TUNAKWAMA WAPI?

Imeandikwa na Joche

• Ni kweli wewe ni kijana ambaye umekamilika kabisa.

Kijana mwenye maono
Kijana mwenye ndoto 
Kijana mwenye kiu
Kijana mwenye nguvu

Lakini changamoto zimekuandama kila mahali, hakuna mahali unaposhika pakashikika lakini pia hakuna jambo umefanya likakamilika.

Nguvu unayo, akili unayo, kusoma umesoma, sasa TUNAKWAMA WAPI?

• Wewe ni Mpenda dini tena dini yako ni safi.

Umepita kila hatua
Umepitia kila aya na kila kitabu
Umesoma majarida kadha wa kadha
Umefanya bidii ya kila hali

Lakini kila inapokuja changamoto kidogo unakwama, unapoteza mwelekeo, unakosa kiu ya kusonga mbele.

Nyenzo unazo, kanisa/msikiti upo, vitabu unavyo, elimu ya dini unayo, sasa TUNAKWAMA WAPI?

• Ni kweli wewe ni mwanafunzi tena wa shule nzuri au chuo kikubwa tu.
Unafundishwa na walimu wazuri wenye wasifu wa kutosha tena wanasifa nzuri ndani na nje ya shule/chuo

Kusoma unasoma
Kuhudhuria class unahudhuria
Kuandika notes unaandika
Kufanya discussion unafanya

Pamoja na hayo yote na bidii zote kuna mahali unateleza swali la Msingi TUNAKWAMA WAPI?

Kwa mifano michache hiyo nakumbuka hadithi  fulani ya zamani kidogo nitaisimulia kwa kifupi.

Hapo zamani za kale palitokea nchi moja kubwa sana yenye mfalme mahiri mno mno ambaye aliweza kuwaunganisha watu wa nchi yake kuwa kitu kimoja.

Mfalme huyu aliweza kuimarisha jeshi la nchi yake kwa kiwango ambacho haikuwahi kutokea katika nyakati zile.

Siku moja ilitokea Vita kubwa sana ambayo walikuwa wamevamiwa na maharamia waliotoka mbali.

Changamoto ikatokea pamoja na kuwa na jeshi kubwa bado walishinda kwa kuhangaika sana.

Na jambo hilo ni ukosefu wa SHABAHA ndani ya ASKARI WAKE, walikuwa hawana uwezo wa kulenga maadui zao. Na hiyo iliwafanya wanajeshi wengi kupoteza maisha na hata maharamia wale wakashinda vita ile.

Watu wengi tumekosa kufanikisha mambo yetu kwa sababu ya ukosefu wa shabaha.

Ndio maana nikaanza na msemo wa Kiingereza

FROM NOW ON AND FOREVER

Nikimaanisha IWE SASA HIVI NA MILELE.

Yaani sasa hivi ndio wakati sahihi wa kutafuta shabaha hasa kiini cha kukufanya usogee ulipo cha kukufanya uvuke hatua moja kwena nyingine cha kukufanya ushinde kila jambo linalokuja mbele yako.

Ni Vijana wengi tumekosa SHABAHA katika maisha yetu.

Kila kinachokuja mbele tunataka kufanya, ukisikia kuuza UBUYU Kunalipa na wewe UMO, ukisikia KUUZA kuuza MAPOCHI kunalipa na wewe umo unaunga, ukisikia MASOMO ya Biashara yanalipa na wewe Umo,  YAANI HUELEWEKI.

Lazima UFANYE LEO NA IWE HIVYO MILELE.



Nikupitishe kwa watu wachache duniani waliofanikiwa kwa KUAMUA KUJIKITA KATIKA JAMBO MOJA na wakakomaa nalo leo WAMEFIKA KILELE cha MAISHA YAO ya Mafanikio katika Dunia hii.

Mmoja wao ni BILL GATE huyu alianza biashara yake na kuiwekea nguvu tangu akiwa kijana mdogo sana na sasa ni mzee bado anayo.

Kuna mtu mwingine anaitwa Jack Ma huyu nae alianza kujishughulisha na Biashara yake tangu enzi hizo mpaka leo ni mtu mwenye miaka mingi

Kuna mwingine anaitwa Warren Buffet huyu alianza kuwekeza katika Soko la HISA tangu akiwa mdogo kabisa lakini mpaka leo ni mzee kabisa lakini bado kajiwekeza hapo.

Nilitaka kumsahau Bakhressa huyu wa Azam naye alianza kuuza vitafunio katika mgahawa wa muhindi mpaka sasa unatumia bidhaa zake ni kwasababu hakukata tamaa.

Cha Msingi hawa watu wamefanikiwa kwa sababu ya kuwa na shabaha katika maisha yao.

Walijua nini wanataka.
Walikutana na changamoto kama ambazo wewe pia wazipitia lakini bado walisimama na kusonga mbele.

Sasa:

Maamuzi ni yako kuamua nini unataka, wapi unataka kufika.

Amua leo kubadilisha mfumo wa maisha yako, amua leo kubadilisha dira ya maisha yako, amua leo kubadilika kuwa mtu wa mazoea na kuwa mtu wa malengo, amua leo kuiishi kesho yako leo au kuuishi jana yako leo.

Asante kwa kunipa muda wako.

Mungu akubariki sana.
_________________________________________
Author: Joseph Geotham Mrema
Calls& Whatsapp: +255 (0) 712 851 687
Email: josephgeotham4@gmail.com

DOWLOAD JocheApp NOW


Joche Team

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...