SIMULIZI: PENIELA (Season 1 Ep 32)
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITRA
“ Hapana.Nisingeweza kufanya hivyo”
“ Kama ni hivyo na mimi naungana nanyi.Ninaweza kulenga shabaha vizuri,naninajua kutumia bastora.Ninaweza kupambana” akasema Dr Michael.
Mathew akaenda chumbani kwake akachukua silaha na vitu vingine ambavvo aliona vitamsaidia katika kazi ile halafu akampatia Dr Michael fulana ya kuzuia risasi pamoja na bastora moja na kisha akaenda sebuleni na kumrushia Kanali Adolf bastora
“ we’re going out.”
“ Out where?
“ To rescue a woman.get ready ” akasema Mathew na kumfuata Anitha
“ Anitha tunakwenda kumchukua mke wa Dr Michael.Tunakutegema sana wewe katika operesheni hii.I promised to get his wife back and that’s what we’re going to do..” Akasema Mathew na kuchomeka sikioni kifaa cha mawasiliano akajaribisha na kuona kiko sawa
“ Usihofu Mathew kila kitu kimekaa sawa.Nitaona kila kitu kutokea hapa kwa kutumia satellite.” Akasema Anitha
Mathew,Noah ,Dr Michael na kanali Adolf wakaingia garini na kuondoka .
ENDELEA…………………..
Peniela akiongozwa na yule jamaa wa miraba minne walifika katika mlango mmoja mkubwa wenye nakshi za kupendeza.Nje ya mlango ule kulikuwa na watu wanne wenye kuvalia suti nyeusi kila mmoja.Kama ilivyokuwa kwa watu wengine aliokutana nao katika jengo hili,watu wale pia walionyesha heshima kubwa sana kwake.Penny aliendelea kushangaa kwa kitendo kile cha kupewa heshima kubwa namna ile na watu wale ambao hakuwahi kuonana hata na mmoja wao.
“ Hello Peniela” akasema mmoja wa wale jamaa waliokuwa wamesimama mlangoni huku akimpa Penny mkono
“ Hallow” akasema penny .Alikuwa nwasi wasi sana lakini alijitahidi kwa kadiri alivyoweza asionyeshe aina yoyote ya wasi wasi mbele ya watu wale
“ karibu sana penny.Nadhani ni mara ya kwanza tumeonana ana kwa ana.Mimi ndiye Code is 00P688 na kwa jina naitwa Osmund mgano.Yule pale ni Victor Alfred,anayefuatia ni Bashir Hussein,Amani sufa,na yule pale ni Ezekiel Sadoe.” Akasema Osmund.
“ Nafurahi kuwafahamu” akasema Penny.Osmund akafungua mlango na kumkaribisha Penny
“ karibu ndani Penny.Tafadhali usiogope” akasema Osmund na Penny akaingia ndani na kukutana na sebule moja kubwa na nzuri yenye samani za kuvutia.Akatabasamu kwa uzuri wa sebule ile.Osmund akamkaribisha sofani akaketi.
“ Penny ,nafahamu utakuwa ukijiuliza ni kwa nini leo tumeamua kukuita mahala hapa.Kwa miaka mingi umekuwa ukipata maelekezo yetu kwa kupitia simu na leo imetulazimu kukuita ili tuonane ana kwa ana.” Akasema Osmund akamtazama Penny kwa sekunde kadhaa kisha akaendelea
“ Hapan ndiyo makao yenu makuu? Akauliza Penny
“ Hapa si makao yetu makuu ,ila hapa ndipo anapoishi mkuu wetu ambaye ndiye anayetaka kuonana nawe leo hii.Ni mgonjwa sana na anatarajiwa kufanyiwa upasuaji muda wowote lakini kabla ya kufanyiwa upasuaji huo anahitaji kukuona,kuna jambo anataka kuongea nawe” Akasema Osmund halafu akasimama
“ Naomba sasa bila kupoteza wakati nikupeleke kwa mkuu wetu ana jambo la kuongea nawe” akasema na kuanza kupiga hatua Penny akamfuata.Walifika hadi katika mlango mmoja wenye rangi nyeupe ,Osmund akasimama na kugonga mara tatu,mlango ukafunguliwa na mtu mwenye mavazi ya kidaktari.Osmund akaongea naye kwa sekunde kadhaa halafu mtu yule akatoka nje na kisha Osmund na Penny wakaingia ndani ya chumba kile kikubwa cha kulala.Macho ya penny yakatua katika kitanda kikubwa alichokuwa amelala mtu mmoja aliyeonekana mgonjwa sana huku akiwa ametundikiwa chupa ya maji .Pembeni ya kitanda chake kulionekana mashine kadhaa na zote zikiwa zimeunganishwa mwilini mwa yule mtu aliyekuwa amelala pale kitandani.Penny alimtazama mtu yule lakini hakuweza kumtambua.Hakuwahi kuonana naye hata mara moja.
“ Huyu mtu ni nani? Sijawahi kuonna naye hata mara moja.Anataka kunieleza nini? Akajiuliza .Osmund akakisogelea kitanda cha yule mgonjwa akamuinamia na kuongea naye kidofo galafu akabonyeza kitufe Fulani ukutani na sehemu ya juu ya kitanda ikanyanyuka yule mgonjwa akaweza kukaa.Penny akamtazama vizuri ,alikuwa ni mzee ambaye kwa kukadiria umri alipata miaka themanini au zaidi ya hapo.Alionekana dhaifu sana.Akamuomba Osmund ampatie miwani yake akavaa .Osmund akamsogelea Penny na kumwambia
“ Penny ,huyu ndiye kiongozi wetu.Ni mgonjwa sana ,anaomba kuongea nawe mambo kadhaa.Tafadhali jitahidi kumsikia kwa makini kile atakachokwambia.Ni mtu anayefahamu mambo mengi sana usimuogope” akasema Osmund na kumshika mkonoPenny akamsogeza karibu na kitanda cha yule mgonjwa akamvutia kiti akakaa.Moyo ulikuwa ukimdunda hakujua yule mzee alitaka kumweleza kitu gani.Yule mzee akageuza shingo na kumtazama Penny akamfanyia ishara asogee karibu
“ Come closer” akasema kwa sauti ya chini.Penny akamsogelea karibu
“ Nipe mkono wako” akasema.Penny kwa uoga akausogeza mkono wake yule mzee akaushika halafu akaonekana kuzama katika mawazo
“ Peniela !..akasema kwa sauti ndogo.
“ I’m glad to meet you before my last breath.”akasema yule mzee halafu akafumba macho yake kana kwamba kuna jambo analifiki kisha akasema
“ I’m sick and I’m going to die soon my princess lakini nimeona kabla sijafa nikuite kuna mambo ya muhimu ambayo natakiwa nikueleze”.
Akanyamaza akafumba tena macho akafikiri halafu akasema
“ Ninaitwa John Mwaulaya.Mimi ndiye kiongozi wa team SC 41 ,kikosi ambacho unafanya nacho kazi.Mimi ndiye niliyekuwa nikiwasiliana nawe kwa miaka hii yote hadi niliposhindwa kuhimili majukumu yangu kutokanana afya yangu kuwa mbovu.” Akanyamza kidogo akafumba macho kwa sekunde kadha halafu akaendelea
“ Mimi ndiye ambaye nimekuwa nikikuangalia toka angali ukiwa mchanga hadi hivi sasa japokuwa hukunifahamu.Peniela una historia ndefu sana na ambayo siwezi kukueleza kila kitu kwa sasa.Kuna mambo mengi ambayo huyafahamu kuhusu wewe na hakuna yeyote anayefahamu zaidi yangu.” Akasema John na macho ya Peniela yakalengwa na machozi.Mtu yule ambaye alikuwa na hamu kubwa ya kumuona na ambaye amekuwa akiongea naye simuni kwa miaka mingi leo hii amefanikiwa kuonana naye ana kwa ana.
“ hatimaye leo nimekuona ana kwa ana John mwaulaya.Sikuwa nikikufahamu hata kwa jina.Nilikufahamu kwa sauti tu.Nina maswali mengi sana ambayo unatakiwa unipatie majibu yake? Akawaza Penny
“ Penny natamani sana nikueleze wewe ni nani na umefikaje hapa ulipofika lakini sina nguvu tena,sina uwezo wa kuongea kwa muda mrefu..” Akasema John halafu akamuomba penny azunguke upande wa pili wa kitanda,akamtajia namba za kufungulia kasiki lililokuwa ukutani,baada ya kubonyeza namba zile kasiki lile likafunguka na ndani yake kulikuwa na vitu vingi.Akamuelekeza achukue kasha lenye nakshi za dhahabu.Penny akalitoa kasha lile akalitazama halafu akalifunga lile kasiki.
“ Peniela,ndani ya kasha hilo kuna kila kitu kinachokuhusu wewe.Thats who you are.”akasema John.
“ John,mbona sielewi? Akauliza Penny
“ Ndani ya hilo kasha kuna kila kitu kinachohusiana na wewe,kuna kila kitu kinachoelezea wewe ni nani.Historia nzima ya maisha yako iko humo ndani ya hilo kasha,kwa hiyo nakuomba ulitunze kama mboni ya jicho lako.Ukilipoteza na kila kitu chako kimepotea.Nimelitunza kwa miaka mingi kwa hiyo na wewe litunze sehemu salama.Watu wanalitafuta kasha hilo na wakilipata you are finished my princess so.Kwa hiyo lilinde kwa kila namna unavyoweza.” akasema John.Penny akalichunguza kasha lile lilikuwa limefungwa
“Mbona limefungwa ? Funguo yake iko wapi? Akauliza
“ Nitakuelekeza namna utakavyoweza kuipata funguo lakini kwanza kuna jambo la muhimu sana nataka kukwambia.” Akanyamaza akafumba tena macho kwa sekunde kadhaa halafu akasema.
“Nilikuingiza katika kazi hii kwa sababu niliamini ndiyo kazi sahihi kwa wewe kuifanya.Kwa mara ya kwanza katika maisha yngu najutia uamuzi wangu wa kukuingiza katika kazi hii.Ni wakati wako sasa wa kuishi maisha huru na ya kawaida.Baada ya mimi kufariki hautakuwa na ngao wala mtu yeyote anayekulinda na kukuchunga kwa hiyo utakuwa katika hatari kubwa.Ndoto yangu ni wewe kuachana na kazi hii na kuishi maisha ya kawaida yenye furaha na amani.With this job you’ll never have a normal life.Lakini hii itawezekana tu kama utaikamilisha kazi uliyopewa sasa.Operesheni hii ni muhimu sana kwa nchi na dunia nzima kwa hiyo lazima uhakikishe kwa kila namna imefanikiwa.Baada ya kuikamilisha operesheni hii ndipo ulifungue kasha hili.Kasha hili halijakamilika.Lina sehemu tatu.Ukihakikisha kazi imekamilika nenda kanisa la bwana na uonane na mchungani Edmund dawson yeye ndiye mwenye funguo na atakuongoza mahala yalipo makasha yaliyosalia.” Akasema JohnMwaulaya ambaye alianza kupumua kwa shida.
Wakati Penny na John Mwaulaya wakiwa ndani Osmund aliyekuwa amesimama nje ya mlango wa Joh Mwaulaya akapigiwa simu.Baada ya kuongea na simu ile akamgeukia mwenzake aliyekuwa amesimama naye pale mlangoni
“ We have a situation.Kuna watu wamevamia mahal tulipomficha mke wa Dr Michael na hivi sasa kuna mapambano yanaendelea .Tuma kikosi haraka sana kwenda kutoa msaada.Hakikisha kwa kila namna hawafanikiwi kumchukua mke wa Dr Michael.Hali ya John inazidi kuwa mbaya na tunamtaka sana Dr Michael amfanyie upasuaji ili kuokoa maisha yake.Bila kuendelea kumshikilia mke wake hataweza kuifanya hiyo operesheni.Tafadhali hakikisheni vijana wanarejea hapa wakiwa na mke wa Dr Michael na wale wote waliojaribu kufanya uvamizi huo” akaamrisha Osmund.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO
No comments
Post a Comment