SIMULIZI: PENIELA (Season 2 Ep 10)

 ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

Baada ya kumtesa sana Sabina aliwaambia kwamba kitu hicho alikupatia wewe umfichie na siku ile alipokupigia na kukutaka umsaidie alipewa simu ili awasiliane nawe.Baada ya hapo walianza kukufuatilia ili wakufahamu nyendo zako na ili kulifanikisha hilo wakamtumia mtaalamu mmoja wa program za kompyuta kutengeza programu itakayowawezesha wao kukufuatilia na leo hii ndiyo maana walikuwa wanakufuatilia ili waweze kutega kifaa katika gari lako cha kuweza kukufuatilia.Kwa hiyo Eva Sababu kubwa iliyowafanya wakufuatilie ni hiyo .Kuna kifaa anacho Sabina na walikuwa wakikihitaji sana.” akasema Mathew na kumuacha Eva akishangaa

“ Eva ni kweli kifaa hicho Sabina alikukabidhi umfichie? Akauliza Mathew

“ Hapana hakunipa.Yawezekana kuna mahala kwingine amekiweka kwa sababu mimi wala sina mazoea naye ya kufikia hatua hiyo.Mimi ninamfahamu kama mteja mzuri wa baa yangu.Ni kitu gani hicho wanachikitafuta hawa jamaa?

“ Eva ni hadithi ndefu sana tutaongea baadae.Kinachotakiwa kwa sasa ni kujitahidi Sabina apate fahamu na atueleze ni wapi alikokiweka kitu hicho.Kwa sasa naomba nenda kamsaidie daktari .Nina maongezi na Anitha” akasema Mathew.Alipohakikisha Eva ametoka Mathew akasema

“ White house killed Edson” akasema Mathew baada ya Eva kutoka mle chumbani.

“ Ouh my God ! Anitha akashangaa

“ Anitha suala hili si suala dogo kama tulivyokuwa tunalifikiria.Ni jambo kubwa na zito” akasema Mathew na wote wakabaki kimya.


ENDELEA………………

“ Mathew I’m so scared.What real happened? Who ordered him killed? Akauliza Anitha

Mathew akamueleza kila kitu alichokipata toka kwa yule jamaa.

“ Dah ! kwa kweli suala hili si dogo kama ulivyosema.Sikufikiria kabisa kama jambo hili linaweza kuwa namna hii.Kwa maana hiyo Elibariki alikuwa sahihi kabisa kumuachia huru Peniela kwani alibambikiwa tu ile kesi.Kuna kitu alikihisi hakikuwa sawa na ndiyo maana akatutaka tufanye uchunguzi” akasema Anitha

“ Hata mimi kutoka mwanzo nilihisi kuwa lazima kuna sababu nzito iliyopelekea kifo cha Edson” akasema Mathew 

“ Kwa hiyo baada ya kufahamu nani waliomua Edson,nini kinafuata? Akauliza Anitha

“ Kinachofuata ni kitu ambacho sikuwa nikitaka hata kukifikiria.”

“ Ni kitu gani Mathew?

“ We’re going to deal with white house.”

Anitha hakujbu kitu akabaki anamuangalia Mathew. hata yeye mwenyewe alitishika

“ Edson aliuawa na watu toka ndani ya Ikulu ,hilo tumekwisha lifahamu.Lakini hatuwezi kuishia hapo.Lazima twende mbali zaidi.Kwanza lazima tukipate hicho kitu alichokiiba na kilichopelekea yeye kuuawa.Nina hakika kabisa mpaka ifike hatua ya kumuua lazima kitu hicho kitakuwa ni kikubwa sana.Nina uzoefu wa kutosha na mambo ya ikulu kwani nimewahi kushughulika na kesi kadhaa kuhusiana na ikulu na ndiyo maana nina uhakika mkubwa kwamba kitu hicho hakitakuwa kidogo.”



“ Mathew unahisi kitu hicho kinachoongelewa inaweza kuwa ni siri Fulani? Akauliza Anitha

“ Inawezekana kabisa ikawa ni siri Fulani au nyaraka Fulani za siri.Ukumbuke kwamba Edson alikuwa akifanya kazi katika idara ya mawasiliano Ikulu kwa hiyo inawezekana kuna siri Fulani aliiba .Nina uhakika huo lakini tutajua kila kitu baada ya kukipata kitu hicho.Lakini tukae tukijua kwamba hatua inayofuata lazima tuingie katika lile jumba jeupe.Kule ndiko kuna majibu ya kila kitu.na tukianza kulichunguza jumba lile it’s a victory or death ” akasema Mathew

“ Vipi kuhusu Peniela na Team SC41? Akauliza anitha

“ Kwa sasa tuna hakika kwamba Peniela hakuhusika katika mauaji yale ya Edson lakini tumeshukuru kwani ametufanya tukagundua kuhusu uwepo wa Team SC41.Yeye pia tutamchunguza ili tufahamu kama anahusika na Team SC41.Tutakapopata majibu ya uchunguzi wetu tutahamia kwa Team SC41.Halafu kuna kitu ambacho tunatakiwa tukifahamu pia kuna huyu mtu ambaye ni mnunuzi wa kifaa hicho anaitwa Habib Soud toka Saudi Arabia .Tunatakiwa tumfahamu ni nani na pengine tunaweza tukagundua kitu toka kwake.Zitafute habari zake ili tumjue” Akasema Mathew na kutoa simu yake akazitafuta namba za Elibariki akapiga lakini simu yake haikuwa ikipatikana,

“ Elibariki na Noah wako wapi?Mbona simu ya Elibariki haipatikani? Inawezekana Noah akawa amemshawishi wapiti sehemu ya burudani.Ninamfahamu vizuri Noah ni mtu wa starehe sana.” Akasema Mathew

“Muache atulize akili kwa sababu tuna kazi kubwa mbele yetu” akasema anitha huku akikaa katika kompyuta yake

“ Anitha wakati unaendelea kutafuta taarifa za Habin mimi ngoja nikamsukume daktari amuamshe Sabina haraka ili aweze kutuonyesha mahala alikokificha hicho kitu.Hatuna muda wa kusubiri sana.Ukipata chochote kuhusiana na Habib utanitaarifu” akasema Mathew na kutoka akaelekea sebuleni ambako daktari alikuwa amemtundikia Sabina chupa ya maji iliyokuwa na dawa ya kuweza kumpa nguvu kwani alikuwa amedhoofu sana.

“ anaendeleaje Sabina” akauliza Mathew

“ kwa sasa nimemtundikia chupa ya maji na nimechoma dawa ya kuweza kumpa nguvu kwani hali yake ni kama unavyoiona amedhoofu sana” akasema daktari

“ Anaweza akachukua muda gani hadi kupata nafuu? Akauliza Mathew

“ Siwezi kuwa na uhakika lakini anaweza akachukua siku mbili hadi tatu ili kuweza kurejea katika hali yake ya kawaida” akasema daktari.Mathew akamuomba Eva waongee pembeni

“ Unasemaje Mathew? Akauliza Eva

“ Eva kuna jambo ambalo sikuwa nimekutaarfu.Ni kwamba nimegunduda kwamba Sabina ana uhusiano na suala ambalo nilikuwa ninalichunguza.Kwa sasa tayari tumepata mwanga Fulani lakini tunahitaji kulichimba zaidi suala hili.Kwa hiyo basi nitahita kikukifahamu kitu hicho ambacho amekificha mahala ambacho hawa jamaa walikuwa wakikihitaji”

“ Hizo ni habari njema sana Mathew.Siku nyingine usikatae kutoa msaaa ukiombwa” akasema Eva

“ Ndiyo Eva ni habari nzuri lakini kuna jambo ambalo lazima lifanyike”

‘ jambo gani Mathew?

“Sabina anatakiwa aamshwe haraka ili tuweze kumuhoji atuonyeshe ni wapi alikokihifadhi kifaa hicho” akasema Mathew

“ Sabina hajitambui na amedhoofu sana.Tutamuamshaje?

“ Kuna sindano ambayo atachomwa na itamuamsha lakini ni ya hatari sana inaweza ikamsababishia kupoteza maisha.Kwa hiyo basi lazima tufanye maamuzi magumu”

“ No Mathew.Hatuwezi kufanya jambo kama hilo kwa huyu binti.Hebu muangalie namna alivyodhoofu.Muonee huruma Mathew”

“ Eva kazi yako ni nyepesi na nina hakika haujawahi kukutana na mikiki mikiki kamahii.Kazi ninazozifanya mimi zinahitaji moyo wa chuma,na tunapokuwa katika kazi kama hizi moyo wa huruma hutoweka na tunavaa moyowa ujasiri.Lazima tufanye maamuzi magumu kwa ajili ya kupata kitu muhimu na kwa sasa kitu muhimu tunachikihitaji ni hicho alichokificha Sabina.Hakuna namna nyingine tunayoweza kufanya kukipata kitu hicho kwa haraka zaidi ya njia hiyo niliyokwambia” akasema Mathew

“ Hapana Mathew,sikubaliani nawe hata kidogo.Hatuwezi kumfanyia Sabina ukatili wa namna hii .Sabina yuko katika mikono yangu na lazima tumsubiri hadi hapo atakapopata nafuu ndipo tuweze kumuhoji taratibu na atueleze mahala alipoweka hicho kifaa.Huyu si mhalifu na hatuwezi kutumia nguvu katika kumuhoji.” Akasema Eva.Mathew akainama akafikri kidogo kisha akasema

“ Eva hebu twende huku nikuonyeshe kitu” akasema Mathew wakaongozana na Eva hadi katika chumba fulani kilichoonekana kama chumba cha kulala .Kulikuwa na kitanda cha chuma na meza moja ndogo.

“Nisubiri hapa ninakuja” Mathew akatoka na baada ya dakika mbili akarejea .

“ Kuna nini humu Mathew? Hiki chumba ni cha nini? ” akauliza Eva lakini kabla hajajibiwa akajikuta amegeuzwa na kukabwa na kutahamaki akajikuta akiwa amefungwa pingu mkononi .alipojaribu kujitetea akapigwa kofi kali linalompeleka mpaka chini na mikono yenye nguvu ya Mathew ikamuinua na kumtupa kitandani na kuifunga pingu ile katika chuma cha kitanda.

“ You will stay here” akasema Mathew

“mathew !!!!!!!..akapiga ukelele Eva

“ Mathew nifungue tafadhali!!...

Mathew hakuzijali kelele zile akatoka na kufunga mlango kwa funguo

“Ninapokuwa katika shughuli nzito kama hizi huwa sina urafiki na mtu yeyote yule.” Akawaza Mathew kisha akaoka ndani ya kile chumba na kukifunga kwa funguo akaelekea sebuleni

“ Daktari kuna jambo moja naomba tuongee” akasema Mathew

“ Jambo gani kaka? akauliza daktari

“ Msichana huyu ana taarifa nyeti sana ambayo tunaihitaji kwa haraka .Ninataka umuamshe walau kwa dakika mbili tu atueleze mahala alipoweka kitu hcho tunachokitafuta”

“ Kaka hilo haliwezekani.Hakuna namna tunayoweza kufanya ili kumuamsha.Hali yake si nzuri hata kidogo na amedhoofu sana.Ninakushauri tuendelee kusubiri hadi hapo atakapopata nafuu.Bila hivyo hakuna namna nyingine ya kufanya ili kuweza kumuamsha “akasema daktari.Mathew akatoka pale sebuleni akaelekea chumbani kwake na baada ya dakika tatu akarejea akiwa na kichupa cha dawa

“ Daktari mchome dawa hii na ataamka” akasema Mathew na kumpatia yule daktari kile kichupa cha dawa ambaye alibaki anashangaa

“Unashangaa nini ? Fanya nilivyokwambia” akasema Mathew.Daktari yule akakichukua kile kichupa cha dawa akakisoma halafu akamgeukia Mathew

“ Hapana siwezi kumchoma mgonjwa kama huyu hii dawa.Ni hatari sana.Umeitoa wapi kwanza? Akauliza yule daktari kwa mshangao

“ Daktari tafadhali usitake kufahamu nimeitoa wapi lakini fanya ninavyokueleza ufanye” akasema Mathew kwa ukali

“ Hapana siwezi kufanya hivyo” akasema yule Daktari.Mathew akakasirika sana

“ Siku zote huwa sitaki mtu yeyote anikwamishe katika kazi yangu” akawaza na kwa kasi ya ajabu akaichomoa bastora na kumuelekezea yule daktari.

“ Sitaki mabishano na wewe tena .Usiku huu tayari nimekwisha ua watu wanne kwa hiyo nihesabu mpaka tatu na kama ukikaidi basi nitakifumua kichwa chako kwa risasi..One…” akasema Mathew

“ two”…akasema huku bastora yake ikiwa imeelekezwa kwa daktari

“ Ok kaka ntafanya unavyotaka lakini naomba ufahamu kwamba ni hatari sana kufanya hivi na mgonjwa anaweza akapoteza hata maisha”

“ Go ahead do it” akasema Mathew.

Daktari akachukua dawa na kuivuta katika bomba halafu akamchoma Sabina.Baada ya dakika kama mbili hivi Sabina akafumbua macho.Mathew akasogea pale kitandani

“ Sabina,Sabina..!! akaita Mathew Sabina akamtazama halafu akafumba macho

“ Sabina ! Sabina ! akaita tena Mathew na Sabina akafumbua macho na kumtazama Mathew na kisha akaitika kwa sauti dhaifu

“ Sabina usihofu uko katika mikono salama,tumekuokoa kutoka katika mikono ya wale jamaa waliokuwa wamekuteka.Usihofu uko huru sasa” akasema Mathew

“ Niko wapi? Akauliza Sabina kwa sauti ndogo

“ Uko sehemu salama.Sabina naomba uniambie umeuficha wapi mzigo uliopewa na mzee Kitwana? Akauliza Mathew

“ Siufahamu mzigo.wo..w..”

akasema Sabina

“ Ouh my gosh this is not going to work” akawaza Mathew halafu akatoka mbio na kuelekea katika chumba alichomfungia Eva akafungua mlango na kumkuta Eva amejilaza kitandani

“ Eva,Eva..! akaita Mathew Eva akamtazama kwa macho makali

“ Eva listen to me” akasema Mathew

“Go away Mathew..You are a monster’ akasema Eva

“ Eva naomba unisikilize.Sabina ameamka.Ni wewe tu ambaye anaweza akakueleza mahala alipouweka mzigo aliopewa na mzee Kitwana.Hatuna muda mrefu.Tafadhali naomba twende ukaongee naye.This is very important”akasema Mathew huku akimfungua Eva na kumshika mkono wakaongozana hadi sebuleni.Eva akamunamia Sabina

“ Sabina..Sabina ! akaita Eva.Sabina akafumbua macho na kumtazama Eva akamtambua

“ Eva..! Umekuja…Niko wapi hapa? akasema Sabina kwa sauti dhaifu

“ Sabina naomba unisikilize.Tumekuokoa kule ulikokuwa.Uko sehemu salama.Naomba uniambie ule mzigo uliopewa na mzee Kitwana uko wapi? Akauliza Eva lakini Sabina hakujibu kitu akafumba macho.Eva akamtikingisha

“ Sabina tafadhali naomba uniambie.Mzigo uleuko wapi? Sabina akamfanyia ishara amuinamie.Eva akamuinamia Sabina akamnong’oneza kitu sikioni halafu Eva akainuka

“ Anasemaje? Mzigo uko wapi?akauliza Mathew

“ Amenielekeza mzigo huo ulipo.Ameuficha kwa bibi yake amesema nikauchukue niufiche.”

“ Ok good.Hatuna muda wa kupoteza.Tunakwenda sasa hivi kwenda kuuchukua mzigo huo kwa bibi yake.” Akasema Mathew halafu akaelekea katika chumba alimo Anitha

“ Anitha tumekwisha fahamu mahala Sabina alikouficha mzigo.Tunakwenda kuuchukua wewe utabaki hapa na kuangalia nyumba kwani Noah hayupo.Hatutakawia sana.Ukipata chochote utanifahamisha kwa simu”akasema Mathew na kurejea sebuleni

“ Eva tunaongozana wote kwenda huko alikokuelekeza “ akasema Mathew

“ Hapana siongozani nawe Mathew.Nitabaki hapa kumuangalia Sabina.” Akasema Eva

“ Eva hili si ombi.Hii ni amri.’ Akasema Mathew .Eva tayari alikwisha muogopa Mathew kwa hiyo hakuweza kukataa.

“ Nadhani na mimi nimekwisha maliza kazi yangu .Ninaondoka pia” akasema yule daktari ambaye kijasho kilikuwa kinamtoka.Kitendo cha kunyooshewa bastora na Mathew kilimuogopesha mno

“ No ! Utabaki hapa hadi tutakaporudi.Endelea kumuangalia mgonjwa na hakikisha amepata nafuu” akasema Mathew kwa ukali

“ Huyu mgonjwa hali yake si nzuri na sitaki apoteze maisha katika mikono yangu”

“ Nimekwambia utamuhudumia na utahakikisha anakuwa salama .Ukikaidi maagizo yangu hautatoka salama ndani ya nyumba hii” akasema Mathew na daktari yule hakuwa na la kusema zaidi ya kukubaliana na matakwa ya Mathew.

Mathew na Eva wakaingia garini na kuondoka

“ Mathew you are a monster.Sikutegemea hata siku moja kama unaweza ukafanya kitu kama kile.Sikutegemea kama unaweza ukawa mkatili namna hii” akasema Eva wakiwa garini

“ Ni kwa sababu hujawahi kunikuta nikiwa kazini.Ninapokuwa kazini huwa si yuleMathew unayemfahamu” akasema Mathew

“ Pamoja na hayo Mathew kwa nini ufanye vile kwa binti yule ambaye hana kosa lolote? Nimeumia sana naomba ulifahamu hilo and I’ll never trust you again”

“ Sabina ana kitu muhimu ambacho tunakihitaji kwa hiyo lazima itumike kila mbinu kukipata.kazi zetu ndivyo zilivyo.Wewe ulitaka nikusaidie kumkomboa na nimefanya hivyo kwa hiyo kwa sasa ninaendel ea na shughuli zangu.” Akasema Mathew 


*******


Dr Kigomba aliwaacha Flaviana na ndugu zake wakiwa nje ya jengo la kuhifadhia maiti akasogea pembeni mahala kusikokuwa na watu akachukua simu yakena kumpigia Dr Joshua.

“ Nipe ripoti Kigomba.Ni mwenyewe ? akauliza Dr Joshua

“No Mr president.Its not him”akasema Kigomba .Dr Joshua akavuta pumzi ndefu.

“ Now its going to get ugly” akasema Dr Joshua.Kimya kifupi kikapita akasema

“ You’ve failed me once again Dr Kigomba.Kutoka na kukosa umakini katika kazi sasa inatubidi tuongie tena katika kazi nyingine ya kuanza kumtafuta Elibariki”

“ mzee hili suala la kunilaumu mimi.Kila kitu kilikwenda kutokana na mipango namna tulivyokuwa tumeipanga kwa hiyo kushindwa kufanikiwa si kwa uzembe”

“ Kigomba rudi haraka hapa tulijaridi suala hili .Hatuwezi kuongea simuni suala zito kama hili” akasema Dr Joshua

“ Ok mzee tunarudi sasa hivi” akasema dr Kigomba na kuwataka akina Flaviana waingie garini waondoke

“ Ninahisi kama akili yangu haifanyi kazi tena” akawaza Flavian akiwa garini

“ Kabla hata mama hajazikwa linatokea tena jambo lingine.Nani waliomshambulia mume wangu? Elibariki yuko wapi? Akaendelea kujiuliza maswali mengi

“ Yule mtu aliyekuwa na gari la Elibaiki ni nani ? Ouh Mungu wangu naomba unisaidie naona akili yangu imefika mwisho wake na kufikiri.Kichwa changu kimejaa maswali mengi ambayo hayana majibu.Tukio zima la kushambuliwa gari la mume wangu linachanganya sana na sijui ni wapi nitapata majibu ya kweli kuhusiana nini kilitokea na mume wangu yuko wapi ” akaendelea kuwaza Flaviana

Aliwaza mambo mengi sana na namna ambavyo wamekuwa wakigombana na mume wake machozi yakaendelea kumtiririka.

“ Sijui nitafanya nini endapo Elibariki atakuwa amekufa.Japokuwa tumekuwa tukilumbana mara kwa mara lakini toka ndani ya moyo wangu ninampenda sana Elibariki.Sijui maisha yangu yatakuwaje bila yeye.” Machozi mengi yakaendelea kumtoka ,Anna akajitahidi kumtuliza

“ lakini nini dhana ya shambulio lile? Ni mume wangu ndiye aliyekuwa akilengwa kuuawa? Kama ni hivyo ni nani basi waliotaka kumuua na kwa nini ? Kikubwa zaidi ninachotaka kukifahamu sasa hivi mume wangu yuko wapi , is he ok? Flaviana akaendelea kujiuliza maswali yaliyokosa majibu

“ Itamlazimu baba atumie vyombo vyake kumtafuta mume wangu na tujue yuko wapi na kama yuko hai ama vipi.Ninapatwa na wasiwasi sana kuhusiana na maisha ya mume wangu.” Akawaza Flaviana

Walirejea nyumbani na bila kupoteza muda Flaviana akamuomba baba yake waongee katika chumba cha maongezi ya faragha.

“ Baba ,mtu aliyeuawa ndani ya gari la mumwe wangu si Elibariki.Inasikitisha sana kwa namna walivyomchakaza kwa risasi .Wamemuua kinyama sana.Watu waliofanya shambulio lile wana roho za kishetani.Ninachohitaji kufahamu hivi sasa ni mahala alipo mume wangu.Dady nina wasi wasi sana na maisha ya Elibariki na sijui mahala aliko.Ni vigumu kuamini kwamba Elibariki hakuwemo ndani ya ile gari kwa sababu nimeongea naye mimi usiku huu na nusu saa baadae gari lake linashambuliwa.Baba nina wasi wasi sana na usalama wa maisha ya Elibariki”akasema Flaviana

“ Flaviana mstuko ulioupata hata mimi umenipata pia.Tukio hili limenistua sana lakini kitu cha kutia faraja ni kwamba hajakutwa ndani ya hilo gari .Kwa maana hiyo basi tuna uhakika kwamba atakuwa hai .Tunachotakiwa kufanya kwa sasa ni kumtafuta mahala aliko.Nina hakika kuna sehemu yupo na kama amepata taarifa kwamba gari lile limeshambuliwa basi anaweza asijitokeze mapema.Kazi anayoifanya mumeo inamfanya awe na maadui wengi ambao hawaridhishwi na hukumu anazozitoa kwa hiyo matukio kama haya kwa majaji ni kitu cha kawaida na ndiyo maana huwa tunawapatia ulinzi lakini nashangaa yeye Elibariki anaendesha gari lake mwenyewe bila ulinzi na wala bila dereva.Ninachokuomba kwa sasa kaa, tulia na uniachie mimi kazi hiyo.Sina wasi wasi kabisa kwamba Elibariki atakuwa amekufa.Lazima yuko mahala na vyombo vyangu vitafanya kazi ya kumtafuta tutampata tu.” Akasema Dr Joshua

“ Baba nitawezaje kukaa wakati sifahamu mume wangu aliko? Kwa nini mambo haya yanatutokea sasa ? kabla hatujamaliza hili linaibuka hili.Kwa nini dady?akauliza Flaviana

“ Flaviana ninakuhakikishia kwamba nitatumia vyombo vyote vya usalama unavyovifahamu kumtafuta mumeo kuwatafuta watu waliofanya kitendo kile.Nakuhakikishia kwamba hakuna ambaye ameshiriki katika shambulio lile atabaki huru.Lazima wote wapitiwe na mkono wa sheria.” Akasema Dr Joshua na kidogo Flaviana akapata faraja .

“ Dr Kigomba amefanya uzembemkubwa sana.Suala lile halikuwa la kuchukulia kirahisi rahisi kama alivyolichukulia.Kwa sasa amesababisha tatizo jingine kubwa.Ametupa tena kazi ya kumsaka Elibariki na kufahamu mahala aliko.Elibariki anaufahamu ukweli wa nini kilimuua Flora na tukio la leo litamfanya aamini kabisa kwamba anatafutwa auawe kutokana na kuufahamu ukweli. Kigomba ndiye aliyesababisha haya yote.” Akawaza Dr Joshua akiwa amekasirika sana

“ lakini inawezekanaje Elibarik i asiwemo ndani ya hilo gari ? Kuna mtu alimpa taarifa? Na huyo mtu ambaye alikuwa akipambana na vijana wetu ni nani? Akajuliza Dr Joshua

“ hapa lazima kuna jambo linaloendelea.Lazima ufanyike uchunguzi wa kina kubaini ni kitu gani ambacho kinaendelea.hainiingii akilini kwamba Elibariki asiwemo ndani ya gari wakati vijana wamemfuatilia toka alipotoka hapa.Kama hakuwemo ndani ya gari yuko wapi? Uchunguzi wa kina unahitajika katika jambo hili.” Akawaza Dr Joshua


TUKUTANE SEHEMU IJAYO……

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...