KUJITAMBUA NA SUBIRA
Imeandikwa na Joche
Habari zenu ndugu wafuatiliaji na wasomaji wa makala zetu katika Application yako ya *JocheApp*.
Muda huu ni wakati mwingine tena wa kukumbushana na kuelimishana baadhi ya mambo ambayo hujiri katika maisha yetu ya kila siku.
Ndugu zangu siku ya leo natamani nikukumbushe kuwa katika ulimwengu huu kuna vitu vitatu vigumu gumu sana.
Vitu hivyo ni kama ifuatavyo:-
1. Chuma (Steel)
2. Almasi (Diamond)
3. Kujitambua (to know one’s self)
Leo natamani kuongelea sana sana kitu cha tatu, nacho ni kujitambua.
Mwanadamu katika kukua kwake huanza kujitambua kwa kupitia njia nyingi, lakini chache kati ya hizo ni:
a. Kusikia
b. Kusoma
c. Kuona
d. Kuhisi n.k
Kwa kupitia njia hizo mwanadamu huyu huweza kujua kuwa yeye ni wa jinsia gani, kwa kupitia njia hizo huweza kufahamu lipi afanye na lipi asifanye kulingana na umri wake na jinsia yake.
Lakini cha ajabu katika mchakato huo kila mtu hujitambua kwa namna yake hasa kulingana na malezi na utamaduni unaomzunguka.
Kuna makabila au tamaduni ambazo mtoto wa kiume hafanyi kazi kabisa yeye ni kufanyiwa kazi na kufanyiwa kila kitu anataka. Huu ni utaratibu tu wa tamaduni..
Sasa katika mazingira hayo kijana huyu wa kiume akifanya hivyo huonekana anajitambua sana lakini kuna jamii nyingine huyu kijana ataonekana hajitambui
Sasa nini nataka kusema.
Dunia inakwenda kasi sana na teknolojia inakuwa kwa mapana yake pasipo kungalia unaenda nayo au upo unaipotezea.
Ni wakati mzuri sana kwa kijana wa kitanzania kujitambua hasa katika maeneo ya uwekezaji na uchumi.
Vijana wengi tumekuwa wavivu hatujitambui kuwa uchumi huu wa sasa sio wa kujengewa tena ni wa kujenga mwenyewe kwa mikono yetu.
Vijana wengi tumekuwa na mitazamo ya kutowekeza tunatamani kupata faida za hapo kwa hapo.
Hakuna aliyetayari kuwekeza 1000/- ili kesho kutwa izae 100,000/- lakini wako tayari kuwekeza asubuhi 20,000/- mchana wavune 20,005/- na wengine ndio hawataki kabisa sawa linaloitwa uwekezaji.
Hatuko tayari kutambua kuwa SUBIRA NDIO UFUNGO WA KUFANIKIWA.
Unapowekeza ni lazima ujue wapi unaelekea, nini unataka, na sababu za kutaka hilo jambo. Kama hujitambui ni vigumu kuwa na subira ya kuleta maendelea katika maisha yako.
Fahamu.
Sio rahisi kujitambua lakini na rahisi kujifunza kujitambua.
Si rahisi kusubiri lakini subira yavuta heri na mafanikio huvutwa pia.
Si rahisi kuwekeza lakini shauku hukufanyia wepesi katika hilo.
Kijana wa kitanzania usikubali kila siku ikaisha na wewe ukabaki kama ulivyo.
Tafuta jambo la kukubadilisha na kukuongeza kiakili au kitaaluma, au kifikra.
Mazingira ya kufanya hivyo yapo swala ni kutaka na kuwa na shauku nalo.
Jifunze
Kama unataka kuonekana, simama
Kama unataka kusikika, zungumza
Kama unataka kuheshimiwa, nyamaza
-(Bill Cosby)
Siri kubwa ya kuweza kufanikiwa katika biashara na katika maisha ni kuwatanguliza wengine katika kila jambo unalolifanya -(Kevin Stirtz)
————————————————
Author: Joseph Geotham Mrema
Calls &Whatsapp: +255 712 851687
Email: josephgeotham4@gmail.com
DOWNLOAD OUR APPLICATION; JocheApp
(Kwa makala nyingi zaidi)
Joche Team
No comments
Post a Comment