NGUVU YA KUKOSOLEWA
JE USHAWAHI KUSIKIA MAISHA NI SAFARI?
Je Unafahamu maisha bila wakosoaji na washauri huwezi kufika unapopata?
Lakini unafahamu njia iliyo sahihi ni kuwapenda wanaokuchukia kwa wazi na kwa siri maana hukusaidia kujua wapi unatakiwa kukaza zaidi na wapi upaache.
Kuwa mwangalifu sana ukifanya jambo ukaona jamii yote hakuna anayekukosoa jiulize sana sana lakini pia ukiona unafanya jambo jamii nzima inakuchukia jichunguze.
Nazungumzia NGUVU YA KUKOSOLEWA
Kiuhalisia hakuna binadamu anayependa kukosolewa.
Iwe ni mtoto mdogo, mtu mzima, mzazi au hata asiye na mwelekeo.
Kila mtu anapenda kusifiwa kila mtu anapenda kupendelewa kwa namna moja au nyingine.
Akinunua gari asifiwe gari yako ni nzuri,
Akinunua saa atataka aambiwe saa yako nzuri,
Akioa/ kuolewa atataka aambiwe mtu wako ni perfect,
Akisema jambo atataka aambiwe umeongea point kubwa sana,
Akisoma atataka asifiwe wewe ndio msomi kuliko wote
Nakadhalika na kadhalika
Hakuna aliye tayari
Kusikia au kuambiwa hili ni jambo bovu, baya, halifai halina mwelekeo.
Hiyo staili ya nguo haikufai
Hayo maneno yako ni mabovu
Hiyo biashara ni mbaya haina faida
Hiyo elimu unayosoma unapoteza muda utakwama mbeleni
Huyo mtu sio sahihi kwako.
Na huu ndio ulimwengu ambao wengi wanauchukia.
Binadamu hataki kukosolewa. Ukimkosoa tu mmegombana.
Lakini Kiuhalisia KUKOSOLEWA KUNAKUSOGEZA KARIBU NA MAFANIKIO YAKO.
Unamkumbuka Samsoni kwenye Biblia.
Alikosolewa juu ya yeye kujihusisha na wanawake wa Kifilisti lakini hakutaka kusikia. Angalia mwisho wake ulikuwaje.
Mtu akikukosoa chukua hatua, Yaliyopita yamepita, ulipodondoka umedondoka, ulipoteleza umeteleza.
Lakini jambo la heri na faraja ni kwamba bado ni mzima unaweza kuibadilisha Historia yako.
Mtazame Daudi alivyokosolewa katika Jambo la Kutembea (kufanya mapenzi) na Mke wa Jemedari wake lakini pia kusababisha kifo cha Jemedari wake huyo. Alipokosolewa alijirejeza kwa upole mbele za Mungu baada ya kutambua makosa yake.
Lakini cha kushangaza sasa.
Sio kila anayekukosoa ana nia njema na safari yako au jambo lako au kitu unafanya.
Open your eyes.
Wengine ni mitazamo yao mibovu, wengine ni wivu tu wa maendeleo yako, wengine hawana sababu za msingi kisa tu wamesikia habari zako na wao wameunga tela kuendelea kuishi na maisha ya stori ile pasipo kukufahamu.
BE CAREFUL
Zingatia haya machache:
- Sikiliza kwa makini unapokosolewa (iwe kwa vitendo au kwa maneno au hisia)
- Rejea katika maisha yako halisi je ni kweli yametokea hayo au umefanya hayo?
- Tafuta ushauri kwa waliokuzidi uweze kupata ushauri wa kimaarifa au kiroho juu ya jambo husika
- Tafuta njia ya kujisahihisha (hata ukimya ni njia pia)
- Jifunze kutunza hisia zako wakati unapata mrejesho wa kazi yako (itakusaidia kujua mengi zaidi na kufahamu mitazamo iliyopo dhidi yako)
- Fanya ibada kuomba Rehema na Neema ya Mungu kwako na kwa wengine.
Nikutakie Wakati mwema
”MWENDO WAKO SI LAZIMA UFANANE NA ULE WAO WANATAKA HATA KAMA SAFARI NI MOJA”
_______________________________
Author: Joseph G. Mrema
Calls & Whatsapp: +255 (0) 712 851 687
Email: josephgeotham4@gmail.com
Usisahau kudownload APP yako ya JocheApp
Joche Team
No comments
Post a Comment