USIACHE KUTENDA WEMA

Habari za muda huu msomaji wa makala zetu za JocheApp. Leo nimekuletea kisa kifupi chenye mafunzo tele. Karibu na ungana nasi.

Mwanamke mmoja alikuwa akifanya kazi katika kiwanda cha kusindika nyama.

 ​Siku moja baada ya kumaliza kazi zake pale kiwandani alienda katika chumba chenye freezer (cold room) ambako nyama zilikuwa zikihifadhiwa kukagua baadhi ya bidhaa.​

Kwa Bahati mbaya wakati yupo kwenye hicho chumba katika harakati za apa na pale akausukuma mlango, ukajifunga na kijilock. 

Hakukuwa na msaada wowote wa kuweza kuufungua mlango ule. 

💦   Alianza kulia na kupiga kelele za kuomba msaada wa kufungiliwa, lakini kelele zake hazikuwa rahisi kusikika nje ya hicho chumba kidogo, na wafanyakazi wote pale kiwandani walikuwa washaondoka.

🗝  ​Masaa mawili baadae akiwa katika hali ya kukaribia kukata roho kutokana na baridi kali iliyoko kwenye hicho chumba,​

​Ghafla mlinzi wa geti la kiwanda hicho alifungua mlango alimokuwamo yule mwanamke.​

Alitahamaki kumkuta mwanamke yule katika hali ile mbaya. 

Bhasi jitihada za kumpa huduma ya kwanza kumpeleka hospitali ikafuata. 

💡Baada ya kutolewa na kupata nafuu alipata wasaa wa kumuuliza yule mlinzi ilikuwaje na akafungua mlango wa cold room wakati ilikuwa si ratiba yake na vile vile ilikua si kazi yake?.

Maelezo ya yule mlinzi yakawa kama ifuatavyo 

🌵​''Nimefanya kazi kwenye hichi kiwanda kwa miaka 38 sasa, mamia ya wafanyakazi wanatoka na kuingia kiwandani lakini wewe peke yako kati ya wote ndiye uliyekuwa ukithubutu kunisalimia asubuhi na kuniaga kila jioni unapoondoka kiwandani"​ 

Ulipokuja kazini asubuhi ulinisalimia kama kawaida na kunijulia hali. 

​Lakini baada ya kazi na wafanyakazi kuanza kutoka kurudi, Nilitegemea kusikia salaam yako, niliendelea kusubiri lakini cha ajabu mpaka watu wote wakawa wametoka na wewe sikuona sura yako,​

🌳Nilianza ingiwa na maswali mengi,na ndipo nikapata wazo la kuanza kuzunguka maeneo yote ya kiwanda na baadae chumba baada ya chumba.

Na ndipo nilipokukuta kwenye chumba cha barafu.​

FUNZO;

​Ishi vizuri na kila mtu,  mheshimu kila Mtu bila kujali hadhi yake,ukubwa wala udogo wake, kwani hujui ya  kesho utakuwa au atakuwa wapi na kugeuka kuwa MSAADA kwako.​Maana tunategemeana maishani.Hivyo tutumikiane kwa Upendo na kuheshimiana watu wote daima.

“JocheApp”
_______________________________________________

Source: Unknown

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...