UWEZO WA KUTOKUOGOPA
Hello
Habari za wakati huu ndugu msomaji na mfuatiliaji wa makala zetu katika Application yako ya JocheApp ambayo inapatikana katika Simu za Android katika Playstore yako.
Kwanza kabisa nitumie muda huu kukushukuru wewe ambae umeweza kuidownload Application hii inayeendelea kukua kwa kasi kutokana na maoni yenu na mawazo yenu.
Siku ya leo natamani kuongea na mtu mmoja juu ya UWEZO WA KUTOKUOGOPA hasa katika maisha yetu ya kila siku.
Kimsingi binadamu tumeumba na hali ya kuhofia vitu kadha wa kadha na hii ni kutokana na hali ya utashi iliyo ndani yetu.
Kuogopa sio jambo baya lakini hugeuka kuwa baya pale uoga unapozidi na kukufanya kuogopa hata yale mambo ya msingi ambayo kiuhalisia ukiyafanya hayakupotezei heshima mbele za watu au kukudhalilisha ila unaogopa kwa sababu ya ule msemo wa WATANIONAJE?
Utakuta mtu yuko na rafiki yake na huyo rafiki zamani alikuwa wa faida ila sasa hivi amekuwa mzigo katika maisha yake ila anaogopa kuwa mkweli na kumrekebisha au kuvunja urafiki akihofia ATANIONAJE au JAMII ITANIONAJE?
Lakini pia kuna wengine ni wana mahusiano (wapenzi) na upendo umekufa kabisa imebaki mazoea ila kwasababu ya KUOGOPA swala la WATANIONAJE umebaki hapo na kuendelea kuumia
Pia wapo ambao wanafanya kazi katika mazingira magumu ambayo hayana faida kwao na kazi imegeuka kuwa TANZI lakini bado yupo hapo anaogopa kuacha kwa sababu ya kujali WATANIONAJE kama sina kazi?
Pia wapo wanaofanya BIASHARA zao yaani wamejiajiri wanaogopa kusema kitu wanacho uza kwa jamii na kwa marafiki zao wakiogopa WATANIONAJE? Anabaki kufanya biashara ya kujificha ficha nakuambulia hasara
Kuna kundi la wanafunzi wapo ambao wanapata shida kweli katika masomo lakini wanaogopa kusema kwa wengine na kuomba msaada kwa kuogopa WATANIONAJE nikiuliza?
Nini nataka kusema?
Kitu ambacho hakikuui kinakufanya kuwa imara zaidi.
Usiogope kusema changamoto yako, usitishwe na changamoto za mwingine kwa misingi kamba fulani alifanya akafeli na wewe ukifanya utafeli.
Fanya wewe kama wewe na utafanikiwa tumia njia zako.
ULIZA, TAFUTA MAARIFA, JIENDELEZE KATIKA JAMBO UNALOTAKA KULIFANYA.
Usiruhusu HOFU ikutawale.
Uzoefu mbovu au mzuri ndio humfanya mtu alivyo na kwa kushinda vipindi vigumu hutufanya IMARA NA UKOMAVU wa KIFIKRA ndani ya maisha yetu.
Usiogope kabisa kabisa.
Kwa WAKRISTO katika Biblia neno USIOGOPE limeandikwa mara 365 ikimaanisha kuwa kila siku UNAKUMBUSHWA KUTOKUOGOPA.
Pambana tu. Usiogope, hiyo changamoto haita kuua itakufanya kuwa imara zaidi na zaidi na kukuongezea MOTISHA WA KUSONGA MBELE ZAIDI.
Duniani huwezi ridhisha kila mtu lakini pia huwezi kuwa mbaya kwa kila mtu.
Pia huwezi fanya kila kitu lakini unaweza fanya japo mambo kadha wa kadha endapo utaitoa hofu na kutokuogopa jambo lolote ambalo halikudhuru kwa namna moja au nyingine..
Kushindwa KWAO sio KUSHINDWA KWAKO.
KUDONDOKA kwao sio KUDONDOKA KWAKO.
Kijana ni Nguvu ya Taifa, endapo nguvu inaogopa kufanya kazi stahiki hakuna kitu kitasogea.
Nikutakie wakati mwema sana
———————————————-
Author: Joseph Geotham Mrema
Call &Whatsapp: +255 (0) 712 851687
Email: josephgeotham4@gmail.com
JOCHE TEAM
No comments
Post a Comment