JIPE TUMAINI JIPYA MAANA KESHO IPO
Imeandikwa na Joche toka JocheApp
Habari Ndugu mfuatiliaji na msomaji wa makala zetu za kuelimisha na kuhamasisha watu mbalimbali kupitia Application yako ya JOCHEAPP
Leo natamani kuongea na wapambanaji katika changamoto za kila siku katika ulimwengu huu uendao kasi na mambo yake
Awali ya yote niwapongeze wanafunzi wote wale walio katika mfumo wa kikanuni yaani rasmi wa kukaa darasani na hata wale ambao hawakai darasani lakini wanajifunza...
Nisiwasahau kuwasalimia na kuwatia moyo wale ambao hawajapata cha kufanya maana wanaona hawana kazi wala hawasomi.... nina neno moja Kwenu FANYA KAZI YOYOTE malipo/faida ni kama ZAWADI usikubali kukaa bila kuwa na lakufanya.
Siku ya Leo nina jambo moja natamani kukuambia nalo ni:-
USIPOTEZE TUMAINI KWA JAMBO/MAMBO ULIYOYAPATA LEO, HUWEZI IJUA SIKU YA KESHO INAVITU GANI
Hapa kwenye tumaini ni eneo la msingi sana kama kijana kuwa nalo...
Haijalishi uliuza Ubuyu ukaharibikia dukani haukuisha na leo umeenda umekuta umeshatia ukungu, usivunjike moyo inua moyo wako jipe TUMAINI kesho ipo usikate tamaa
Haijalishi ulifuga mifugo ikafa au walivunja wakaiba na kuondoka nayo... usikate Tamaa Jipe Tumaini Kesho inakuja inuka na anza hapo ulipokwamia utavuka tuu
Haijalishi ulilima na mvua zikagoma... piga hesabu zako upya anza tena usipoteze Tumaini kesho inakuja
Haijalishi shule inakwama na unapata matokeo ambayo sio mazuri suluhisho sio kuacha ila kaza mwendo ungeza bidii utavuka
Mwanafalsafa mmoja alisema... HUWEZI KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOKUKABILI KWA KUTUMIA AKILI/NJIA/MPANGO ULE ULE ULIOLETA HIYO CHANGAMOTO
Maana yake ni nini?
Ili uweze kuvuka changamoto inayokufanya usisogee mbele ni lazima utafute maarifa ya zaidi kuliko changamoto inayokusumbua na kukufanya usipige hatua.
Soma Vitabu vyenye mlengo wa eneo ambalo unafanya litakusaidia kukuimarisha na kukuinua zaidi.
Soma VITABU SAHIHI ni chakula cha Nafsi/Roho ili kuiimarisha roho yako isimame upya kwa ujasiri mpya na Roho wa Mungu akiwa Pamoja nawe...
Epuka Marafiki wasio na faida katika maisha yako.
Pata muda wa kujikagua kwa kila hatua unayopiga katika Maisha yako.
NIKITAKIE WAKATI MWENA NDUGU YANGU.
*NEVER LOSE HOPE, TOMMOROW IS COMING*
TUKUTANE TENA WAKATI MWINGINE MUNGU AKITUPA UZIMA.
_______________________________________
Mwandishi: Joseph Geotham Mrema
Mawasiliano: +255 712851687
Barua Pepe: josephgeotham4@gmail.com
Application: JOCHEAPP
_______________________________________
No comments
Post a Comment