SIMULIZI: PENIELA (Season 1 Ep 35)
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Nilifahamu toka mapema team SC41 ni watu hatari sana.Kwa mara nyingine tena leo hii nimenusurika toka katika mikono yao.Nitapambana nao.safari hii sintaogopa wala kukata tamaa lazima nihakikishe nimepambana nao na kulipa kisasi cha familia yangu na wenzangu walioteketezwa kikatili.Tukio la leo ni salamu kwao kwamba watu wanaopambana nao kwa sasa si wa kawaida.” Akawaza Mathew wakiwa garini
“ kwa sasa tunahamia kwa Peniela.Kwa sasa inabidi tuanze kumchunguza Peniela.Katika hili itabidi kuwatumia akina Elibariki.Tunatakiwa kuzifuatilia nyendo zake.Siku ile wale watu wa Team SC41 walitokea kwake ndipo wakaelekea hospitali kwa John Mwaulaya.Ninashawishika kuamini kwamba yawezekana kabisa Peniela akawa na mahusiano naTeam SC41.Endapo tutagundua kwamba Penny ana mahusiano na Team SC41 basi nitawaunganisha katika kifo cha Edson.Baada ya hapo tutaanza kuitafuta sababu ya kumuua.Kama ni kweli TeamSC41 walihusika katika mauaji ya Edson it’ll be for something big.very big”akawaza Mathew
ENDELEA……………………
Waliwasili katika hospitali inayomilikiwa na Dr Robert.Kwa kutumia simu ya Mathew Dr Michael akamfahamisha Dr Robert kwamba tayari wamekwishafika ,akawafuata katika maegesho halafu akawachukua na kuwaongoza hadi ndani ya hospitali.Mathew na Anitha wakaombwa wakae katika viti vilivyokuwa katika sehemu ya kupumzikia wakati Dr Michael na mwenzake wakiendelea kuzifanyia uchunguzi sampuli toka kwa mwili wa Dr Flora .Kabla hawajaanza kazi Dr Robert akamuuliza Dr Michael
“ Michael,kuna tatizo gani? Kwa nini jambo hili lifanyike usiku na haliwezi kusubiri hadi kesho? Akauliza Dr Robert
“ Dr Robert kuna sampuli ninazotakiwa kuzichunguza usiku huu na siwezi kusubiri hadi kesho.” Akasema Dr Michael.Robert akamtazama kwa sekunde kadhaa kisha akauliza
“ Niambie Michael, nini kimetokea? Macho yako yanaonyesha kabisa kwamba kuna tatizo Fulani.Na hawa watu ulioongozana nao ni akina nani?
“ Robert wewe ni rafiki yangu mkubwa na siwezi kukuficha kitu lakini naomba nitakachokueleza kiwe ni kati yetu wawili.”
“ Niambie Michael kitu gani kimetokea?
“ Mke wangu alitekwa nyara na watu wasiojulikana ambao walitaka kunilazimisha nimfanyie upasuaji mgonjwa wao waliyemtorosha toka hospitali.Vijana hao nilioongozana nao ndio waliopambana hadi wakafanikiwa kumuokoa mke wangu toka katika mikono ya watekaji.Mwenzao mmoja alifariki dunia katika mapambano hayo kwa hiyo unapowaona hapo wako katika majonzi makubwa lakini bado hawakati tamaa wanaendelea na mapambano.Kuhusu kilichonileta hapa usiku huu ni kwamba mke wa rais alifariki ghafla na mpaka sasa sababu ya kifo chake haijajulikana na imetolewa amri ya kutochunguza chanzo cha kifo chake.Vijana hawa wanataka kuufahamu ukweli wa kilekilichomuua mke wa rais .Tulifika katika hospitali ulikohifadhiwa mwili wa mke wa rais kwa dhumuni la kuufanyia uchunguzi kwa siri lakini wakati tukiendelea na kazi hiyo wakapokea taarifa kwamba tumegundulika tunaufanyia uchunguzi mwili wa Dr Flora.Ilitulazimu kuacha kila tulichokuwa tunakifanya na kukimbia.Kabla ya kutoka nilichukua sampuli kadhaa kwa ajili ya kuendelea kuzifanyia uchunguzi.Kwa hiyo niko hapa na wale vijana ili kuufahamu ukweli wa nini kilimuua mke wa rais” akasema Dr Michael.
“ Michael umejiingiza katika matatizo makubwa na vyombo vya dola.Kwa nini ulikubali kufanya kitu cha hatari kama hiki? Unafikiri ikijulikana kwamba ulishiriki katika jambo kama hili utakuwa salama? Akauliza Dr Robert
“ Robert nililazimika kukubali kufanya hivi kwa sababu waliahidi kunisaidia kumpata mke wangu na wamefanya hivyo kwa hiyo na mimi nalazimika kutimiza ahadi yangu.Lazima niwasaidie kufahamu chanzo cha kifo cha mke wa rais.Kuhusu usalama wangu usijali kuhusu hilo tayari nina mpango mzuri baada ya kumaliza kazi hii” akasema Michael.Robert akamtazama kwa muda kidogo na kusema
“ Sawa Michael mimi nitakusaidia kufanya uchunguzi huo lakini tafadhali kuwa makini sana,na sitaki ijulikane kwamba hospitali yangu imehusika kwa namna yoyote ile na jambo hili.Je unaweza ukanihakikishia hilo?akauliza Robert
“Ndiyo Robert.Nakuhakikishia kuhusu hilo”akasema Michael.Robert akavaa koti tayari kwa kuanza kazi
“ Katika uchunguzi mliokwisha ufanya mligundua chochote?
“ Tuligundua kwamba mishipa ya damu ilipasuka ishara kwamba kulikuwa na mgandamizo mkubwa wa damu,tunachotaka kufahamu ni kitu gani kilisababisha hali hiyo kutokea?.Hapa nina sampuli kadhaa ambazo tunatakiwa tuzifanyie uchunguzi na tutapata jibu.”akasema Dr Michael na mara moja shughuli ya uchunguzi ikaanza.
“ Mathew whats next? Akauliza Anitha wakiwa katika sehemu ya kupumzikia.
“ Baada ya kupata majibu ya nini kilimuua Dr Flora ,tutaendelea na kazi yetu ya msingi yaani kuchunguza kuhusu kifo cha Edson.Kazi hii ya kuchunguza kiini cha kifo cha Dr Flora imeingia tu kwa dharura na haikuwa katika mpangilio wetu wa kazi.Kuanzia kesho tutaelekeza nguvu katika kuchunguza kama Team SC41 walihusika katika kifo cha Edson.Tutaupata ukweli wa jambo hilo kwa kumchuguza Peniela.Tukifahamu mahusano yake na Team SC41 basi itatuwia rahisi sisi kufahamu kama walihusika katika mauaji ya Edson na kwa nini.” Akasema Mathew
“ Kuna zile kamera mbili ulizozitega nyumbani kwa penny zinaweza kutusaidia sana kufahamu nyendo zake”akasema Anitha
“Kweli Anitha.Kamera zile zitatusaidia sana kufahamu kila kinachoendelea nyumbani kwa Penny lakini hata hivyo tutawatumia rafiki zake wa karibu,Jason na Elibariki katika kupata taarifa tunazozihitaji”akasema Mathew
*******
Miili ya vijana sita waliouawa katika mapambano na akina Mathew ikawasili katika makazi ya John Mwaulaya ambako vijana wote walikuwa wamekusanyika.Gari lile ilimokuwamo ile miili ilikuwa imechafuka kwa damu.Osmund alitaarifiwa kuwasili kwa miili ile akashuka kwa kasi na kwenda kushuhudia.Alipandwa na hasira zilizochangayika na mstuko baada ya kuzishuhudia maiti zile namna zilivyochakazwa kwa risasi.
“ Whoever did this must be in our hands by sunset tomorrow “akawaza .
“ Lakini ni nani huyu ambaye anaweza kuwa amefanya kitu kama hiki? Nani huyu ambaye anathubutu kucheza na team SC41 na kuua vijana wetu sita? Hii haijawahi kutokea kuanzia kuanzishwa kwake.Lazima tuwatafute watu hawa na tuwafahamu ni akina nani.” Akaendelea kuwaza Osmund akiwa amesimama kandoni mwa gari lililobeba miili.Mara akastuliwa na sauti ya Victor
“ Bosi, kile kidole ulichoniambia nikichukue hiki hapa.”akasema Victor na kumkabidhi kidole gumba cha mkono wa kulia ambacho kilikuwa ndani ya kifuko kidogo cha nailoni
“ Poleni sana Victor” akasema Osmund
“ Ahsante sana bosi.Yalikuwa ni mapambano makali .Ilikuwa ni kama vita” akasemaVictor
“ Watu hawa ni akina nani?
“ Ni vigumu kusema ni akina nani lakini ninaweza kusema kwamba watu wale ni wapiganaji hasa wenye ujuzi na uzoefu wa hali ya juu.Wanatumia vifaa vya hali ya juu vya mawasiliano.They are professionals.Hata yule mwenzao tuliyemuua alikufa wakata kiwakinga wenzake wasishambuliwe na risasi ” akasema Victor
“ Tukimfahamu huyu mwenzao ni nani basi tutaweza kuwafahamu watu hao ni akina nani”akasema Osmund
“ Kitu kingine,nimeahirisha mazishi ya vijana wetu niliyokuwa nimepanga tuyafanye usiku wa leo.Vijana wetu wamekufa kishujaa na tutawazika kwa heshima zote.Kuanzia kesho tutaanza kuwazika mmoja mmoja katika makaburi tofauti tofauti.Kesho asubuhi shughulikia suala hilo.Kila kitu kuhusu jambo hilo ninakuachia wewe,hakikisha mpaka kesho saa tatu asubuhi kila kitu kuhusiana na maziko ya vijana wetu kiwe kimekamilika na kuanzia saa tano tuanze kuwazika mmoja mmoja”akasema Osmund
“ Sawa bosi ninalishughulikia suala hilo.” Akasema Victor na mara simu ya Osmund ikaita akaipokea na kuiweka sikioni
“ Hallow Joseph” akasema
“ Bosi ,Edwin Mackson yupo katika laini anakusubiri”akasema Joseph
“ Ok Joseph ninakuja sasa hivi”akajibu Osmund na kukata simu
“ Victor tutaendelea na maongezi baadae lakini kwa sasa hakikisha kila aliyeumia anapatiwa matibabu na wanapewa mapumziko katika zahanati yetu kule makao makuu. Hakikisha kila kitu kimekwenda sawa,nina mambo mengi ya kufanya siku ya leo”akasema Osmund na kuondoka kwa kasi kuelekea juu ghorofani hadi katika chumba cha mikutano ya ana kwa ana kilichokuwa na runinga nne kubwa ukutani..Kwa kutumia remote control akawasha runinga namba mbili.
“ Hallow Edwin”akasema Osmund
“ Osmund .Habari za Tanzania?
“habari za huku si njema sana”
“ Kuna tatizo gani?
‘ tatizo la kwanza ni kuhusiana na ugonjwa wa John mwaulaya.Anaumwasana.Tulitegemea kumfanyia upasuaji lakini daktari tuliyemtegemea kufanya upasuaji huo hataweza tena kupatikana.Hali yake inazidi kuzorota kila dakika na kama asipofanyiwa upasuaji wa haraka tunaweza tukampoteza.” Akasema Osmund
“ Osmund,tulipokukabidhi nafasi kubwa kama hii ya kuongoza kikosi chenye nguvu kama hiki tulitegemea kwamba una uwezo wa kushughulikia masuala madogo madogo kama haya.Suala kama hili si suala la kutaka maelekezo toka makao makuu.Unatakiwa kuomba msaada wa makao makuu kama kuna jambo kubwa na zito lakini katika masuala kama haya ya ugonjwa tumewapa uhuru huko huko wa kufanya kila linalowezekana kutafuta matibabu..Umenielewa Osmund ? akasema Edwin.
“ Nimekuelewa Edwin lakini John Mwaulaya anahitaji kutibiwa.Huyu ni mtu mkubwa katika Team SC41.Suala la ugonjwa wake si la kulichukulia kirahisi rahisi namna hiyo” akasema Osmund huku akionyesha wazi kukakasirishwa na matamshi ya Edwin
“ Ni kweli John ni mtu mwenye wadhifa mkubwa katika Team SC41 lakini tunaweza tu kutoa msaada endapo utatuhakikishia kwamba mmeshindwa kabisa kumtibu.”
“ Edwin mpaka kufikia hatua hii ya kukupigia simu na kukuomba msaada ni wazi tumeshindwa”akasema Osmund
“ Sawa Osmund ,tutamtuma Dr Marcus burke atafika huko ndani ya siku mbili zijazo kuangalia ukubwa wa tatizo la John halafu atashauri nini cha kufanya”
“ Ahsante sana Edwin kwa kulipa uzito suala hili.Kuna suala lingine vile vile. “
“ suala lipi tena?
“ Kuna tatizo limetokea usiku wa leo”
“tatizo gani?
“ Kuna vijana wetu sita wameuawa katika shambulizi .”
“Mbona sikuelewi Osmund,wameuawa vipi? Nani kawaua? Akauliza Edwin
“ Bado hatufahamu ni nani lakini tumegundua kuna watu ambao wamekuwa wakitufuatilia.”
“ Umechukua hatua gani mpaka hivi sasa za kuwafahamu watu hao ni akina nani na wanataka nini? Akauliza Edwin
“Bado hatujawafahamu watu hao ni akina nani na wanataka nini toka kwetu lakini tutalishughulikia suala hilo kuanzia kesho.kwa hivi sasa ninashughulikia kwanza kuihifadhi miili ya vijana waliopoteza maisha na baada ya kukamilisha shughuli za mazishi yao kesho tutaanza rasmi kuwasaka na kuwafahamu watu hao ni nani na wanataka nini.”
“ Osmund lipe uzito mkubwa suala hili kwani ni suala zito sana.lazima tuwafahmu watu hawa ni akina nani na wametufahamu vipi na nini wanatafuta toka kwetu.Team SC41 ni kikosi kinachofanya kazi zake kwa siri kubwa kiasi kwamba hata ndani ya serikali ya marekani ni watu wachache wanaofahamu uwepo wake kwa hiyo kwa watu hao kuanza kutufuatilia ina maana kwamba tayari wanatufahamu sisi ni akina nani.Kujulikana kwa Team SC41 na kazi zetu kutahatarisha kwa kiasi kikubwa maslahi ya marekani katika afrika mashariki .Pamoja na kumtuma Dr Marcus Burke kuja kuangalia afya ya John,ataambatana vilevilena timu ya watu watatu ambao watakuja kusaidiana nanyi katika kuwabaini watu hawa ni akina nani.Nataka ndani ya kipindi kifupi tuwe tumewafahamu na kuchukua hatua zipaswazo.Nitaongea nawe tena kesho saa saba mchana kwa saa za Afrika mashariki ili kufahamu namna mnavyoendelea na kama mmekwisha wafahamu watu hao” akasema Edwin na kutoka katika laini..
“ Afadhali aje daktari toka Marekani kuja kuangalia afya ya John.Lazima apatiwe matibabu anayostahili.Hakuna sababnu ya kuendelea kusumbuka wakati kuna uwezekano mkubwa wa kumpeleka Marekani au nchi nyingine yoyote na akatibiwa ” Akawaza Osmund wakati akipanda ngazi kuelekea chumbani kwa John.Moyo wake ulifarijika sana baada ya kuhakikishiwa ujio wa Dr Burke.Aliufungua mlango wa chumba cha John na kumuomba daktari aliyekuwa akimuhudumia atoke nje .
“ Kuna nini Ossy?akauliza John kwa sauti ya chini
“ John nimeongea na makao makuu,wameahidi kumtuma daktari haraka iwezekanavyo.Ndani ya siku mbili hizi Dr Marcus Burke atakuwa amewasili kuja kuangalia afya yako na kutoa ushauri wa nii kifanyike” akasema Osmund.Pamoja na kuwa dhaifu lakini aliposikia jina la Marcus Burke John akastuka sana.Akamfanyia ishara Osmund asogee karibu
“ Umesema Dr Marcus Burke?
“ Ndiyo John.Anakuja Dr marcus Burke kuja kuangalia afya yako”
“ No Ossy.Dont let him.” Akasema John Mwaulaya
Osmund akamtazama kwa mshangao
“ Do you know him? Akauliza
“ yes I know him” akajibu John
“ John unaumwa na Dr Marcus anakuja kuangalia afya yako na kutoa ushauri nini kifanyike.Unatakiwa ufanyiwe upasuaji wa haraka ili kuokoa maisha yako“ akasema Osmund.John akaushika mkono wa Osmund na kusema
“ Osmund listen to me my boy.Ninamfahamu Dr Burke.He’s coming for one reason only”
“ One reason? Osmund akashangaa.
“ Yes.He’s coming to kill me.Please don’t let him.I need to die a natural death” akasema John na kuzidi kumshangaza Osmund
“ John nashindwa kukuelewa una maanisha nini.Dr Marcus anakuja kuangalia afya yako na si kukuua” akasema Osmund
“ Osmund please listen to what I’m telling you.Nilikataa kwenda kutibiwa marekani kwa sababu nilifahamu lazima wataniua.”
“ kwa nini wakuue John?
“ Kuna siri nzito ambayo hauifahamu kwa hiyo tafadhali usimruhusu Dr Burke kuja kuniangalia.Ninajua sina maisha marefu sana lakini ninataka nife kifo cha kawaida.”
“ John ni siri gani hiyo ambayo ingepelekea uuawe endapo ungeenda kutibiwa marekani?
“ Siwezi kukwambia Ossy.Ni siri ambayo nitakwenda nayo kaburini.” Akasema John.
“ John unataka nikusaidie na wakati huo huo unanificha siri uliyonayo.Tafadhali niambie na nitakusaidia”
“ Hapana Osmund siwezi kukwambia.Lifanyie kazi hilo nililokueleza .You can go now I need to be alone.”akasema John.Osmund akamtazama na kuondoka .
“Nitakufa hivi karibuni.Sifahamu kama ninaweza kusamehewa kwa mambo niliyoyatenda hapa duniani.Nimefanya mambo mengi mabaya lakini kuna jambo moja tu linalonipa faraja hata kama nikifa muda huu nitakufa huku nikitabasamu.I didn’t kill an Innocent child.I didn’t kill Peniela” akawaza John na kumbu kumbu zikamrudisha May 30 1990
30 May 1990
Gari la kifahari linafunga breki katika maegesho ya shule ya kimataifa ya watoto wadogo.John Mwaulaya anashuka ndani ya gari lile huku akivuta sigara .Kwa mbali akasikia kelele za watoto wakicheza.Akachukua simu na kumpigia mtu aliyekuwa akimtafuta.Baada ya dakika tano akatokea Bi Bernadetha mlezi wa kituo cha yatima anakoishi Peniela
“hallo mama Bernadetha.Habari za siku?
“ habari nzuri sana John.Pole na safari”
“ahsante sana mama nimekwisha poa.NashukuruMungu nimerejea salama.Peniela anaendeleaje?
“ Peniela anaendelea vizuri sana na zawadi zote ambazo umekuwa ukimtumia kutoka Marekani amezipata na anafurahi sana.John unamjali sana mwanao .Kwa nini lakini hutaki akuone wala akujue?
“ Mama Bernadetha,kama nilivyokwambia siku ninamkabidhi kwako ,sihitaji Peniela anifahamu kwa sasa.Hii ni kwa ajili ya usalama wake .Yuko wapi mida hii?nahitaji kumuona”akasema John.Bi Bernadetha akamchukua John na kumpeleka katika ofisi ya mkuu wa shule ile na kumtambulisha kama mfadhili wa Peniela.Waalimu walifurahi sana kumfahamu John na kumpongeza kwa namna alivyojitolea kumsomesha peniela katika shule ile ya gharama kubwa.Wote walimsifu Peniela kwamba ni mtoto mwenye bidii sana ya kujifunza.John akaomba akaonyeshwe mahala alipo Penny,akaongozana na mwali mmoja pamoja na bi Benrnadetha hadi katika uwanja wa michezo,kulikokuwa na michezo mbali mbali.Peniela alikuwa amejumuika na watoto wenzake wakicheza na kuruka kwa furaha.John alihisi furaha ya ajabu baada ya kumuona Peniela.
“She’so cute.Ni mtoto mzuri na mrembo.Nitahakikisha kwa kila nitakavyoweza anakuwa na maisha yenye kujaa furaha kubwa” akawaza John huku uso wake ukiwa umepambwa na tabasamu .Alitamani akae pale kwa siku nzima ili aendelee kumuangalia peniela .
“ Natamani kama ningekuwa na mke ningemchukua Peniela niishi naye.Kwa mara ya kwanza natamani na mimi kuitwa baba lakini kazi hii hainiruhusu kuwa na familia.Anyway nitaendelea kumtunza Peniela kwa siri .”akawaza John halafu akaondoka na kurejea garini.Akafungua albamu lililojaa picha za Peniela ambazo alikuwa akitumiwa na Bi Bernadetha wakati akiwa kikazi nchini marekani
“ You are such a cute baby.I’ll take a good care of you Penny.You’ll never see me but I’ll always take very good care of you.”akasema John.
********
“ Mathew ..mathew..” akaita Anitha na kumstua Mathew toka katika usingizi uliokuwa umempitia. Aliitazama saa yake ilipata saa kumi na dakika kumi na tatu.Mbele yake walikuwa wamesimama Anitha,Dr Michael na Dr Robert.
“ Pole sana Mathew” akasema Dr Michael huku akitabasamu
“ Sorry nilipitiwa na usingizi kidogo “
“ Usijali Mathew,ni kutokana na zile dawa nilizokupa.Zina nguvu sana “akasema Dr Michael
“Nini kinaendelea Dr Michael? Akauliza Mathew
“ Tumemaliza kuzifanyia uchunguzi zile sampuli ingawa imetuchukua muda mrefu”
“Good.tayari mna majibu?
“Ndiyo Mathew,tayari tuna kila kitu” akajibu Dr Michael na kuketi kitini.
“ Mathew kilichosababisha kifo cha mke wa rais ni sumu iitwayo Spinolin .Tumekuta chembe chembe za sumu hii katika sampuli ya ini tuliyochukua.Sumu hii inapatikana katika dawa iitwayo Encozynes ambayo hutumiwa na watu wenye shinikizo la damu.Matumizi ya dawa hii mgonjwa hutumia mara moja kila baada ya mwezi mmoja tena kwa kiwango kidogo kwa sababu endapo ikitumiwa kwa kiwango kikubwa ina madhara makubwa na husababisha kifo kwa mgonjwa.Inaonekana mke wa rais alichomwa kiwango kikubwa cha dawa hii na hivyo kusababisha kifo chake.Nina mashaka na mtu aliyemchoma dawa hii kama alikuwa akifahamu madhara yake au alidhamiria kufanya alichokifanya.Inatakiwa kuchunguza ni nani aliyemchoma sindano hiyo kama ni daktari wake au ni mtu mwingine ili kufahamu dhamira yake ilikuwa nini .” akasema Dr Michael na kumkabidhi Mathew bahasha iliyokuwa na majibu ya vipimo walivyovifanya
“ Ahsante sana Dr Michael.Nashukuru sana kwa msaada wako.”akasema Mathew akasimama.Akapeana mkono na Dr Robert wakaagana wakaingia garini na kuondoka
“ Dr Flora alichomwa sindano iliyokuwa na kiwango kikubwa cha dawa tofauti na inavyotakiwa.Hapa inaonyesha wazi kwamba aliyemchoma alidhamiria kumuua.Naikataa hoja ya kwamba mchomaji hakuwa na ufahamu kuhusu madhara ya dawa ile.Ni nani basi aliyemchoma sindano ile na kwa nini? Hilo ndilo swali ambalo tunatakiwa kujiuliza kwa sasa.Tukimfahamu ni nani aliyemchoma Dr Flora sindano ile tutakitegua kitendawili hiki.” Akawaza Mathew wakiwa garini wakirejea nyumbani
“ Mathew ! akaita Dr Michael
“ Nimeikamilisha kazi yangu.Nadhani hatudaiani tena” akasema .Mathew akatabasamu kidogo na kujibu
“ Ahsante sana Dr Michael kwa msaada huu mkubwa.Pole sana kwa misukosuko mikubwa iliyokupata katika siku ya leo.Ninatumai ni mara yako ya kwanza kupitia misukosuko mikubwa kama hii.Ninashukuru kwamba baada ya misuko suko kumalizika nyote mu salama.Wewe na familia yako yote mko salama salimini.Hatuna deni tena mimi na wewe lakini ninachoweza kukushauri ni kwamba usifikirie kwenda nyumbani kwako wala kazini katika kipindi cha wiki moja au mbili mpaka hapo tutakapohakikisha kumekuwa salama.Wale jamaa wataendelea kukutafuta bila kuchoka hadi wahakikishe wamekutia mikononi.Kama hutajali naomba wewe na familia yako muendelee kukaa pale kwangu hadi hapo tutakapohakikisha kwamba hali ya usalama imeboreka.” Akasema Mathew.Dr Michael akatabasamu na kusema
“ Mathew nakiri kwamba kwa mara ya kwanza uliponifuata pale ofisini kwangu na kunielekezea bastora nilikuchukia mno.Nilikuona ni mtu mbaya sana na kwa hasira nilizokuwa nazo nilitamani hata nitafute kitu nikupige nacho nikuue kabisa.Lakini baada ya kukaa nawe kwa saa kadhaa nikagundua kwamba uko tofauti na nilivyokuwa nakufikiria.Wewe ni mmoja wa mashujaa wa taifa hili.Wewe ni kijana mwenye roho nzuri na huruma.Sina shaka yoyote kuhusu kukaa pale kwako ambako ni sehemu salama sana kwangu na kwa familia yangu kwa sasa lakini baada ya matukio ya leo tayari nimekwisha fanya maamuzi.Ninaondoka hapa nchini.”
“Unakwenda wapi?
“Mwezihuu nilikuwa namalizia mkataba wangu wa miaka mitano na hospitali ile ninayofanya kazi .Tayari nimekwisha pata kazi nyingine nchini Philipines katika jiji la manila.Ninataka kuelekea huko.Sitaki kuendelea kupoteza muda tena hapa.Kwa maana hiyo basi kuna jambo moja ambalo nitataka unisaidie.”
“Hizo ni habarinzuri.Umefanya maamuzi mazuri na familia yako itaendela kuwa salama.Ni kitu gani ambacho unataka nikusaidie?akauliza Mathew
“ Ninahitaji unisaidie kupata ndege .Kwa sasa mimi na familia yangu hatuwezi kutoka na kuanza kuzunguka kutafuta ndege.Naomba unisaidie kuifanya kazi hiyo.Nataka ndege ya kunitoa hapa na kunifikisha afrika ya kusini na kutokea pale nitakuwa salama. “ akasema Dr Michael
“ usijali kuhusu hilo Dr Michael ,tukifika nyumbani Anitha ataingia mtandaoni na kuangalia kama anaweza akapata ndege ya kukufikisha Afrika ya kusini na pale unaweza ukawa salama kutafuta ndege ya kuelekea kokote unakotaka”akasema Mathew
“Nitashukuru sana Mathew.”akasema Dr Michael na safari ikaendelea
Saa kumi na moja na dakika ishirini na saba wakawasili nyumbani kwa Mathew.Ni Noah peke yake ambaye hakuwa amelala licha ya kuwa na maumivu makali ya mguu.
“ Poleni sana.”akasema Noah
“Ahsante Noah.Elibariki yuko wapi? Akauliza Mathew,Noah akamfahamisha kwamba yuko chumbani amelala,akamfuata akamuamsha
“ Mathew !!..akasema jaji Elibariki kwa uchovu uliochanganyika na maumivu ya kidonda alichokuwa nacho kichwani mahala alijkopigwa chupa na Jason.Akaitazama saa yake ilikuwa ni saa kumi na mbili kasoro za asubuhi.
“Its morning.!! Akasema
“ yah ! Kumekucha.”
‘ Kuna taarifa gani ?akauliza Elibariki
“ Ile kazi yako imekamilika.”
“ Thank you Lord ! akasema
“Ripoti ya uchunguzi hii hapa.kwa ufupi tu ni kwamba Dr Flora alichomwa dawa iitwayo Encozynes yenye kiambata kijulikanacho kama Spinolin.Dawa hii hutumiwa na watu wenye matatizo ya shinikizo la damu lakini ni kwa kiwango kidogo sana.Mgonjwa akipewa dawa hii kupita kiwango chake basi husababisha kifo ndani ya muda mfupi kutegemea na kiwango alichopewa.Kwa hiyo tunatakiwa tuchunguze ni nani aliyemchoma dawa hiyo na kwa nini alimchoma.Tukimpata mtu aliyemchoma tutakitegua kitendawili hiki”akasema mathew
“ Kwa maana hiyo kuna kila dalili zinazoonyesha kwamba Dr Flora aliuawa kwa kuchomwa kwa makusudi sindano ile .Na hii ni sababu kumekuwa na jitihada kubwa za kutaka kuzuia uchunguzi wa kifo cha Dr Flora usifanyike kwa sababu waliogopa itabainika kwamba aliuawa.” Akasema Jaji Elibariki
TAYARI MATHEW ANA MAJIBU YA KILICHOMUUA MKE WA RAIS,NINI KITAFUATA? KWA NINI JOHN MWAULAYA ANAMUOGOPA DR MARCUS BURKE? TUKUTANE TENA KATIKA SEHEMU YA MWISHO YA SEASON ONE YA SIMULIZI HII YA KUSISIMUA…..………………
“
No comments
Post a Comment