TAFUTA DIRA YA MAISHA YAKO

JocheApp

Hello

Habari yako ndugu yangu. Pole na majukumu ya siku nzima ya leo. Ni wakati mwingine tena natamani nikukumbushe mambo kadha wa kadha ambayo ni ya kawaida katika maisha yetu lakini kama hatuyafanyi kazi basi hugeuka kuwa na madhara hasi katika maisha yetu.

Siku moja nikiwa nimekaa na rafiki zangu tukibadilishana mawazo mtu mmoja akasema ni vigumu mtu kupotea kama hajui anapokwenda.

Mfano: Wewe umetoka home umeoanda gari lakini hujui unapokwenda, ghafla ile gari ikaharibika sehemu usiyoifahamu wala huna mwenyeji. Ukajaribu kuuliza njia ukitaka kupata maelezo ya safari yako. Mtu utakaye kutana nae ukamwambia ndugu yangu nimepotea, mtu huyo atakuuliza umepotea unakwenda wapi? Ukamjibu sijui ninapokwenda unadhani atakupa majibu yenye kutosheleza kiu ya moyo wako? Jibu ni HAPANA.

Hili ndio jambo ambalo mara nyingi katika maisha yetu hutokea.

Unaamka asubuhi na mapema unawahi ofisini.  Lakini ukimuuliza mtu huyu unataka kufanikisha nini? Hana jibu

Mwingine anakimbizana na biashara ukinuuliza unataka kufanikisha nini? Atakwambia niendeshe maisha. Yaani hana malengo hajui anataka biashara yake impeleke.

Mwingine ni hodari sana wa kufanya hili na lile lakini hajui anapokwenda. Hajui mwisho wa safari yake ni wapi.

Mwingine anasoma. Ukimuuliza kwanini unasoma hicho unachokisoma, hana majibu kamili ya wapi anaenda. 

Mwingine anatakaa kuwa kiongozi ukimuuliza katika kuwa kiongozi unataka kufikia wapi?? Hana majibu yanayoeleweka.

Maisha ya wengi wetu yamekosa dira, yamekosa mkakati thabiti wa njia tunayotaja kuifikia. 

Wahenga walikuwa na maana kubwa sana waliposema MALI BILA DAFTARI HUISHA BILA  HABARI.


Je umechora ramani ya maisha yako wapi unaenda? Je unajua baada ya hatua uliyopo inayofuata ni ipi? Na kwanini uende hatua hiyo? Ni changamoto kufika unapotaka kama huna dira huna kituo cha kufika. 

Hii inamaanisha kwamba popote utakapokuwa  umefikia ndio mwisho wa safari yako.

Kama unadira utakuwa na kiu ya kupambana kutoka hapo ulipo uende kituo kinachofuata kuikaribia safari yako maana kadiri unavyopungiza vituo na umbali ndio unazidi kupungua kukaribia mwisho wa safari yako.

Nikusihi sana chora ramani ya maisha yako, panga mikakati ya kila unachokifanya unataka ufike wapi? Na kwanini ufike huko, nini faida ya kufika huko? Je ukifika kuna faida au hasara?

Mimi nataka Application yangu ya JocheApp iwe application namba moja ya kutoa elimu wa watu na kuwainua watu waliovunjika moyo katika Nchi yangu ya Tanzania na hata Bara la Africa na nje ya Africa.  Je wewe unataka kufanya nini?? Jibidiishe ongeza nguvu zaidi. 

Kijana kukata tamaa na maisha yake ni MWIKO hasa kijana wa KIAFRIKA. Kila kitu kinawezekana ni wewe tu kuzichanga karata zako sawia na kuweka msisitizo katika kitu unataka kukifanikisha.

Usiogope ukadhani muda/umri umekuacha. Anza sasa na mafanikio yako utayaona tu.

▶️Karibu tushauriane, Mawasiliano yangu yako hapo chini.

KEEP ON FIGHTING TO THE TOP

—————————————————
Author: Joseph Geotham Mrema
Calls&Whatsapp: 0712851687
Email: josephgeotham4@gmail.com

✍🏼KARIBU UDOWNLOAD APPLICATION yako ya JocheApp UPATE MAKALA NYINGI ZAIDI ZA KUELIMISHA.

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...