PENIELA (Season 2 Ep 7)
SEHEMU YA 7
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Peniela nimetoka kuongea na makao makuu Marekani sasa hivi na wanasisitiza kwamba tufanye haraka iwezekanavyo kukamilisha operesheni 26 B.Nataka tuonane kesho ili tuweke mikakati mipya ya namna tutakavyoimaliza operesheni hii ndani ya kipndi cha mwezi mmoja”
“ Osmund naomba tuelewane.Mlinikabidhi kazi hii kwa hiyo niachieni nilishughulikie jambo hili kwa namna ninavyoona linafaa.Sitaki shinikizo lolote.Nipeni wiki mbili nitakuwa na jibu zuri la kuwapa. Halafu Osmund ninataka kuonana na John Mwaulaya .Kuna mambo ya maana ambayo nahitaji kuongea naye” akasema Paniela
“ Unataka kuongea naye jambo gani?
“ Ni mambo binafsi”
Osmund akafikiri kidogo halafu akasema
“ Ok nitaongea naye na kumtaarifu kwamba unataka kumuona ila naomba tuwasiliane mara kwa mara kuhusiana na operesheni yetu.”
“ Wanatumwa watu kuja kuchunguza kilichosababisha mapigano yale.Ni wazi nilifanya makosa makubwa kumteka mke wa Dr Michael kwani ndiye chanzo cha haya yote kutokea.Lakini nilifanya hivyo kwa ajili ya kumsaidia John Mwaulaya .Lakini nini kitatokea endapo nitabainika kwamba ni mimi ndiye niliyesababisha vijana wale wote kuuawa? Tuhuma zote zinaniangukia mimi .I have to do something very fast .I have to kill John”
ENDELEA…………………………….
Noah na jaji Elibariki waliendelea na safari .Noah aliyekuwa akiendesha gari kuupa mazoezi mguu wake aliendesha kwa uangalifu mkubwa hadi walipofika katika makazi binafsi ya rais ambako Elibariki alikwenda kuonana na mke wake Flaviana..Watu walikuwa ni wengi na kwaya mbali mbali ziliendelea kutumbuiza kuwafariji waombolezaji
“Noah kama hutajali naomba unisubiri humu humu garini kwa sababu sintachukua muda mrefu.Nataka nimsikie tu mke wangu anataka kuniambia kitu gani halafu ninakuja tuondoke tukamsubiri Mathew.Lazima nionane naye usiku wa leo.Kuna mambo ya msingi sana ya kuongea naye. “ akasema jaji Elibariki halafu akashuka na kumuacha Noah mle garini.Kutokana na watu kuwa wengi ikamlazimu Elibariki kumpigia simu mke wake atoke nje ili waonane.Bila kupoteza muda Flaviana akatoka wakaelekea bustanini ambako hakukuwa na watu
“ Vipi maendeleo yako? Unajisikiaje sasa hivi? Akauliza Elibariki
“ Kwa sasa ninaendelea vizuri sana.Sina tatizo lolote.Dr Amosa kanipima na kasema hakuna tatizo lolote ” akasema Flaviana
“ Good.Kuna mabadilio yoyote katika ratiba ya kesho kuhusu mazishi? Akauliza Elibariki
“ Mpaka sasa hakuna mabadiliko yoyote ya ratiba.Ninadhani kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa” akasema Flaviana
“ Ok Flaviana nimekuja mara moja kukuona kama ulivyonitaka .Kuna sehemu nahitaji kufika usiku huu.Niambie ni kitu gani ulichotaka kuniambia ? akasema jaji Elibariki
“ Elibariki nimekuita ili tuongee kuhusiana na kile kilichotokea jioni ya leo kuhusu zile ripoti za uchunguzi wa kifo cha mama” akasema Flaviana
“ Flaviana tuongee kuhusu nini? Mjadala kuhusiana na suala lile umekwisha fungwa na baba yako amesema hataki tena jambo hili liendelee na hata wewe mwenyewe umekwisha ridhika na matokeo.Nilihangaika na kuwaletea ripoti ya ukweli mmeikataa tena kwa maneno ya kashfa sana.Sasa tuongee kuhusu nini? Akauliza jaji Elibariki
“ Elibariki naomba uelewe kwamba ripoti yako haijadharauliwa.Ninakushukuru kwa kazi kubwa na ngumu uliyoifanya hadi ukaipata ripoti ile lakini naomba uelewe kwamba suala hili ni gumu sana kwangu kiasi cha kuniweka njia panda .Nashindwa kuamua taarifa ipi ni sahihi.Lakini kwa hali halisi hata kama ungekuwa ni wewe uko mahala pangu ni wazi ungekubalina na taarifa ile ya madaktari bingwa.Sisemi kwamba taarifa yako haikuwa na ukweli lakini inawezekana madaktari uliowatumia katika kuipata taarifa hiyo kuna kitu walikikosea ama waliifanya kwa haraka na ndiyo maana wakaja na majibu yale.Taarifa yako inasema kwamba mama alikufa kwa kuchomwa sindano yenye sumu lakini taarifa ya madaktari bingwa inasema kwamba hakukuwa na aina yoyote ya sumu iliyokutwa iliyopelekea mama kufariki.Taarifa hizi mbili zinakinzana kwa hiyo ninapata wakati mgumu sana wa kuamua ni taarifa ipi iko sahihi lakini kutokana na mazingira yalivyo ninalazimika kuiamini taarifa ya madaktari” akasema Flaviana.Jaji Elibariki akatabasamu kidogo na kusema
“ Flaviana kama nilivyokwambia awali kwamba sikulazimishi uniamini au kuiamini taarifa niliyokupa.Najua unamuamini baba yako kuliko mimi.Hata hivyo ninashukuru kwa dharau za baba yako alizozionyesha kwangu leo ila kinachonisikitisha ni kwamba uhai wa mtu ulipotea katika kuipata taarifa ile lakini juhudi zote hizi zimekuwa kazi bure na badala yake ninaambulia dharau na matusi.Nilikosea sana kukubali kuifanya ile na kusahau kwamba ni familia hii hii ambayo imekuwa iinidharau kila uchao na kuniona kama takataka.” Akasema jaji Elibariki
“ Eli nimekwambia usiyajali maneno ya baba.Nina hakika aliyasema maneno yale kutokana na hasira na pengine hasira zake zikipoa mnaweza mkakaa na kumaliza tofauti zenu.”
“ si mara ya kwanza kwa baba yako kunitamkia maneno ya kejeli kama aliyoyatamka leo.Nimeyapokea yote lakini nakuhakikishia kwamba siku moja nyote mtakubaliana na kile nilichowaambia,lakini mpaka mtakapoubaini ukweli tayari mtakuwa mmekwisha chelewa sana“
“ Eli naomba tafadhali tusifikie hatua ya kuanza kulumbana.Mama yangu bado hajazikwa na sitaki machungu mengine kwa hivi sasa.Nilikuita ili tuongee kama watu wazima lakini naona mwenzangu bado umepandwa na hasira na umenikasirikia mimi kama ndiye niliyekutamkia maneno yale”
“ Hatulumbani Flaviana ila ninakueleza ukweli kwamba kuna jambo linaloendelea hapa ikulu lakini nyote hamtaki kuniamini.Nina hakika kuna siku itakuja mtayaamini maneno yangu” akasema jaji Elibariki
“ Eli naomba usiendee kuniumiza kichwa changu .Nina mambo mengi ya maana yanayopaswa kuumiza kichwa changu na si suala hili ambalo halina umuhimu wowote tena.Ninadhani hatutaweza kuelewana kwa sababu bado una hasira.You can just leave.Nenda unakotaka kwenda” akasema Flaviana akionekana kukasirika
“ Ahsante sana Flaviana.Ni kweli hatuna tena kitu cha kuongea.Mimi ninaondoka nitarejea baadae au asubuhi kwa ajili ya kuwahi ndege ya kuelekea kijijini” akasema jaji Elibariki na kuondoka .Hakutaka kukaa tena pale msibani .Maneno aliyokuwa ametamkiwa na Dr Joshua yalimchefua sana.Moja kwa moja akaelekea katika gari lake ambako alikuwemo Noah.Akakishika kitasa kwa ajili yakuufungua mlango lakini kabla hajaufungua simu yake ikaita.Akaichukua na kutazama mpigaji.Zilikuwa ni namba ngeni kabisa katika simu yake
“ Halow” akasema jaji Elibarki
“ Elibariki don’t get in that car” ikasema sauti ya mwanamke upande wa pili wa simu
“ What ?! jaji Elibariki akastuka na kusogea pembeni
“ Usiingie ndani ya hilo gari.” Ikasema tena sauti ile
“ Wewe ni nani na kwa nini nisiingie ndani ya gari langu? Akauliza jaji Elibariki
“ Ninakuonya usiingie ndani ya gari lako.You are going to die”
“ I’m going to die? Akauliza
“ yes you are going to die.Please listen to me and don’t get in that car” akasema Yule mwanamke
“ Wewe ni nani? Uko wapi.Who are going to kill me?” akauliza Elibariki
“ Elibariki tafadhali sina muda wa kupoteza.Naomba tafadhali unisikilize ninachokwambia na kama huniamini basi ingia ndani ya hilo gari lako” ikaonya sauti ya Yule mwanamke.Jaji Elibariki akabaki amesimama hajui afanye nini.Akageuka akalitazama gari lake halafu akasema
“ Sikufahamu wewe ni nani na siwezi kukuamini.Goodbye” akasema jaji Elibariki
“ Elib…………..” kabla Yule mwanamke hajamaliza , Elibariki akakata simu.Akavuta pumzi ndefu .Alionekana kuchanganyikiwa
“ Ni nani huyu aliyenipigia simu? Kwa nini ananionya nisiingie katika gari langu? Ni akina nani wanaotaka kuniua? Akajiuliza
“ I have to talk to Mathew.Yeye ndiye anayeweza kunishauri kitu cha kufanya” akawaza na kuzitafuta namba za Mathew akapiga lakini hazikuwa zikipatika
“ Ouh my God ! Mathew hapatikani.Nitafanya nini? Akawaza kwa sekunde kadhaa
“Ngoja tu niingie garini niondoke.Hakuna lolote litakalotokea.Vitisho kama hivi nimevizoea.” akawaza jaji Elibariki huku akiufungua mlango wa gari lake na kuingia.
“ Eli kwema huko utokako ? Akauliza Noah baada ya kumuona namna jaji Eibariki alivyobadilika
“ Kwema Noah.Ni mambo ya kawaida ya wanawake” akasema huku akijifuta jasho
“ Can we go? Akauliza Noah
“ Yes .Let us go” akasema jaji Elibariki Noah akawasha gari wakaondoka.Jaji Elibariki alionekana kama mtu aliyechanganyikiwa.Alikuwa akitazama huku na huku.
“ Noah umekumbuka kutembea na bastora yako? Akauliza jaji Elibariki
“ Hapana Eli,sikuchukua bastora.Kwani kuna tatizo lolote? Akauliza Noah
“ Hapana Noah.Hakuna tatizo nilitaka tu kujua kama ulikumbuka kuchukua bastora yako”
“ Sikuichukua .Katika matembezi ya kawaida kama haya huwa sitembei na silaha “ akasema Noah huku akiendelea kukanyaga mafuta.Bado jaji Elibariki aliendelea kumtafakari mwanamke Yule simuni
“Simfahamu mwanamke Yule na sifahamu amezitoa wapi namba zangu za simu.Kwa nini aniambie maneno kama yale? Akaendelea kujiuliza
“ Yawezekana ikawa ni moja ya njama za Flaviana kunitaka niendelee kukaa pale msibani ,akampa mmoja wa marafiki zake namba zangu anipigie na kunitisha.Lazima atakuwa ni mwenyewe kwani hakuonekana kufurahi nilipomwambia kwamba kuna mahala ninakwenda.Labda anadhani kwamba ninakwenda kwa mwanamke mwingine.Lakini wivu wa nini wakati hanithamini mimi kama mume wake? Angejua kwamba kwa hivi sasa moyo wangu haudundi kwake hata kidogo wala asigethubutu kuwa na wivu.Kwa sasa akili yangu yote inamuwaza mtu mmoja kwa sasa,Peniela.Sijui ni kwa nini msichana yule ameniingia katika damu yangu kiasi hiki.Pamoja na tukio lile lililotokea la kugombana na Jason lakini bado akili yangu haiachi kumuwaza.Bado amejaa tele katika kichwa changu.Natamani sana kumuona na kuongea naye” akawaza jaji Elibariki na kumbu kumbu ya ugomvi uliotokea nyumbani kwa Peniela kati yake na Jason ikamjia akauma meno kwa hasira.
“ Sikujua kama Jason ni kijana mshenzi kiasi kile.Nimetokea kumchukia sana kwa kitendo alichokifanya cha kuingia na kuanzisha ugomvi huku akijinadi kwamba Peniela ni msichana wake.Mbona hakuwahi kuniambia kama ana mahusiano na Peniela? Asicheze na mimi Yule kijana nitamuhamisha huu mji.Sisi ndio wazawa wa jiji hili na akitaka mashindano na mimi nitamfanyia kitu kibaya.Lakini inawezekana akawa kweli na mahusiano na Peniela? Halafu siku ile ya ugomvi kuna wale watu walitokea na kuondoka na Peniela na mimi wakanipeleka hospitali ni akina nani wale? Wana mahusiano gani na Peniela? Mbona walikuwa wamevalia nadhifu sana na hata magari yao yalionekanakuwa ni ya kifahari sana? Peniela alikwenda wapi na wale jamaa usiku ule? Kuna haja ya kumuuliza Peniela na kuufahamu ukweli.Kuna hajaya kumfahamu msichana yule kiundani.Inawezekana akawa na mabwana kibao . ” Akawaza jaji Elibariki
*********
Mara tu gari ya jaji Elibariki ilipotoka katika makazi binafsi ya rais,mtu mmoja aliyekuwa amesimama nje ya gari moja jeusi akiwa amevalia suti nyeusi ,akachukua simu yake ya mkononi na kupiga katika namba Fulani
“ He’s moving out now” akasema Yule jamaa
“ We’ re in position waiting”
“ Kunaonekana watu wawili ndani ya gari.Take them all.Remember no mistake “ akasema Yule jamaa
“ Ok tumekusoma” ikasema sauti ya upande wa pili.
Yule jamaa akaingia katika gari lake na kuondoka maeneo yale.Akiwa ndani ya gari lake akazitafuta namba za simu za Dr Kigomba akampigia
“ Hallow Festo” akasema Dr Kigomba baada ya kupokea simu
“ Mzee kila kitu kinakwenda sawa.Tayari jamaa yuko barabarani na vijana wamekwisha jipanga.Ila kama nilivyokufahamisha awali kwamba kwa mazingira haya ya jiji la Dar es salaam kutengeneza ajali ambayo inaweza ikamuondoa Yule jamaa ni magumu sana kutokana na msongamano lakini tutakwenda na plan B.”
“ Vyovyote itakavyokuwa Festo lakini hakikisheni mmeikamilisha kazi.Wakumbushe vijana kuwa makini sana”
“ Vijana wako makini sana.Nitakupa taarifa baada ya nusu saa.” akasema Yule jamaa na kukata simu
*******
Mathew na Anitha waliendelea kuwafuatilia wale jamaa japokuwa haikuwa kazi rahisi kwa usiku ule . Iliwalazimu kutumia mbinu za hali ya juu sana kuwafuatilia wale jamaa .Mathew alikuwa makini katika usukani na Anitha hakubandua jicho katika kompyuta yake iliyokuwa ikionyesha mwendo wa ile tablet waliyopewa wale jamaa kwani aliiwekea program maalum ya kuweza kuifuatilia .
Safari yao iliwafikisha hadi Kigamboni katka nyumba moja kubwa iliyokuwa na uzio mrefu kiasi kwamba haikuwa rahisi kutazama kilichokuwa kinaendelea mle ndani.Mathew na Anitha waliipita nyumba ile na kwenda kusimamisha gari mbele kidogo kulikokuwa na baa
“ Anitha utabaki ndani ya gari.Mimi ninarudi katika ile nyumba nataka nikawafuatilie wale jamaa.” Akasema Mathew
“ Mathew ni hatari sana kama ukienda peke yako.Hatuwajui watu wale ni akina nani kwa hiyo kuna kila ulazima wa kuchukua tahadhari.Naomba tuongozane wote.Nitakulinda” Akasema Anitha
“ Anitha wewe ndiye mtu ninayekutegemea sana katika kazi zangu nyingi kwa hiyo sitaki kabisa upatwe hata na mkwaruzo.Hakuna ajuaye yawezekana kule ndani kukawa na makabiliano ya risasi na wewe huna uzoefu sana na mambo kama kwa hiyo niachie mimi nikaifanye hii kazi.Nitakuwa nikikupa taarifa ya kila kinachoendelea” akasema Mathew huku akilifungua begi lake na kutoa kisanduku Fulani kidogo na kuchukua kidude kidogo akakiweka sikioni na kubonyeza kitufe chenye rangi ya kijani katika kile kisanduku taa nyekundu ikawaka.
“ Good.Kila kitu kinakwenda vizuri” akasema na kulivaa begi lake mgongoni akashuka na kuanza kupiga hatua kuelekea katika ile nyumba waliyoingia wale jamaa.
“ Anitha nipe ripoti.Kuna mabadiliko yoyote katika kompyuta yako? “ akasema Mathew akiwa hatua chache kuifikia ile nyumba
“ bado kifaa kipo ndani na hakijatoka”
“Ok good .Nimekaribia sana“ akasema .Alitaka kuzunguka kwa nyuma lakini akagundua kwamba mlango mdogo katika geti ulikuwa haukuwa umefungwa,ulikuwa umerudishwa tu, akausukuma taratibu na kuchungulia ndani.Kulikuwa na gari mbili zimeegeshwa na nyingine namoja ilionekana mbovu kwani ilikuwa imefunikwa na turubai.Mbwa mkubwa alionekana kuzunguka zunguka mle ndani.
“ Kitu cha kwanza ni kumnyamazisha yule mbwa,kwa sababu akibweka tu atawastua watu waliomo ndani.” Akawaza Mathew na kisha akaitoa bastora yake yenye kiwambo cha kuzuia sauti akajiweka vizuri na kumlenga mbwa aliyekuwa amesimama pembeni ya gari.
“ Help me Lord.Nikimkosa huyu mbwa nitakuwa nimeharibu kila kitu”akawaza Mathew na kuachia risasi iliyompata yule mbwa kichwani ,akatoa ukelee mdogo na kuanguka chini akatapa apa.Kabla mbwa yule hajakata roho tayari Mathew aliingia ndani na kukimbia kama paka hadi nyuma ya gari moja akajibanza .Aliangza angaza kama kuna mtu yeyote aliyesikia ukulele uliotolewa na yule mbwa lakini hakukuwa na mtu yeyote aliyetoka .Ndani ya ile nyumba taa zilikuwa zinawaka na sauti za watu wakicheka kicheko kikubwa zikasikika..Taratibu akanyata na kuzunguka hadi nyuma ya ile nyumba ambako kulikuwa na mlango ambao haukuwa umefungwa.Akaufungua taratibu mlango ule na kuingia ndani.Alijikuta ametokea jikoni.Hakukuwa na mtu pale jikoni na kwa mbali alisikia sauti za watu wakiongea na kucheka.Akiwa bado anatafakari namna ya kufanya mara akasikia hatua za mtu akielekea maeneo yale ya jikoni.Hakukuwa na sehemu ya kujificha kwa haraka hivyo ikamlazimu kujibanza pembeni ya mlango.
“ Yvone..!! mtu yule aliyekuwa akielekea kule jikoni akaita na kuchungulia lakini hakuona mtu akaondoka.Bado sauti za watu wakiongea nakucheka kwa nguvu zilisikika..Mathew akaufungua ule mlangowa jikoni taratibu na kuchungulia .Katika Chumba kilichofuata kulikuwa na meza ya duara na viti sita.Moja kwa moja akajua kile ni chumba cha kulia chakula.Alipohakikisha kwamba hakuna mtu yeyote katika kile chumba akatoka jikoni na kuingia katika kile chumba cha chakula.Bado aliendelea kuzisikia sauti za watu wakiongea na kucheka.Kulikuwa na mlango mkubwa wa kioo akachungulia na kuwaona watu wanne wamekaa katika sebule wakiongea na huku ile tablet iliyotoka kwa Arnold ikiwa mezani.Mathew akawasoma vizuri na kujiweka sawa kwa ajili ya kuwakabili wale jamaa lakini mara akatokea mtu mwingine na kumfanya Mathew asite kidogo.Mtu yule aliyeingia sebuleni alikuwa amekasirika na alikuwa akiongea kwa sauti kubwa hadi Mathew akasikia
“ Yule mtoto mpumbavu sana na leo pia amegoma kula.Tutamfanya nini? Hali yake inazidi kuwa mbaya.Tukifanya mchezo atakufa yule binti” akasema yule jamaa
“ Sijui tutamfanya nini huyu binti lakini hata kama akigoma kula lazima tutaupata mzigo wetu.Kwa sasa tuna uhakika asilimia mia moja kuupata. Ninahakika lazima atakuwa ameuficha kwa huyu msichana .” akasema mwingine huku akiitazama ile tablet
“ Lakini Kwa nini yule kijana aliyetutengenezea hii program tumuue? Ana kosa gani? Akauliza mmoja wao
“ Yule kijana ni hatari sana kwetu.Vijana kama wale mara nyingi huwa wanaingiwa na tama kwa hiyo angeweza hata kuja tena siku za usoni na kututishia kuturipoti kwa vyombo vya dola na kudai pesa nyingi.Kwa kuwa hatuna kazi naye tena,basi kinachofuata ni kumuua tu.Hivyo ndivyo mambo huwa yanakwenda”akasema mmoja wa wale jamaa aliyekuwa ameishika ile tablet.
“Hebu twendeni tukamuone yule binti tujue namna ya kufanya.Haliyake si nzuri hata kidogo” akasema yule jamaa aliyewafuata wenzake pale sebuleni.Wote wakainuka na kumuacha mtu mmoja aliyekuwa ameishika ile tablet.Mathew alikuwa akiona kila kitu kilichokuwa kinaendelea kupitia kioo cha mlango.Wale jamaa walipoondoka pale sebuleni ,akaufungua ule mlango taratibu .Mtu yule aliyekuwa pale sebuleni akiwa hana hili wala lile ameiinama ile tablet mara akahisi kama kuna mtu amesimama mbele yake.Akainua kichwa na kukutana na bastora ikimtazama.Akastuka sana na kuiangusha chini ile tablet
“Shhhhhh!!!!..Usijaribu kufanya chochote.Kaa hivyo hivyo”akasema Mathew kwa sauti ya chini .Yule jamaa alikuwa anatetemeka.Hakuamini kama ni kweli alikuwa akitazamana na bastora
“ tafadhali naomba usiniue.Kuna fedha nyingi ndani nitakupatia”akasema yule jamaa kwa sauti yenye kitetemeshi.Alikuwa ameogopa sana
“ Wenzako wamekwenda wapi? Akauliza Mathew
“ wamekwenda ..wamekwenda….’ akasita,alikuwa anatetemeka
“ Niambie wenzako wako wapi la sivyo nitakifumua kichwa chako kwa risasi” akafoka Mathew
“ Usi.usi..usiniue tafadhali..Wamekwenda kumtazama mgonjwa amegoma kula.”
“ kwa nini mnamfuatilia Eva? Akauliza Mathew.Yule jamaa aliyekuwa amekaa akitetemeka akashindwa kujibu
“Nakuuliza kwa nini mnamfuatilia Eva? Akauliza Mathew.Yule jama alishindwa aseme nini midomo ilikuwa inamcheza.Mathew hakutaka kupoteza muda akamsogelea na kumuwekea bastora kichwani
“ Niambie kwa nini mnamfuatilia Eva? Akauliza Mathew.Kabla yule jamaa hajajibu kitu ukasikika mlio wa glasi kuanguka na kuvunjika .Mathew akageuka haraka haraka na kuangalia kilichotokea.Msichana mmopja alikuwa ameangusha sinia alilokuwwa amelibeba baada ya kuingia pale sebuleni na kumkuta Mathew akiwa amemuelekezea yule jamaa bastora.Yule mwanamke aligeuka haraka na kuanza kukimbia huku akipiga kelele.Kufumba na kufumbua Mathew akampiga yule jamaa pigo moja kichwani na kumpoteza fahamu.Kelele za yule mwanamke zakuomba msaada ziliwastua jamaa wale wengine na kuwafanya watoke mbio kuja kuangalia nini kimetokea.Mathew alikwishawaona na bila kupoteza muda akacheza vizuri ma bastora yake kama vile alizaliwa nayo na kuzimimina risasi .Lilikuwa nishambulio la kustukiza na kutahamaki wote wakajikuta wakiwa chini wamelalia sakafu iliyojaa damu.Hawakuwa na uhai tena.Yule msichana aliyekuwa akipiga kelele alikuwa ameanguka chini akilia akiomba ahurumiwe.Mathew ambaye kwa sasa alikuwa mithili ya Simba akamuamuru ainuke.
“Kulikuwa na watu wangapi humu? Akauliza Mathew.Huku akitetemeka yule msichana akajibu
“Kulikuwa na watu..” akasita kidogo kama vile anajaribu kukumbuka idadi ya watu
“ Kulikuw ana watu wangapi ? akauliza Mathe kwa ukali
“Kulikuwa na watu sita .Hawa jamaa wanne uliowapiga risasi na yule mwingine kule sebuleni na mmi.halafu kuna……”akasita
“ Kuna nini?
“Kuna msichana mwingine yuko chumbani”
“ Anafanya nini chumbani? Akauliza Mathew.Yule msichana akabaki kimya
“ Nipeleke huko chumbani ”akasema Mathew na msichana yule akamuongoza katika chumba fulani wakaingia halafu wakaanza kushuka ngazi kuelekea chini.Kulikuwa na chumba fulani kilichokuwa kama mahabusu.Kulikuwa na mlango wenye nondo nzito na kufuli kubwa.Ndani ya chumba hiki Kulikuwa na kitanda na juu ya kitanda kile kuna msichana aliyekuwa amelala pale akiwa hajiwezi kabisa na mguu wake mmoja ulifungwa pingu
“ Ouh my God ! akasema Mathew na kumtikisa yule msichana pale kitandani lakini hakuamka .Hali yake haikuwa nzuri.Kwa hasira Mathew akamgeukia yule msichana na kumnasa kibao kikalikinachompeleka hadi chini
“ Mmemfanya nini huyu binti? Yule msichana hakujibu kitu zaidi ya kulia.Mathew akakipiga piga kile kidude cha mawasiliano alichokuwa amekichomeka sikioni
“ Anitha..do you read me?
“ yes Mathew.Whats going on? Akasema Anitha
“ I need your help.Kuna msichana mmoja ana hali mbaya sana amefungwa ndani ya hiki chumba.” Akasema Mathew
“ Unahitaji msaada gani?
“ We need to take her out of here.Njoo na gari usiogope ni sehemu salama.Watu wanne wako chini na mmoja hana fahamu.Njoo haraka”akasema Mathew na kumgeukia yule msichana
“ nani ana funguo za pingu hii? akauliza
“ Ni John” akajibu kwa uoga
“ Yuko wapi huyo John?
‘ Ni mmoja wa wale uliowapiga risasi”
“ Ok twende ukanionyeshe” akasema Mathew na kupanda haraka haraka hadi katika sehemu wale jamaa walipokuwa wameanguka .Damu ilikuwa imetapakaa .Yule msichana akam John mifukoni na kumkuta na funguo halafu wakakimbia na kwende kumfungua yule msichana.
“ Mathew nimekwishafika niko hapa nje” Anitha akamtaarifu Mathew ambaye alimuamuru yule msichana kwenda kufungua geti na Anitha akaingiza gari.Mathew akambeba yule msichana asiyejiweza akamtoa nje hadi katika gari
“ Gosh.! Wamemfanya nini ? Who are these people? akauliza Anitha huku akimsaidia Mathew kumuweka vizuri yule msichana ndani ya gari.
“ I don’t know yet.Lakini tutafahamu ndani ya muda mfupi.Bado kuna mtu tunayetakiwa kuondoka naye,yeye ndiye atakayetueleza kila kitu.” akasema Mathew na kuongozana na Anitha wakaingia ndani na kumchukua yule jamaa ambaye hakuwa na fahamu wakamfunga mikono na miguu wakampakia katika buti ya gari.Mathew akarudi tena ndani na kuichukua ile tablet na kumgeukia yule msichana aliyekuwa ameegemea ukuta ka woga
“ Wewe sintakufanya chochote lakini utaondoka nasi.Tutajua kitu cha kukufanya mbele ya safari” akasema Mathew na kumuongoza msichana yule hadi katika gari wakaondoka.
“ kaka naombeni msinifanye kitu chochote.Mimi ni mfanyakazi tu wa ndani katika ile nyumba na sifahamu chochote.” Akasema yule msichana huku akilia.
“ Mathew who are these people? Walikuwa wanafanya nini na huyu msichana ? akauliza Anitha.kabla Mathew hajajibu kitu yule msichana aliyedai nimfanyakazi wa ndani akasema
“ Huyu msichana alikuwa anashikiliwa mateka na wale jamaa.Wamekuwa na tabia ya kuteka watu na kuwafungia katika kile chumba cha chini.Mimi ndiye waliyenipa kazi ya kumuhudmia huyu dada kwa chakula na kila kitu”akasema
“ Nina wasi wasi yawezekana msichana huyu akawa ndiye yule ambaye aliniambia Eva” akasema Mathew
“ Umesema Eva? Akadakia yule msichana wa kazi .
“ unamfahamu? Akauliza Mathew
“ simfahamu Eva lakini kuna siku hapa katikati walimtesa sana huyu msichana na kumlazimisha aseme alikoweka sijui kitu gani wanachomlazimisha kila siku awaambie amekiweka wapi ndipo akamtaja Eva.Wakampa simu ampigie Eva lakini yeye hakuongea vile walivyotaka wao badala yake akamuomba Eva amuokoe. Wakamnyanga’anya simu na kumpiga sana.Wamekuwa wakimtesa kila siku wakimtaka awaelekeze mahala alikoweka hicho kitu wanachokitaka”akasema yule msichana wa kazi
“ Ouh my God, we’ve found her.Huyu ndiye msichana aliyemuomba Eva amsaidie.”akawaza Mathew na kisha akachukua simu na kumpigia Eva.
“Hallow Mathew”akasema Eva
“ Eva naomba uache kila unachokiganya hivi sasa tukutane nyumbani kwangu”
“ Kuna nini Mathew? Wewe uko wapi? akauliza Eva lakini Mathew hakujibu kitu akakata simu
“Mathew kwa nini tusimpeleke kwanza huyu binti hospitali? Hali yake si nzuri hata kidogo” akasema Anitha
“Hapana Anitha.Hatuwezi kufanya hivyo.Tutamuachia Eva yeye ndiye atakayetusaidia katika hilo.Anafahamiana na madaktari wengi na atatusaidia kumpata daktari wa kuweza kumuhudumia.Tukimpeleka hospitali tutahitajika kutoa maelezo na sisi hatuna maelezo yoyote.
“ Huyu binti ana siku ya tatu leo amegoma kula chakula na ndiyo hali yake ni mbaya .Walikuwa wanajadiliana wamtafute daktari “akadakia yule msichana ambaye alionekana muongeaji sana
“ Kuna kitu gani anacho huyu msichana kiasi cha kuwafanya wale jamaa wamteke na kumfungia na kumtesa kiasihiki ili awaonyeshe mahala alipokificha hicho kitu ? Lazima kitakuwa ni kitu muhimu sana.Ngoja tutafahamu muda si mrefu sana” akawaza Mathew
“Namuonea huruma sana huyu binti kwa namna walivyomtesa.Amedhoofu na ana makovu mengi ya kuumia.Inaonekana walikuwa wakimpiga sana.Yule jamaa tuliyemchukua leo ataomba ni bora kama angekutana na mtoa roho kuliko kukutana na mimi kwa sababu kitu nitakachomfanyia ataeleza kila kitu.Haiwezekani wamfanyie huyu binti ukatili wa namna hii.” Akawaza Mathew
********
Jaji Elibariki na Noah waliendelea na safari yao kama kawaida huku kichwa cha Elibariki kikijaa mawazo mengi sana kuhusiana na kile kilichotokea na zaidi sana picha ya Peniela ndiyo iliyokuwa ikimjia kichwani mara kwa mara na kumfanya asiache kumuwaza.Walipofika katika taa za kuongozea magari katika makutano ya barabara za Mkwavinyika na Kilimanjaro iliwalazimu wasimame baada ya taa nyekundu kuwaka.Wakati wakisubiri waruhusiwe Jaji Elibariki akamuuliza Noah.
“ Noah umeoa?
Noah akatabasamu na kusema
“Hapana bado..”
“Kama bado basi unatakiwa uw……………” kabla hajamalizia alichotaka kukisema zilizotokea piki piki mbili na Ghafla Noah aliyekuwa ameleekeza macho yake nje akapiga ukelele mkubwa
“ Elibariki get down..!!!!!!!.. akasema na kumrukia Elibariki akamgandamiza katika kiti.Milio ya risasi ikarindima mahala pale na kusababisha taharuki kubwa.Watu wakashuka katika magari na kukimbia hovyo ili kujinusuru .Kwa takribani dakika tano risasi ziliendelea kurindima eneo lile.Mara kukawa kimya halafu mlango wa gari ya jaji Elibariki ukafunguliwa na mtu mmoja aliyekuwa na bastora mkononi na usoni akiificha sura yake kwa kofia nyeusi na kuacha sehemu ya macho.
“ Elibariki….!!” Akaita mtu Yule ambaye alikuwa ni mwanamke.Elibariki aliyekuwa amegandamizwa na Noah alishindwa kuitika alikuwa amechanganyikiwa .
Yule mwanamke akamsukuma Noah aliyekuwa amemgandamiza Elibariki kitini.Hakuwa na uhai tena.Alikuwa hatazamini kwa namna alivyoharibiwa na risasi.Jaji Elibariki alikuwa ameloa damu na hakuwa na hata nguvu za kusimama.Yule mwanamke akamshika mkono na kumtoa ndani ya lile gari na kumpeleka hadi katika gari ra rangi nyeusi lililokuwa nyuma ya gari la Elibariki halafu wakaondoka kwa kasi kubwa.Eneo lote halikuwa na mtu hata mmoja.Magari yalikuwa matupu watu walikuwa wameyaacha na kukimbia kuokoa maisha yao.
NOAH AMEFARIKI DUNIA KATIKA SHAMBULIO LAKINI ANAMUOKOA JAJI ELIBARIKI.MWANAMKE ALIYEONDOKA NA ELIBARIKI NANI?
No comments
Post a Comment