UNAKULA MEMA YA NCHI? AU MAKOMBO YA NCHI?
Unakula mema ya Nchi au Unakula Makombo ya Nchi?
Inawezekana kuwa ulizaliwa na kukuta mazingira si mazuri kwako.
Inawezekana ulizaliwa na kujikuta una maumbile fulani ambayo unadhani yamekuzuia kwenda mbele.
Inawezekana kila ukijaribu jambo unaishia kupoteza.
Inawezekana imekuchukua miaka mingi, kila unalo jaribu kufanya linafeli, umedhulumiwa, umepoteza na umepotea.
Dhambi KUBWA unayoweza kuifanya na ikakumaliza ni kujiona umeonewa, hufai, hujiwezi na kukata tamaa.
DUNIA haina huruma kwa binadamu mwenye sababu za kwanini hawezi, hata kama ni kweli zipo.
LAZIMA UTAFUTE WAPI PA KUTOKEA NA SI KUTOA SABABU KWANINI HUWEZI KUTOKA.
Kuna kauli huwa napenda kutumia "Whatever means necessary" iwe ni kwa njia yoyote halali hata ikibidi kuvunja utaratibu.
Chunguza watu wanaokufa na kumalizwa kila siku kwa kukubali matokeo .
Dunia haiwezi kumpa nafasi yule aliyejikatia tamaa hata kama ameonewa.
Dunia haiwezi kumpa nafasi yule aliyejikatia tamaa hata kama ana mapungufu ya kimwili.
Dunia inayo nafasi kwa binadamu mbishi tu.
Maisha hayaangalii uso wa mtu. Hata kama upo katika mazingira magumu vipi usipokomaa utatokomezwa na kusahaulika.
Hujawahi kukutana na mtu amelala barabarani , hajiwezi , hajala, anaumwa na wengine wanakufa njiani no body cares.
Sikia nikuambie, kuishi duniani yataka moyo. Ukiwa mlegevu utaishia kula makombo wakati wengine wanakula mema ya Nchi.
Siyo wote wanakula mema ya nchi.
Wapo wanaokula makombo ya nchi.
Wengine hata makombo wanakosa.
Maisha si kutuwama kama maji taka dimbwini kutokana na mabonde na miinuko unayokutana njiani bali ni kutembea na kuendelea bila kukata tamaa.
Mambo makubwa ya maisha yamefanywa na watu walioendelea kujaribu, kupigana hata katika mazingira ambayo hayana matumaini kwao.
Waswahili husema Kabla ya kukata tamaa , jaribu tena.
Mimi sijui wewe unapitia maisha gani?
Labda utasema maisha yananionea mara utasema sijui mimi sina bahati…
Why me?
Ukiendekeza why me...utakufa unalia badilisha na kusema why not? Why not me? Why not me?
Maisha ni magumu sawa, tena ni magumu kweli lakini hayawezi kuwa na nguvu kwa mwanadamu aliyeamua kuwa mgumu na mbishi zaidi.
Kumbuka kuwa wanadamu wanaofanikiwa siyo tu wale wenye vipaji pekee au wenye viungo vilivyokamilika mwilini bali ni wale walioamua kupambana na kila aina ya mawaa bila kukata tamaa. Hujawahi kukutana na walemavu matajiri?
Hujawahi kukutana na kipofu Tajiri?
Hujawahi kukutana na mtu asiye na miguu anamiliki gorofa. Wapo wengi tu.
Dunia inahitaji wanadamu wanaoishi, wanaoamua maisha yao na kung’ang’ania mpaka mwisho hata ikibidi kufa.
Unataka kula mema ya dunia? Jaribu kuwa jeuri kwenye kitu unachokitaka. Bora ufe unakipigania kuliko kufa umelala barabarani kwa kukosa hela ya hospitali. Nosense kabisa...
Usikate tamaa.
Narudia tena Usikate tamaa.
Usikate tamaa.
Iwe upo gizani or upo kwenye mwanga, Usikate tamaa.
Fursa 101 Africa.
SINTAKATA TAMAA.
MIMI NI SOKOWORLD.COM

No comments
Post a Comment