NAMNA YA KUFANYA SAVING YA HELA YAKO

Imeandikwa na Oscar Nyirenda

1. Unatakiwa kujua unaweza kutenga, kuhifadhi, kutotumia, Ku save kiasi gani kutokana na kipato chako.

Yaani ile hela ambayo ukiitoa ktk mapato yako, bado utaishi hata kama nikwakujibana sana maana future is yours.

Kwa mfano, kama unaweza kusema unatenga, unahifadhi, unatunza, una save, unatoa ktk matumizi yako labda sh. 200,000 au 100,000, au 50,000 au 30,000 au 10,000 au 5,000. 

Yoyote ile ambayo *ukiitunza bado utaishi*

2. Kisha jaribu kujua kama hicho kiwango (ulichoamua ktk 1. Hapa juu) unakipata kwa muda gani? Yaani Mara ngapi? Kwa mwezi, au wiki, au siku. Yaani tunasema "frequency"

Ukishajua, basi hakikisha unakibadilisha kiwe kwa mwezi. Maana yanke ni kwamba, kama unakipata/kinapatikana/ kinakuwepo kwa wiki basi zidisha Mara 4 ili upate kitakuwa sh ngapi kwa mwezi.

3. Baada ya kupata hicho kiwango cha mwezi sasa amua ita save kwa miaka mingapi???

Yaani amua *muda ambao unataka Ku save* sio lazima miaka. Inaweza kuwa miezi kadhaa au hata mwaka mmoja.

Ukishaamua kuwa unataka Ku save miezi mingapi kisha fuata hatua ya 4.

4. Chukua kile kiwango chako ulichopata kwenye kisha zidisha kwa idadi ya miezi unayotaka Ku save.

Mfano, 
Kama unaweza kuwekeza 20,000 kwa wiki, kwa mwezi itakuwa kama 80,000. 

Ukiamua unaweka kwa miezi 6 maana yake itakuwa 480,000 kama sijakosea

Baada ya kujua kuwa unaweza kuwekeza 480,000 kwa miezi 6, sasa nenda hatua inayofuata.



5. Nenda kakope 500,000 kwa rafiki yako yeyote yule au mzazi au jirani au mchumba au yeyote.

Ukipata mkopo wa 500,000, mwambie na mhakikishie kuwa utamrejeshea ndani ya wiki mbili hivi kiasi kisichopungua 400,000

6. Nenda na ile 500,000 bank fastaaaa. Fungua account, weka 500,000 haraka sana. Bila kuchelewa.

7. Wakati unafungua account ya kawaida ya savings, waambie unataka kufungua na FDR. ile account ya kuweka pesa kwa muda maalum.

Hapo hapo watakujazisha na form za kufungua hiyo account na hivyo ziweke hizo hela zote ktk hiyo account.

Muda utaamua wewe kama ni miezi mitatu au sita au mwaka.m

Wakisha maliza fuata hatua ya 8

8. Baada ya siku mbili au tatu, rudi Bank haraka sana.  Fastaaaa. Waambie unataka mkopo kwa dhamana ya ile FDR yako. Yaani unakopa lakini dhamani ni hela yako mwenyewe

Mara nyingi bank wanakopesha mpaka 90% ya dhamana yako. Hivyo ktk ile 500,000 (hela uliyoiweka) unakopa mpaka 450,000.

Sasa kopa hiyo 450,000. Na Mara nyingi mkopo huu ni siku mbili au tatu unapata hela yako ya mkopo.

9. Sasa rudi kamlipe yule jamaa wa 500,000. Mlipe 450,000 na mwambie 50,000 itakuja ndani ya mwezi tu. 

Ukikopa kule bank, waambie/waombe marejesho yasianze mwezi huo bali mwezi unaofuatia. Ili mwezi huo umalizie kulipa ile 50,000 ya watu. Uwe umemaliza deni LA 500,000.

Hapo utakuwa umemaliza like deni la "mjomba" shangazi, kaka, Dada n.k. ambalo halina dhamana. Umebakiza deni LA bank ambalo lina dhamana ya hela yao. 

10. Sasa anza kulipa deni LA bank kila mwezi, bila stress. 
Marejesho yanatoka ktk ile hela uliyoipata kwenye no.2.

HITIMISHO:
Kama ulikopa mkopo wa miezi 6 kule bank, na marejesho yakaenda sawa maana yake kwa miezi 6 utakuwa umemaliza mkopo wa bank. Na hivyo amana yako ileeee ya 500,000 iko huru unaweza kuichukua.

Hapa ni kwamba unatafuta uwezo wa Ku save angalau 80,000 kila mwezi kwa maana ya kulipa mkopo wa bank.

Faida za kusave kwa njia hii:
1. Kwanza inakongezea imani na nidhamu ya kulipa madeni na unapata sifa nzuri kuwa wewe ni "mlipaji' yule uliyechukua 500,000 yake na kumlipa, hata wiki ijayo anaweza kukuazima tena. Na kama hana anaweza kukuazimia kwa wenzake.

2. Unaeleweka bank na Mara nyingine ukitokezea hauwi mgeni kiviiiile kwenye mikopo.  Na unajiongezea sifa ya kulipa pia 

3. Unalazimika Ku save kwa *kulipa deni* tofauti na kuweka tu hela bank au chini ya mto, utazitoa kidogo kidogo na kuzila kiti moto hadi ziishe. 

4. Utaepuka matumizi ya dharura hata harusi utachangia kwa mahesabu. Wale waomba nauli n.k. hutakuwa na hela ya kuwapa ukifikiria rejesho la bank. 

5. Fedha unayoiweka bank ktk account maalum inakuwa na RIBA kidogo. Hata kama ni 3% kwa mwaka si haba. Ungeweka chini ya mto usingeipata .

KUJITOA KUNAKUHITAJI ZAIDI na NIDHAMU YA PESA NI MUHIMU
——————————————
Oscar R NYIRENDA.
CPA (T)
MSc Accounts and Finance
BCOM Accounting

Senior Manager: Credit
Exim Bank (T) Ltd


Mstaafu M.Kiti wa Vijana KKKT, DMP.
From: UMOJA WA VIJANA DMP


Joche Team

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...