APPLE (MATUFAA) KWA AFYA,LISHE NA TIBA

"An apple a day will keep the doctor away An apple before bed makes the doctor beg his bread" 

(kula tunda moja la tufaa kila siku humfanya mtu asiwe na haja ya kuonana na daktari kula tunda la tufaa kila siku 

humkosesha daktari mapato yake). Misemo hii ya Waingereza inaonyesha umuhimu wa matunda ya matufaa 

kwa ajili ya kudumisha afya ya binadamu, kukinga na kutibu magonjwa mbalimbali. Matufaa yana Vitamini K, 

nyuzinyuzi za chakula pamoja na dawa-lishe (phytochemicals) aina ya quercetin flavonoid.


Faida za kiafya

Matufaa ni tiba nzuri ya ugonjwa wa kuharisha.

Husaidia katika matibabu ya uvimbejoto wa utumbo (colitis)

Husaidia katika matibabu na kuzuia shinikizo la damu

Husaidia katika tiba na kuzuia magonjwa ya mzio (allergy) pamoja na pumu ya mapafu.

Hutibu tatizo la kupata choo kikavu au kutokupata choo (constipation)

Ni dawa nzuri sana kwa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.

Husaidia katika matibabu na kuzuia mawe katika figo.

Hupunguza hatari ya kupata saratani ya mapafu, saratani ya utumbo na ugonjwa wa kisukari.

Huimarisha afya ya ini.

Husaidia figo kuondosha sumu aina ya uric acid ndani ya damu.

Matumizi na kipimo

Kwa ajili ya tiba kula matufaa kiasi cha kilo mbili kila siku kwa muda wa siku saba mfululizo.

Kunywa juisi ya matufaa bilauli moja kila baada ya saa nane kila siku.


JocheApp

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...