NAMNA GANI MALENGO YAKO YANAISAIDIA JAMII?
Imeandikwa na Joche
Hello.
Nakusalimu na kukupa pole na hongera kwa shughuli za siku zima ya leo. Kwa kuendelea kuyaatamia malengo yako ya kila siku.
Leo tena tukiwa tuko mwisho wa mwezi wa nne. Ni wakati wa kujiuliza maswali kadha wa kadha ambayo yakuweza kupima umefanikiwa kiasi gani katika yake malengo yako, au umekwama wapi na tatizo ni nini? Je kipi kiongezwe na kipi kipunguzwe katika ile ramani ya kuelekea malengo yako (Rejea iliyopita Makala iliyokuwa na kichw cha habari Dira ya Maisha).
Leo natamani kuzungumza na mtu mmoja juu ya ni NAMNA GANI MALENGO YAKO YANASAIDIA JAMII?
Nilipokuwa napata wazo la kuandika juu ya hiki kichwa cha habari niliwaza sana juu ya watu ambao tayari washapanga malengo yao na tayari wameshaanza kuyafanyia kazi.
Kiuhalisia wengi wetu tunaposema malengo kutimia wengi wetu huwaza haraka juu ya UHURU WA KIFEDHA.
Yaani huwa tunahesabu mtu mwenye fedha nyingi huyo ndiye aliyefanikiwa zaidi kuliko wengine. Hivyo hata malengo yetu wengi ni yamewekezwa hasa katika kuongeza kipato au kuzalisha fedha zaidi
Lakini katika maisha vipo vitu vingi sana ambavyo mtu anaweza kuwa amepanga avitimize na akivitimiza malengo yake yamekamilika kabisa.
Lakini pia katika malengo hayo hayawezi fanana. Wakati mwingine anawaza akisha kuwa na baiskeli basi maisha yake haitaji jambo lingine wapo wengine wanawaza kumiliki ndege na meli.
Lakini huwezi dharau malengo ya mtu maana hata mitazamo haifanani. Kiwango cha furaha ya nafsi havitofautiani japo hakuna anayependa maisha ambayo hatakuwa na furaha nayo.
Watu wa namna hii mara nyingi ni lazima wawe na vyanzo vingi vya kuwaingizia fedha ambazo zitawasaidia kuibuka na kufikia malengo yao. Jambo la kusikitisha ni kwamba pamoja na kufanya mambo mengi mfano: kuuza nguo, kuuza Viatu, kuuza Maji, Kuwa na Maduka, kuwa na mifugo na kadhalika lakini bado mambo hayastawi kwa kiasi ambacho wanatamani. Swali ni kwanini?
Nianze kwa kujibu hivi:
Swala sio ni biashara ni ngumu, au mtaji ni mdogo au huna bahati.
Jibu ni kwamba vyanzo vingi ambavyo tunavyovianzisha havina MAJIBU YA SHIDA ZA JAMII au niseme kwa namna nyingine ni kwamba biashara nyingi/vyanzo vingi ambavyo tunategemea tupate faida kutokana na jamii kushiriki havina FAIDA KWA JAMII yaani JAMII HAWAONI KAMA WANAHITAJI hilo. Hivyo ndio maana hata ugumu wa wao kununua wazo lako inakuwa ngumu (samahani kwa kusema hayo).
Na hii husababishwa zaidi na kuanzisha vitu ambavyo tunaona sisi tunavitaka lakini hatuangalii kama jamii inavitaka?
Na hii utaona hata baadhi ya miradi mingi imekufa si kwasababu haikuwa bora ila ni kwasababu jamii haikuona umuhimu au haikuwa na uhitaji wa hiyo huduma kwa eneo hilo hivyo hata ushiriki wao utakuwa ni mdogo sana.
NINI UNAWEZA FANYA:-
Hakikisha unapopata wazo lako ambalo unatamani uliwekeze au uliuze kwa jamii ili upate faida.
SWALI LA KWANZA liwe Je hili wazo Jamii wanafaidika na nini? Je wazo hili ndio kitu wanataka? Usifanye jambo kwa hisia zako binafsi utaishia kuumia moyo na kupata hasara.
Kama ni Duka je hiyo jamii wana uhitaji na Duka? Isije ikawa ni jamii ya watu ambao wananunua katika Masupermarket utaishia kupata hasara maana hawana uhitaji na hiyo huduma japo unaweza kuwashawishi ila itahitajika nguvu ya ziada kuweza kukuelewa.
KEEP ON FIGHTING LETS GROW TOGETHER
———————————————
Author: Joseph Geotham Mrema
Calls&Whatsapp: 0712851687
Email: josephgeotham4@gmail.com
KARIBU UJIPAKULIE APPLICATION yetu katika PLAYSTORE inatwa “JocheApp”
Joche Team
No comments
Post a Comment