RAFIKI NA TABIA


Hellow Ndugu? Habari za muda huu?

Poleni na majukumu ya hapa na pale yakuelekea katika ukamilifu wa malengo yako

Leo ningependa kuongea na mtu au watu kuhusiana na watu au mazingira yanayotuzunguka

Kuna masemo usemao show me your friends i will tell you who you are..(nionyeshe marafiki zako nitakwambia tabia zako/wewe ni nani)

Tujifunze kuchagua watu wakuwafanya rafiki zetu au watu wetu wakaribu na unapokuwa nao jiulize ni vitu gani mnalishana au ni mawazo gani mnapeana? ni mada gani mnajadili mara kwa mara?

Je vinawajenga au vinawabomoa?

1 Wakorintho 15:33
Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.

Kunamchango mkubwa sana katika mazingira yako na marafiki zako ambao huchangia katika mwenendo wa mtu na tabia yake.

Swali la Msingi?

Nani ni rafiki yako? Ana tabia gani?

Nimeuliza Tabia maana tabia ni kama ugonjwa wa Ebola (ni mfano) huambukiza toka kwa mto mmoja kwenda mwingine kwa njia nyingi. Unaweza ona uko salama na uko katika mfumo stahiki wa jamii. Kumbe la hasha ushatoka kwenye mfumo wako wa maisha kwa kuambukizwa tabia mbaya/nzuri.

Muda mwingine wahenga wakasema Ndege wanaofanana huruka pamoja. Walikuwa na maana kubwa sana maana unayeongozana nae kuna eneo mnalofanana tu. Huwezi kuwa rafiki na mtu kama hamna kunachowaunganisha na huu mfanano ndio tunaita tabia ambazo zinawaunganisha.

Mfano wa Yesu na wanafunzi wake.
Kuna kipindi Petro anafananishwa na Yesu kwa muonekano hata mwenendo wake. Hii ni kutokana na tabia ambayo waliambukizana na Yesu. Si kwamba Petro alifanana kimo na Yesu la hasha, si kwamba Petro alifanana na Yesu kitaaluma la hasha (kwanza Petro alikuwa mvuvi naweza hisi alikuwa mtu wa miraba minne). Lakini wakipomuona wakasema hata kuongea kwake anafanana na Yesu. Hii ni ule mfumo halisi wa maisha ya Petro katika kila kitu ukifanana na Yesu.

Swali la Msingi?

Rafiki yako anakuambukiza nini? Kina msaada gani kwa maisha yako ya mbeleni? Jamii inafaidikaje na hiyo tabia uliyoambukizwa?

Je ni Uvivu? Je ni Kufanya kazi kwa Nguvu?, Je ni kudanganya? Je ni Kusema Kweli? Je ni kukata tamaa au Kutokukata tamaa? Je ni ugomvi au kuwa na nidhamu?

Wewe wajua ni nini umevuna kwa rafiki yako?
Kama ni kibaya Badili sasa Hivi huyo Rafiki, Tafuta wa kufanana nae. PERIOD.
Hiyo haina kupapasa wala kuitazama kwa upole.

Ukijidai kumuonea haya jua WEWE NI NAHODHA WA MELI YAKO (Maisha yako) unaitoboa hiyo meli wewe mwenyewe na utazama mwenyewe..

Karibu sana.

_________________________________


Author: Joseph Geotham Mrema
Contacts & Whatsapp: +255 712 851687
Email: josephgeotham4@gmail.com

Visit:
Instagram: joseph_geotham_mrema
Fb: Joseph Geotham Mrema

Download our Application called JocheApp

Joche Team
KEEP FIGHTING TO THE TOP

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...