MATOKEO YAKE HAUTAFANIKISHA
Hellow.
Nipende kukusalimu sana ndugu msomaji wa makala zetu za JocheApp.
Leo natamani tuongelee jambo ambalo ni muhimu kulizingatia katika maisha yetu kama watu wenye mitazamo na mlengo mkubwa wa kufanikiwa katika maisha ya kila siku.
Mahangaiko ya kubadilisha maisha ni halisi na huwa ni vigumu kuikamilisha kwa kufunga macho na kufungua. Kuna gharama na pia kuna kujitolea sana hasa kama unajua nini unakitaka na dira ya unapokwenda unaielewa.
Ninachotaka kuongea nawe ndugu msomaji ni kwamba, “ni vigumu kufanikisha malengo yako kama utajali ni nini watu wanakuwazia”.
Ni sentensi nyepesi kwa kuisoma lakini ina madhara makubwa sana katika maisha ya mtu ambaye hana msimamo na maisha yake. Ni kweli tuna marafiki na pia tuna ndugu na tuna watu wasio ndugu wala sio marafiki ambao wanatuzunguka. Nimewaongelea hawa watu ambao wasio marafiki wala ndugu kwa maana pia ni sehemu ya watu ambao katika maisha tunakuna nao na kwa namna moja au nyingine wana impact pia katika maisha yetu ya kila siku.
Ni vyema sana kupata ushauri na ni vyema kupewa dira na wanaokuzunguka au hata waliopiga hatua au hata ambao hawajapiga hatua. Maana kwa kupitia ushauri wao na mitazamo yako katika maisha yetu huwa tunapata mwanga mara pale tunapopotea njia.
Upande wa pili sasa ambao ni mtu binafsi anayeshauriwa ni vyema kujifuanza kuchuja ni kipi kinafaa na kipi hakimfai, kipi kitamletea matokeo chanya kwa haraka zaidi yasiyo na madhara hasi. Maana kuna wakati unaweza kuchagua ushauri ambao utakuletea matokeo uliyokuwa unayahitaji kwa haraka lakini nyuma yake madhara hasi yanaambatana na wewe.
Hivyo ni nini basi unataka kufanya? Au unakifanya? Je ni shule? Je ni kazi? Je ni biashara? Je ni mahusiano?
Katika vyote hivi ukitaka kufanya kila mtu atakuja na ushauri wake na fikra zake:
Wapo watakaokuunga mkono (japo uanza kupata changamoto unaweza usiwaone),
Wapo watakaokupinga (japo ukianza wanaweza kukusapoti)
Wapo watakaokuwa katikati tu (kwamba ukifanya sawa usipofanya sawa)
Ukiwa na kazi wapo wanaowaza na wapo watakaopata nguvu ya kuja kukuambia hisia zo juu ya jambo husika wazi wazi wengine utaona kwa matendo na mengine utaona kwa vitendo hizi zote ni namna ya kufikisha meseji kwako juu ya uhalisia wa kile wanachowaza.
Kumbuka
“Kila tendo/neno ambalo mtu anaongea na wewe au anafanya kuna meseji nyuma yake anaiwasilisha”
Sasa hapo ni wewe tu unaitafsiri vipi hiyo meseji unayofikishiwa.
Hivyo basi unapotaka kufanya jambo amua ndani ya Moyo wako pima kwa mizani yako binafsi maana changamoto na mafanikio yake yatakurejea wewe. Jitofautishe na mitazamo hasi pindi utakapo amua kupiga hatua katika jambo unaloliendea.
Nikutakie Asubuhi njema na Harakati njema siku ya leo.
“JocheApp”
_______________________________________________
Author: Joseph G Mrema
Contacts: 0712 851687
Email: josephgeotham4@gmail.com
07th Nov 2018
No comments
Post a Comment