PENIELA (Season 2 Ep 3)

 SEASON 2

SEHEMU YA 3

ILIPOISHIA SEHEMUILIYOPITA

Sauti za watu wakijadiliana jambo zilisikika katika chumba cha kulia chakula.Hakutaka kupoteza muda akaufungua mlango ule kwa kasi na kujitoma ndani.Kitendo kile kiliwastua sana wazee wale waliokuwemo mle ndani.Kufumba na kufumbua bila hata kutamka neneo moja John akaanza kuifanya kazi iliyompeleka mle,aliwamiminia risasi wazee wale ,Seneta Joe Burke na DrElisante wakaanguka chini hawakuwa na uhai tena,Risasi nyingi zilizotoka katika bastora mbili za John zilizokuwa na viwambo vya sauti ziliwasambaratisha na kuwaharibu vibaya.Bila kupoteza hata sekunde moja John akakusanya makaratasi yote yaliyokuwapo pale mezani,akayapakia katika sanduku dogo akaenda chumbani na kuchukua kompyuta ndogo ya seneta Burke pamoja na kila kitu ambacho alikiona kinafaa kuchukuliwa halafu akaufunga mlango na kurejea katika chumba kile alichoacha mavazi yake akavua zile nguo za wahudumu wa hoteli akaziweka katika sanduku dogo na kuondoka.

“That’s how I killed seneta Burke.Baada ya miaka mingi kupita mwanae anakuja kulipiza kisasi,he’s coming to kill me”

Akawaza John Mwaulaya


ENDELEA…………………………….


Arnold alimtazama Mathew machoni na kugundua kwamba hakuwa akihitaji masihara.Aliogopa sana.

“Brother unanipeleka wapi? Kama una shida ya pesa tafadhali naomba uniambie” akasema Arnold huku akitetemeka na uso wake tayari ulikwisha loa jasho

“ Drive !..akasema Mathew kwa ukali.Mita kama mia tano toka waliache jengo lile Mathew akafanya kitu kimoja ambacho Arnold hakuwa amekitegemea.Kwa kasi ya ajabu alimpiga pigo moja kichwani kwa kitako cha bastora na Arnold akapoteza fahamu.Mathew akaudaka usikani wa gari na kulizuia gari lisiyumbe na taratibu akaliongoza gari hadi pembeni ya barabara akalisimamisha .Hakuna aliyeweza kuona kilichokuwa kinatendeka ndani ya ile gari kutokana na kuwa na vioo vyeusi.Anitha aliyekuwa analifuatilia gari lile kwa nyuma naye alisimamisha piki piki na kujiweka tayari kwa chochote ambacho kingejitokeza

Kwa haraka Mathew akachukua waya na kumfunga Arnold mikono na miguu halafu akamrushia katika kiti cha nyuma akaukalia usukani na kuliwasha gari akaendelea na safari

“Huyu jamaa ni nani?Mbona haonekanai kama nimtu hatari? Mbona hana silaha yoyote? Akajiuliza Mathew

“ Tutapata majibu muda si mrefu” akawaza Mathew na safari ikaendelea hadi nyumbani kwake.Wakamtoa Arnold na kumuingiza katika chumba kilichokuwa na kitanda cha chuma.Wakamlaza juu ya kile kitanda

“Huyu jamaa haonekani kama ni mtaalamu wa mambo haya.Nimempekua na hana silaha yoyote.Katika mkoba wake kuna vitu vya kawaida tu pamoja na ile tablet aliyopewa na wale jamaa kule City centre”akasema Mathew

“ Hata mimi ninahisi hivyo .Haonekani kama ni mtu anayefahamu chochote.Lakini lazima tumfahamu ni nani na nini lengo la kumfuatilia Eva.”akasema Anitha

“ Inawezekana akawa anatumiwa na watu Fulani.Anatakiwa ahojiwe na aseme kila kitu” akasema Noah.

Mathew akatoka mle chumbani na baada ya muda akarejea kiwa ameshika kitu Fulani mkononi mithili ya dawa,akakifungua na kukiweka katika pua za Arnold na baada ya sekunde kadhaa Arnold akapiga chafya mfululizo.Akafumbua macho na kujikuta ndani ya chumba akiwa amelazwa kitandani na kufungwa mikono.Akaangaza huku nahuku na kumbu kumu za nini kilichotokea zikamjia

“ Mmenileta wapi? Ninyi ni akina nani? Mnataka nini kwangu? Kama mnahitaji fedha niambeni m,mnataka kiasi gani niwapatie? Akasema Arnold huku machozi yakimtoka

“ Relax Arnold.Hatutakufanya kitu chochote kibaya .Kuna mambo tunayohitaji kuyafahamutoka kwako na baada ya hapo tutakuachia uendelee na shughuli zako lakini endapo utashindwa kutupatia kile tunachokihitaji basi itatulazimu kutumia nguvu ”

“ Tafadhali naombeni mnifungue ninasikia maumivu.Nitawapa kila mnachokihitaji lakini mniachie huru.Mimi si mtu mbaya .” Akasema Arnold.Mathew akatazamana na Anitha na kumpa ishara amfungue mikono

“ Arnold kuna kitu kimoja tu tunachokihitaji toka kwako”

“Kitu gani ? Pesa? Gari ? Chukueni chochote lakini mniache mzima” akasema Arnold

“ Hatuna shida na pesa Arnold.Tunahitaji utuambie ukweli.Kuna vijana Fulani wanne ambao mmoja wao ulikutana naye pale City center na akakupa kifaa chenye muundo kama tablet walikuwa wakimfuatilia dada mmoja anaitwa Eva.Vijana wale walitega kifaa Fulani katika gari la Eva ambacho hutuma taarifa katika ile tablet.Tunataka kufahamu ni kwa nini mnamfuatilia Eva? Kwa nini mnataka kujua mizunguko yote ya Eva? Ukitupa majibu ya kuridhisha basi tutakuachia huru uende zako lakini endapo utatudanganya ni wazi itatulazimu tutumie nguvu.Ninakushauri usitufanye tufike huko .Utapata maumivu makali sana ambayo hujawahi kuyapata toka uzaliwe” akasema Mathew

“ Jamani naombeni msitumie nguvu.Nitawaeleza chochote mnachokitaka” akasema Arnold

“ Kusema ukweli mimi simfahamu huyo msichana Eva na wala sijawahi kumuona.” Akasema Arnold

“ Tafadhali Arnold usitulazimishe tutumie nguvu .Sipendi tufike huko .Tueleze ukweli kwa nini mnamfuatilia Eva?

“ Nawaelezeni ukweli ndugu zangu,huyo Eva simfahamu na wala sijawahi kumuona.Ninaomba mniamini ndugu zangu.Mimi ni mtaalamu wa program za kompyuta na nina ofisi yangu katika jengo lile mlikonikuta.Ninachofahamu mimi kuhusu huyu msichana unayemuita Eva ni kwamba wiki iliyopita walikuja watu Fulani wawili ofisini kwangu na kuniomba niwafanyie kazi yao fulani na wakaahidi kunilipa pesa nyingi kama nikiifanya wanavyotaka.Waliniambia kwamba wanahitaji niwatengenezee program ya kompyuta kwa ajili ya kumfuatilia mtu Fulani bila ya yeye kufahamu kama anafuatiliwa.Waliahidi kunipa shilingi million kumi na mbili endapo ningefanikisha kazi hiyo ambayo ilionekana ni ya muhimu sana kwao.Sijawahi kuifanya kazi yenye malipo makubwa kama hii kwa hiyo nilishawishika kukubali kufanya kwa sababu nilikuwa na uwezo wa kuifanya .Nilitengeneza program ambayo ingeweza kuonyesha mizunguko yote ya mtu huyo waliyemtaka.Baada ya kuikamilisha program hiyo kilichofuata ilikuwa ni kukiweka kifaa hicho katika gari la mlengwa.Ili kuifanyakazi hiyo ilinilazimu kuwakodisha wale vijana mliwaona kule City centre kwaniwao ni wazoefu wa mambo kama hayo.Walifanikiwa kukiweka kifaa kile katika gari la Eva na programu yetu ikafanya kazi vizuri jinsi inavyotakiwa.Hicho ndicho ninachokifahamu .Huyo Eva simjui na wala sijawahi kumuona.” akasema Arnold

“ Baada ya kuikamilisha kazi uliyopewa nini kitafuata? Akauliza Anitha

“ Kinachofuata baada ya hapo ni kuwakabidhi kazi yao na wao kunipatia malipo yangu yaliyobaki.”

“Hao jamaa walikupa sababu ya kwanini wanataka kumfuatilia Eva? Akauliza Noah

“ Hapana hawakunieleza chochote kuhusiana na sababu ya kumfuatilia huyo mtu.” Akasema Arnold

“ saa ngapi utaonana nao ili uwakabidhi kazi yao?

“Tumepanga tukutane leo saa moja jioni.Wamesemawatanipgia simu kunipa maelekezo ya mahala kwa kukutana” akasema Arnold

“ Ok vizuri.sasa utaendelea kukaa hapa hadi jioni na tutakwenda sote katika hayo makabidhiano na halafu tutakuacha uende zako.Sisi hatuna shida na wewe hata kidogo.Sisi shida yetu ni hao jamaa waliokupa hiyo kazi” akasema Mathew

“ Tafadhalini jamani nimekwisha waeleza kila kitu mlichokuwa mnataka ,niachieni basi niende zangu” akasema Arnold

“ Usijali Arnold,tutakuachia uende zako ,lakini hadihapo tutakapohakikisha kwamba makabidhiano yamefanyika” akasema Mathew halafu wakaufunga mlangowa kile chumba wakatoka wakaingia katika chumba cha kupangia kazi .

“Wakati tunasubiri kuonana na Elibariki ili kuliweka sawa suala la Peniela,limeibuka suala hili la watu hawa wanomfuatilia Eva na hatuwezi kuliacha.Eva ni rafiki yangu mkubwa na wa miaka mingi na ni mtu ambaye nina hakika anaweza akawa ni wa msaada mkubwa sana kwetu .Ametusaidia katika kulifanikisha suala lile la kuipata ripoti ya kifo cha Dr Flora.Bila yeye tusingeweza kumpata kanali Adolf.Kwa hiyo wakati tunamsubiri Elibariki naombeni mnisaidie kuwabaini watu hawa ni akina nani na nini wanakitafuta kwa Eva? Nina imani kuna kitu tunaweza kukigundua hapa” akasema Mathew

“ Mathew ! akaita Noah

“ Wewe ni rafiki yangu mkubwa na ni kwa msaada wako nimefika hapa nilipo.Umenitoa mbali sana.” Akanyamaza kidogo halafu akaendelea

“ Umetuita hapa ili tukusaidie kazi ya kutafuta nani muuaji wa Edson, Lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda sielewi ni kazi gani iliyotuleta kwani kila siku kazi zinabadilika na hatuelewi kazi ya msingi ni ipi.Jana tumefanya kazi isiyotuhusu na ilibaki kidogo tungepoteza maisha.Leo tena imeibuka kazi nyigine mpya.Mathew tumeyaweka maisha yetu rehani kwa ajili ya kukusaidia ,tuko hapa kwa ajili ya kusaidiana nawe kama ulivyotuomba lakini naomba utuweke wazi ,tunakusaidia kufanya kazi ipi? Akauliza Noah

“Noah !!...akasema Anitha

“ No ! Anitha,Noah ana haki ya kuuliza .Ni kweli niliwaiteni kwa ajili ya kunisaidia kufanya uchunguzi wa suala la Edson lakini kadiri tunavyoendelea na uchunguziwetu mambo mengine zaidi yanaibuka .Ni sawa na unapotafuta madini.Ili uyafikie utakutana na vizingiti vingi kama mawe n.k lakini kwa vile nia yako nikupata madini basi itakulazimu kuyaweka pembeni ili upate njia ya kukufikisha yalipo madini.Hilo ndilo linalotutokea sisi.Tunafanya uchunguzi wa kifo cha Edson tufahamu ni nani alimuua na kwa nini,lakini ndani ya uchunguzi huo yanaibuka mambo mengine mfano Team SC41.Hatuwezi kuacha kuchunguza kila kitu kinachoibuka mbele yetu ambacho tunahisi kinaweza kuwa na mahusiano na kifo cha Edson.Suala lililojitokeza jana na hili la leo ni mambo ambayo nisingeweza kukataa kuyafanya.Elibariki ndiye aliyetupa kazi hii ya kuchunguza kuhusu kifo cha Edson na ndiye anayetulipa kwa hiyo alipokuja na kazi nyingine nakuomba tumsaidie ili kuwa ngumu kukataa.Hata hivyo tumefanikiwa kugundua jambo kubwa sana kuhusiana na kifo cha Dr Flora mke wa rais.Leo hii Eva naye amepatwa na matatizo.Eva ni rafikiyangu wa siku nyingi na amekuwa ni mtu mwenye msaada mkubwa kwangu.Ni yeye aliyetusaidia tukampata kanali Adolf jana na mkumbuke pia kwamba tulikuwa na makubaliano kwamba atanisaida kumpata kanali adolf lakini naye ana kazi yake ambayo anahitaji msaada na niliahidi kumsaidia.Leo hii amenipigia simu na kuniomba tena msaada kuna watu waliokuwa wakimfuatilia toka alipotoka nyumbani kwake.Ilikuwa vigumu sana kwangu kukataa kumsaidia .Kwa kujibu swali lako Noah ni kwamba bado hatujatoka nje ya kazi yetu ya msingi.Bado tunaendelea na uchunguzi kuhusiana na kifo cha Edson lakini hatuwezi kuachana na mambo madogo madogo yanayojitokeza wakati wa uchunguzi huo”akasema Mathew

“ Ninakuelewa Mathew .lakini je ni lini basi tutamaliza kazi hii kama tukiendelea na mpango huu wa kuifanya kila kazi inayojitokeza mbele yetu ? Akauliza Noah

“Noah Please stop that !!..akasema Anitha ambaye alionekana kukerwa na maswali yale ya Noah.

“ I’m sorry Anitha but I need to know .Jana almanusura nipoteze uhai wangu kwa hiyo nahitaji kufahamu kuhusu mpangilio maalum wa kazi tunazozifanya.”akasema Noah

“Usihofu Noah.Kazi itaendelea hata kama hautakuwepo.Inavyoonekana hauko tayari kuendelea na kazi hii.Endapo unahitaji kuondoka uko huru kufanya hivyo.Simzuii mtu yeyote kuondoka.Nina watu wengi ambao wanaweza wakanisaidia katika kazi hii lakini niliona ninyi ni chaguo langu la kwanza ndiyo maana nikawaita.Kwa hiyo kama kuna yeyote kati yenu ambaye hajisikii kuendelea kuifanya kazi hii anaweza akaondoka” akasema Mathew

“ Please Mathew don’t say that.You know I’m always with you.Tumefanya kazi nyingi pamoja na tumepitia hatari nyingi sana kuliko hata hizi za sasa.kwa hiyo siwezi katu kukuacha .Noah kama unajisikia kutaka kuondoka you can just leave!! Akasema Anitha



“Jamani naomba msinielewe vibaya .Sina maana ya kwamba ninataka kuondoka.Siwezi kuondoka na kuwaacha kwani hii ni kazi yetu sote.Samahani kama niliwakera kwa maneno yangu .Tusipoteze muda tuendelee na kazi.”akasema Noah

“Kabla hatujaendelea na kazi nahitaji kufahamu who is with me ? akauliza Mathew

“ I’m with you Mathew” akasema Anitha

“ Me too “ akasema Noah

“ Ok good.Nawashukuruni sana .Saa moja jioniya leo Arnold anakwendda kuonana na watu waliompa kazi na kuwakabidhi kile kifaa ambacho kazi yake ni kuonyesha mienendo yote ya Eva.Katika tablet ile kuna ramaniyote ya jiji la Dar es salaam kwa hiyo kila sehemu aliko Eva ataonekana.Kitu cha kufanya Anitha utaichukua tablet hii na kuiwekea programu nyingine ya siri ya kutuwezesha sisi kuifuatilia.Arnold atakabidhiana nao na baada ya hapo sisi tunatakiwa kuwafuatilia watu hao na kuwafahamu ni akina nani na nini lengo lao kwa Eva.Can you do that Anitha?akauliza Mathew

“Yes I can.Ni kazi ndogo sana hiyo kwangu”akasema Anitha

“Ok thank you.Do it” akasema Mathew na kutoka akaelekea chumbani kwake na kumpigia simu Eva

“ Halow Mathew” akasema Eva baada ya kupokea simu

“ Eva unaendeleaje?

“Ninaendelea vizuri Mathew.Nipe habari.Mmegundua nini kuhusu wale jamaa?

“ wale jamaa hawakuwa na hatari yoyote,walipewa kazi ya kukiweka kifaa kile cha kukufuatilia katika gari lako na kazi yao ikaisha.Tumempata mtu aliyetengeneza program ile na amedai kwamba alipewa kazi hiyo na watu wawili ambao waliahidi kumlipa pesa nyngi.Kwa namna Programu hiyo ilivyotengezwa ni kwamba kifaa kile kilichowekwa katika gari lako hutuma taarifa katika kifaa kingine muundo wa tablet ambacho kina ramani nzima ya jiji la Dar es salaam na hivyo kila sehemu utakayokwenda utaonekana .”

“ watu hao ni akina nani? Na kwa nni watumie gharama kubwa hivyo kunichunguza? Mathew nimeanza kuingiwa na woga .Inaonekana maisha yangu yako hatarini.Inaoenekana hawa jamaa ni watu wanaonifahamu sana”

“Bado hatujawafahamu watu hawa ni akina nani lakini hautapita usiku wa leo kabla ya kuwafahamu ni akina nani.Mpaka wakati huo tutakapolifahamu lengo lao ni nini nakushauri chukua tahadhari kubwa”

“ Ahsante Mathew kwa msaada wako mkubwa.Ninahamu sana ya kuwafahamu watu hawa ni akina nani na kwa nini wanamfuatilia”

“ Usijali Eva.Nitafanya kila linalowezekana ili kuwafahamu watu haoi” akasemaMathew na wakati huo huo ikaingia simu ya jaji Elibariki.Akamuomba Eva akate simu ili aweze kuipokea

“ Hallow Elibariki “akasema Mathew

“ Mathew utanisamehe nilishindwa kufika hapo nyumbani mchana kuna tatizo lilitokea.Mke wangu alipoteza fahamu ghafla na kukimbizwa hospitalini.Lakini mazingira ya kupoteza kwake fahamu yananipa shaka sana”

“ Ilikuaje hadi akapoteza fahamu? Akauliza Mathew

“ Wakati shughuli ya kuuaga mwili wa Dr Flora zikiendelea katika viwanja vya ukombozi,mke wangu alifuatwa na mtu Fulani na kumwambia kwamba anahitajika katika gari la wagonjwa na alipoelekea huko alijikuta akipoteza fahamu na kukimbizwa hospitali.Mathew mazingira ya tukio hilo yanatia shaka sana” 

“ Ni kweli Mathew,mazingira hayo yanatia shaka sana .Ninachokuomba kwa sasa chukua tahadhari kubwa.Watu waliomuua Dr Flora ni watu toka ndani ya ikulu na watafanya kila njia kuhakikisha kwamba hawajulikani.Yeyote yule ambaye ataonekana kuwa ni hatari kwao watamshughulikia kwa namna wanavyojua wao kwa hiyo mpe tahadhari mke wako awe makini sana kwa wakati huu.Elibariki tutaliongea vizuri zaidi suala hili jioni naomba ujitahidi usikose kuna jambo la muhimu sana la kuongea kuhusiana na Peniela”

“ Peniela? !..Jaji Elibariki akastuka

“ Kuna nini kuhusu Peniela?

“ Kuna jambo la muhimu sana la kujadili kuhusu Peniela”

“ Ok Mathew nitafika baadae lakini endapo nitashindwa kufika basi tutaonana kesho jioni au kesho kutwa kwa sababu kesho tutakwenda kumzika Dr Flora kijini kwao alikozaliwa na tutarejea jioni na endapo hatutaonana hiyo jioni basi tutaonana kesho kutwa asubuhi”

“ sawa Elibariki.Tutaonana utakapopata nafasi” akasema Mathew na kukata simu

“ Kuna kitu gani kinachoendelea pale ikulu ? Dr Flora ameuawa na nina uhakika mkubwa waliofanya jambo hili wako ndani ya ikulu.Nguvu kubwa imetumika kutaka kuzuia sababu ya kifo cha Dr Flora isijulikane lakini tumefanikiwa kujua nini kilimuua.Kuna kitu gani kinachoendelea ikulu? Lazima liko jambo kubwa hapa linalotakiwa kuchunguzwa.Kwa vile suala hili liko tayari mikononi mwa rais basi nina hakika litashughulikiwa ipasavyo.Kazi yangu mimi ilikuwa ni kuchunguza na kuwapa majibu” akawaza Mathew na kuelekea katika chumba cha kulia chakula .Alihisi njaa.Noah aliyekuwa amebaki nyumbani alikwisha andaa chakula

“ Watu hawa wanaomfuatilia Eva ni akina nani? Nafahamu Eva ana fanya kazi kwa siri katika idara ya usalama wa taifa.lazima kuna wau watakuwa wanataka kumchunguza.Hizi kazi niza hatari sana.Siku zote unaishi kama ndege.” Akawaza Mathew na mara Anitha na Noah wakaingia kujumuika naye pale mezani

“Anitha umefikia wapi kuhusu ile program ?

“ Ninaendelea na hiyo kazi .Lakini huyu jamaa Arnold anaonekana ni mtu anayeifahamu sana kompyuta .Nimeangalia namna alivyoitengeneza ile program dah ! yuko vizuri sana” akasema Anitha

“ Nimezungumza na Elibariki kwamba atajitahidi kufika jioni ya leo ili tuweze kuongea naye kuhusu lile suala la Peniela.Yeye ndiye tutakayemtumia katika kumchunguza Peniela.Peniela lazima kuna kitu anakifahamu kuhusiana na kifo cha Edson na Team SC41.Ili tuufahamu ukweli yatubidi tumfanyie uchunguzi mkubwa sana na nina hakika yeye ndiye atakayetuongoza kwenye ukweli ”akasema Mathew


TUKUTANE SEHEMU IJAYO……

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...