WOSIA WA BABA
1. Naikamata kalamu,wosia huu natuma
Naanza nayo salamu,ndilo jambo la hekima
Wanangu nawasalimu,baba yenu ninasema
Nyakati hizi za mwisho,wanangu ziepukeni
2. Moyo unanisukuma,niseme yangu ya ndani
Mawazoni nimezama,sijui nianze nini
Isikieni kalima,inayo mambo yakini

3. Nalotaka mfahamu,ni kuhusu jambo hili
Siku hizi wanadamu,wamejawa ujahili
Msije kupewa sumu,kweli mkaacha mbali

4. Kutabana kwa henezi,wala hawaoni shida
Wanaufanya ulozi,wameiacha ibada
Chuki zao zipo wazi,wanaupoteza muda

5. Wengine hawashakiki,kwa kupenda kujivuna
Wana mwingi uzandiki,mambo yao ni bayana
Kweli wao hawataki,wamechagua laana

6. Zitambueni nyakati,kuwa huu ndio mwisho
Ukomboeni wakati,kwa kujenga yenu kesho
Msipende shotikati,mouvu hayana posho

7. Wapo wataowabeza,kisa mmeshika kweli
Lisiwafanye kuwaza,kweli kuitupa mbali
Dunia itawameza,wana sikieni hili

8. Kungekuwapo na simu,wana ningewapigia
Niwafungue fahamu,kuhusu hii dunia
Nipo na nangoja hukumu,simu siwezi tumia

9. Kituo sasa nafika,hii ndo yangu hatima
Kalamu chini naweka,wosia kwenu natuma
Kamwe msiache shika,yangu niliyoyasema

________________________________
Mtunzi: Kinyafu Marcos.
Contact: +255 714 129 520
Barua pepe: kinyafumarcos@gmail.com
Imeletwa na Joche App
Joche Team

No comments
Post a Comment