kabla sijakata simu nataka kesho tukutane kwa ajili ya kuongelea kuhusu operesheni 26B “


“ Nitaangalia kama nikipata nafasi nitakueleza Osmund” akasema Peniela na kukata simu akamgeukia jaji Elibariki


“ Are you going somewhere? Akauliza jaji Elibariki


“ Utanisamehe Elibariki kuna mtu ninahitaji kuonana naye asubuhi ya leo lakini sintakawia sana.Sipendi kuondoka na kukuacha peke yako lakini ni mtu wa muhimu sana kuonana naye leo hii” akasema peniela


“ Usijali Peniela.Hata hivyo ninajisikia vizuri na hupaswi kuacha shughuli zako nyingine na kunihudumia mimi” akasema jaji Elibariki

“ Usiseme hivyo Elibarki.Wewe ni mtu muhimu sana kwangu na niko tayari kuahirisha kila kitu isipokuwa mtu huyu ni muhimu sana kuonana naye “ akasema Penny


“ Ni mchumba wako? Akauliza Elibariki.Penny akatabasamu na kusema


“ Sina mchumba ..”

“ Usinidanganye Penny.Usione aibu kuniambia kama una mchumba kwa sababu hata mimi ni mume wa mtu na kisheria sitakiwi kuwepo hapa lakini niko hapa kwa sababu mbili kubwa .kwanza kwa usalama na pili ni kwa furaha ya moyo wangu . I feel so happy around you kwa hiyo basi kama una mchumba ni vizuri ukaniambia ili yasije yakatokea kama yaliyotokea siku ile” akasema jaji Elibariki


“ Elibariki naomba naomba unisamehe sana kwa kilichotokea siku ile lakini nitakaueleza kwa undani baade kuhusiana na suala lile “ akasema Peniela


“ Foregt about what happened Penny.Huna haja ya kutoa maelezo yoyote yale.Hata kama ulikuwa na mahusiano yoyote na Jason mimi hayanihusu kwa sababu mwenye uamuzi na maisha yako na nani uwe naye maishani ni wewe mwenyewe lakini ni vizuri kuwa wazi kama uko katika mahusiano na mtu Fulani ili niweze kufahamu na hasa katika kipindi hiki ambacho niko mafichoni” akasema jaji Elibariki.Peniela akasogelea akambusu na kusema


“ Elibariki naomba uniamini sina mahusiano na mtu yeyote Yule.Jason sina mahusiano naye alikuwa akinitaka siku nyingi lakini sikuwa tayari kumkubalia.Unajua nimepitia kipindi kigumu sana baada ya Edson kuuawa kwa hiyo moyo wangu ulikuwa mzito kufunguka kwa mtu mwingine yeyote lakini nashangaa kwa namna ulivyofunguka kwako kiurahisi.Elibariki you are safe here na utakaa hapa kwa muda wowote utakaotaka hata maisha yako yote kama utahitaji” akasema Peniela na wote wakacheka


“ Ninatamani sana kama ningepata nafasi ya kukaa hapa kwa maisha yangu yote lakini tayari niko katika kiapo cha ndoa kwa hiyo siwezi kuishi hapa maisha yangu yote japokuwa ninatamani sana kama ingekuwa hivyo” akasema jaji Elibariki.Penny akanyoosha mkono wake na kuigusa midomo ya jaji Elibariki halafu akasema


“ Marriage is in hearts and not papers.” Akasema Peniela na kumuacha jaji Elibariki na mawazo mengi


*******


Saa nne za asubuhi tayari Peniela alikwisha jiandaa kwa ajili ya kwenda kuonana na John mwaulaya.Dr Jonesia tayari alikwisha fika na kumuona Elibariki na kuridhika kwamba alikuwa anaendelea vizuri akamchoma sindano na kuondoka.

Gari iliyotumwa kuja kumchukua Peniela na kumpeleka kwa John Mwaulaya iliwasili na akamuaga jaji Elibarki.

“ Elibariki nasikitika kukuacha mwenyewe kwa muda lakini sintachukua muda mrefu sana nitarejea baada ya muda mfupi.Usihofu chochote uko salama.Ili kuongeza usalama zaidi nitafunga mitambo ya usalama na kuweka kamera za ulinzi kila kona ili kuweza kuimarisha ulinzi “ akasema Peniela

“ Nashukuru sana Peniela.Usihofu chochote kuhusu mimi niko salama sana.Hakuna yeyote anayweza kufikiri kwamba ninaweza kuwa hapa” akasema Jaji Elibariki na Peniela akambusu akatoka.

“Sielewi ni kwa nini sehemu ya kwanza kufikiria kujificha nilichagua kwa Peniela ? Ningeweza kwenda kwa Mathew ambako ni salama zaidi lakini sielewi ni kwa nini niliacha sehemu hizo zote na kuchagua kuja kwa Peniela.Nilikuwa sahihi kabisa kuchagua kuja hapa kwa sababu pamoja na matatizo niliyonayo lakini ninapata furaha ya ajabu nikiwa na Peniela na kuna wakati ninasahau kabisa kwamba nina matatizo.Moyo wangu haujawahi kujisikia furaha ya namna hii nikiwa na Flaviana.Ninahisi Flaviana hakuwa mtu sahihi kwangu na ndiyo maana ndoa yetu haina furaha hata kidogo.Kila siku mikwaruzano haiishi.Penny ananijali sana na ananifanya nijsikie furaha ya ajabu” akawaza Elibariki akainuka na kwenda dirishani akachungulia nje

“ Ama kweli maisha ni kitu cha ajabu sana.Leo hii nimekuwa mtu wa kujificha ndani na sitakiwi kuonekana nje.Ni akina nani hawa wanaoitafuta roho yangu? Nimewafanya kitu gani hadi watake kunitoa roho yangu? Lakini bado nina uhakika mkubwa sana kwamba kilichotaka kunipotezea uhai ni taarifa ile ya kifo cha Dr Flora.Ninaufahamu ukweli kwa hiyo wanahofu kwamba siri yao haiko salama.Ni nani walimuua Dr Flora na kwa nini? Hiki ni kitendawili ambacho lazima kiteguliwe na ndipo tutakapoweza kupata majibu ni nani anayetaka kuniua,kwani jambio hili limetokea baada tu ya kuufahamu ukweli ” akawaza jaji Elibariki na kurejea kitandani akakaa


“ Yule mwanamke aliyeniokoa ni nani? Sijawahi kumuona hata mara moja na hakutaka hata kujitambulisha kwangu yeye ni nani na kwa nini aliniokoa.Ninahisi ndiye Yule aliyenipigia simu na kunionya kwamba nisipande gari langu.Laiti kama ningemsikiliza ningeweza hata kuokoa maishaya Noah .Endapo nikifanikiwa kumpata mwanamke Yule yeye ndiye anayefahamu kila kitu kuhusiana na mpango wa kuniua na nina hakika lazima atakuwa akiwafahamu watu waliopanga njama ile. Kazi hii nitakabidhi Mathew yeye ndiye mwenye uwezo wa kulichunguza jambo hili.” Akawaza Elibariki halafu akajilaza kitandani

Peniela aliwasili katika makazi ya John.Lilikuwa ni jumba kubwa sana na la kupendeza.Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa Penny kufika mahala hapa.Geti likafunguka wakaingia ndani na gari likaenda kusimama mbele ya jumba kubwa lenye rangi nyeupe.Dereva akashuka haraka haraka na kumfungulia Peniela mlango na kumuongoza kuelekea ndani


“ Nilipokuja siku ya kwanza ilikuwa usiku na sikuushuhudia uzuri wa jumba hili.Dah ni nyumba nzuri sana.” Akawaza Penny huku wakiingia ndani na kupanda ngazi kuelekea ghorofani kilipo chumba cha John Mwaulaya.Yule kijana akagonga mlango wa chumba cha John halafu ukafunguliwa na mtu mwingine aliyekuwa amevaa koti jeupe la kitabibu.Huyu ni kijana mwenye taaluma ya ukadktari naye akiwa ndani ya Team SC41.Alipomuona Peniela akamsalimu kwa heshima kisha akamruhusu aingie ndani na kumuogoza moja kwa moja hadi chumbani kwa John.Uso wa John siku hii ulionekana kuwa na nuru tofauti na siku zilizotangulia


“ Ouh my queen is here” akasema John kwa sauti ndogo na kumfanya Peniela atabasamu


“ Come here.Hug me my queen” akasema John Mwaulaya.Peniela akamsogelea na kumkumbatia pale kitandani

“ Nilikuwa nikihitaji siku nyingi sana kuipata nafasi hii ya kukuona siku moja na kukukumbatia kwani umenifanyia mambo mengi mazuri” akawaza Peniela na kisha akainuka na kuchukua kitambaa.Macho yake yalikuwa yamejaa machozi


“ Unalia nini Peniela? Akauliza John ambaye naye macho yake yalionekana kuwa na machozi


“ Ni miaka mingi nimekuwa nikikuomba nionane nawe nikufahamu lakini umeniruhusu nikuone katika kipindi hiki unachoumwa.Umenihudumia toka nikiwa mtoto mdogo hadi leo hii .Japokuwa sikuwahi kukuona lakini wewe ni zaidi ya baba yangu.” Akasema Penny


“ Peniela usilie tafadhali.Huu ni wakati wa kufurahi na si kutoa machozi” akasema John


“ Ninashindwa kujizuia kutoa machozi kupata nafasi ya kukuona wakati ukiwa katika hali hii.Ninaumia sana kukuona hivi” akasema Penny na mara mlango wa chumba cha John ukafunguliwa akaingia Josh


“ Josh ! naomba unipishe kwanza nina maongezi muhimu na binti yangu Peniela” akasema


“ John ni jambo la muhimu” akasema Josh.John akamfanyia ishara Peniela atoke nje kidogo ili aongee na Josh


“ Mzee ile kazi yako nimeimaliza” akasema Josh


“ Dr Burke is dead? Akauliza John

“ Ndiyo tayari amekwisha fariki.Lakini ilinilazimu kumuua vile vile na Osmund”

“ Good Job.How it happened? Akauliza John


“ Asubuhi ya leo nilimfuatilia Osmund hadi uwanja wa ndege bila ya yeye kufahamu.Alimpokea Dr Burke na kumpeleka katika hoteli aliyompangishia na baada tu ya kuingia katika hoteli hiyo niliwatokea ghafla na bila kupoteza hata sekunde moja niliwamiminia risasi kupitia bastora yenye kiwambo cha sauti kwa hiyo hakuna mtu yeyote aliyeweza kusikia kitu chochote kilichotokea.Dr Burke na Osmund wote wamekufa.Kwa hiyo mzee uko salama.You are safe now” akasema Josh

“ Josh nakushukuru sana kijana wangu.Umeyaokoa maisha yangu.Nina deni kubwa kwako” akasema John Mwaulaya


“ sijali mzee.Siku zote nitakuwa mtiifu kwako “ akasema Josh na kutoka.Peniela akaingia na kumkuta John akiwa na uso wenye furaha sana


“ Nina furaha sana Peniela kwanza kwa kutembelewa na wewe na vile vile kwa kuletewa habari njema na Josh” akasema John

“ Hata mmi ninafuraha sana ya kukutana nawe japokuwa ni kwa muda mfupi kwani Osmund aliniambia kwamba leo kuna daktari anakuja kukufanyia uchunguzi wa afya yako kwa hiyo sitakiwi kuchukua muda mrefu sana.Ninatamani sana kupata muda mrefu wa kukaa nawe ninatamani kukuhudumia hasa katika kipindi hiki unachoumwa na nina mambo mengi ambayo ninahitaji kuongea nawe” akasema Penny


“ Penny usijali kuhusu alichokwambia Osmund.Hakutakuwa na huo uchunguzi wa daktari kama alivyodai.Tafadhali naomba ushinde nami leo hii.Hata mimi nina hamu sana ya kukaa na wewe kuna mambo mengi ambayo nahitaji kukueleza” akasema John


“ Hakutakuwa na uchunguzi wa daktari? Aliniambia kwamba anaelekea uwanja wa ndege kwenda kumpokea Dr Burke.” Akauliza Penny

“ Ugonjwa wangu si wa kutibiwa na Dr Burke.Nahitaji daktari mtaalamu sana wa mishipa ya fahamu.”


“ Kwani unasumbuliwa na nini baba ? akauliza

“ Nina tatizo katika mishipa ya fahamu ya kichwa na ndiyo maana kuna baadhi ya viungo Fulani vya mwili havifanyi kazi sawasawa,”


“ Umepata matibabu gani mpaka sasa hivi? Akauliza Penny


“ Bado sijapata matibabu ya maana mpaka sasa.” Akajibu John


“ Wewe ni kiongozi wa Team SC41 ambayo inafanya kazi ya kulinda maslahi ya marekani kwa nini basi wasikutibu? Marekani kuna hospitali kubwa na nzuri na zenye wataalamu wakubwa sana wanaoweza kuutibu ugonjwa huu.Kwa nini wanakuacha uteseke? Hivi ndivyo team SC41 ilivyo kwamba ukiumwa wanakuacha bila huduma? Akauliza Penny

“Si hivyo Peniela.Jambo hili ni gumu tofauti na unavyofikiri.” Akasema John na kumpa namba Peniela afungue kasiki lililokuwa ukutani na achukue albamu la picha amletee.Peniela akachukua albamu lile kubwa la picha akamletea.Ukurasa wa tatu kulikuwa na picha ya kijana mmoja mtanashati aliyevaa suti nzuri yenye kupendeza akiwa amekaa juu ya jiwe ukingoni mwa bahari


“ Unaiona picha hii? Akauliza John


“ Ndiyo ninaiona” akajibu Penny


“ Huyu kijana unayemuona hapa katika hii picha ni mimi” akasema John.Penny akapatwa na mshangao mkubwa.Kijana Yule aliyeko katika picha ile na John Mwaulaya ni watu wawili tofauti kabisa.


“ This is you? Akauliza Paniela

“ Ndiyo “

“ Mbona hamfanani kabisa “ akauliza Penny


“ Hapa ilikuwa ni kabla ya kujiunga na Team SC41.Wakati huu nilikuwa katika chuo cha kijeshi nchini Marekani nikijifunza masuala ya urubani wa ndege vita.”



“ Wewe ni mwanajeshi? Akauliza Penny

“ Yah nilikuwa mwanajeshi.Wakati nilipopiga picha hii sikuwa na wazo kama siku moja nitakuwa kiongozi wa Team SC41.” Akasema John

“Nilikuwa kijana mtanashati sana nyie vijana mnasema Handsome boy “ akasema John na kumfanya Penny atabasamu


“ IIinilazimu kuibadili sura yangu mara mbili na ndiyo maana unaniona nikiwa katika sura hii ya tofauti kabisa na ile iliyoko katika hiyo picha.” Akasema John

“ Kitu gani kilisabababisha ukabadilisha sura yako? Akauliza Penny


“ Penny ni mambo mengi sana makubwa yametokea ndani ya Team SC41 na ndiyo maana nkalazimika kuibadili sura yangu mara mbili .Nilianza kusumbuliwa na ugonjwa huu baada ya kufanyiwa upasuaji wa pili wa kuibadili sura.”


“ Kitu gani kilipeleka ukabadili sura yako ? akauliza Peniela


“ Penny kuna mambo mengi sana ambayo huyafahamu na ninatamani sana kukueleza lakini ninashindwa kwa sababu Team SC41 si sehemu sahihi unayostahili kuwepo.”

Peniela akamtazama John na kusema


“ Bado hujanieleza ni kwa nini team Sc41 wameshindwa kukupatia matibabu?akauliza tena Penny

“ Its because I’m dead “

“ You are dead? Akauliza Penny kwa mshangao

“ Yes I’m dead” akasema

“ Ninashindwa kuelewa baba John umekufa vipi?

“ Ngoja niliweke hivi ili unielewe.Ni kwamba kwa miaka kadhaa sasa hivi ninajulikana kwamba nimekwisha fariki.Mimi ni mtu niliyekuwa nikitafutwa sana na serikali mbalimbali duniani kwa hiyo nililazimika kutumia njia hii ya kutengeneza kifo changu ili nisiendelee kutafutwa na ndiyo maana kuna ugumu mkubwa kwa mimi kutibiwa hapa nchini na nje ya nchi”akasema John

“ Kitu gani kilisababisha utafutwe? Akauliza Peniela

“ Nilifanya jambo kubwa sana ambalo sintaweza kukueleza” akasema John


JOHN MWAULAYA ALIFANYA JAMBO GANI KIASI CHA KUTAFUTWA NA SERIKALI MBALI MBALI DUNIANI? ENDELEA KUIFUATILIA SIMULIZI HII…

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...